Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Masatu,
Unajua kabisa sina tabia ya kuropoka na wala kutamka kitu sina uhakika nacho. Kipindi chote tulichosemwa wakati wa msiba wa Wangwe tulikaa kimya kwa sababu hatukuwa na kitu mikononi mwetu. Sasa tunacho na hatuna wasiwasi. Mwulizeni Makamba akanushe na aone tutakavyomwumbua. Kwa taarifa yenu wala siyo huyo tu.

Ahsante Dr. Slaa kwa juhudi zako za kutuokoa watanzania, katika sentensi yako hapo juu nilivofahamu mimi ni kwamba hivi sasa una ushahidi wa Makamba kumpa rushwa Mtikila, kama hii na sahihi basi naomba umfungulie mashtaka ya rushwa bw. Makamba kwani utakuwa unasaidia taifa kuondoa uchafu toka kwa viongozi wabovu, najua siasa ni mchezo wa karata na wewe unasubiri wakati mwafaka wa kutupa hii Ace uliyonayo lakini kusubiri huku ni kutowatendea haki watanzania, kutokana na nafasi yako nasema weka wazi na fungua kesi dhidi ya makamba kwa manufaa ya Umma, Ahsante.
 
Masatu,
Unajua kabisa sina tabia ya kuropoka na wala kutamka kitu sina uhakika nacho.

Mheshimiwa kuna kipindi wakati Marehemu Ballali yuko Marekani ulisema umepewa taarifa kuwa amekimbilia Malta. Hukuwahi kuja kukanusha wala hukuwahi kuja tena kututhibitishia kwamba alikuwa huko. Labda ulikuwa na uhakika sijui.
 
^^Kafanya uchunguzi wake binafsi... na ameeleza mengi zaidi ya hiyo nukuu
 
Ni vizuri kusubiri na kuona ni namna gani waliotuhumiwa watareact. Ila sio vibaya pia tukijiuliza ni kwanini hizi habari ametoa leo baada ya muda wote kupita? Mchungaji alikuwa wapi wakati suala lilipokuwa hot, ni kwanini iwe wakati ambao vyama vipo mbioni kuzindua kampeni zao kugombea nafasi iliyoachwa na Marehemu Chacha Wangwe? Ni kwanini iwe wakati ambao Chadema wanaadhimisha siku ya kupiga vita Ufisadi? Why now? I hope the quick and analytical thinkers will come up with their contributions.
 
Hakika hii ni kazi aliyotumwa na RA ili amfutie lile outstanding loan ya 3,000,000/=.

Ninaelekea kukubaliana na wewe, lakini pia nitalishangaa jeshi la polisi wasipo mshikilia mtu huyu ili aweze kuwa shahidi number 1 kwani kwa maelezo yake inaelekea alikuwepo wakati wa mauaji hayo anyao yadai hadi akiona anapulizwa dawa, anapigwa nyundo anabaki bila kufa hadi anapigwa tena na kuweka jiwe.. vinginevyo basi apelkwe milembe si bure!
 
Masatu,
Unajua kabisa sina tabia ya kuropoka na wala kutamka kitu sina uhakika nacho. Kipindi chote tulichosemwa wakati wa msiba wa Wangwe tulikaa kimya kwa sababu hatukuwa na kitu mikononi mwetu. Sasa tunacho na hatuna wasiwasi. Mwulizeni Makamba akanushe na aone tutakavyomwumbua. Kwa taarifa yenu wala siyo huyo tu.



Huyo Makamba atakanusha tu...tumesha wazoea kwa kukanusha mambo ya ukweli ni jadi.........mbona wanadai wao hakuna fisadi......jana wamekanusha fedha za EPA hazijatumika kwenye kampeni za CCM....ndo zao hizo.....
 
Kama ana upako wa Mwenyezi Mungu, mbona hakutabiri kifo hicho kabla hakijatokea?
Huyu mtu kwa sasa anaonekana yupo zaidi kuganga njaa
 
Siasa za maji taka na njaa zitatumaliza wa TZ.
Aliyekufa hajui kitu na atajitetea huko kwa maulana kwa nini walio hai wahangaike na mambo yake tena ya kutaka kuleta machafuko ndani ya familia na jamii?
Je huyu Mchungaji amekuwa msemaji wa serikali waliokabidhiwa dhamani ya usalama wa raia na mali zao?Serikali na daktari wao walisema Chacha amepata ajali,na katika cheti cha uchunguzi inaonesha hivyo,na waandishi na vyombo vya habari viliripoti hivyo,kWA KUWA umekaribia uchaguzi Tarime ndipo zinakuja tena habari za kuawawa.Watu wakichinjana huko Tarime kwa habari hizi ndiyo furaha ya Mtikila?Poor pastor under the sun!
 
Mimi ninaunga mkono wote waliopendekeza Mtikila akapimwe akili. Tunamsifu tu kwa kuishinda serikali katika suala la mgombea binafsi, lakini haya mengine madai yake yote huwa hayana uthibitisho. Kuna wakati kama mnakumbuka liishia jela.

Ni huyu huyu Mtikila aliyeituhumu CCM kumuua Kolimba lakini hakuwa wala na uthibitisho, ni huyu huyu Mtikila aliyemshutumu na kumkashifu Baba wa Taifa Hayati Nyerere na akaishia jela, ni huyu huyu Mtikila aliyemtuhumu Ben Mkapa kwamba si raia, na ni huyu huyu Mtikila aliyemtuhumu Sumaye kuwa ni mwizi na akaahidi kupeleka mahakamani lakini mpaka leo hajampeleka. Hivi si huyu Mtikila aliyejiunga na Chadema wakati fulani akafukuzwa? Ama si huyu huyu Mtikila aliyejiunga na CUF kisha akafukuzwa? Sasa kweli huyu ni mtu wa kuamini analolisema?

Sasa mimi ningemshauri kuwa kabla ya kwenda Tarime kufanya alichokikusudia, kwanza awaeleze Watanzania vizuri misingi ya urafiki wake na Rostam Aziz na kama alikwisha zirudisha zile pesa alizochukua kwa huyo fisadi. Vinginevyo tutaamini kuwa yeye ndiye anmtuma kuimaliza Chadema ili asamehewe deni.
 
Hizi maneuver za Mtu Killer...
The following was written 7 days ago.




Masatu,
Sembuse ungelijua ninayoyajua sasa! Kwa bahati mbaya si tabia ya Chadema kwa unafiki wa aina yeyote ile. Tukishindwa Tarime ni kwa sababu nyingine wala si kwa kuachana na Ushirikiano. Nimeeleza kwingineko kuwa sasa tunaushahidi wa wazi. Hatuna sababu ya kuwa na ushirikiano na watu ambao usiku wanatuchoma visu.

Nimesema tuna video recording ya Mwenyekiti mmoja wa Ushirikiano, aliyemwita Mhariri wa Gazeti, tena linalomilikiwa na tuliyemtaja katika Listi ya Ufisadi, na "wakatunga" story ya Mbowe kuangusha Sherehe Tarime baada ya kupata Taarifa ya kifo. Unahitaji ushahidi gani zaidi! Mwenye macho na masikio haambiwi! Ni wakati sasa watanzania wakaelezwa kwa uwazi aina ya vyama tulivyonavyo hapa Tanzania.

Kuna Chama sasa hivi kimepewa fedha kwenda Tarime, na mtawasikia na kuwaona siku chache zijazo.
Chadema huwa hatusemi bila kuwa na ushahidi mnajua. Tutatoa yote wakati ukifika. Lakini ujue kuwa hakuna sababu kujilazimisha katika ndoa ambayo umethibitisha kabisa haiwezekani.

Tungetaka kuweka ki theolojia tungeliiweka, lakini labda si mahali pake. Kwa kifupi hizi ni zile ndoa ambazo hata kwa wakatoliki zinakuwa "dissolved" kwa kuwa ni null and void Ab initio.


Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

.
 
Nadhani ni vizuri tuone Chadema na watajwa watachukua hatua gani?......Inawezekana anawatega wataposhindwa kumfikisha mahakamani atasema unaona wanaogopa hata kwenda mahakamani....wakijua nitawaumbua.....Maana ni same argument Chadema walitumia dhidi ya watuhumiwa wa "list of shame"

Vile vile inawezekana ikawa muendelezo wa kutaka kuidhohofisha Chadema ....kwa Mtikila kutumiwa na watu in the background au kukawa na ukweli kiasi fulani ......nadhani ni vizuri kusuburi tuone watuhumiwa watafanya nini.

Napenda niamini kuwa Katika harakati za kisiasa Tanzania na hasa wakati huu wa uchaguzi kila chama kitatumia any possible way kupata ushindi.Sitaki kuamini kuwa mtikila anatafuta kura Tarime kwa kukidhoofisha chama kama Chadema kwa kuwa DP haijasimamisha mgombea.Lakini nataka kuamini kuwa Mtikila kama binadamu mwingine yeyote anaweza kuwa na sababu za msingi na hata zisizo za msingi kutoa allegstions kama hizoata hivyo napata wakati mgum sana kuzichekecha taarifa za Mtikila kwa kuwa yeye ni aina ya watu wenye tabia ya undumilakuwili na tena ni mtu ambaye anaendesha siasa zisizo wazi.

Taarifa alizotoa kuwa wahusika wa kifo cha Wangwe ni top officials wa chadema zaweza kuwa ni kampeni chafu dhidi ya chadema na Mtikila akawa anatumiwa kisiasa.Ni wakati sasa Mtikila akatakiwa kutoa uthibitisho wa madai na kaka kweli ana uhakika hakutakiwa kusubiri bali angeutoa palepale.

Pia inashangaza sana kuoana walioattend press conference yake ni wanafamilia wa Wangwe.What an organised kind of political comedy?Siamini kama Mtikila ndiye aliyepanga na kuandaa mazungumzo hayoTravetine.Anaweza lakini kwa nimjuavyo mimi, lazima kuna jambo la kisiasa.
 
Masatu,
Unajua kabisa sina tabia ya kuropoka na wala kutamka kitu sina uhakika nacho. Kipindi chote tulichosemwa wakati wa msiba wa Wangwe tulikaa kimya kwa sababu hatukuwa na kitu mikononi mwetu. Sasa tunacho na hatuna wasiwasi. Mwulizeni Makamba akanushe na aone tutakavyomwumbua. Kwa taarifa yenu wala siyo huyo tu.

Dr Slaa, pole sana kama uovu huo umefikia hapo hata mtu aitwaye mchungaji anaweza kutumika hivyo. Au 'title' hii ni feki tu? Binafsi sina mashaka yoyote na msimamo wako. Kila mtu anajua jinsi unavyokuwa unatetea hoja bungeni kwa nguvu zako zote licha ya kuwa huwa unawekewa vikwazo hapa na pale ili usieleze kile ulichopanga kuwaelewewesha Watanzania.

Kwa kweli nasikitika sana kuona Watanzania tulivyowajinga tunapokubali kutumiwa na wakubwa fulani kuwaharibia wengine. Siyo tofauti sana na mtu kuwa kichaa au tuna kile kinachoitwa 'invincible ignorance'?
 
Ama kweli njaa/tamaa nikitu kibaya sana!! ktika yoooote sikutegemea Mtikila mzee wa magabachori kama angeweza nunulika kirahisi namna hii!!

Duuu yaani ogopa shilingi bwana, inakufanya mtu unasahau utu wako kabisa unatumiwa upside down hadi unaonekana kituko mbele ya jamii?? walio karibu na huyu mzee msaidieni jamani!! Anakoe elekea siko.. watanzania si mbumbu tena wakuto weza ngamua kati ya pumba na mchele.

Kesi iko mahakamani ina mkabili Malya apeleke ushahidi wake huko badala ya kuichanganya jamii na kutaka watu wauane kwa tamaa yake ya tujisenti!
 
Huyo Makamba atakanusha tu...tumesha wazoea kwa kukanusha mambo ya ukweli ni jadi.........mbona wanadai wao hakuna fisadi......jana wamekanusha fedha za EPA hazijatumika kwenye kampeni za CCM....ndo zao hizo.....

Fidel ni kweli CCM ni zao kukanusha kila ovu wafanyalo.Fedha za EPA asilimia kubwa zilikwenda CCM hakuna ubishi na hata CCM wakiendelea kubisha sisi tunaoelewa tunabaki kuwashangaa sana.Kama wana uhakika basi Kikwete angewataja majina wahusika wa EPA kama angepona mtu CCM.

Hata ishu ya Mtikila kuwahusisha Chadema na kifo cha Wangwe ni propaganda chafu za kiimla na za kudhoofisha nguvu ya Chadema.Ni na hakika Mtikila anatumiwa kama magazeti ya Habari Leo na Rai yalivyotumiwa wakati wa msiba wa Wangwe kuichafua Chadema.Hizi ni siasa za uendawazimu Tanzania.
 
huyu hakuwa specific. ni uzushi wa hali ya juu na ni hatari kwa amani yetu
 
Sio bure Mtikila anatumiwa au ni "insane". Akina RA (mafisadi) wamemuahidi zaidi na wanamtumia ili kukidhoofisha chadema. Alete ushahidi wa kutosha aache porojo.
 
Mtikila is one of the cheapest politicians in the World. Yaani kama anaweza kwenda kuomba omba kwa kina Rostam hata shs milioni tatu, huyo mtu siku mkimpa nchi ataifilisi ndani ya mwaka mmoja! Huwezi kumtambua fisadi kwa kumwangalia usoni, ufisadi ni tabia ya kuzaliwa nayo!

Bila shaka kashapewa vijisenti na watu fulani ili awachanganye CHADEMA!
 
Kwa nini taarifa hizi anazileta kipindi hiki ambacho ni cha kampeni huko Tarime? Mtikila na mafisadi wenzake wanatambua wazi kuwa sasa chadema "is for people and people are for chadema". Wanasiasa wa sampuli hii lazima jamii iwahukumu kwa matendo yao wenyewe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom