Mwawado
JF-Expert Member
- Nov 2, 2006
- 993
- 265
Meseji za Mallya kwa Kabwe zanaswa, Ajitambulisha ni mtaalam wa kompyuta, Aomba tenda ya kuchapisha nyaraka, Siri ya kukutana na Wangwe yabainika
*Ajitambulisha ni mtaalam wa kompyuta
*Aomba tenda ya kuchapisha nyaraka
*Siri ya kukutana na Wangwe yabainika
Na Hassan Abbas
MBINU ya Bw. Deus Mallya, kijana aliyenusurika katika ajali iliyomuua mbunge wa Tarime, Bw. Chacha Wangwe, ambaye sasa anahusishwa na ujasusi, kuwaingia wanasiawa mashuhuri nchini na kujenga urafiki nao, imebainika.
Mbinu hiyo imefahamika kufuatia uchunguzi wa gazeti hili kuzinasa meseji zake kadhaa alizowahi kumtumia Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Bw. Zitto Kabwe, ikiwa ni kabla ya kufahamiana na marehemu Wangwe.
Imebainika Mallya akijitambulisha kuwa ni mtaalamu wa mifumo mbalimbali ya programu za kompyuta katika uchapishaji wa nyaraka na vitu mbalimbali kabla ya kufahamiana na marehemu Wangwe, alijipenyeza kupitia kwa Bw. Kabwe akijinasibu kuwa angeweza kuifanya biashara hiyo vyema.
Kwa meseji zake kwenda kwa Kabwe, ambazo Majira Jumapili linazo, Mallya, alianza 'kumuingia' mbunge huyo kijana na kufanikiwa kufanya naye kazi kadhaa za uchapishaji.
Chanzo chetu kinaonesha kuwa, Deus, ambaye baba yake mzazi alikaririwa hivi karibuni akidai kuwa mwanae huyo hana elimu zaidi ya darasa la saba, katika mawasiliano yake na Bw. Kabwe,alisisitiza pia kuwa yeye ni kijana wa chama kutoka mjini Moshi.Alianza kutuma meseji hizo Oktoba, 2006.
'Kijana wa CHADEMA'
Mallya alianza kwa kujitambulisha kwa Bw. Kabwe kuwa yeye ni kijana wa CHADEMA.
"Mhh. Hata hivyo Brother, mimi ni mmoja kati ya vijana wa CHADEMA," aliandika Mallya akimtumia Zitto Kabwe kupitia blogu rasmi ya mbunge huyo machachari.
'Chakula meza moja'
"...tulikuwa wote kwenye dinner party (hafla ya chakula cha usiku) ya vijana wafanyakazi iliyofanyika Istana Restaurant (mimi Mallya) ni kiongozi wa vijanaMoshi."
Mallya katika ujumbe wake huo ndipo akaanza kumuingia Bw. Kabwe kibiashara.
"Sasa ni mfanyakazi ktk (katika) kampuni ya THE CORPORATE IMAGE kama marketing (masoko) na Graphic Designer (mbunifu wa michoro katika kompyuta)."
Mallya akaendelea: "Kama una kazi yoyote ya printing (kuchapisha) like (kama) tshirts, kaps, wheelcovers, banners, coffee mugs, flayers,etc,."
Mallya aomba kazi
" Nakuomba uwasiliane nami muda wowote nitakufanyia kazi yako vizuri kwa muda mfupi na kwa gharama nafuu sana. Pia tuna embroidery machine (mashine ya kudarizi) yenye high quality (ubora wa hali ya juu).
"Pamoja na kuwa siyo sehemu yake kuacha message ka (kama) hii, niwie radhi ndugu yangu mpendwa. Email yangu ni deusmallya@yahoo.com," alimaliza Mallya.
Katika blogu hiyo, Kabwe hakuonekana kumjibu chochote Mallya mbali ya kuwajibu watu wengine waliomtumia ujumbe katika mada mbalimbali alizokuwa akizijadili.
Alipoulizwa na gazeti hili kwa njia ya simu jana kuhusu 'sms' hizo na kama aliwahi kufanyabiashara na Bw. Mallya kama alivyoombwa kupitia blogu yake hiyo inayopatikana katika anuani ya www.chadema.net/blogu/zitto/, Bw. Kabwe alisema:
"Nina muda mrefu sasa sijaangalia blogu yangu, lakini hata hivyo siwezi kukana kwamba nnamfahamu Mallya. Ni kijana ambaye tumekuwa tukifanya naye kazi katika chama za printing (uchapishaji).
"Sifahamiani naye sana, niliwahi kuonana naye ana kwa ana Mei mwaka huu tu mjini Dodoma na juzi alipokuja bungeni (kabla ya tukio la ajali), alitaka kuonana nami lakini nikamuelekeza aende kwa msaidizi wangu."
Alipoulizwa kama alishawahi kufanyabishara na Mallya kama alivyokuwa ameomba kwenye 'sms' hizo za mwaka 2006, Kabwe alijibu:
"Ndiyo, Mallya tulifanya naye kazi za printing, kwa mfano nilimpa kazi ya kuchapisha kitabu chenye maswali yote niliyopata kuyauliza bungeni na majibu yake, kazi ambayo alishaikamilisha na tumeshakitoa kitabu hicho.
"Pia kuna kazi nyingine tulikuwa tukitaka kumpa ya kuchapisha maswali na majibu ya waheshimiwa wabunge kadhaa wa CHADEMA lakini hata hivyo katika matukio yote hayo sikuwa nikikutana naye, alikuwa akijishuhghulisha na msaidizi wangu anaitwa David Kafalalil, labda umtafute yeye atakueleza zaidi walikutana vipi." Bw. Kafalila hakupatikana alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi.
Ujasusi na kukutana na Wangwe
Akimzungumzia Mallya na tetesi za kuwa ni jasusi, Bw. Kabwe alisema hakumfahamu sana lakini anafahamu ndani ya CHADEMA alikuwa akifanya shughuli kadhaa za uchapishaji na hata mara ya mwisho kuna kazi alikuwa akitaka kumchapishia marehemu Chacha Wangwe na ndio maana wakawa wote.
"Huwa sipendi kutoa conclusion (hitimisho) kuhusu namna ninavyomuona mtu. Mallya sikumfahamu sana kama nilivyosema hivyo kuhusika kwake na masuala hayo (ujasusi) siwezi kujua, nampa benefit of doubt (hamtilii shaka sana)."
Kuibuka kwa hisia za Mallya kuwa ni jasusi kunaweza kumfanya kuonekana kuwa alianza siku nyingi kujipenyeza kwa viongozi wa CHADEMA, hata hivyo Jeshi la Polisi nchini, lilisema wiki hii kuwa ushahidi uliowasilishwa kwao na viongozi kadhaa wa upinzani ukimhusisha kijana huyo na ujasusi, haujitoshelezi.
Bw. Mallya kwa sasa ameshtakiwa kwa makosa ya kuendesha gari kizembe na kusababisha kifo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi, Dodoma.
source. Majira. 10.august'08