Wanne washikiliwa kwa tuhuma za kumteka mtoto na kudai milioni 50 kwa baba yake ili wamwachie

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Jeshi la polisi mkoani Katavi linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kumteka mtoto wa kike, mwenye umri wa miaka 9 mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Mizengo Pinda iliyoko manispaa ya Mpanda kwa kumfungia chumbani na kudai pesa kwa baba yake kiasi cha Shilingi milioni 50 ili wamwachie.

Kaimu Kamada wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi ACP Kaster Ngonyani amewataja waliokamatwa kuwa ni Joseph John (24), Yusuph Sadick (27), Abraham Kassim (2) na Samwel Nzobe (41).

Kamanda Ngonyani Amesema tukio hilo la kikatili la kumteka mtoto huyo lilitokea Juni 13, mwaka huu, saa 8 mchana katika Manispaa ya Mpanda, wakati alipokuwa akitoka shule kufanya usafi.
Kamanda Kaster alisema moto huyo akiwa njiani maeneo ya jirani na Kanisa Katoliki limbo la Mpanda, anakwenda nyumbani kwao ndipo watuhumiwa hao walimteka na kumpeleka kusikojulikana na kumtishia kumuua vinginevyo sh. milioni 50 ndiyo wamwachie bila kumdhuru.

Alisema baada ya taarifa hizo, polisi walianza msako usiku na mchana katika maeneo yote ya mkoani Katavi, hatimaye Juni 14, mwaka huu, walimpata mtoto huyo akiwa salama katika maeneo ya Mtaa wa Milupwa, Manispaa ya Mpanda akiwa amefichwa chumbani kwa John ambaye ni miongoni mwa watuhumiwa.

Wazazi wa mtoto huyo wameeleza kuwa walijibizana na watuhumiwa hao kwa njia ya simu ambao watuhumiwa hao waliwatishia wazazi na kuwataka kutoa Shilingi milioni hamsini ili waweze kumwachia mtoto huyo.
 
Hopeless kabisa!

Usawa huu wapewe milioni hamsini kirahisi tu! Na hapo usikute walishapanga tayari mpaka matumizi ya hizo hela baada ya kupewa!!
 
Jeshi la polisi mkoani Katavi linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kumteka mtoto wa kike, mwenye umri wa miaka 9 mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Mizengo Pinda iliyoko manispaa ya Mpanda kwa kumfungia chumbani na kudai pesa kwa baba yake kiasi cha Shilingi milioni 50 ili wamwachie.

Kaimu Kamada wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi ACP Kaster Ngonyani amewataja waliokamatwa kuwa ni Joseph John (24), Yusuph Sadick (27), Abraham Kassim (2) na Samwel Nzobe (41).

Kamanda Ngonyani Amesema tukio hilo la kikatili la kumteka mtoto huyo lilitokea Juni 13, mwaka huu, saa 8 mchana katika Manispaa ya Mpanda, wakati alipokuwa akitoka shule kufanya usafi.
Kamanda Kaster alisema moto huyo akiwa njiani maeneo ya jirani na Kanisa Katoliki limbo la Mpanda, anakwenda nyumbani kwao ndipo watuhumiwa hao walimteka na kumpeleka kusikojulikana na kumtishia kumuua vinginevyo sh. milioni 50 ndiyo wamwachie bila kumdhuru.

Alisema baada ya taarifa hizo, polisi walianza msako usiku na mchana katika maeneo yote ya mkoani Katavi, hatimaye Juni 14, mwaka huu, walimpata mtoto huyo akiwa salama katika maeneo ya Mtaa wa Milupwa, Manispaa ya Mpanda akiwa amefichwa chumbani kwa John ambaye ni miongoni mwa watuhumiwa.

Wazazi wa mtoto huyo wameeleza kuwa walijibizana na watuhumiwa hao kwa njia ya simu ambao watuhumiwa hao waliwatishia wazazi na kuwataka kutoa Shilingi milioni hamsini ili waweze kumwachia mtoto huyo.
Kwa hiyo mtoto wa miaka miwili nae kawa mtekaji aisee tena kamteka mtoto wa miaka 9!!
 
Binadamu hawajui kuwa hata wangepewa hio millioni hamsini ndani ya miezi michache hio hela waingeona ndogo. Hela haina thamanai ya utu.
 
Back
Top Bottom