Kiingereza cha kiTanzania

Kiingereza cha kiTanzania

Wapendwa wana JF na wale wote wenye mapenzi mema na nchi yetu Tanzania; hapa ulimwenguni katika nchi zote zilizotawaliwa na mwingereza takriban kila moja ina kiingereza chake mfano kuna kiingereza cha Australia, Belize, Canada, Caribbean, Hong-Kong-S.A.R., India, Indonesia, Ireland, Jamaica, Malaysia, New-Zealand, Philippines, Nigeria, Singapore, South-Africa, Trinidad-&-Tobago, UK ,US, na Zimbabwe.

Ukifuatilia kwa makini kila nchi iliyotajwa hapo imeongeza au imepunguza au imebadili neno au herufi fulani kutoka kwenye kiingereza cha asili cha Uingereza.

Mfano Mwingereza anatumia neno POST CODE lakini mMarekani anatumia neno hilo hilo kama ZIP CODE

Kinachosikitisha ni kwamba sie waTanzania tunatumia either American English or British English.

Kuna maneno mengi ambayo wataalam wa lugha mnayafahamu (mie sio mtaalamu wa lugha bali ni Mchungaji) ambayo mnaweza kuyabainisha hapa ili tuweze kuwa na kiingereza chetu cha kiTanzania.

Mie nilikuwa ninapendekeza tuanzie hapa: - Badala ya kumuita baba mkubwa na/au baba mdogo UNCLE tuwe tunawaita ELDER FATHER na YOUNGER FATHER. Badala ya kumuita mama mkubwa na/au mama mdogo AUNT tuwe tunawaita ELDER MOTHER na YOUNGER MOTHER ... ... ... nakadhalika.

Naomba kuwasilisha.

Mkuu nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa.
Mimi nilishawahi kufanya kazi na wacanada, wa australia, na wasauzi.
Siku ya kwanza atakapojitambulisha utajua kabisa huyu ni msauzi au muaustralia.

Wa Africa Magharibu hususani wanaijeria ndio wanafahamika kabisa, mfano wao 'thanks' huweza kutamka 'thankoo' na asione tatizo kabisa.
Mi nafikiri nasisi tuwe na kaluga ketu ka kibongobongo.
 
Sawa kabisa mchungaji lakini wakati huohuo tukienzi kiswahii chetu kwa kuifanya iwe lugha ya kufundishia kuanzia chekechea hadi vyuo vikuu na kiingereza, kifanransa, kichina na lugha nyingine tujifunze kama lugha pekee ili watanzania tuweze kujieleza barabara badala ya kuchanganya lugha na 'yaani' kibao.

Watanzania wachache mno wana uwezo wa kujieleza kwa ama Kiswahili au Kiingereza bila kuchanganya lugha au kujitafunatafuna, taifa linakwenda pabaya. Wakenya wana Kiswahili chao ambacho tunadhani ni broken lakini wako mbele sana katika kujifunza kiswahili na baada ya miaka michache watakuwa juu kuliko sisi, kwani wataandika vitabu na kuviuza nchi zinazoibukia kuongea Kiswahili kama vile Rwanda, Burundi, DRC, Somalia, n.k. Mnaonaje wana JF?
 
What difference does it make? Ninavoelewa hapo maneno yote yamekua ya kiingereza ila umeamua tu kurefusha sentensi. Ama umeunga maneno mawili na kuyalazimisha yalete maana ya neno moja.
 
Natumai huko mahakamani, mahakimu na waendesha mashtaka huwa wanaandika maelezo kwa kiingereza.

Sentensi kama hii wataiandikaje? ........"nilitoka kwa baba mdongo na kuelekea kwa mjomba ambako nilikuta mauaji yametokea........"

Nadhani wataandika majina ili kutofautisha, kazi ipo kama wanamajina yanayo fanana,
 
What difference does it make? Ninavoelewa hapo maneno yote yamekua ya kiingereza ila umeamua tu kurefusha sentensi. Ama umeunga maneno mawili na kuyalazimisha yalete maana ya neno moja.

Badili hiyo kwenda kwenye kiswahili....
 
Hivi lugha yetu ni SWAHILI LANGUAGE au KISWAHILI LANGUAGE......nimekutana na mgongano huu kwenye vyombo vyetu madafu vya habari vinavyoandika ki-british
 
Hivi lugha yetu ni SWAHILI LANGUAGE au KISWAHILI LANGUAGE......nimekutana na mgongano huu kwenye vyombo vyetu madafu vya habari vinavyoandika ki-british

Ukiongea kiingereza lugha hii ni "Swahili" wala si "Kiswahili"

Ki ilivyotumika hapa ni kitangulizi (prefix) katika lugha ya kiswahil kinachoonyesha hii lugha imetoka wapi, ndiyo maana kila lugha inaanzwa na Ki, Kisambaa, Kizulu, Kiingereza, Kirusi n.k.

Kwa hiyo ukiweka "Ki" unatoka katika Kiingereza na kusema kiswahili, na "Kiswahili Language" inachanganya kiswahili na kiingereza.

Ama utasema "Lugha ya Kiswahili" au "The Swahili Language"
Ama utasema "Lugha ya Kiingereza" au "The English Language"
Huwezi kusema "Kiswahili language" kama usivyoweza kusema "Kienglish language" au "Kiingereza Language"

Utakuwa unachanganya mambo.
 
Swahili and Kiswahili are interchangeable.

It is perfectly alright to say "Tanzanians speak Kiswahili" or "Tanzanians speak Swahili"

... xo xo xo ...
 
Swahili and Kiswahili are interchangeable.

It is perfectly alright to say "Tanzanians speak Kiswahili" or "Tanzanians speak Swahili"

... xo xo xo ...

You did not attempt to address the reasoning given above.

If you interchange "Swahili" and "Kiswahili" you should easily be able to interchange "English" and "Kiingerezaish "

Ki is to Swahili what "ish" or "ese" is to English. Ki is a Swahili prefix and has no business in English (in this context) the same way ish and ese are English suffixes with no business in Swahili.
 
Ukiongea kiingereza lugha hii ni "Swahili" wala si "Kiswahili"

Ki ilivyotumika hapa ni kitangulizi (prefix) katika lugha ya kiswahil kinachoonyesha hii lugha imetoka wapi, ndiyo maana kila lugha inaanzwa na Ki, Kisambaa, Kizulu, Kiingereza, Kirusi n.k.

Kwa hiyo ukiweka "Ki" unatoka katika Kiingereza na kusema kiswahili, na "Kiswahili Language" inachanganya kiswahili na kiingereza.

Ama utasema "Lugha ya Kiswahili" au "The Swahili Language"
Ama utasema "Lugha ya Kiingereza" au "The English Language"
Huwezi kusema "Kiswahili language" kama usivyoweza kusema "Kienglish language" au "Kiingereza Language"

Utakuwa unachanganya mambo.

'Kiswahili langunge' is palatable too for lateral thinkers. Otherwise, everything would be boring under their sun.
 
Back
Top Bottom