Kibri Kitaangamiza Marekani na Israel

Kibri Kitaangamiza Marekani na Israel

Uhodari wa Iran ni upi wakati Israel imewaua zaidi ya viongozi 40 akiwemo Ayatollah Khomenei aliyekufa kiaibu kwa kufukuliwa ndani ya kifusi ? unawezaje kupambana na nchi inayokuzidi mbinu kwenye uwanja wa mapambano ujione una umahiri ?
Yoso,
Uhodari wa Iran kule kupigana na Marekani na Israel na kukataa kudhalilishwa.
 
Uhodari wa Iran ni upi wakati Israel imewaua zaidi ya viongozi 40 akiwemo Ayatollah Khomenei aliyekufa kiaibu kwa kufukuliwa ndani ya kifusi ? unawezaje kupambana na nchi inayokuzidi mbinu kwenye uwanja wa mapambano ujione una umahiri ?
People will die but nation cannot die ,if you know then you will fight to the bitter end.
Leaders can be replaced but nation cannot be replaced you fight to protected it to the bitter end.
America will go ,iran oman and gulf will remain as neighbors ,American empire is coming to its end cycle like any other empires in the past,
Roman empires ,alexander the great ,spanish and portuguese empire,british empire
Now American petrodollar is finish and american empire will decline.
Acha chuki na ubaguzi.
 
KIBRI KITAANGAMIZA MAREKANI NA ISRAEL

Tatizo kubwa la Marekani ni kibri.

Hiki kibri kimewaelemea kiasi hawawezi kuwaza kama binadamu mwenye uwezo uliokuwa na kikomo.

Hata hapa walipofikishwa kutafuta amani kwa mazungumzo na diplomasia bado hawajatambua kuwa wao si washindi.

Halikadhalika hawajatambua kuwa Wairani ndiyo washindi.

Israel ipo katika hali ngumu kwani wao hawamo katika mchezo.

Mazungumzo ni kati ya wakubwa wawili na wao hawana hata moja katika hayo mazungumzo.

Ujumbe unarejea Washington kichwa chini hakuna cha kuonyesha na hali ni mbaya na inaendelea kudidimia kila kukicha.

Hormuz bado.

Iran imejitolea nafsi yake hadi ushindi wake na heshima yake isimame.

Uislamu upate heshima yake na ulimwengu ujue kuwa Marekani hana nguvu hizo dunia ilidhani wanazo.

Marekani ni nyati aliyeingia ndani ya duka la vyombo vya udongo.

Sasa anavunja sahani na vikombe ovyo.

Ile "long haul strategy" dhidi ya Israel bado ipo.

Iran inajua fika na Marekani inajua pia kuwa vita virefu Israel haiviwezi.

In Shaa Allah tusubiri tuone Capitol Hill itakuja na lipi jipya?
Iran ameshinda !.

Labda maana ya ushindi siijui.

Viongozi wakuu wa Iran wameuwawa.Huo ni ushindi ?.

Viongozi Wakuu walio hai wanajificha kama Digidigi uhai wao ni hisani ya USA & Israel.

Jeshi la wanamaji la Iran limeangamizwa.Meli vita zipo katika sakafu ya Bahari.Huo nao ushindi ?.

Jeshi la anga na ulinzi wa anga wa Iran umeangamizwa.Ni ushindi kwa mujibu wa Ustadhi Mohamed Said.

Iran ya leo ulinzi wa miundombinu ya umeme,madaraja... ni raia !.

Vita ya Iran na USA & Israel unaweza kuinyambusha katika sehemu kuu mbili.
Mosi ni usalama wa Israel iwapo Iran itaachwa kurutubisha Uraniuam.

Pili USA inaangazia suala uchumi na hasa kulinda fedha ya Usd isiangamizwe na Yuan ya uchina.Unaweza kuitazama Venezuela ilichofanyiwa pale hakuna Uislam ni maslahi ya Kiranja wa Dunia.

Wamatumbi hawezi kuona mbali wanakimbilia dini kama sababu kuu ya vita.
 
KIBRI KITAANGAMIZA MAREKANI NA ISRAEL

Tatizo kubwa la Marekani ni kibri.

Hiki kibri kimewaelemea kiasi hawawezi kuwaza kama binadamu mwenye uwezo uliokuwa na kikomo.

Hata hapa walipofikishwa kutafuta amani kwa mazungumzo na diplomasia bado hawajatambua kuwa wao si washindi.

Halikadhalika hawajatambua kuwa Wairani ndiyo washindi.

Israel ipo katika hali ngumu kwani wao hawamo katika mchezo.

Mazungumzo ni kati ya wakubwa wawili na wao hawana hata moja katika hayo mazungumzo.

Ujumbe unarejea Washington kichwa chini hakuna cha kuonyesha na hali ni mbaya na inaendelea kudidimia kila kukicha.

Hormuz bado.

Iran imejitolea nafsi yake hadi ushindi wake na heshima yake isimame.

Uislamu upate heshima yake na ulimwengu ujue kuwa Marekani hana nguvu hizo dunia ilidhani wanazo.

Marekani ni nyati aliyeingia ndani ya duka la vyombo vya udongo.

Sasa anavunja sahani na vikombe ovyo.

Ile "long haul strategy" dhidi ya Israel bado ipo.

Iran inajua fika na Marekani inajua pia kuwa vita virefu Israel haiviwezi.

In Shaa Allah tusubiri tuone Capitol Hill itakuja na lipi jipya?
Una madini mazuri sana sana sana mdau...
Ila acha udini, vita ya sasa na zijacho ni za KIUCHUMU mdau, siyo udini, hata papa katahadharisha hilo mdau.
Ni viongozi wenye tamaa, wenye kupenda kumwaga damu kwa tamaa na uroho wao na siyo kwa jina la nchi zao..
Endelea kutupa madini bila kujali udini mdau.
🙏
 
Chizi Maarifa,
Pole kwa kumpoteza ndugu yako.

Sina haja ya hapa kujadili kuhusu Uislamu na Ugaidi kwani tutazidisha ubishi usio na maana.

Ushauri wangu kwako ni jaribu kuusoma Uislamu huenda ukashangaa kuona uko mbali mno na Ugaidi unaotangazwa na maadui wa Uislamu.

Ninayo mada niliwasilisha Chuo Kikuu Cha Ibadan mwaka wa 2006 naeleza suala hili ikiwa utaisoma huenda ikakuonyesha upande wa pili wa shilingi:

Mohamed Said: ISLAM, TERRORISM AND AFRICAN DEVELOPMENT ISLAM, TERRORISM AND AFRICAN DEVELOPMENT
Nigeria kaskazini wakristo wanauawa kila siku na wanamgambo wa kiislamu. Juzi hapa kuna shehe ameweka dau la naira milioni moja kwa muislam atakayeweza kumuua mchungaji ambaye amekashifu uislamu.

Tangu mwaka 2000 zaidi ya watu laki 2 wameuawa duniani kwa ugaidi wa taasisi za waislamu. Dini zingine zote kubwa hazifanyi ugaidi dhidi ya watu ambao sio wa dini zao isipokuwa wasilamu.
 
BigBro,
Natoa jibu kwako pamoja na wachangiaji wengine hapa ambao inaelekea wanataabishwa na Uislamu.

Hili ni tatizo kubwa na tunalo nchini kwa miaka mingi kuanzia pale Tanganyika ilipopata uhuru mwaka wa 1961.

Nitaweka mfano hapa.
Historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika inaanza mwaka wa 1929 ilipoundwa African Association.

Waasisi wa chama hiki ni Kleist Sykes, Ibrahim Hamisi, Mzee bin Sudi, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Suleiman Majisu, Cecil Matola, Rawson Watts na Raikes Kusi.

Hapa kuna Waislam sita na Wakristo watatu.

Sitaki kuongeza mengi katika historia hii.

Walipokuja kuandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kama mlivyokuwa nyinyi wao halikadhalika walitaabishwa na majina haya ya waasisi wa harakati za uhuru kuwa yametawala majina ya Waislamu.

Majina haya yakafutwa katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Hayapo popote katika vitabu vya historia yetu.

Sishangai kuona nashambuliwa kwa kuutaja Uislamu hapa.
Hivi mzee Mo unauhakika gani kuwa hao kina Sykes walikuwa waislamu?

Vipi ukiambiwa walikuwa wapagani
 
Huyo mdingi anaonyesha rangi zake halisi sasa,
Ni al shabaab aliyepooza
 
Mimi ni Muislam, na Dini naifahamu kabisaa, hivi vita ni vya kimaslahi ambapo Marekani anaionea wivu wa kimaendeleo IRAN hasa maendeleo ya ya kisayansi na teknolojia. Pia Marekani na Irael wataka kutawala Middle East na wanaogopa Domination ya Iran

Ndio hawapendezwi na Dola Imara ya Kiislam wa kishia iliyopo Iran ila sio sababu ya vita Sheikh
Iran ina technology gani inayoisaidia dunia au wewe binafsi?

Marekani na Israel wamekupa Technology ya simu na mitandao ya kijamii ikiwemo hii JF bila wao isingekuwepo 90% ya vitu unavyotumia kila siku ni Technology ya mzungu wa marekani.

Haya Iran kafanya yepi ki tech unayoizungumzia hadi aonewe wivu nieleweshe
 
Bezo,
Hata mimi sijui.

Labda ni historia ya Marekani ya kuanzisha vita, Laos, Cambodia, Vietnam nk. wakijua watu wasio na hatia pasi na sababu.

Mimi nimepata kuwaeleza haya Marekani uso kwa macho wakati natoa mada ya Ugaidi Chuo Kikuu Cha Ibadan, Nigeria.

Makubwa yalinifika.

Ikiwa utapenda kufahamu nifahamishe nikuwekee video.
Mahdi hawezi kuja mpaka waislam watakapo waangamiza wayahudi. Siku ya kiyama hitafika mawe na miti iseme myahudi kujificha huku ili waislamu wawaue.

Iran ni utawala wa kidini unaoamini huu utabiri,ndiyo maana wanajua hii ni kazi yao kuu ili kutimiza unabii wa dini ya kiislam.
 
Kinachowaconfuse wakristo wengi wa Tanzania,ambao kiuhalisia wengi ni wasomi sana kuliko waislam na hii hupelekea kuonekana WAPUMBAVU ni hiki:-🤣😆😃
1.Iran Ina waislam 97% inaungwa mkono na mataifa yenye wakristo wengi duniani zaidi ya 90% kama Russia,South Africa,Venezuela etc, sasa wao Kila kinachofanywa na UISLAM wao wanakipinga kiwe kizuri kiwe kibaya😆😆
2.wayahudi maadui zao wakubwa ni wakristo kuliko hata waislam,thus why Israel kuna idadi ya waislam mara 9 ya wakristo,lakini wakristo wa bongo wanaiunga mkono mayahudi sababu tu inapigana na Iran yenye waislam wengi😃😄😁
3.Papa ambaye ni kiongozi wa kanisa katoliki,dhehebu ambalo lina wakristo wengi duniani yupo pamoja na IRAN na VENEZUELA,sasa wafuasi wa PAPA wa Bongo hawajui wamsikilize PAPA ama wamsikilize TRUMP🤣🤣
Mpaka hapa umeshathibitisha kuwa ma abdol huwa hamna akili kweli yani shule hamna.

Huyo Iran ana faida gani kwenye dunia hii? Si ni kama Tanzania tu haina faida yoyote duniani ama sivyo?

Faida za marekani si unazishuhudia na kuzihusudu kila uamkapo na ulalapo au huoni?

Na hili oni kuwa Israel kuna waislam mara tisa kuliko Wakristo mbona ni hoja ya kitufudenge sana, hujui hao wengi ni wapalestina kiasili?
Mkristo toka lini akapenda kukaa sehemu isiyo na amani?

Afrika ya kati?
Ebu elezea
 
Hivi mzee Mo unauhakika gani kuwa hao kina Sykes walikuwa waislamu?

Vipi ukiambiwa walikuwa wapagani
Nakfa,.
Hawa ni ndugu zangu nawajua.

Kleist Abdallah Sykes alikuwa Katibu muasisi wa Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislamu wa Tanganyika) 1933.

Kleist alimuoa Bi. Mruguru bint Mussa mwanamke wa Kindengereko shoga wa bibi yangu Bi. Zena bint Farijala mwanamke wa Kimanyema.

Kleist Sykes alikuwa mjumbe wa Maulid Committee hadi kufa kwake 1949.
 
Watoto wa hao waasisi ni kina nani? Walio hai ama wamekufa kwa uchache mzee
 
Nakta,
Watoto wa waasisi wa taasisi gani.
Ni heshima kubwa kujibiwa na wewe Mzee kwa umri wangu huu mdogo sanaaa.

Ila nashangazwa sana inawezekanaje ukawa na umri mkubwa kama wako mzee wangu na bado ukawa na fikra ambazo mimi binafsi naziona ni za mtu mjinga kama ambaye hajasoma n.k (samahani hili neno kwetu wakristo si tusi)

Ila wewe mzee wangu una elimu kubwa sana WHY?
 
Back
Top Bottom