Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Polisi wabeza ushahidi wa kifo cha Wangwe
Shadrack Sagati
Daily News; Thursday,August 07, 2008 @00:01

Polisi imebeza ushahidi uliowasilishwa kwao juzi na viongozi wakuu watatu wa vyama vya upinzani juu ya utata wa kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe (Chadema), kwa maelezo kuwa ushahidi huo ni wa kuokota mitaani.

Kamishna wa Polisi Paul Chagonja ambaye alipokea ushahidi huo juzi, aliliambia gazeti hili kuwa kilichowasilishwa na viongozi hao sio ushahidi bali ombi la kutaka jeshi hilo lifanye uchunguzi wa kina wa kifo cha Wangwe, kwa maelezo kuna utata.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, juzi walikwenda ofisini kwa IGP kuwasilisha kile walichosema ni ushahidi juu ya ujasusi na umafia wa Deus Mallya aliyekuwa na Wangwe wakati ajali iliyosababisha kifo chake (Wangwe) ilipotokea eneo la Pandambili, Dodoma, siku 10 zilizopita.

Mallya, kwa sasa yuko rumande baada ya kufikishwa mahakamani Ijumaa iliyopita, akituhumiwa kwa makosa matatu ya kusababisha kifo cha Wangwe, kuendesha gari kwa kasi na bila leseni. Kabla ya kwenda Polisi, viongozi wa upinzani waliwaambia wanahabari kuwa wana ushahidi, kuwa Mallya yuko kwenye mtandao wa Mafia na ana mafunzo ya ujasusi, hivyo wanaamini atakuwa amehusika kwenye ajali ya Wangwe.

Waliahidi kumpatia ushahidi huo IGP ili aufanyie kazi. “Ni kweli wamekuja tukaonana, lakini hakuna cha ushahidi wowote juu ya yale waliyowaambia waandishi wa habari juu ya Deus Mallya na utata wa ajali. “Wameniomba suala hilo polisi tutumie busara kubwa kutokana na utata uliopo, lakini hakuna ushahidi mwingine…kitu walichonisisitizia ni kwamba ajali ile ina maslahi kwa taifa, kwa Chadema hasa kutokana na maneno yanayosemwa,” alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, viongozi hao walimwomba aamuru Polisi wafanye uchunguzi wa kina wa suala hilo na katika kipindi kifupi walimaliza mazungumzo. Kwa mujibu wa Chagonja, kwa vile viongozi hao hawakuwapo eneo la ajali Polisi wanaamini kuwa walichowaeleza ni mambo ya kusikia mitaani.

Kwa mujibu wa Kamishna huyo, Polisi wameridhika kwa kiasi kikubwa na uchunguzi uliofanywa na madaktari na taarifa ya madaktari wa familia. Aliongeza yeye binafsi alitarajia kupokea ushahidi mzito lakini badala yake viongozi hao hawakuuwasilisha na muda mwingi walizungumzia kuishukuru Polisi na Mkuu wa Mkoa wa Mara Issa Machibya, kwa busara walizotumia wakati wa vurugu kwenye msiba wa Wangwe.

Chagonja alisema; “Waliniomba nifikishe shukrani zao kwa mamlaka za mkoa wa Mara.” Kamishna huyo aliongeza kuwa baada ya majadiliano hayo, baadaye Mrema alianza kutoa maombi yake ya kutaka Polisi imrudishie vifaa vyake ambavyo vilikamatwa miaka kadhaa iliyopita. “Mrema aliomba kama kesi dhidi yake imemalizika ni heri wamrudishie vifaa hivyo kwani ana kazi navyo,” alisema.

Kamishna Chagonja alisema baada ya kupata maelezo hayo yeye aliwataka wao kama viongozi wa vyama vya siasa kutofanyia kazi mambo yanayosemwa mitaani. Chagonja alisisitiza kuwa ajali iliyotokea ni ajali ya kawaida na kwa kuwa viongozi hao hawakuwapo eneo la tukio hawawezi kukusanya ushahidi wa mitaani juu ya tukio hilo.

Kamishna huyo alisema baada ya kuona ushahidi huo hauisaidii Polisi, aliwaeleza kuwa busara wanayotaka polisi waitumie ni kwa wao kama viongozi wa watu kutofanyia kazi maneno yanayoweza kuhatarisha amani. Kuhusu tamko la familia, Chagonja alisema kuwa tamko hilo halijafikishwa ofisini kwa IGP, hivyo hawezi kulizungumzia.

“Sisi tunasema kama kuna watu wana ushahidi wakiwemo wana familia wajitokeze waje tuzungumze, watusaidie namna ya kupata ushahidi wa kile wanachodai". Bosi huyo wa Polisi alivitaka vyombo vya habari pia kuwa makini katika kuripoti masuala hayo, kwani baadhi ya mambo yanayoandikwa yanaweza kuzidisha chuki miongoni mwa jamii.
Hawa viongozi wa polisi ni wanafiki wakubwa na wamejiunga katika mtandao wa mafisadi maana hata wanapostaafu wote utasikia wanatangaza kugombea ubunge kwa tiketi ya ccm sasa hapo si unaweza kujua kwa nini wanajikomba?
Kama hawafanyi kazi kwa uvumi tu ikawaje wakaenda kum search Kubenea kwa uvumi wa wanasiasa na wakati hawakuwa na ushahidi?
Wanafiki wakubwa na wao inabidi tuanze kuwalipua manyanga yao wanayofanya kwani hatuyajui?
Sitaki hata kusikiliza porojo zao.
 
Hata kama the writer got it wrong na DPP "alishauri" tu, DPP was wrong as thi infringes freedom of the press, their right of expression and their right to earn a living.

Sasa wasiandike kwa kina habari hot magazeti yasipouzwa wakija nyumbani kwake kutafuta chakula atawalaumu?

Tuko pamoja Mkuu Pundit, DPP ni mtu mkubwa hasa ktk masuala ya mashtaka hivyo ushauri wake unakuwa na nguvu kuliko wa mtu wa kawaida hivyo kunyima uhuru wa vyombo vya habari hasa 'wale waoga'. lakini kwa waandishi makini, hawawezi kutishwa na ushauri.

Kwa mawazo yangu mwandishi amemnukuu vibaya kwa kusema 'habari za Wangwe sasa zapigwa `stop`.
 

Wanafiki wakubwa na wao inabidi tuanze kuwalipua manyanga yao wanayofanya kwani hatuyajui?
Sitaki hata kusikiliza porojo zao
.
Taratibu Kamanda,
soma vizuri hilo bandiko na utawajua wapiga porojo na wanafiki ni kina nani...
 
Kwa swala la Mrema niko na Jmushi
ebu tuacheni ushabiki wa vyama na turudi nyuma tujikumbushe kipindi kile Mrema akiwa CCM na akiwa kiongozi, je alifanya kazi yake kwa kuwatumikia wanyonge na alikuwa akitimiza wajibu??

Tukishapata majibu ya maswali hayo, then turudi tujadili sasa kwanini watu mnampinga mushi akisema mrema ni mtetezi wa wanyonge sema nguvu ya Mafisadi kupitia vyombo vyao vya Media wameamua kumuaribia ili kufaidiaka na sio watanzania wafaidi.
 
Hata A. Hitler alikuwa mtetezi wa wanyonge..... Mrema alitumia Wanyonge kujipandisha chati katika siasa. Kwani siku hizi hakuna tena wanyonge?
 
Alikuwa hajasikika siku nyingi, ameshatoa pumba zake, amesikika, tumwache tuendelee na mambo muhimu
 
Sikusema Mrema aingile uchunguzi wa polisi...Nilisema Mrema ni MKOMBOZI WA WANYONGE NA NDIYE CHAGUO LA RAS.

Jmushi1,

Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100 juu ya hili. Mrema alikuwa mtetezi wa Wanyonge na pia alitimiza wajibu wake kama waziri labda kuliko waziri mwingine yeyote wa TZ ambaye namjua mimi.

Kwangu mimi Mrema anawakilisha kundi la viongozi ambao ningependa kuwaona wanapewa nafasi Tanzania. Wale ambao wanajua kutafuta jawabu kwa matatizo yetu.

Inasikitisha hawa wasomi wetu wengi wanashindwa kutatua hata matatizo yanayowazunguka. Hata takataka zikijaa nje ya nyumba zao wanashindwa kutatua.

Mimi ni mpenzi wa Mrema na hata museme nini hamuwezi kunibadili kwi kwi kwi!!!
 
Mrema alimaliza ngwe yake alipokuwa waziri wa mambo ya ndani. Sasa hivi amekwisha.Tumwache apumzike.
 
Heshima Mbele,

Hii ni habari ambayo nimeiona kwenye Mtandao,Habarileo.co.tz,naomba kuwasilisha.
Makachero wa Polisi wamewahoji wazazi wa Deus Mallya ambaye alikuwa kwenye gari lililopata ajali iliyosababisha kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, Jumatatu wiki iliyopita.

Taarifa za kuaminika ambazo HabariLeo imezipata zinasema makachezo hao waliwahoji wazazi hao nyumbani kwao Umbwe, mkoani Kilimanjaro, juzi. Haikuweza kufahamika kwa undani kuhusu mahojiano hayo, ingawa wanafamilia waliliambia gazeti hili kwamba Polisi walitaka kupata taarifa za undani za Deus (27) kutoka kwa wazazi hao.

Baba wa Deus, Francis Mallya, alilithibitishia gazeti hili jana kwamba watu waliojitambulisha kuwa Polisi walifika kijijini hapo juzi wakimtafuta. Alisema kwa vile hakuwa nyumbani makachero hao walielekezwa mahali alikokuwa akifanya kazi zake, wakamfuata huko na wakafanya mahojiano naye ambayo zaidi yalimhusu Deus. Hakutaka kuingia kwa undani kuhusu suala hilo.

Kwa sasa Deus yuko rumande mjini Dodoma baada ya kufunguliwa mashitaka wiki moja iliyopita ya kusababisha kifo cha Wangwe, kuendesha gari kwa mwendo kasi na kutokuwa na leseni. Kesi yake itatajwa tena Ijumaa wiki ijayo. Jina la Deus limekuwa likitajwa na kufahamika baada ya kunusurika katika ajali iliyosababisha kifo cha Wangwe iliyotokea eneo la Pandambili, Dodoma, wakati wakiwa njiani kwenda Dar es Salaam.

Awali Deus alidai kwamba wakati ajali ilipotokea, Wangwe ndiye alikuwa akiendesha gari lakini kauli yake ilipingwa na wanawe marehemu Mbunge huyo, ambao walisisitiza kwamba ni kijana huyo aliyekuwa akiendesha gari hilo wakati walipokuwa wakiondoka Dodoma.

Hata baada ya kufunguliwa mashitaka ya kuendesha gari hilo, wanafamilia na viongozi wa vyama vya siasa walitaka Polisi wamchunguze, wakidai wana shaka na urafiki wake na Wangwe ambao ulikuwa wa karibu katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja. Baadaye yalikuja madai kwamba ni jasusi ambaye alipata mafunzo nchini Libya. Mallya aliwahi pia kukaririwa akisema kwamba alisoma nchini Kenya lakini maelezo hayo yalikanushwa na baba yake aliyesema mwanawe hakuwahi kusoma huko.
 
Bado hatuwezi kuanza kuzidharau kazi za wazalendo kama Mrema.
Kwangu binafsi Mrema is one of the bravest....Na ni CHAGUO LA RAS!
Kama kweli media ilitumika kuwamaliza kina Sumaye na Maleccela..Itakuwa vipi kwa Kamanda wetu aliyehama chama?
Mrema FOR PRESIDENT...
Kama kuna mwenye namba ya Mrema naomba munisaidie kwani wengine tunataka kuwasliliana na MKOMBOZI WA WANYONGE!


JMushi unatisha! From Mbowe to Mrema! Kaaaazi kweli kweli...
 
•Meseji za Mallya kwa Kabwe zanaswa, Ajitambulisha ni mtaalam wa kompyuta, Aomba tenda ya kuchapisha nyaraka, Siri ya kukutana na Wangwe yabainika

*Ajitambulisha ni mtaalam wa kompyuta
*Aomba tenda ya kuchapisha nyaraka
*Siri ya kukutana na Wangwe yabainika

Na Hassan Abbas

MBINU ya Bw. Deus Mallya, kijana aliyenusurika katika ajali iliyomuua mbunge wa Tarime, Bw. Chacha Wangwe, ambaye sasa anahusishwa na ujasusi, kuwaingia wanasiawa mashuhuri nchini na kujenga urafiki nao, imebainika.

Mbinu hiyo imefahamika kufuatia uchunguzi wa gazeti hili kuzinasa meseji zake kadhaa alizowahi kumtumia Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Bw. Zitto Kabwe, ikiwa ni kabla ya kufahamiana na marehemu Wangwe.

Imebainika Mallya akijitambulisha kuwa ni mtaalamu wa mifumo mbalimbali ya programu za kompyuta katika uchapishaji wa nyaraka na vitu mbalimbali kabla ya kufahamiana na marehemu Wangwe, alijipenyeza kupitia kwa Bw. Kabwe akijinasibu kuwa angeweza kuifanya biashara hiyo vyema.

Kwa meseji zake kwenda kwa Kabwe, ambazo Majira Jumapili linazo, Mallya, alianza 'kumuingia' mbunge huyo kijana na kufanikiwa kufanya naye kazi kadhaa za uchapishaji.

Chanzo chetu kinaonesha kuwa, Deus, ambaye baba yake mzazi alikaririwa hivi karibuni akidai kuwa mwanae huyo hana elimu zaidi ya darasa la saba, katika mawasiliano yake na Bw. Kabwe,alisisitiza pia kuwa yeye ni kijana wa chama kutoka mjini Moshi.Alianza kutuma meseji hizo Oktoba, 2006.

'Kijana wa CHADEMA'

Mallya alianza kwa kujitambulisha kwa Bw. Kabwe kuwa yeye ni kijana wa CHADEMA.

"Mhh. Hata hivyo Brother, mimi ni mmoja kati ya vijana wa CHADEMA," aliandika Mallya akimtumia Zitto Kabwe kupitia blogu rasmi ya mbunge huyo machachari.

'Chakula meza moja'

"...tulikuwa wote kwenye dinner party (hafla ya chakula cha usiku) ya vijana wafanyakazi iliyofanyika Istana Restaurant (mimi Mallya) ni kiongozi wa vijanaMoshi."

Mallya katika ujumbe wake huo ndipo akaanza kumuingia Bw. Kabwe kibiashara.

"Sasa ni mfanyakazi ktk (katika) kampuni ya THE CORPORATE IMAGE kama marketing (masoko) na Graphic Designer (mbunifu wa michoro katika kompyuta)."

Mallya akaendelea: "Kama una kazi yoyote ya printing (kuchapisha) like (kama) tshirts, kaps, wheelcovers, banners, coffee mugs, flayers,etc,."

Mallya aomba kazi

" Nakuomba uwasiliane nami muda wowote nitakufanyia kazi yako vizuri kwa muda mfupi na kwa gharama nafuu sana. Pia tuna embroidery machine (mashine ya kudarizi) yenye high quality (ubora wa hali ya juu).

"Pamoja na kuwa siyo sehemu yake kuacha message ka (kama) hii, niwie radhi ndugu yangu mpendwa. Email yangu ni deusmallya@yahoo.com," alimaliza Mallya.

Katika blogu hiyo, Kabwe hakuonekana kumjibu chochote Mallya mbali ya kuwajibu watu wengine waliomtumia ujumbe katika mada mbalimbali alizokuwa akizijadili.

Alipoulizwa na gazeti hili kwa njia ya simu jana kuhusu 'sms' hizo na kama aliwahi kufanyabiashara na Bw. Mallya kama alivyoombwa kupitia blogu yake hiyo inayopatikana katika anuani ya www.chadema.net/blogu/zitto/, Bw. Kabwe alisema:

"Nina muda mrefu sasa sijaangalia blogu yangu, lakini hata hivyo siwezi kukana kwamba nnamfahamu Mallya. Ni kijana ambaye tumekuwa tukifanya naye kazi katika chama za printing (uchapishaji).

"Sifahamiani naye sana, niliwahi kuonana naye ana kwa ana Mei mwaka huu tu mjini Dodoma na juzi alipokuja bungeni (kabla ya tukio la ajali), alitaka kuonana nami lakini nikamuelekeza aende kwa msaidizi wangu."

Alipoulizwa kama alishawahi kufanyabishara na Mallya kama alivyokuwa ameomba kwenye 'sms' hizo za mwaka 2006, Kabwe alijibu:

"Ndiyo, Mallya tulifanya naye kazi za printing, kwa mfano nilimpa kazi ya kuchapisha kitabu chenye maswali yote niliyopata kuyauliza bungeni na majibu yake, kazi ambayo alishaikamilisha na tumeshakitoa kitabu hicho.

"Pia kuna kazi nyingine tulikuwa tukitaka kumpa ya kuchapisha maswali na majibu ya waheshimiwa wabunge kadhaa wa CHADEMA lakini hata hivyo katika matukio yote hayo sikuwa nikikutana naye, alikuwa akijishuhghulisha na msaidizi wangu anaitwa David Kafalalil, labda umtafute yeye atakueleza zaidi walikutana vipi." Bw. Kafalila hakupatikana alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi.

Ujasusi na kukutana na Wangwe

Akimzungumzia Mallya na tetesi za kuwa ni jasusi, Bw. Kabwe alisema hakumfahamu sana lakini anafahamu ndani ya CHADEMA alikuwa akifanya shughuli kadhaa za uchapishaji na hata mara ya mwisho kuna kazi alikuwa akitaka kumchapishia marehemu Chacha Wangwe na ndio maana wakawa wote.

"Huwa sipendi kutoa conclusion (hitimisho) kuhusu namna ninavyomuona mtu. Mallya sikumfahamu sana kama nilivyosema hivyo kuhusika kwake na masuala hayo (ujasusi) siwezi kujua, nampa benefit of doubt (hamtilii shaka sana)."

Kuibuka kwa hisia za Mallya kuwa ni jasusi kunaweza kumfanya kuonekana kuwa alianza siku nyingi kujipenyeza kwa viongozi wa CHADEMA, hata hivyo Jeshi la Polisi nchini, lilisema wiki hii kuwa ushahidi uliowasilishwa kwao na viongozi kadhaa wa upinzani ukimhusisha kijana huyo na ujasusi, haujitoshelezi.

Bw. Mallya kwa sasa ameshtakiwa kwa makosa ya kuendesha gari kizembe na kusababisha kifo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi, Dodoma.
 
Mimi nilisema hapa mapema kabisa kwamba huyo kijana Deus Mallya ni mjanja mjanja sana na hakuna la kuficha kwamba amepitia kwingi kabla hajafikia hili ambalo polisi hawataki kabisa kusikia habari ya kulifanyia kazi.

lingine mimi nilisema wazi kwamba tusitegemee lolote kutoka kwa hawa mbwa wa mafisadi maana hawawezi kuwabwekea mafisadi wakati wao ndio wanaowalisha. Kwa vyovyote watawabwekea na kuwakimbiza vibaya tena kuwatia meno ikiwezekana hao wapita njia wanaojidai kwamba wanageuza geuza macho kuangalia shughuli za mafisadi. La msingi nilishauri tufuge mbwa wetu wa kutulinda ama basi tuanzishe kampuni ya kuuza vyakula vya mbwa kisha tuanzishe urafiki na mafisadi, tutakuwa tunawauzia vyakula vya mbwa halafu baadaye tunawauzia kimeta wanakufa taratibu wakati sisi tunawapa mbwa wetu protein ya kutosha.

Mwisho wa siku tunawasikisia mafisadi mbwa wetu, wanakimbizwa hadi uganda na ikibidi wanakimbizwa hadi nje ya Uganda. Nguvu na nia tunayo, ni kwamba tu hatujaweka mawazo yetu pamoja, tunaishia kuongea tuuuu....!
 
Hivi kumbe Bwana Malya ni Mchaga?

Nimekuwa nikijiuliza sana kujua ni nini Polisi wanakitafuta kuhusiana na kifo hiki,Ajali nyingi zimetokea ila hakuna ahata siku moja walipofanya uchunguzi wa kina hadi kwenda kuwahoji familia yake.


Mie nadhani Uchaguzi unaokuja wa Tarime utakuwa ni wa kihostia na uliojaa Propaganda ambazo hazijawahi kutokea.Nafasi ya CHADEMA wana nafasi finyu sana..
 
Hivi kumbe Bwana Malya ni Mchaga?

Nimekuwa nikijiuliza sana kujua ni nini Polisi wanakitafuta kuhusiana na kifo hiki,Ajali nyingi zimetokea ila hakuna ahata siku moja walipofanya uchunguzi wa kina hadi kwenda kuwahoji familia yake.


Mie nadhani Uchaguzi unaokuja wa Tarime utakuwa ni wa kihostia na uliojaa Propaganda ambazo hazijawahi kutokea.Nafasi ya CHADEMA wana nafasi finyu sana..

Gembe,
Huo uchunguzi sijui utaishi wapi, hapa atabanwa mtu ilimradi jina la mtu lichafuliwe tu.
 
Mimi nilisema hapa mapema kabisa kwamba huyo kijana Deus Mallya ni mjanja mjanja sana na hakuna la kuficha kwamba amepitia kwingi kabla hajafikia hili ambalo polisi hawataki kabisa kusikia habari ya kulifanyia kazi.

lingine mimi nilisema wazi kwamba tusitegemee lolote kutoka kwa hawa mbwa wa mafisadi maana hawawezi kuwabwekea mafisadi wakati wao ndio wanaowalisha. Kwa vyovyote watawabwekea na kuwakimbiza vibaya tena kuwatia meno ikiwezekana hao wapita njia wanaojidai kwamba wanageuza geuza macho kuangalia shughuli za mafisadi. La msingi nilishauri tufuge mbwa wetu wa kutulinda ama basi tuanzishe kampuni ya kuuza vyakula vya mbwa kisha tuanzishe urafiki na mafisadi, tutakuwa tunawauzia vyakula vya mbwa halafu baadaye tunawauzia kimeta wanakufa taratibu wakati sisi tunawapa mbwa wetu protein ya kutosha.

Mwisho wa siku tunawasikisia mafisadi mbwa wetu, wanakimbizwa hadi uganda na ikibidi wanakimbizwa hadi nje ya Uganda. Nguvu na nia tunayo, ni kwamba tu hatujaweka mawazo yetu pamoja, tunaishia kuongea tuuuu....!

Mkuu hapo sijakupata una maana................... au?
 
polisi wanatakiwa kufanya uchunguzi wa kina wa kila ajali hsa ile inayohusisha kifo. ......na iwpo huko nyuma hawakufanya hivyo basi walikuwa hawawatendei haki familia za waliofiwa.
 
MOD Hii sio part of Closed topics?
wewe ndiyo huwa unafunga thread?

hii itaendelea kuwapo mpaka pale nitakapoomba niifunge..

Isaya Mwita,

Mie nina uhakika hiki kifo ni mtaji wa kisiasa na umetafutwa kwa muda mrefu sana,na lazima mtu ahusishwe na hili ili uchaguzi uwe rahisi kwa chama Flani.

Kwanza ni habrai yenyewe kwammba Malya nimtu wa Moshi ni mbinu iliyotumiwa tena kuendelea kuweka mazigira mazuri zaidi,Na kwa taarfa niliyoipata hivi jioni kutoka Nyumbani ni kwamba uchaguzi utafayika ndani ya miezi miwili kutoka sasa na watu wa NEC wameshaanza kuandaa Bajeti.

Sidhani kama kuna baadhi ya viongozi wa vyama wataweza kuthubutu kwenda Kemakorere..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom