Kigoma: Mganga amuua Mteja aliyetaka kuzindika Fedha za Biashara Tsh milioni 9

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma linawashikilia watu wawili akiwemo dereva wa pikipiki na mganga wa kienyeji kwa tuhuma za kumuua na kisha kumfukia mwanamke aliyekuwa ameenda kuzindika fedha za biashara kiasi cha shilingi milioni 9.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo katika wilaya ya Kasulu na kukamatwa kwa mganga huyo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP James Manyama, amesema baada ya kutekeleza mauaji hayo walichimba shimo la kumfukia kisha kuchukua fedha zake ambazo katika upekuzi jeshi la polisi walizikamata nyumbani kwa mganga.


EATV
 
Tamaaa mbele mauti nyuma.
kwa nini utegemee uganga na ushirikina ili utajirike?!
Mtegemee Mungu kwa kila Jambo.

Imani za kishirikina zinawatesa sana watanzania walio wengi, kila jambo wanalo lifanya lazima ushirikina uhusike!
1. Sehemu za Biashara
2 . makazini
3. maofisini
4. vyeo
5. mahotelini mntulisha uchfu

n.k,
 
Tamaaa mbele mauti nyuma.
kwa nini utegemee uganga na ushirikina ili utajirike?!
Mtegemee Mungu kwa kila Jambo.

Imani za kishirikina zinawatesa sana watanzania walio wengi, kila jambo wanalo lifanya lazima ushirikina uhusike!
1. Sehemu za Biashara
2 . makazini
3. maofisini
4. vyeo

n.k,
Kuna pahala miaka ile ukisikia uteuzi wa Wakuu wa Idara..basi huo mwezi ni kupishana na watu wananuka mavi ya Ng'ombe .
Kuuliza unaambiwa watu hawalali ..mara wengine wanaojua wanasema leo flani amekusaliamia ee alikuwa uchi aisee.
 
Kuna sehemu/ makabila wanaamini Sana mambo ya uchawi kupitiliza, hivyo huwezi kumwambia lolote. Kwao kila kitu kinatokea kwa "mkono" wa mtu. There is no natural causes of the events, no science, no nothing!
 
...Yaani mtu una Shilingi Milioni 9 halafu unakwenda kwa Mganga ili ziongezeke?
Ina maana hata hizo ulizipata kwa Mganga?

Halafu sijui ni kwa nini watu wanaamini katika uchawi. Biashara wala haihitaji hivyo vitu!

Zaidi tu ya akili ya haraka! umakini katika mahesabu, majambazi na matapeli! uaminifu na utoaji wa huduma nzuri kwa wateja! kuanzisha biashara yenye tija kwa eneo husika, nk.
 
Kuna sehemu/ makabila wanaamini Sana mambo ya uchawi kupitiliza, hivyo huwezi kumwambia lolote. Kwao kila kitu kinatokea kwa "mkono" wa mtu. There is no natural causes of the events, no science, no nothing!

Kwani kwenye nyungu na yale matango pori kulikuwa na science ipi mjomba?

In the case, that sehemu = Tanzania (typical).

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom