Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Mazishi yanaendelea hivi sasa, ila kuna jipya linaanza kuzuka tena ,baada ya ripoti kutoka sasa narudisha majeshi eneo la tukio na nitawapa kinachojiri huko.



Mkuu wangu Kiranja.
tunaomba utu-update kila mara ili tupate pure information kabla hazijapita kwa mafisadi
 
Ama kweli JF kuna wengi!! Kama magazeti yalivyonunuliwa na kuwekwa habari zinazomfurahisha RA hata hapa kuna wenye wajibu wa kumburudisha RA.
Haya endeleeni na kazi yenu kwa kuangalia mnamteteaje mtanzania.

Mungu Ndiye muweza wa yote.Hata kama mashujaa wa taifa hili watauwawa hawataweza kuzuia mageuzi yajayo.

I salute to the revolutionary movements!
 
kiranja



Duh!!!!! ............. kweli wewe ni kiboko. Hii hata wazee wa propaganda, akina Kingunge na wenzake hawaoni ndani. Hiki ni kizazi cha dot com!!! lol!
 
wewe mkuu,acha kulalamika.Tatizo ni watu ambao hawataki kufikiri nje ya box na kuhusisha kifo chake na CHADEMA tu.Lazima tufikirie mbali zaidi ya hapo ili kuwe na justice otherwise kwa nini mtu usifikirie CCM walikua na maslahi zaidi kwenye hilo suala? Maanake walishaapa kuisambaratisha CHADEMA

Ben nakutaka radhi. Sikuwa nimekuangalia sawa sawa. Sasa nakupata!!!

Hoja ya upembuzi deeper ni muhimu kuliko inavtyopewa nafasi na discussants hapa jukwaani. Lazima tuunganishe vita za Chacha Wangwe kwenye madini, na kifo chake. Mafisadi wanafanya kila bidii kujificha kwenye mgogoro wa Chacha na Chadema.

Weweeeeeeee!!!

Hatudanganyiki kirahisi tena.
 
Naomba muhtasari wa yote yalioandikwa hadi hapa tulipofikia maana kama si peke yangu basi kuna na wengine tumeachwa njiani.
 
Nyie mnaosema VYOMBO VYA HABARI kwani JAMII FORUMS NI NINI?

Serikali na chadema vina nguvu kubwa hapa...Na ndio maana nasema ni UNAFIKI kama kuna mtu mwenye INFLUENCE YA CHADEMA HAPA Jamvini akidai kuwa anasikitishwa na kifo cha Wangwe....

Taarifa mlizokuwa mkileta hapa na Mgagagigikoko ambaye ni lazima anaweza kuwa RA ama mtu wake...Lakini akawa anampigia kifua marehemu hapa na sapoti ya credible Members wengine kuwa kuna UKABILA chadema ilipekea sisi kuwa na wakati mgumu kuujuwa ukweli.

Kutaka kusema kuwa ccm na chadema hawahusiki na sawa na kusema ccm na chadema hawahusiki kwenye EPA.

Nilisema EPA iwe ya kwanza kufuatiliwa...!

Nimekuja kugunduwa kuwa mimi na marehemu tulikuwa tukiona eye to eye...Ila manipulation za news na kina RA na ccm kuwa na nguvu hapa kwa kupitia huyo anayejiita SILENCER!

Kwa wale waliokuwa wakisema kuwa chadema walinisikiliza na kumpiga risasi Wangwe..Je kwanini hawasemi kuwa ni serikali ilinisikiliza kama nia si kuleta UKABILA?

Niliweka wazi kuwa chadema wamsikilize marehemu kama ni wa kweli!
Na kama tukitaka kupata ukweli hapa ndani...Basi tumuunge mkono KIRANJA..Mimi niko nje lakini nimeona kuna watu hawachoki kutaka kunihusisha mimi na mauwaji haya...!

Na kwa jinsi mambo yalivyo..Nina mashaka makubwa sana...NA MIMI NILISHASEMA WAZI...HAKUNA HAJA A KUWAULUMU SERIKALI WALA ccm KWANI INAWEZEKANA TUKIBADILISHA VIONGOZI NI SAWA NA KUONDOWA DIKTETA MMOJA NA KUWEKA MWINGINE!

Wangwe ni RASTAFARIAN....NA mimi naweka DREADS KUM HONOR...Pia nawaomba msikilize ALBAM ya Bob Marley ile yenye Afrika Unite,Survival,War,Zimbabwe..nk.

Na pia msikilize ile nyiombo a Bob ya RUNNING AWAY...Hii nyiombo imenifanya nitowe posting hii kwasababu inasema YOU CAN RUN AWAY BUT YOU CAN'T RUN AWAY FROM YOURSELF!

Hata kama ni kweli siasa hizi ni HATARI..LAKINI KUYAFUMBIA MACHO MAMBO MENGINE NI SAWA NA KUIKIMBIA NAFSI YAKO KAMA WEWE NI MWANAMAPINDUZI!

Na tumia FURSA HII KUSEMA KUWA WACHAGGA WASIINGIZWE WOTE KWENYE SAKATA HILO KWANI SI WACHAGGA WOTE WALIOHUSIKA NA EPA!

Pia nimeshatowa kauli ya Mnyika na yeye ili aweze kunijibu ni kivipi wakibosho waonekane ni wasaliti halafu muuwaji ama huyo Deus awe ametokea KIBOSHO.

Na kwasababu mlinifungia hapa kwaajili ya kauli isiyo na uzito wa kunifungia..Na huku hii forum ikisemekana ni ya wachagga...Basi hii ni questionable kwasababu kauli ya Mnyika pia kuhusu usaliti wa wakibosho..Halafu msaliti aliyekuwa kwenye ajali ya utata wa marehemu kuwa ni mkibosho...Huku mwenyekiti aliyekuwa na ugomvi naye ni mmachame...NI KIZUNGU ZUNGU KWANGU NA WACHAGGA WOTE CHADEMA WAHAME KAMA MABADILIKO HAYAFANYWI...Kama kweli RASTA ALIKUWA MKWELI KIASI HIKI BASI HAKI IPATIKANE!

Kama chadema hawawapendi wakibosho ni kwa vipi wakibosho waingizwe kwenye ukabila?

Mbona Mrema alitowa kauli kuwa NG'OMBE WA MASIKINI HAZAI KAMA KWELI WANGWE NI MSALITI!

Viongozi wengine wa chadema pia nawaonea huruma kwani mko kwenye wakati mgumu sana...ILA SASA WA KUSKILIZWA NI MREMA.
 
mwimba umeongea........hebu tupeni summary....
manake some of the dots are overlapping and some are too far apart!
 
jmushi nilifikiri utakuwa umekoma kukurupuka na maneno ya vitisho ndugu yangu....kumbe ndo kwanza mkoko!
 
Ama kweli JF kuna wengi!! Kama magazeti yalivyonunuliwa na kuwekwa habari zinazomfurahisha RA hata hapa kuna wenye wajibu wa kumburudisha RA.
Haya endeleeni na kazi yenu kwa kuangalia mnamteteaje mtanzania.

Acheni unafiki, mlisema Wangwe ni mzigo kwenu na anastahili kuuawa kwa kupigwa risasi, iweje leo mnachukulia kifo chake kama mtaji wenu wa kisiasa huku nyoyo zenu zikighubikwa na furaha ya kufa kwake? Unaweza ku-twist kadri unavyotaka kwa kuchanganya majina ya watu unaowachukia ili mradi tu mko ndani ya sherehe.
 
punda milia,
hivi alosemwa wangwe apigwe risasi anacheo gani ndani ya chedema?
 
Kinto,
Tatizo lingine ambalo lipo hapa JF ni kwamba mtu mmoja anakuwa na ID nyingi tofauti ambazo huzitumia kwa malengo machafu yaani kupotosha ukweli wa mambo halisi. Kwa mfano, inaonekana ni sawasawa kuhusisha kifo cha Wangwe na kundi lolote lile lakini usidiriki kuhusisha CHADEMA au Mwenyekiti wake (nadhani umekwishapitia postings humu). Hawa watu ni wanafiki wa hali ya juu wanachokifanya hapa kwanza hawamtendei haki marehemu kwa vile walimkana na kumtakia afe. Pili, mijadala yote hii wanayoendeleza ni ya kujipongeza kwa kifo cha Wangwe, hakika wako na furaha isiyo kifani, nadhani hata wale waliokwenda Tarime nahisi ni kwenda kuhakikisha wanauona msumari wa mwisho ukigongwa katika jeneza la Wangwe. Hebu tujiulize, katika hali ya kawaida Mbowe, ana majonzi ya kweli kwa kifo cha hasimu wake ambaye alikuwa ameshamtahadharisha kumng'oa katika nafasi ya uenyekiti?
Acheni unafiki!

Punda
Na mbaya zaidi inafanyika humu kwa watu ambao karibu wote wana atleat shahada zao.

wana copy mbinu inayotumiwa na wahasimu wao,wakati wahasimu wao ,wao ni wajanja propaganda zao wanazipeleke vijini kwa wtz wengi ambao kwa bahati mbaya hawakupita shule zaidi ya miaka saba ,huko ndiko akina chenge wanaibuka kidedea, hata pale jangwani pia wanaibuka videdea .Na hiyo ndio tofauti yao kubwa.

Lakini ukijaribu kuleta propaganda za kinafiki kwenye mi forums humo kumesheni wajuzi ambao kwa propaganda zinazopigiwa paragumu na parapanda ndio unaona wajuzi ambao wangekuunga mkono wanapeperuka kivyao. na kujisemea kimya kimya ALA!!! kumbe jogoo la kuku ni lile lile ila limepakwa rangi kichwani tu.

Unafiki ni kitu kibaya sana na ule unafiki wakupendelea mwenzako achunguzwe lakini wewe hapana na usafi unajipa mwenyewe inakua ni unafiki wa hatari.

Hata enzi zile shule ya msingi mwezako alikua akikutuhumu umwemwibia kalamu ama daftari wote mnakwenda kwa mwalimu na mwalimu ndiye anafanya uchunguzi huru kubaini je ni kweli ama unamsinginzia .

Lakini hawa wenzetu wanadhani sijui nini Tuhuma ikielekea CHADEMA sio kweli na anayeleta maada hiyo ni fisadi ama ametumwa.

Lakini ikielekea kwingine mfano CCM ama Mtikila utasikia wanajipa THX nyingi harafu wasema ni kweli huyo ni fisadi inabidi achunguzwe.Hapa inakua vipi?

RIP CHACHA kafariki na kama uchunguzi ukifanyika lazima maeneo yote mhimu yafanyiwe ili ukweli ujulikane.
 
Jambo kubwa na ambalo ningetaka wenzangu humu mulijadili kwa kina na kuangalia kinachoendelea ni kuwa ukisoma magazeti yote ya leo isipokuwa Tanzania daima na Mwananchi ambayo yaliripoti taarifa hiyo utaona ya kuwa mwandishi wa habari hiyo alikuwa ni mtu mmoja.

Ukianza kusoma Nipashe,majira,mtanzania,kulikoni,uhuru na habari leo utaona hiki ninachosema ,kwani kuna paragrafu tatu zinafanana kila sentensi na ni zile zinazohusiana na Mbowe jinsi alivyowasili Kemakorere.


Wahariri wa magazeti kadhaa (Nipashe, Majira, Mtanzania, Uhuru, kulikoni) wameruhusu magazeti yao kutumika kuudanganya umma wa watanzania. Wamefanya hivyo kwa kuchapisha habari moja (inayosadikiwa kuandikwa na mtu mmoja) kwa kutumia majina ya watu tofauti. Hii inafanya habari ambayo watanzania walidhani imeandikwa na watu tofauti wa vyombo tofauti vya habari, kuwa udangayifu mkubwa na upotoshaji wa makusudi.

Habari hiyo inahusu kufanyiwa vurugu haswa kwa Mheshimiwa Mbowe wa CHADEMA na wakazi wa Tarime wakati shughuli za msiba wa Mheshimiwa Marehemu Chacha Wangwe. Habari hio iko chini ya vichwa vya habari vilivyotofautiana kidogo na kuuonyesha waandishi tofauti katika kila gazeti waliohusika kuiandika. Lakini ukweli ni kwamba habari hiyo imeandikwa na mtu mmoja na kubadilishwa kidogo sana. Kubwa ni kwamba kwenye baadhi ya vipengele ukiacha mtiririko wa maneno kulandana kabisa, hata mahali ambapo alama za mkato na nukta zimewekwa vinafanana kabisa. Pili habari zote hizo zimelikosea jina la Mheshimiwa Mbatia wa NCCR-Mageuzi, katika sehemu mmoja inayofanana.

Swali kubwa la kujiuliza ni kwa nini habari hii ambayo kwa uhakika imeandikwa na mtu mmoja, imeripotiwa katika magazeti haya kwa majina ya waandishi tofauti? Je huku sio kuwadanganya watanzania? Tena kwa makusudi kabisa? Kuna hisia pia majina ya waandishi hao sio ya kweli(kwamba hakuna watu kama hao). Je nini kilichowasukuma wahariri wa magazeti haya kufikia hatua hii mbaya na yakusikitisha?

Swala hapa sio kubisha vurugu zimetokea au la? Hilo litaonyeshwa kwenye sehemu yake na labda wakati mwingine. Hapa swala la msingi ni wahariri kwa kujua au kwa kutokujua kuudangaya umma wa watanzania, kuhusu chanzo cha habari hii. Na hivyo kwa kiasi kikubwa kuwanyima watanzania haki yao yakupata habari sahihi na za kuaminika. Wakati msomaji alitakiwa kusoma habari nne tofauti ili kupata mwanga wa yaliyotokea huko Tarime anajikuta anasoma habari mmoja chini ya vichwa vya habari tofauti kidogo tu na majina ya kutunga ya waandishi. Je huku sio kuupotosha umma wa watanzania na kuunyima haki yake ya msingi?

Wahariri wa vyombo hivi vya habari wanawajibu wakuwaelezea watanzania nani haswa anahusika na uandishi wa habari hii? Pili kwa madhumuni gani majina ya waandishi yalibadilishwa? Tatu, nani aliyeshinikiza ichapishwe? Na Nne inabidi waombe radhi kwa watanzania wote, haswa kwa wakazi wa Tarime ambao wanaonyeshwa katika habari hii kwamba ni wapenda vurugu, na wasio na ustaarabu hata kidogo hata katika wakati huu wa Msiba.
 
mwimba umeongea........hebu tupeni summary....
manake some of the dots are overlapping and some are too far apart!

Mwiba ndio lenyewe ,naona umebambikiza, sawa ni shauku ya kutaka kujuwa palipofikiwa,kuhusu mauaji ambayo yanaonekana kuelekea kwenye mystery.maana nashindwa kuunganisha baada ya mambo mengi kuunganishwa na hadi sasa sijaona kama ripoti imetoka .Je dakitari ameruhusiwa au ndio wametumia wa madakitari madeinhumhum.
 
jamani wana JF nimepitia kona zote juu ya hii ishu lkn bado nina pata wasi wasi

mbona cjaona post yoyote iliyotoka kwa JMUSHI au ndio niamini kwamba DEUS MALLYA ni JMUSHI?
 
sra nenda posti ya 1467 utamkuta mushi kaandika......
mushi ni kijana mdogo ambae alipayukwa tu .....sio kwa kukusudia.
 
The very latest: Hizi nimezipata kwa wadau waliopo Dar na Tarime muda mfupi uliopita, naripoti kama zilivyo, kila mtu achambue mchele na pumba:

  1. Post Morterm imefanyika. matokeo: hakuna risasi wala kitu kingine, bali ni ajali iliyomuua Wangwe.
  2. Marehemu ameshazikwa.
  3. Mbowe hakufanyiwa fujo yoyote. Kilichofanyika, Rostam na akina Balile na George Marato, wameandaa stori kwa malengo ya kisiasa.
  4. Kesho Jukwaa la Wahariri linakaa kufanya uchambuzi wa kitaalamu wa stori hiyo (ambayo ilisambazwa vyombo vya habari kadhaa); na watatoa tamko kali dhidi ya ufisadi uliofanyika.
  5. Kuna wazalendo walienda kamera za video kwenye msiba.. Picha zinaonyesha halihalisi ya matukio yote. Zitatumika katika kueleza umma kilichotokea.
  6. Tunaambiwa mkakati uliokuwepo ni kama ule uliotumika na utakaoendelea kutumika kummaliza Sumaye na Malecela kisiasa
    [
 
jamani wana JF nimepitia kona zote juu ya hii ishu lkn bado nina pata wasi wasi

mbona cjaona post yoyote iliyotoka kwa JMUSHI au ndio niamini kwamba DEUS MALLYA ni JMUSHI?

Acha ushabiki jmushi si huyo post 1467?
 
Kama hizo habari mnaweza kuziweka hapa tukaziona kwani wengine hatuna njia ya kupata magazeti yote na kuanza kupitia mstari kwa mstari,nahisi itakuwa vizuri sana kuweka vipande hivyo na gazeti lililochapisha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom