Kinto,
Tatizo lingine ambalo lipo hapa JF ni kwamba mtu mmoja anakuwa na ID nyingi tofauti ambazo huzitumia kwa malengo machafu yaani kupotosha ukweli wa mambo halisi. Kwa mfano, inaonekana ni sawasawa kuhusisha kifo cha Wangwe na kundi lolote lile lakini usidiriki kuhusisha CHADEMA au Mwenyekiti wake (nadhani umekwishapitia postings humu). Hawa watu ni wanafiki wa hali ya juu wanachokifanya hapa kwanza hawamtendei haki marehemu kwa vile walimkana na kumtakia afe. Pili, mijadala yote hii wanayoendeleza ni ya kujipongeza kwa kifo cha Wangwe, hakika wako na furaha isiyo kifani, nadhani hata wale waliokwenda Tarime nahisi ni kwenda kuhakikisha wanauona msumari wa mwisho ukigongwa katika jeneza la Wangwe. Hebu tujiulize, katika hali ya kawaida Mbowe, ana majonzi ya kweli kwa kifo cha hasimu wake ambaye alikuwa ameshamtahadharisha kumng'oa katika nafasi ya uenyekiti?
Acheni unafiki!