Daktari Slaa,
Naona kwa huu mtazamo wenu wa holier than thou, nafikiri mko hatarini kuanguka kwa kishindo kibaya. Vyama vikubwa na vya kugeresha vitakuwepo nchini TZ hata kama kutatungwa sheria ya kuvibana.
Lakini hiki kiburi cha CHADEMA cha kujiona kuwa wao ni bora kuliko vyama vingine, including NCCR, CUF, UDP n.k., na kujaribu kutumia maneno ya Mtikila kama kielelezo cha ubovu wa wanamageuzi wengine, ni jambo la kusikitisha sana na sidhani kama litavifikisha vyama vya upinzani mbali. Sitashangaa Chadema ikipoteza Tarime, kama vyama vingine navyo vikiamua kupingana nao huko. Mh. Daktari, mmekosea sana kuacha ushirikiano na wapinzani wengine, na kiburi chenu nafikiri kinawaingia vichwani hivi sasa na nafikiri unaelewa matokeo yake. Mungu ibariki Tanzania.