Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Hivi kama huyo kijana angekufa kwenye hiyo ajali pia; tungekuwa na maswali?
jamani.... kuna neno wanasema "to err in the side of caution". Wasipofanya au kuhurusu uchunguzi huru watakuwa wanachochea hisia zote hasi ambazo zimekuwa zikienea. Ukifiria sana utaona kuwa yawezekana ilikuwa ni ajali ya kawaida na kosa kubwa ni la kijana Malya kusema kuwa yeye hakuwa dereva na baadaye kukiri alikuwa dereva; hilo ndilo lililochanganya watu sana. Yawezekana kama walivyosema wengine hana leseni n.k
So yawezekana kuwa ni kifo cha kawaida kabisa kama Katibu Tarafa anavyosema, lakini jinsi mambo yalivyokwenda na yanavyoshughulikia yanafanya kifo hiki kisiwe cha kawaida na hivyo kulazimu uchunguzi huru ili kuwahakikishia wananchi kuwa ni kifo cha kawaida kabisa na ni ajali tu.
Kuna ubaya gani kati hilo Katibu Tarafa?
nadhani sasa is getting out of hand; tusubiri uchunguzi kama utafanyika. kwa sababu kama nilivyosema kwenye clue ya pili; gari. Sasa hivi mimi ningekuwa niko interested kuona nani analiangalia gari na kama limesafishwa n.k sasa hivi hilo gari lilitakiwa lisiguswe wala kufanyiwa nini hadi uamuzi utakapotolewa kama kuna inquiry. kwa sababu kama bunduki n.k ushahidi uko kwenye gari zaidi. Kwa sababu mtu anaweza kuangalia majeraha aliyo sustain Wangwe na kuangalia ndani ya gari ni kitu gani kimesababisha. So, ningeuliza where is the car?
Wanapoteza Muda Mwisho Watazika Tu Hao Wanasubiri Tu!!!wagawane Mali Kabla Ya Kuzikwa!!!wamefanyiwa Sokoine Ije Kakayangu Wangwe Wapi Iliishia
R.i.p Wangwe
Tafadhalini Naombeni Mpumnzisheni Braza Wetu Msijejiundia Tume Kula Ulaji Kwa Jina La Marehemu
Ulale Pema Peponi
Kusema alikua haendeshi harafu baada e kukili hilo sio kosa la kutia wasiwasi ,hata juzi tu jamaa yangu kafa ila driver aligonga mti upande wake akafa palepale yule aliyekua anaendesha akasema yule aliyekufa ndiye alikua anaendesha harafu akili ilipomkaa sawa akabadili usemi akasema yeye ndiye alikua mshika usukani.
Hiyo siyo hoja kabisa hoja hapa ni Je Chacha kafa kwa ajali ya gari ama Lah na kama ndiyo nani kahusika.
Ktk nyanja za ufundi kunapotokea tatizo fundi mara nyingi hukimbilia maeneo ambayo huleta tabu mara kwa mara ili afanye Troubleshooting.
Na unapomtafuta nyoka aliyeingia chini ya uvungu wako ukiwa umeshikilia tochi lazima uanzie miguuni mwako kupiga tochi na ukienda mbali sawia na mkabala zaidi.
Eneo la toableshooting ambalo tunaweza Anzia ni wale wote ambao CHACHA amekorogana nao kwa siku hizi za usoni.
Na miguuni kwa RIP Chacha pa kuanzia kupiga tochi kumsaka nyoka aliye uvunguni ni CHADEMA.
How old was he? What was his profile?
Getting out of hand? It's beyond that my friend. No one in Tanzania can die without controversy......
Mi nadhani kuna watu humu wanakatabia kaku-sensationalize mambo....
Tenda haki. Kama unaweza kusema tuanzie Chadema, ndio unatuambia uchunguzi ufanyike, ili kama ni Chadema, CCM ijulikane. Lakini kumbuka Chadema, CCM, Polisi, Usalama, JWTZ kama taasisi haziwezi kuua, wanaoweza kuua ni watu ndani ya taasisi hizo. Tumewahi kusikia polisi, wanajeshi wakihusika na uhalifu, juzi mwanajeshi kaua mkewe, halafu tumesikia wanajeshi wamekamatwa na mitambo ya gongo, tukasikia, kiongozi wa CCM kakutwa na nyara za serikali, tukasikia wabunge wa CUF wamefoji document kusafirisha vimada, tukasikia kuna viongozi wa Chadema ni majambazi, huko Tarime kuna wana Chadema ni wahalifu. Uhalifu upo sehemu yoyote hata humu JF kuna wahalifu na watu wanaolipwa kuandika tofauti na wengine wanaoandika kwa kuwa ni sehemu ya "kiburudisho" cha maisha yao. Tusibadili muelekeo, TUTALAANIWA. Ingekua Waislamu, angekwisha kuwa amezikwa pale pale Dodoma juzi Jumanne, tena baada ya adhuhuri. KWa sisi kuchelewa kuzika na kunyanyasa maiti ni jambo la kawaida haswa sisi watu wa bara
NN.. there is nothing more sensational than death; kwani Marilyn Monroe ilikuawaje? JF ilikuwaje, MLK Jr ilikuwaje, it is by very nature sensational.
.....
Eneo la toableshooting ambalo tunaweza Anzia ni wale wote ambao CHACHA amekorogana nao kwa siku hizi za usoni.
Tarime palikuwa na mpango uliopangwa tangia jana kuwa watu wa CHADEMA na haswa Mbowe wazomewe na kujenga image kuwa wanahusika na msiba huo na hilo lingeondoa mpango wao wa kutaka ifanyike independent investigation.
Leo asubuhi walipofika huko wakina Mbowe pamoja na viongozi wengine wa vyama vya upinzani wakapokelewa na hakukuwa na hicho walichopanga, sasa kuna juhudi zinafanywa kwa kumshirikisha RPC atoe statement kuwa wamemnusuru Mbowe kuuwawa ,sasa sijajua kama ataitoa wapi ila najua kuwa kuna waandishi wameitwa kwa ajili ya kupata hiyo statement japo kwa umakini mkubwa.
Vyombo vya habari vimechaguliwa mahususi kuwa ni vyombo gani vihusike kupata hiyo statement.
Mtindo huu wa kutaka kutwist mambo huko yanaweza kuiingiza nchi kwenye matatizo makubwa sana ambayo wanaopanga ,na haswa waliokaa nyumbani kwa waziri mmoja wa serikali mjini Dodoma na kuandaa mpango huo mahususi eti kwa vile Mbowe alimshinda Kikwete kura huko Tarime utakuwa na matatizo kwao binafsi.
Vijana waliokuwa wamendaliwa wamesema kuwa wataweka mambo hadharani na kusema mpango huo na haswa baada ya kuona utata wa kifo hiki.
Nawatakia kila la kheri.