Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Mkuu tuko kwenye defining moment hapa duniani.
Mmarekani alifanikiwa kuwagawa washia na wa suni...Sasa kama wakirudi pamoja in the name of uislam na wakisaidiwa na mrusi na mchina si ni HATARI HII?

Ok...Naona umesahahu kuwa agenda hapa ama toka mwanzo ilikuwa kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini ama ukabila...UMESHASAHAU YA Mtikila na Kwaya ya Kinondoni.

Naomba sana mnisamehe kama RA si muislam basi naomba msamaha RASMI kwa kumuhusisha na uislam...Kwani mimi siamini kabisa UBAGUZI...NA mimi binafsi nakiri wazi kuwa wenye msimamo mkali...Either walokole ama wasilam...Hawa watu wajiangalie sana..Kwani dunia hii ni ya kuishi pamoja....Na pia tusisahahu kuwa too much of anything is harmfull.

Ila BANTU...Kaeni makini naona hamjafuatilia historia yetu ya Afrika!
Sisi sote ni ndugu kabla hata mwarabu hajaja kutukamata na kutuuza kwa Mzungu!

America hajawagawa Sunnis na Shiates...... Shiates na Sunnis hawatokuabliana kwa misingi yao na Taasubi zao!..... Unasema sio mdini, wewe ni MUONGO!!! Hapo juu umesema kwamba

Sasa kama wakirudi pamoja in the name of uislam na wakisaidiwa na mrusi na mchina si ni HATARI HII?

Are you trying to say kwamba waislam ni hatari in nature?. Kwamba wakipata supportkidogo tu watakuwa hatari duniani!?.....

Unasema mdomoni lakini humaanishi moyoni!.......
 
America hajawagawa Sunnis na Shiates...... Shiates na Sunnis hawatokuabliana kwa misingi yao na Taasubi zao!..... Unasema sio mdini, wewe ni MUONGO!!! Hapo juu umesema kwamba

Are you trying to say kwamba waislam ni hatari in nature?. Kwamba wakipata supportkidogo tu watakuwa hatari duniani!?.....

Unasema mdomoni lakini humaanishi moyoni!.......

https://www.jamiiforums.com/member.php?u=2260
tHe NapSTer of BonGo LaNd
tHe NapSTer of BonGo LaNd has no status.
Senior Member
Join Date: Fri Mar 2007
Posts: 53
Rep Power: 22
Thanks: 3
Thanked 5 Times in 4 Posts
Credits: 730

Quote:
Originally Posted by Zitto

Mwaka mmoja tangu kuingia madarakani
Serikali ya CHADEMA ina ahidi kufanya yafuatayo:

Elimu

Bajeti ya elimu kuongezeka kutoka 18% hadi 35%, kuongeza ajira za waalimu na kuboresha mishahara ya waalimu.

Afya

Kufuta VAT kwenye huduma na vifaa vya kina mama waja wazito na watoto.

Madawa ya kurefusha maisha kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kugawiwa kwa wote walioathirika.

Kupandisha mishahara ya madaktari na wauguzi.

Kilimo

Kufuta kodi zote pamoja na VAT kwa pembejeo za kilimo.

Kuweka mpango thabiti wa kutofautisha ardhi kwa ajili ya umwagiliaji.

Uchumi

Bajeti 2006/07 kupunguza VAT iwe 16%.

Kufanya mapitio ya mikataba yote ya uwekezaji na ubinafsishaji.

Tanzania kujiunga upya na COMESA.

Kutengeneza ajira milioni moja kwa kufanya mabadiliko makubwa katika sekta za madini, utalii, ujenzi na huduma za jamii.

Mfumo wa Utawala Bora

Kurudisha serikalini mali zote zilizochangwa na wananchi na kuhodhiwa na CCM kama viwanja vya mpira na majengo yanayotumiwa na CCM n.k.

Kupiga marufuku uuzaji wa nyumba za Serikali na kurejesha zilizokwisha uzwa kiupendeleo.

Kuvunja PCB na kuweka majukumu yote ya kupigana na rushwa chini ya Mkurugenzi wa makosa ya Jinai (DCI).

Kuboresha maisha ya kina mama kwa kuwawezesha kielimu na kuwapa nafasi katika utawala.

Inaendelea

Hey hey!!!!
Listen they are two political parties that will give us what we need;
CUF and CCM

thats it!!!!!!!!!!!! Nothing else!!!!!!!!!!!!
Ahsanteni kwa kampeni zenu!!!!!!!!!!!!! gudnyt!!!!!!!!!!!!!!

Maneno hayo uliyoyasema hapo juu...ESPECIALLY KWENYE RED HIGHLIGHT...YANAONYESHA KILA DALILI YA KUWA "MHAFIDHINA"
Yani mwenzako Zitto katumia muda woote kukuelewesha kuhusu mambo mazuri wenzako waliyoyafanya na wewe jibu lako ni fupi na la kijeuri kuwa eti vyama ni cuf na ccm tu...Na sasa unampa nani darasa la Msunni na Mshia?
 
Sema basi walichokupa waarabu wa cuf na ccm kiasi cha kuwadharau chadema.
Na wewe ni mtanzania gani mwenye kuzifagilia cuf na ccm?
Kweli vituko vya combination ni vingi...Sasa baada ya ccm-chadema...Sasa ni cuf-ccm combination ya waafdhina kama sikosei...Wabantu tutachaguwa ni nani wa kumwamini na wewe huwezi kutupangia...Na ni bora muwe makini na movement hii kwani la sivyo mtapata shida.
Mtajaribu lakini mwishowe hamuelewi RESOLVE YA WAZALENDO WA KWELI....TUTAPIGANA KWA MASLAHI YA TAIFA NA AMANI YETU...HILO LIKO WAZI...NA MWARABU AMA HATA MWAJEMI AWE SHIA AMA SUNNI NA MKABURU WAJUWE HILO...WASITULETEE MCHEZO KWENYE ARDHI YETU HATA SIKU MOJA!
 
...Hivi Bungeni kinajadiliwa nini vile?

ama kweli funika kombe mwanaharamu apite, hili 'spin' limehamisha macho na maskio ya watanzania walio wengi mpaka kinachojiri Bungeni kuhusu mustakbali mzima wa uendeshwaji serikali umefumbiwa macho, au ndio changa la macho?

Kufumba na kufumbua bajeti zinapita bila kokoro, hali ya Mwananchi ndio hivyo tena mungu n'saidie, kisa (?), ...wakati wao wanajadili sie tulikuwa tunatafuta mchawi Bungeni, na alomuua Wangwe. Wanasiasa wa Upinzani badala ya kung'ang'ania ujuaji wa nani jasusi, rudisheni attention ya mijadala ya kusaidia wananchi bungeni!

la sivyo ndio 'Changa la Macho'!
 
Field Marshall ES, Kitila

Nawapongeza kwa maneno mazito!

Muda unavyoenda naanza kubadili msimamo wangu kuhusu Kitila, nilipenda agombee uongozi CHADEMA kwa muda mrefu sana... lakini huyo bwana huenda akiwa kama mwanachama mtiifu tu wa CHADEMA, akawa mshauri anaweza kutumikia taifa vizuri zaidi kuliko akiwa ndani ya chama.

Nimeona maoni yake mara nyingi yananifanya niendelee kushikilia msimamo wangu kwamba kiongozi mzuri... huanza kuonekana mashuleni na kama kuna uongozi mzito hapa nchini ni kuongoza watu wote warefu... na hapa nina maanisha kuongoza jumuia kama ya University.
 
............swali lingine la kujiuliza ..JE HUYU DOGO NI TISS..au kitengo[upande wa chama]????.....aliwezaje kuwemo kwenye top delegation ya serikali ziarani swiss?????[ na hata mbunge juma kilimba amekiri walikuwa naye pamoja na kusema hamfahamu role yake kwemye ziara yao..anakiri alimsaidia pale mallya aliposahau passport ndani ya ndege zurich]..katika ziara hiyo kulikuwa na wabunge kadhaa na viongozi wa ccm....je tutasema huyu ni mtu wa kawaida????
 
kama Prof. Samwel Wangwe ni CCM na ni ndugu wa Marehemu haruhusiwi kuwa nao?Hoja za zitto ni nyepesi sana..Hili suala ni zito na inabidi zitto atulie na kutafuta hoja nzito

Ndugu wa marehemu kuwa na mali ya marehemu haimaanishi kuwa na chama fulani cha siasa kinaweza kumiliki.Hoja ya Zitto imeweza kuwa nyepesi kwa kuwa wewe umekuja na wazo jepesi,lakini kama ilivyowasilishwa bado ni nzito ukiondoa wepesi unaoulazimisha kwa maneno yako hapo juu
 
Duuuh!!! Mzee MKJJ Dunia ina wingi wa miujiza. Watu ni hodari na makini katika kazi zao lakini si wakamilifu, wameacha nyufa ambazo sasa zinapelea kuvunjika kwa ukuta. " You can only fool some people sometimes but NOT all the people all the times"
Haya yote yana mwisho wake. Sasa Mzee MKJJ nini kitafuatia?
 
Sioni sababu ya kukuza sana mambo, ati jasusi!

Huyu alikuwa mhangaikaji tu wamjini, akitafuta order za kusuply tona za photocopy, cabon paper, printing etc. akisikia tenda fulani hata waziri atamzoea tu ili apate connection.

Ukweli ile corolla ilikuwa mkangafu, uwezekano ilikuwa na tube zenye viraka vilivyozibwa kwa patex na engine kuchemsha ni mkubwa. Haiwezi tembea mchana toka dom hadi dar, magari ya mtindo huu hutembea usiku kwa usiku.

mh. aliwahi kuwa rastafarian siku za nyuma, hivyo uwezekano alikuwa mtu wa dope ni mkubwa, ndo maana washkaji zake nimajanki, kama walilipuliza ndo wakaanza safari? kama alipata balimi mbili na dope uwezekano wa mzinga ni mkubwa, hakuna aliyempima alcohol baada ya ajali.

Kama dogo angekuwa kamanda asingepiga kelele kuomba msaada, angetambaa kwani alitoka fiti, madereva wangapi wanapiga mzinga na kulala mbele.

Eddy umepima kweli unachosema kabla ya kukiweka hapa??
 
Na Kizitto Noya - Mwananchi

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Said Mwema, kumhoji Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, kuhusu kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alisema jana kuwa, chama chake kina wasiwasi na jinsi CCM ilivyopata waraka wa marehemu kuhusu mgogoro wake na Chadema na kuanza kuusambaza siku moja kabla ya kifo chake.

Alisema, Makamba anapaswa kuhojiwa ili aeleze uhusiano wake na marehemu ambaye alikuwa Mbunge Chadema, hata akapata nyaraka hizo za siri katika kipindi kifupi kabla ya kifo chake na kuzisambaza.

''Hatutaki kuhitimisha kwa sababu sisi ni wanademokrasia, ila tunataka IGP sambamba na maombi yangu ya awali ya kumhoji Mkurugenzi wa TBC1, amhoji Makamba ili tujue uhusiano wake na marehemu na jinsi alivyopata waraka huo na kuusambaza siku moja kabla ya kifo chake,'' alisema Kabwe na kuongeza:

''Waraka huo ulipotolewa kwa mara ya kwanza na TBC1, mimi (Kabwe) nilikuwa na mashaka na Jumamosi iliyopita, niliwasiliana na IGP na Mkuu wa Usalama wa Taifa kuwataka wamhoji Mkurugenzi wa taasisi hiyo ya umma. Lakini leo (jana) tumefumbuliwa macho kwamba waraka huo ulianzia CCM na ikabidi niwasiliane naye (IGP), tena ili zoezi hilo limguse pia Makamba,'' alisema.

Alisema Makamba anapaswa kueleza alikopata waraka huo na sababu za kutumwa kwake muda mfupi kabla ya kifo cha marehemu ikiwa ni pamoja na msukumo uliomfanya ausambaze kwa viongozi wa CCM.

Kwa mujibu wa Kabwe, sheria ya usalama wa taifa ya mwaka 1996 inatambua ndugu wa marehemu kuwa wamiliki wa mali na taarifa muhimu zinazomhusu marehemu, hivyo ni ajabu CCM kumiliki waraka huo wakati haina uhusiano wa kindugu wala kiitikadi na marehemu Wangwe.

''Hivi CCM ina uhusiano gani na mbunge wa Chadema au ndugu wa marehemu hata ikahalalisha kumiliki waraka huo na kuusambaza bila woga?'' alihoji Kabwe na kusisitiza kuwa Chadema haijauona waraka huo na wala kuambiwa na ndugu wa marehemu.

Akizungumzia suala hilo, Makamba alikanusha kuhusika na waraka huo na kueleza kuwa, CCM haina haja wala sababu ya kuwa nao na kuusambaza.

Alisema CCM haihusiki na waraka huo na kubainisha kuwa wanaofanya hivyo ni watu wanaomwunga mkono marehemu Wangwe katika migogoro yake na chama chake.

''Mimi sijauona waraka wenyewe na sina taarifa nao, lakini kwa nini CCM iusambaze, ina shida gani na Chadema?'' alihoji na kuongeza:

"Chadema sisi hatuiogopi, tuliishinda Jimbo la Kiteto na tutaishinda mwaka 2010, hatuna haja nayo wala haitusumbui."

Kauli za Makamba na Zitto zimefuatia taarifa kwamba, CCM imekuwa ikisambaza waraka wa marehemu Wangwe wenye kurasa sita unaoelezea jaribio la Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kutaka kumvua wadhifa wake na uanachama.

Waraka huo unadaiwa kusambazwa kwa viongozi wa CCM kwa lengo la kuwafahamisha mgogoro wa Chadema ambao umekuwa ukihusishwa na chanzo cha kifo cha mbunge huyo.

Ukurasa wa nne wa nakala ya waraka huo unaonyesha kwamba, kwa mara ya kwanza ulitumwa kutoka Dodoma Julai 27 mwaka huu majira ya saa 9:42 alasiri toka namba (026) 2322965 ambayo imeonyesha kusajili kwa jina la ‘KATIBU MKUU CCM DOM’ tarehe ambayo ni siku moja kabla ya kifo cha Wangwe.

Uchunguzi umebaini kuwa waraka huo ulianza kusambazwa kutoka Dar es Salaam kwa namba za faksi 2667457 iliyotanguliwa na kodi namba ya mkoa (022) ikimaanisha kutumwa kutoka Dar es Salaam Julai 31, mwaka huu saa 5:50 asubuhi na mmiliki wa namba hiyo akitambuliwa kama SIGMA ICT.

Waraka huo, umetumwa kwa baadhi ya viongozi wa CCM mikoani, wakiwemo Makatibu wa Mikoa na Wilaya na wengine ukiwa ni mahususi kwa ajili ya kuwaonyesha kwa kina mgogoro wa Chadema ulivyo.

''Kufuatia Uchaguzi Mkuu wa 2005, Mbowe alitufahamisha wanachama kuwa alikuwa anakidai chama dola za Kimarekani 181,949.00, sawa na Sh 218,338,546 na mpaka sasa chama kimemlipa Sh175 milioni.

''Baada ya kupata wadhifa wa Makamu Mwenyekiti na kwa kuzingatia takwimu zionekanazo hapo juu katika kulinganisha matumizi ya fedha wilayani na makao makuu, niliamua kumshauri Mbowe asitishe kujilipa deni kutokana na fedha za ruzuku, kwani siamini kuwa kulipa madeni yaliyopita kunaendana na utaratibu wa usimamizi wa pesa za ruzuku kwa vyama vya siasa kutoka serikali.

''Mbowe alichachamaa na ndipo nilipomshauri kuwa kama ni hivyo, basi atuthibitishie pesa hizo anazodai alikopesha chama ziliingia kwenye akaunti gani ya Chadema kupitia hundi ipi na lini?'' ilieleza sehemu ya waraka huo.
 
Nadhani Mh. Zitto au Dr. Slaa wanaweza kulitumia Bunge letu kushinikiza uchunguzi wa kina ufanyike kuhusu kifo hiki.
 
Haya mambo yalikua yanaonekana kama yanaisha..ila naanza kupata Picha kua bado kazi ipo...tutarajie mengi kuhusu hili
 
https://www.jamiiforums.com/member.php?u=2260

Maneno hayo uliyoyasema hapo juu...ESPECIALLY KWENYE RED HIGHLIGHT...YANAONYESHA KILA DALILI YA KUWA "MHAFIDHINA"
Yani mwenzako Zitto katumia muda woote kukuelewesha kuhusu mambo mazuri wenzako waliyoyafanya na wewe jibu lako ni fupi na la kijeuri kuwa eti vyama ni cuf na ccm tu...Na sasa unampa nani darasa la Msunni na Mshia?

Naona mzee umeenda kwenye archive!...

Kwa kusema hivyo sijamdharau Zitto, yeye kaleta opinion yake.. I brought up mine, except mine was short and clear thats it!...

Ndugu ukubali tu wewe ni mdini! hata hapo uliposema;

TUTAPIGANA KWA MASLAHI YA TAIFA NA AMANI YETU...HILO LIKO WAZI...NA MWARABU AMA HATA MWAJEMI AWE SHIA AMA SUNNI NA MKABURU WAJUWE HILO...WASITULETEE MCHEZO KWENYE ARDHI YETU HATA SIKU MOJA!

Sijui point unataka kuleta hapa!

Kutaja CCM na CUF tu! haina maana nimeidharau CHADEMA!....

Na hiyo sio mada ya hapa!
 
Swali jingine pia ni hili...Ni watu wangapi zaidi ya Spika waliojuwa kuwa keshakabidhi hoja?
Maana nafikiri alimwuliza makamu spika na makamu spika akamwambia amsubiri spika six ili aweze kuikabidhi hoja yake hiyo...Sasa sijui sana kuhusu taratibu za hapo bungeni..Je kuna uwezekano wa kuvujishwa kwa habari ya yeye kumkabidhi spika hoja yake ama lilikuwa ni jambo la wazi lenye kujulikana na kila mbunge kuwa imeshakabidhiwa?
Je habari kwamba hoja imeshakabidhiwa ilitoka kabla ya kifo ama baada ya kifo?

Wangwe alitafutwa siku ile jioni ili awasilishe hoja yake lakini hakuonekana (alikuwa ameshaanza safari ya dar). Kwa maana hiyo, kwa mujibu wa kanuni za Bunge, alishawasilisha hoja yake kwa Spika (Ofisi) kwa sababu hakuna mtu anaruhusiwa kuwasilisha hoja Bungeni kabla haijapitiwa na Spika (Ofisi).
kwa hiyo, hadi anafariki, nakala ya hoja hiyo ilikuwa katika ofisi ya Spika.
Sina hakika iwapo alimkabidhi mtu mwingine yeyote hoja hiyo zaidi ya Spika kwa sababu hata kiongozi wa Upinzani Bungeni, na viongozi wa chama chake, hawajasema kama walipatiwa nakala ya hoja hiyo.
Ilipotangazwa kuwa wangwe anatafutwa ili awasilishe hoja yake, wabunge wote walifahamu kuwa imeshakabidhiwa
 
Kunguru maneno haya ni MAZITO...Ila usisahau kuwa UKABILA NA CHUKI DHIDI YA KABILA JINGINE...Chuki ya namna moja ama nyingine inaweza kutupeleka pabaya!
Kila kabila lina watu wasio wazuri bila kujali tofauti za kabila hizo...Kuna watu prejudice na watu wazalendo...WABANTU HALISI WALIOPATA ELIMU YA UASILIA WAO WA AFRIKA!
Ambao hawana mabwana waarabu wala wazungu...Bali wenye kujali UTU,UBINADAMU NA HESHMA YA MWAFRIKA..WENYE KUJALI MAENDELEO YA BINADAMU KWA KUSHIRIKIANA NA BINADAMU WENZAKE BILA KUJALI UTOFAUTI WA RANGI,DINI WALA KABILA....HAO NI "THE CITIZENS OF THE WORLD!"

Mkuu JMushi,

Nakubaliana na maneno yako.

Pia nataka nimalizie kwa kusema kwamba, hao watu wazalendo uliowaongelea ni wachache sana tanzania. Mfano mzuri wa wazalendo hao ni Marehemu Nyerere na Wangwe.

Kuna pia aina nyingine ya 'wazalendo' ambao tatizo lao kubwa ni kwamba, ukiwachunguza vizuri utauona huo uzalendo wao ni wa kinafiki , na wana ajenda zao za siri ambazo zaweza kuwa ni ama tamaa ya utajiri wa kifisadi au ukabila uliowazi au uliojificha na usiowasaidia watanzania walio wengi. Uzalendo wa aina hii ya pili inafaa upigwe vita na kila mtu hapa JF bila kujali tofauti zetu za kiitikadi au uzawa wa kimikoa, kimajimbo au kikabila!
 
kwa upande wangu mm sioni ulazima wa ishu hiyo kwani pande zote mbili zimekiri kwamba ni ajali ya kawaidia kwahiyo hata iweje haiwezi kubadilisha ukweli wa mwanzo ili hali wao wenyewe familia wamekwisha tuthibitishia hivyo!!!

itakayo baki ni historia tu na ushindi kwa wale waliokusudia hilo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom