Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Hapo sasa polisi inabidi waanike ukweli kabisa watu saizi wanafuatilia dot baada ya nukta wakituchuuza watakiona cha moto ni bora waweke wazi hiki kifo wamechemka kama mpirani hii ni rafu mbaya wamechemka.

Moto walianza kuuona polisi wa Tarime ambao walitaka kuleta siasa kama kawaida yao. Mimi nawapa ushauri polisi kuwa waendelee kulinda usalama wa wananchi wa Tarime na wasijaribu hata kidogo kukubali kuyumbishwa na wanasiasa na kuingilia kinachoendelea hapa kwenye msiba mkubwa uliowakumba raia wa Tarime.

Ninaamini kuwa watu wa Tarime ni watu makini na hawatafanya mambo ya ajabu kwa kukubali ushawishi wa wanafiki wachache wanaotumia vyombo vya habari TBC1 na magazeti ya Rostam Azizi kutaka kuwavuruga na kuleta fujo.
 
nadhani sasa is getting out of hand; tusubiri uchunguzi kama utafanyika. kwa sababu kama nilivyosema kwenye clue ya pili; gari. Sasa hivi mimi ningekuwa niko interested kuona nani analiangalia gari na kama limesafishwa n.k sasa hivi hilo gari lilitakiwa lisiguswe wala kufanyiwa nini hadi uamuzi utakapotolewa kama kuna inquiry. kwa sababu kama bunduki n.k ushahidi uko kwenye gari zaidi. Kwa sababu mtu anaweza kuangalia majeraha aliyo sustain Wangwe na kuangalia ndani ya gari ni kitu gani kimesababisha. So, ningeuliza where is the car?
 
Habari za UHAKIKA, zinaeleza kwamba, Deus Mallya ni kijana aliyepata mafunzo yake nchini Misri na ni dereva mzuri sana, pamoja na kuwa hajawahi kuwa na leseni ya udereva. Nani aliyempeleka Misri na kwanini akaenda Chadema kuwa "mpiga debe" wa kawaida tu!!! Hayo ni maswali yanayohitaji majibu, kabla ya kuwajua kina Mallya wengine zaidi
 
Getting out of hand? It's beyond that my friend. No one in Tanzania can die without controversy......
 
mna uhakika anaitwa "Mallya"? wekeni picha yake mtaona aliases alizokuwa anatumia au kwa wengine anajulikana vipi; sitoshangaa ana jina jingine.
 
Habari za UHAKIKA, zinaeleza kwamba, Deus Mallya ni kijana aliyepata mafunzo yake nchini Misri na ni dereva mzuri sana, pamoja na kuwa hajawahi kuwa na leseni ya udereva. Nani aliyempeleka Misri na kwanini akaenda Chadema kuwa "mpiga debe" wa kawaida tu!!! Hayo ni maswali yanayohitaji majibu, kabla ya kuwajua kina Mallya wengine zaidi

Mbona Kitila Mkumbo ana digrii mbili ni Tutor wa chuo kikuu cha Dar-es-Salaam lakini ni mpiga debe wa kawaida ndani ya Chadema, ana aliwahi kugombea Uenyekiti wa vijana mkoa wa Dar-es-salaam na ujumbe wa Baraza kuu kupitia CCM,jee huyu naye utasema ni pandikizi au ndio Guninita no 2?
 
Inawezekana sasa watu wawe macho , huwenda mapandikizi wengine wamo kwenye sehemu nyeti za vyama vingine na wanalipwa donge nono ili akihitajika kujipalestina iwe ni rahisi.

Ila ushahidi wa kama kweli ni risasi ndio utakaobainisha mbivu na mbichi.Na ukipekuwa huyu Marehemu alikuwa na siri maana kilichotokea karibuni ni majibizano ndani ya Chama chake vilevile kuwa na ushirikiano na Chama cha CCM kama inavyodaiwa , ila kuhusiana na machimbo pia inawezekana kwani mambo ya vito yanagharimu maisha ya watu ni biashara ambayo unabidi ukubali kama utataka kuifanya na wengi wanaofanya biashara hii huwa na walinzi pembeni lakini ionyeshavyo Marehemu hana walinzi.

Yote weka kando kwanza tutafute ushahidi kutoka kwa waliobaki hai ndani ya msafara wake ambao sasa ni kazi ya Polisi kuwajibika baada ya kushindwa kuichungua maiti kama ilijeruhiwa kwa risasi,na walioichungua maiti naona wapo matatani ,mkuu wa upelelezi na mkuu wa Polisi kazi kwenu dongo na vumbi lililochanganyika na upepo linaanza kuelekea kwenu. Msicheze mbali.
 
mna uhakika anaitwa "Mallya"? wekeni picha yake mtaona aliases alizokuwa anatumia au kwa wengine anajulikana vipi; sitoshangaa ana jina jingine.
Hana tofauti na wana JF mahiri wenye majina zaidi ya kumi labda amekopi hapa hapa JF kwa vigogo wetu.
 
Moto walianza kuuona polisi wa Tarime ambao walitaka kuleta siasa kama kawaida yao. Mimi nawapa ushauri polisi kuwa waendelee kulinda usalama wa wananchi wa Tarime na wasijaribu hata kidogo kukubali kuyumbishwa na wanasiasa na kuingilia kinachoendelea hapa kwenye msiba mkubwa uliowakumba raia wa Tarime.

Ninaamini kuwa watu wa Tarime ni watu makini na hawatafanya mambo ya ajabu kwa kukubali ushawishi wa wanafiki wachache wanaotumia vyombo vya habari TBC1 na magazeti ya Rostam Azizi kutaka kuwavuruga na kuleta fujo.

Mkuu nimesikia jamaa Dr.atafika saangapi mbona huyu Halisi anadai atafika saa 12.
 
Yani kama kuna kitu nilicho na hamu nacho kujua kwa sasa ni kumjua huyu jamaa ( Deus Mallya)kwa hapa JF anatambulika kwa jina gani...maana naskia alishawahi kujitambulisha katika moja ya magazeti ya kila wiki kua yeye ni Invisible....bila shaka atakua ni mtumiaji na mchangiaji katika hii forum....eeh mungu saidia tumjue..nafkiri baada ya hapo tutakua tumepiga hatua kubwa ya kumuelewa huyu jamaa vizuri...........
 
Kuna kitu ambacho huyu kijana alimwambia Chacha;

a. Kitu ambacho kilimfanya Wangwe akubali kumkaribisha nyumbani kwake kwa siku chache alizokuwa dodoma;
b. Kitu ambacho kilimfanya Chacha amuamini
c. Kitu ambacho kilimfanya Chacha akubali kurudi naye kutoka Dodoma; Chacha alikuwa anaenda msibani, Mallya alikuwa anarudi Dar kufanya nini?
d. Kama kuna mtu mwingine aliongezeka mbele ya safari, instincts zinaniambia aidha alikuwa anakubalika na Wangwe, Malya au wote wawili.
e. Aliyekuwa boardguard wake wa kawaida na ambaye amekuwa akisafiri naye mara kwa mara yuko wapi na kwanini hakuweza kwenda nao siku hiyo?
 
Nazidi kusisitiza kuwa kifo cha mh Wangwe kina utata mkubwa kuliko vifo vingine vyote vyenye utata, hata chupa za maji na soda zilizokutwa kwenye gari nani akubali kuwa pamoja na gari kupinduka mara kadhaa kama inavyodaiwa chupa hizo zaweza kubaki kama ambavyo zimeelekea kuonekana! CHADEMA TELL US PLEASE!
 
Habari za UHAKIKA, zinaeleza kwamba, Deus Mallya ni kijana aliyepata mafunzo yake nchini Misri na ni dereva mzuri sana, pamoja na kuwa hajawahi kuwa na leseni ya udereva. Nani aliyempeleka Misri na kwanini akaenda Chadema kuwa "mpiga debe" wa kawaida tu!!! Hayo ni maswali yanayohitaji majibu, kabla ya kuwajua kina Mallya wengine zaidi[/QUOT
Halisi fanya utafiti wa kina kabla ya kuandika,la sivyo tutashusha hadhi ya jamvi letu.
mimi naamini kuwa baada ya muda na watu kutulia chadema members waliopo hapa watakuja kutupa yaliyojiri kwa kituo.lakini hii ya kusoma au mafunzo mmmmmmmmmm,
 
Mbona Kitila Mkumbo ana digrii mbili ni Tutor wa chuo kikuu cha Dar-es-Salaam lakini ni mpiga debe wa kawaida ndani ya Chadema, ana aliwahi kugombea Uenyekiti wa vijana mkoa wa Dar-es-salaam na ujumbe wa Baraza kuu kupitia CCM,jee huyu naye utasema ni pandikizi au ndio Guninita no 2?

Unajua wewe mkuu unaonekana una matatizo ya akili.Naona umeingia kwenye kijiwe kisichokufaa.Hili ni jamvi la watu wenye akili timamu sasa sijui unafanya nini hapa
 
Msiba wa Chacha Wangwe hivi sasa umetekwa na SIMU za mkononi na INTERNET. Tunakoelekea sio kuzuri hata kama nia ni kuusaka UKWELI. Madhara yatakuwa makubwa zaidi kwa walioko msibani kuliko sisi tulioko mbali kwenye mitandao na simu.
 
Habari za UHAKIKA, zinaeleza kwamba, Deus Mallya ni kijana aliyepata mafunzo yake nchini Misri na ni dereva mzuri sana, pamoja na kuwa hajawahi kuwa na leseni ya udereva. Nani aliyempeleka Misri na kwanini akaenda Chadema kuwa "mpiga debe" wa kawaida tu!!! Hayo ni maswali yanayohitaji majibu, kabla ya kuwajua kina Mallya wengine zaidi[/QUOT
Halisi fanya utafiti wa kina kabla ya kuandika,la sivyo tutashusha hadhi ya jamvi letu.
mimi naamini kuwa baada ya muda na watu kutulia chadema members waliopo hapa watakuja kutupa yaliyojiri kwa kituo.lakini hii ya kusoma au mafunzo mmmmmmmmmm,

Ahsante kaka!!!!!! Itabidi niende kwao Manushi, Kibosho kupata uhakika
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom