Kiingereza cha kiTanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiingereza cha kiTanzania

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Ladslaus Modest, Dec 11, 2008.

 1. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kiingereza cha kiTanzania

  Wapendwa wana JF na wale wote wenye mapenzi mema na nchi yetu Tanzania; hapa ulimwenguni katika nchi zote zilizotawaliwa na mwingereza takriban kila moja ina kiingereza chake mfano kuna kiingereza cha Australia, Belize, Canada, Caribbean, Hong-Kong-S.A.R., India, Indonesia, Ireland, Jamaica, Malaysia, New-Zealand, Philippines, Nigeria, Singapore, South-Africa, Trinidad-&-Tobago, UK ,US, na Zimbabwe.

  Ukifuatilia kwa makini kila nchi iliyotajwa hapo imeongeza au imepunguza au imebadili neno au herufi fulani kutoka kwenye kiingereza cha asili cha Uingereza.

  Mfano Mwingereza anatumia neno POST CODE lakini mMarekani anatumia neno hilo hilo kama ZIP CODE

  Kinachosikitisha ni kwamba sie waTanzania tunatumia either American English or British English.

  Kuna maneno mengi ambayo wataalam wa lugha mnayafahamu (mie sio mtaalamu wa lugha bali ni Mchungaji) ambayo mnaweza kuyabainisha hapa ili tuweze kuwa na kiingereza chetu cha kiTanzania.

  Mie nilikuwa ninapendekeza tuanzie hapa: - Badala ya kumuita baba mkubwa na/au baba mdogo UNCLE tuwe tunawaita ELDER FATHER na YOUNGER FATHER. Badala ya kumuita mama mkubwa na/au mama mdogo AUNT tuwe tunawaita ELDER MOTHER na YOUNGER MOTHER ... ... ... nakadhalika.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ur funny, young mother, sasa na mama aliyezaa akiwa na umri mdogo ataitwaje?

  Hicho si Kiingereza cha Kitanzania, ni Kiswahili katika maneno ya Kiingereza.
   
 3. Kisura

  Kisura JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2008
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 363
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Tukiwa kwenye kuelimishana, it is "Younger" not "Young"
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hii inafaa kuwepo kule kwenye jukwaa la lugha/elimu
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Dec 11, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Yeah labda utajifunza kiingereza lol
   
 6. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #6
  Dec 11, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Kwanza asante Kibunango kwa kubonyeza "Report this" icon. Kijakazi has been banned for misbehaving.

  The topic is being moved to the proposed forum
   
 7. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2008
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,552
  Likes Received: 1,310
  Trophy Points: 280
  Ladislaus,
  Its very interesting topic, ila umeweka mada mbili, moja nikutaka kufahamu kama kuna maneno ya kiingereza cha kitanzania so kama yapo ni yapi????

  Pili umepropose kutohoa maneno ya kiswahili kuwa kiingereza ama kutranslate swhili words to English as you have proposed two words.

  Maoni yangu, kwanza kabisa pronounciation yetu inatutambulisha sisi kama watanzania mfano wa neno Determine (sisi tunasema ditamain badala ya ditamin, kuna maneno kama cafee, .....
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Dec 11, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  elite (ilit) sisi tunasema elait
   
 9. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #9
  Dec 11, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  kuna advert moja itv ya chuo kimoja called Gold.... something .. mtangazaji huyu sijui vipi .. mambo mengine yote anayasoma uzuri mathalan certificate for ..... mpaka mwisho kashese inakuja pale anaposema "wraiten" instead of written .. english .. naona aibu kama nimesema mm.
   
 10. M

  Mutu JF-Expert Member

  #10
  Dec 11, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sisi english sio first language kwetu Tanzania kwa hiyo ni vigumu kusema english ya Tz .Nchi wanaotumia english kama lugha yao ya kwanza kweli wantofautia vitu fulani kiwemo hata matamushi .Kama vile kiswahili cha Kenya ,Tanzania na pia ndani ya Tanzania Pwani kiasi fulani wanatofautiana na bara.
  Sisi hatuna english yetu tunakopa na kutumia kama ilivyo ,wengi bongo wantumia english ya Uk ,na siku za karibuni american english kwa kuwa kunawatu wametokea kuishi US na kusikiliza american english kupitia movie na songs.

  Unachoweza kusema ni kuwa uncle na aunt kwenye kiswahili tunatofautisha kama mjomba na shangazi tu ,na english wanaendelea kujumuisha baba mdogo na mkubwa kama uncle na mama mdogo na mkubwa.Na ukitaka hivyo sidhani kama kwenye kiswahili tuna nephew and neice.
  Nikutumia tu english kulikana na sehemu unapokuwa kama US ,UK ,kukijichanga kwa Jamaica ukutnane na patois kazi unayo.
   
 11. Tanzania 1

  Tanzania 1 Senior Member

  #11
  Dec 11, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 197
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tukiamua kuwa na Kiingereza chetu (Mmmh!) tutakuwa tunachangia kuharibu lugha ya wenyewe, kwani lugha si maneno tu bali hata utamaduni wa lugha husika unajumuishwa. Muhimu ni kuimarisha lugha yetu.

  Hivi sasa tunaiharibu lugha yetu kwa kuichanganya na lugha nyingine za Kimagharibi, hasa Kiingereza. Kwa mfano, badala ya kutafuta neno sahihi la Kisw. la kutumia, mtu anasema: "Leo nimeboreka (akimaanisha I'm bored) sana!". Msemaji km huyu anaonesha manung'uniko, lkn anachosema, kikitafsiriwa kwa Kisw. si manung'uniko -- kwani kuboreka maana yake ni kuwa bora! Km tunavyoiharibu lugha yetu, ndivyo vivo hivyo tutachangia kuharibu za wengine.
   
 12. Tanzania 1

  Tanzania 1 Senior Member

  #12
  Dec 11, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 197
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Huku pwani ambako ni chimbuko la Kiswahili, dada hasa ni ndugu mkubwa wa kike, na kaka ni ndugu mkubwa wa kiume. K/sbb ya kuiga lugha na utamaduni wa Kiingereza, hata mdogo wangu (wa kike) ni dadangu, na mdogo wangu wa kiume naye ni kakangu!
   
 13. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #13
  Dec 11, 2008
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Huwezi kusema,Younger Father,kwa sababu Younger Father inayo precise meaning. Kama watu wawili,wote ni fathers,na mmoja ni younger,basi yeye ni Younger Father. Kwa hiyo,hizi suggestion zako haziwezi kukubalika to the subconcious mind ambayo inachukua kila kitu very literally.
   
 14. p

  pitapita Member

  #14
  Dec 11, 2008
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Niliwahi kuomba passport ya Tanzania. Katika sehemu ya Emergency contact niliandika jina la baba mdogo na sehemu ya uhusiano na mwombaji niliandika " baba mdogo" . Wakati nilipopata passport ilitafsiriwa kama: young father ...story ya mwaka 1992 approx.
   
 15. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #15
  Dec 11, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama ni utamaduni wa kiingereza. Kwa waswahili, Dada ni 'ndugu wa kike' na Kaka ni 'ndugu wa kiume' bila kujali umri wao. Tizama kamusi zote za kiswahili, hasa zile zilizoandikwa zamani utaliona hili. Kwa asili neno 'ndugu' ni mtu ambaye mmechangia baba na/au mama. Kwa hivi ukimtambulisha mtu kwamba ni nduguyo, moja kwa moja mtu anajua huyo ni dada yako au kaka yako.
   
 16. Tanzania 1

  Tanzania 1 Senior Member

  #16
  Dec 11, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 197
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Jaribu kuulizia kwa wazee wa pwani (hasa Kimtang'ata) khs tofauti kati ya "kaka/dada" na "mdogo" (eg wangu).
   
 17. bokassa

  bokassa JF-Expert Member

  #17
  Dec 11, 2008
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kizungu kimekuharibu!!!!!!!
   
 18. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #18
  Dec 12, 2008
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ha Ha ha kaka mi naiunga mkono hoja yako kimsingi hayo maneno yamekaa vibaya. Kwa kuwa shangazi anaitwa Aunt na Mjomba anaitwa Uncle nadhani nivema kumtofautisha baba mkubwa na mdogo vile vile mama mkubwa na mdogo.

  Hii ni mada muhimu naomba wataalam wa lugha watusaidie si jambo la kupuuza.

  cheers
   
 19. inovasqo

  inovasqo Member

  #19
  Dec 12, 2008
  Joined: Dec 5, 2008
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Daaa!!!hapo umenipa mwanga maana nilijua ndugu ni jamaa yako,awe mtoto wa baba mdogo,mjomba au hata mliyetoka naye ukoo mmoja
   
 20. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #20
  Dec 12, 2008
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  Lugha yoyote mpaka ikaitwa ni lahaja ya sehemu fulani, lugha hiyo ama lahaja hiyo hujitengeneza yenyewe kutoka kwa wazungumzaji na si kwa kupanga kwamba waTanzania tuwe na kiingereza chetu tofauti na kungine. hata sasa kiingereza chetu(waTanzania tulio wengi) ni tofauti na wengine. hivyo tungoje ijitengeneze yenyewe.

  Vilevile maneno ya BabaMdogo BabaMkubwa ama Shangazi, Mjomba. huu ni mfumo wa kiswahili si lazima mfumo huu utumike kwenye lugha nyingine. Kama kuna lazima kutofautisha basi ni bora utumie hivyohivyo BabaMdogo hata kwenye Kiingereza.
   
Loading...