Jamani, naona kumekuwa na kulaumiana na kunyoosheana vidole hapa. Nawaomba tuombolezeni kwa amani na tuendelee kutoa sala zetu bila kutoa lawama. Ajali ni ajali, na tulifundishwa kuwa ajali haina kinga. Mheshimiwa Mudhihir alipata ajali wakati akiwa anendesha gari zuri sana. Marehemu Sokoine alipata ajali huku akiwa anaendeshwa na dereva professional tena akiwa na walinzi. Tujifunze kukubali matokeo ya kazi ya Mungu, ingawe wakati mwingine matokeo yake huwa magumu kwetu kumeza, lakini ndiyo ilivyo: Kazi ya Mungu haina makosa