Kifo cha Nabeel chahusishwa na ushirikina, kafara imetimia!!!, Watanzania tuna mawazo ya ovyo sana

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,446
21,140
Aisee sisi Watanzania tuna mawazo ya ajabu sana.

Naona watu wengi wanahusisha kifo Cha Nabeel na imani za kishirikina.

Pointi yao ya msingi ni dhaifu sana ,eti kisa ile ajali ilikuwa mbaya sana na Chino katoka poa kabisa kana kwamba hakijatokea kitu.

Yani wao walikuwa wanataka eti na Chino angepata vijeraha kadhaa ndipo wangeamini ni ajali isiyohusisha nguvu za giza.

Na wameenda mbali zaidi kwa kusema eti kafara imetimia tutegemee mambo makubwa kutoka kwa Chino kupitia hiyo ajali.

Dah inasikitisha sana kwa kweli kama tumefikia huku.
 
IMG-20231112-WA0118.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umasikini shida sana Walahi
Kweli Dunia hii mtu anaamini nguvu za giza kisa mtu katoka bila majeraha
Kuna ndege ilianguka watu wote walikufa kasoro msichana mdogo ambae wazazi wake walikuwemo pia
Lakini hakuna aliewaza upumbavu huu
Fanyeni kazi hela haziji kwa kafara
Kijana huenda alikuwa hajavaa mkanda na pia wakati umefika

Eti tegemeeni mengi kana kwamba nae hatakufa
 
Ajali ya imetokea wapi?
Ajali imetokea wakiwa njiani kutoka dar kwenda tanga kwenye shoo ambayo walipewa dili na ummy ticha, maeneo ya ajali siyakumbuki ila nahisi walikuwa washakaribia tanga maana majeruhi walikimbizwa bombo.
Gari yao aina ya noah iligongana na roli na marehemu alikuwa ndio dereva. Ila huyo chino na marehemu mi siwajui
 
Back
Top Bottom