Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Taarime naijua vizuri
Hakuna mwingine zaidi ya hao atayenufaika na kifo cha CHACHA ,Labda uniambie kama kuna mtu mwingine anataka kuchukua Ubunge wa TAARIME.

Taarime hua wanaamua kumweka mtu wanayemtaka na ndio maana ni halimashauri hiyo tu ambayo CHADEMA inaongoza na kwanini isiwe DODOMA, DAR, Shinyaga,Kigoma,Karatu ,singida ama Moshi?

Ni kwasababu watu wa taarime wameamka na wanatambua nini wanachotakiwa kufanya .Ni bahati ya CHADEMA baada ya RIP chacha kuingia chadema watu waliowapenda nao walienda chadema.

Hivyo nakuambia watu wa Taarime bado wataleta mtu mwingine kama CHACHA ama zaidi,maana wao wanamleta wampendaye hivyo kama kuna mtu anategemea uhauheni ktk hilo amekosea na bahati nzuri kila mmoja analitambua hilo vyema.
Ndio maana % ktk hilo yani mtu aliona kumutosa CHACHA ndio suluhu nalipa 0.1%.

Miguuni kwa CHACHA kulikua CHADEMA lazima tochi hilo lipigwe kuanzia hapo no way out.

Kwa kuanzia tu, jina la record la wilaya yetu ni Tarime na sio Taarime. Wewe unaongelea Tarime ipi?
 
Kuna kitu ambacho huyu kijana alimwambia Chacha;

a. Kitu ambacho kilimfanya Wangwe akubali kumkaribisha nyumbani kwake kwa siku chache alizokuwa dodoma;
b. Kitu ambacho kilimfanya Chacha amuamini
c. Kitu ambacho kilimfanya Chacha akubali kurudi naye kutoka Dodoma; Chacha alikuwa anaenda msibani, Mallya alikuwa anarudi Dar kufanya nini?
d. Kama kuna mtu mwingine aliongezeka mbele ya safari, instincts zinaniambia aidha alikuwa anakubalika na Wangwe, Malya au wote wawili.
e. Aliyekuwa boardguard wake wa kawaida na ambaye amekuwa akisafiri naye mara kwa mara yuko wapi na kwanini hakuweza kwenda nao siku hiyo?

Hivi kumbe wabunge wa TZ wana ma-boardguards!!!!!!
 
mungu ni mkubwa ukweli utajulikana maan penye ukweli uongo hujitenga.
 
Chadema hao hao walisema kuwa Wangwe ni mzigo ndani ya chama ina maaana alikuwa LIABILITY hakuwa ASSET, walikuwa wanatafuta timing ya kuutua mzigo kauli hizo zimetolewa na waandamizi wa Chadema.

kuna mtu maarufu chadema alisema kuwa Chadema sio kama ccm inayolea mafisadi ndio maana wamemnyanganya umakamu mwenyekiti akamalizia kwa kusema ni maamuzi mazito ambayo ni unpopular kwa manufaa ya Chadema.

Mwenyekiti wa Chadema Taifa alisema hayuko tayari kufanya kazi na Wangwe,kama ni mtu muhimu ndani ya Chama na mbunge anayethaminiwa,mbowe asingesema hayo,
sawa na JK aseme kuwa siko tayari kufanya kazi na ANNA KILANGO halafu utokee msiba wa KILLANGO waje wana CCM na kusema Kilango kahujumiwa na CUF, nadhani polisi wangeanza kufutilia kauli hizi za ajabu ajabu toka kwa waandamizi wa Chadema.
Chacha Wangwe alitangaza vita na wahafidhina wa Chadema na kuahidi kuwa atashinda uenyekiti wa Chadema Taifa na kufuta ukabila na udini ambayo ni kansa mbovu ndani ya Chadema,
alisema na kukwambia Mwanakijiji kuwa HADI DEREVA MAKAO MAKUU YA CHADEMA ni mchagga na mama KOMU kila kukicha anazaa watoto wachagga,

unafikiri kama Mbowe alisema hayuko tayari kufanya kazi na Mbowe na kumzushia kuwa anakigawa chama na anauza siri kwa CCM, nadhani wa kushikwa uchawi kwa kifo cha Wangwe ni yule mwenye siri zake ambaye hataki CCM wasijue, kwa CCM walimuhitaji sana ili wajue siri za Chadema na Mbowe alikuwa na hofu kubwa siri yake isitoke nje.
Mbowe kumtumia Mnyika kuandika barua haraka haraka kwa IGP haisaidii kuwazuga polisi wasifanye kazi yao kitalaam na kuvifuatilia vyanzo vilivyo MMBOWESHA mpiganaji Wangwe.

Haya yako ni habari iliyopita, wamejaribu TBC wameshindwa. Watu wa Tarime hawana mawazo finyu kama haya. Yanayoongelewa Tarime sasa hivi sio kabila la mtu bali maelezo ya utata kuhusu kifo cha Wangwe.

Ona aibu ndugu yangu. Kuleta mambo ya kikabila kwenye msiba huu ni upuuzi na kitu kinachoangaliwa kwa uchungu na masikitiko makubwa sana toka kwa wakazi wa Tarime kama mimi.
 
taarime Naijua Vizuri
Hakuna Mwingine Zaidi Ya Hao Atayenufaika Na Kifo Cha Chacha ,labda Uniambie Kama Kuna Mtu Mwingine Anataka Kuchukua Ubunge Wa Taarime.

Taarime Hua Wanaamua Kumweka Mtu Wanayemtaka Na Ndio Maana Ni Halimashauri Hiyo Tu Ambayo Chadema Inaongoza Na Kwanini Isiwe Dodoma, Dar, Shinyaga,kigoma,karatu ,singida Ama Moshi?

Ni Kwasababu Watu Wa Taarime Wameamka Na Wanatambua Nini Wanachotakiwa Kufanya .ni Bahati Ya Chadema Baada Ya Rip Chacha Kuingia Chadema Watu Waliowapenda Nao Walienda Chadema.

Hivyo Nakuambia Watu Wa Taarime Bado Wataleta Mtu Mwingine Kama Chacha Ama Zaidi,maana Wao Wanamleta Wampendaye Hivyo Kama Kuna Mtu Anategemea Uhauheni Ktk Hilo Amekosea Na Bahati Nzuri Kila Mmoja Analitambua Hilo Vyema.
Ndio Maana % Ktk Hilo Yani Mtu Aliona Kumutosa Chacha Ndio Suluhu Nalipa 0.1%.

Miguuni Kwa Chacha Kulikua Chadema Lazima Tochi Hilo Lipigwe Kuanzia Hapo No Way Out.

Mbowe Alisema Hayuko Tayari Kufanya Kazi Na Wangwe Anayevujisha Siri Za Chadema. Walijaribu Kumnyamazisha Kidemokrasia Wakashindwa, Sasa Wameenda South Africa Kumtafutia Sangoma La Kumuondoa.
 
Chadema hao hao walisema kuwa Wangwe ni mzigo ndani ya chama ina maaana alikuwa LIABILITY hakuwa ASSET, walikuwa wanatafuta timing ya kuutua mzigo kauli hizo zimetolewa na waandamizi wa Chadema.

kuna mtu maarufu chadema alisema kuwa Chadema sio kama ccm inayolea mafisadi ndio maana wamemnyanganya umakamu mwenyekiti akamalizia kwa kusema ni maamuzi mazito ambayo ni unpopular kwa manufaa ya Chadema.

Mwenyekiti wa Chadema Taifa alisema hayuko tayari kufanya kazi na Wangwe,kama ni mtu muhimu ndani ya Chama na mbunge anayethaminiwa,mbowe asingesema hayo,
sawa na JK aseme kuwa siko tayari kufanya kazi na ANNA KILANGO halafu utokee msiba wa KILLANGO waje wana CCM na kusema Kilango kahujumiwa na CUF, nadhani polisi wangeanza kufutilia kauli hizi za ajabu ajabu toka kwa waandamizi wa Chadema.
Chacha Wangwe alitangaza vita na wahafidhina wa Chadema na kuahidi kuwa atashinda uenyekiti wa Chadema Taifa na kufuta ukabila na udini ambayo ni kansa mbovu ndani ya Chadema,
alisema na kukwambia Mwanakijiji kuwa HADI DEREVA MAKAO MAKUU YA CHADEMA ni mchagga na mama KOMU kila kukicha anazaa watoto wachagga,

unafikiri kama Mbowe alisema hayuko tayari kufanya kazi na Mbowe na kumzushia kuwa anakigawa chama na anauza siri kwa CCM, nadhani wa kushikwa uchawi kwa kifo cha Wangwe ni yule mwenye siri zake ambaye hataki CCM wasijue, kwa CCM walimuhitaji sana ili wajue siri za Chadema na Mbowe alikuwa na hofu kubwa siri yake isitoke nje.
Mbowe kumtumia Mnyika kuandika barua haraka haraka kwa IGP haisaidii kuwazuga polisi wasifanye kazi yao kitalaam na kuvifuatilia vyanzo vilivyo MMBOWESHA mpiganaji Wangwe.

NINA wasiwasi kuwa kilichomuua ni juu ya yeye kukutana na watu wengi na haswa viongozi wengi wa CCM waandamizi na ilifikia mahali wakasema kuwa aliwarekodi wakati wa vikao na hilo aulizwe Wassira anaweza kulitolea jibu kwani lilikuwepo mwezi April mwaka huu kuwa kila kikao alichokuwa anafanya na viongozi wa CCM basi aliweza kuwarekodi.

Kuna kila sababu ya kutaka kufanyika kwa uchunguzi tena wa kina ili kujua ni nani muuaji hata kama ni CHADEMA ama CCM basi lazima sheria ichukue mkondo wake mara moja.

RA yuko wapi? Makamba anasema nini juu ya hili?
 
Mbowe Alisema Hayuko Tayari Kufanya Kazi Na Wangwe Anayevujisha Siri Za Chadema. Walijaribu Kumnyamazisha Kidemokrasia Wakashindwa, Sasa Wameenda South Africa Kumtafutia Sangoma La Kumuondoa.

Pamoja na kutoongelea mambo ya kikabila kama unayoleta hapa, watu wa Tarime hatuaamini mambo ya usangoma. Ningekushauri utupatie heshima ili tumzike mbunge wetu.

Huu upuuzi wa kutaka kuanzisha fujo Tarime kwa sababu za kisiasa kama zako ushindwe kwa jina la YESU wa Nazareth aliye hai.
 
Somo:Familia ndio yenye uwezo wa kusema mwili wa Marehemu uchunguzwe. Kwa hiyo kuanzia leo. tuachane na upuuzi wa chama, au watu binafsi kusema mwili wa fulani uchunguzwe etc.

By the way: Naomba muchunguze kama wachangiaji kama akina MM Mwanakijiji watalala leo.
 
Ina maana Mazishi yatafanyika Lini?hao ndugu zangu wakurya watakuwa wanagombania Mali tu na hizo Rambi rambi,nakujua huko..

Mkuu....unahakika unawajua wakurya....una uhakika na ulilolisema? Hizi stereotypical statements, haziendani na hekima zako!
 
NINA wasiwasi kuwa kilichomuua ni juu ya yeye kukutana na watu wengi na haswa viongozi wengi wa CCM waandamizi na ilifikia mahali wakasema kuwa aliwarekodi wakati wa vikao na hilo aulizwe Wassira anaweza kulitolea jibu kwani lilikuwepo mwezi April mwaka huu kuwa kila kikao alichokuwa anafanya na viongozi wa CCM basi aliweza kuwarekodi.

Kuna kila sababu ya kutaka kufanyika kwa uchunguzi tena wa kina ili kujua ni nani muuaji hata kama ni CHADEMA ana CCM basi lazima sheria ichukue mkondo wake mara moja.

RA yuko wapi? Makamba anasema nini juu ya hili?

Wote hawa wanajaribu tu kupindisha ukweli wa mambo. Hili jambo lisiangaliwe kwa misingi ya vyama la sivyo ukweli utapotea. Polisi wafanye kazi yao ya kuchunguza hii ajali yote, kuanzia kwa "mallya", shahidi waliofika kwenye tukio la ajali, bastola iliyokutwa kwenye gari, mawasiliano ya polisi na Mallya, na mengine mengi ambayo madakitari watasema likiwemo hili la majeraha ya risasi kwa Wangwe bila kutumia bias za vyama kwa sasa.
 
Wewe unadai kuwa ni mtu wa Tarime wakati maandishi yako hapa yanaonyesha kabisa kuwa hujali feelings za watu wa Tarime bali unataka kupata pointi kisiasa.

Ondoa siasa kwenye kifo cha Wangwe, wamejaribu TBC1 na magazeti ya Rostam wameshindwa. Kuna mengi inabidi yajulikane sasa hivi na sio pointi za kisiasa kwenye msiba mkubwa kama huu.

Shame on you.

Kwahiyo nipeleke kwetu wewe unakokujua.

Hakuna msiba mdogo wala mkubwa Na mtu akifa unajisikitkia wewe mwenyewe sio kumsikitikia marehemu.

Kwenye msiba sio lazima ukikuja uso ndio utaonekana umeguswa na msiba,kwetu Taarime tuna imani kifo kikitokea yule anayejifanya kusikitika sana na kulia kwa sauti kuu huyo huyo ndio mchawi aliyemloga marehemu.

Kwenye msiba watu huwa wanacheza karata na kucheka pia .

Kumbe wewe hapa JF unafanya SIASA? mimi huko siko

Ila lazima tochi lipigwe kutoka mguuni alipokua amesimama chacha yani kutokea CHADEMA ndani.
 
kiranja,
Ni Kweli Mbowe Sasa Hivi Yuko Musoma Mjini.

Hakukuwa Na Mbowe,slaaa Wala Zitto Kwenye Msafara Wa Maiti Toka Dodoma Hadi Musoma. Huyo Mnyika Anasubiri Amri Za Mbowe Nini Aandike Badala Ya Kwenda Kwenye Msiba.
Wanajitia Wana Uchungu Na Wangwe,wakati Wiki Tatu Zilizopita Wamesema Kuwa Hawako Tayari Kufanya Kazi Na Wange Na Mzigo Mkubwa Ndani Ya Chadema.
Wangwe Anafamilia Yake Ndiyo Yenye Uwezo Wa Kuhoji Kifo Cha Ndugu Yao, Sio Wanafiki Waliosema Kuwa Ni Mzigo Kwenye Chama Chao.
 
Mbowe Alisema Hayuko Tayari Kufanya Kazi Na Wangwe Anayevujisha Siri Za Chadema. Walijaribu Kumnyamazisha Kidemokrasia Wakashindwa, Sasa Wameenda South Africa Kumtafutia Sangoma La Kumuondoa.

Mallya ni nani? Kwa nini alienda Misri ?alipata mafunzo gani huko? kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la leo amesema kuwa alipelekwa Libya mwaka jana na huko alienda akiwa na Mufti wa Tanzania,Mheshimiwa Juma Kilimba,Makongoro Nyerere .

Hawa wanatakiwa kusema walifuata nini huko Libya na baada ya hapo huyu Mallya akapelekwa Uswisi alilipiwa na nani?

Je?ni kweli alisoma Nairobi? alisoma kitu gani?

Huwa anafanya shughuli gani pale LUMUMBA?KILA MCHANA AMA JIONI?

Huyu anaishi Masaki ni kwa nani huko?
 
Somo:Familia ndio yenye uwezo wa kusema mwili wa Marehemu uchunguzwe. Kwa hiyo kuanzia leo. tuachane na upuuzi wa chama, au watu binafsi kusema mwili wa fulani uchunguzwe etc.

By the way: Naomba muchunguze kama wachangiaji kama akina MM Mwanakijiji watalala leo.

Kasheshe,

So far waliosema kuwa mwili wa marehemu uchunguzwe ni familia ya Wangwe na wakazi wa Tarime. wao ndio wamekataa kuzika hadi uchunguzi ufanyike. Haya mengine ya polisi kufanya kazi yao ni suala la common sense ambayo mtu yeyote makini anatakiwa kufanya.

Ningekuwa JK ningeamuru uchunguzi huru mara moja mara tu baada ya Mallya na mashahidi kutoa taarifa zinazopingana kuhusu muda, eneo la ajali, idadi ya abiria, na namna ajali ilivyotokea.

Hii sio kitu kikubwa sana cha kuuliza. Ungekuwa Tarime leo hii ungeshuhudia uchungu na dissapointment kubwa toka kwa wakazi wa Tarime. Hili ni suala la muhimu sana kwa vyombo vya usalama kuja na report makini kwenye hili.
 
Hakukuwa Na Mbowe,slaaa Wala Zitto Kwenye Msafara Wa Maiti Toka Dodoma Hadi Musoma. Huyo Mnyika Anasubiri Amri Za Mbowe Nini Aandike Badala Ya Kwenda Kwenye Msiba.
Wanajitia Wana Uchungu Na Wangwe,wakati Wiki Tatu Zilizopita Wamesema Kuwa Hawako Tayari Kufanya Kazi Na Wange Na Mzigo Mkubwa Ndani Ya Chadema.
Wangwe Anafamilia Yake Ndiyo Yenye Uwezo Wa Kuhoji Kifo Cha Ndugu Yao, Sio Wanafiki Waliosema Kuwa Ni Mzigo Kwenye Chama Chao.

Mbowe, Zitto na viongozi wengi wa siasa walikuwa kemakorere (kijijini kwa marehemu) kwa maziko ya Wangwe. Wewe unatia aibu sasa na habari zako hizi za uongo.

Mbona unataka sana kuleta ukabila kwa wakazi wa Tarime? unafaidika na nini kwenye hili?
 
Kwahiyo nipeleke kwetu wewe unakokujua.

Hakuna msiba mdogo wala mkubwa Na mtu akifa unajisikitkia wewe mwenyewe sio kumsikitikia marehemu.

Kwenye msiba sio lazima ukikuja uso ndio utaonekana umeguswa na msiba,kwetu Taarime tuna imani kifo kikitokea yule anayejifanya kusikitika sana na kulia kwa sauti kuu huyo huyo ndio mchawi aliyemloga marehemu.

Kwenye msiba watu huwa wanacheza karata na kucheka pia .

Kumbe wewe hapa JF unafanya SIASA? mimi huko siko

Ila lazima tochi lipigwe kutoka mguuni alipokua amesimama chacha yani kutokea CHADEMA ndani.

Wanatumia mbinu hizi chafu ili kupata jimbo, wenzetu akili yao iko kwenye ruzuku wanajua kuondoka kwa wangwe ruzuku imepungua. wampeleke TUNDU LISSU akagombee kwani ndiye alisema kuwa alimsaidia Wangwe kuwa Mbunge.
 
mgagagigikoko unaonekana wazi kwamba umetumwa au unatumwa na fikra zako ambazo zinaweza kuwa siyo sahihi. Wenzako bado hatujajua ni nani mhusika ila tunatambua na kukubali kwamba kunawatu au vikundi vingi tunavyoweza kuvihisi, lakini wewe umekomalia chadema tu thats why nahisi umetumwa.
 
Kwahiyo nipeleke kwetu wewe unakokujua.

Hakuna msiba mdogo wala mkubwa Na mtu akifa unajisikitkia wewe mwenyewe sio kumsikitikia marehemu.

Kwenye msiba sio lazima ukikuja uso ndio utaonekana umeguswa na msiba,kwetu Taarime tuna imani kifo kikitokea yule anayejifanya kusikitika sana na kulia kwa sauti kuu huyo huyo ndio mchawi aliyemloga marehemu.

Kwenye msiba watu huwa wanacheza karata na kucheka pia .

Kumbe wewe hapa JF unafanya SIASA? mimi huko siko

Ila lazima tochi lipigwe kutoka mguuni alipokua amesimama chacha yani kutokea CHADEMA ndani.

Hiyo Tarime (ambayo wewe unaiita Taarime) haipo. Watu wa Tarime hawaamini mambo ya kishirikina labda kama unataka kuyaleta hapa. Kama ni uchungu unataka kusema kuwa spika wa bunge aliyelia bungeni wakati wa kuahirisha bunge ndiye mchawi?
 
Mbowe, Zitto na viongozi wengi wa siasa walikuwa kemakorere (kijijini kwa marehemu) kwa maziko ya Wangwe. Wewe unatia aibu sasa na habari zako hizi za uongo.

Mbona unataka sana kuleta ukabila kwa wakazi wa Tarime? unafaidika na nini kwenye hili?
Muongo wewe, HAKUNA KIONGOZI WA KITAIFA WA CHADEMA ALIYEONGOZANA NA MAITI TOKA DODOMA HADI MUSOMA, hakuna SLAA wala Mbowe.nipe ushahidi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom