Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Status
Not open for further replies.
 
Au ndio mbio za kugombea urais 2010?maana traditionally wenyeviti wa chama huwa candidates, hii haitanishangaza nakumbuka huko nyuma huyu jamaa alishasema ndoto zake ni kuwa rais.Kila la heri ila kama Mbowe kamind tutarajie mengi siku za usoni.
 
Cha Msingi ni Kampeni Safi ambazo hazitaacha Vidonda wala Visasi kwa Watakaoshindwa baada ya Uchaguzi. Wote Zitto na Mbowe naamini wana Dhamira Safi hata kama hazifanani! Hatuna Haja ya kuogopa kwamba Fulani aweza kuwa ametumwa ( After all hizi ni Hisia za Wapambe) coz kwa nyakati hizi ngumu sana kwa Mamluki kuambatana na wapiganaji wa Kweli. Chadema chagueni Viongozi then watakaopatikana kama ni Makuwadi watafahamika tu within very short time na hakutakuwa na msalie mtume.

For Now Demekrasia iache ichuke Mkondo wake
 
Au ndio mbio za kugombea urais 2010?maana traditionally wenyeviti wa chama huwa candidates, hii haitanishangaza nakumbuka huko nyuma huyu jamaa alishasema ndoto zake ni kuwa rais.Kila la heri ila kama Mbowe kamind tutarajie mengi siku za usoni.

Hapana Ndugu yangu, 2010 Zitti bado hatakuwa na Sifa za kugombea Urais may 2020
 
Au ndio mbio za kugombea urais 2010?maana traditionally wenyeviti wa chama huwa candidates, hii haitanishangaza nakumbuka huko nyuma huyu jamaa alishasema ndoto zake ni kuwa rais.Kila la heri ila kama Mbowe kamind tutarajie mengi siku za usoni.

Hapana Ndugu yangu, 2010 Zitto bado hatakuwa na Sifa za kugombea Urais may 2020
 

Kweli Safari bado ni Ndefu, ulitaka awe kwanza makamu mwenyekiti?
 
Sasa naanza kukuelewa
 

Jana nililitaja kundi la 'Vijana Wajinga' kwa majina na wengine wamenijibu kwa sms na simu wakinitaka yaishe kwani wanadai eti tunaelekea kufichua siri nyingi zaidi.

Mbali ya kuwataja wawili kati yao wamejitokeza katika jamvi jana na leo na mmoja nikamjibu. Soma sawasawa kaka. NALIONA ANGUKO LA ZITTO linalokuja. Anguko hilo litakuja akishinda uenyekiti au la, akiwa Chadema au nje ya chama hicho. Tatizo si kama atashinda au la bali ni matokeo ya kuingia kiringeni kwa staili yake ya kuvizia akifunga goli toka nje ya uwanja. Subirini muone.

Tanzania Daima inajiendesha kwa faida kubwa. Haitegemei ruzuku au uenyekiti wa Mbowe. Hata hivyo nguvu ya kambi ya upinzani (demokrasia madhubuti) ni sehemu ya uimara wa Tanzania Daima na uhalali wangu wa kuendelea kuwapo hapa. Sina njaa, sina sababu hata moja ya kujikomba kwa yeyote zaidi ya kusimama katika kile ninachokiamini. Niko tayari kubakia peke yangu kwa kuwa na mtazamo ambao ni unpopular. Tumeona vitu popular nchi hii na vyote mwisho wake vimetuingia nyongo...Mrema...Mkapa (Baada ya kuwa Rais na kabla ya kumaliza muda wake)...Kikwete na sasa Zitto...Tusubiri tuone. Amkeni mashabiki
 

Duh. Huu mparanganyiko kweli. Zitto na Kibanda wote wanatumiwa na RA! History will judge u wrong and us right. Leo tumetofautiana na Zitto, huyo RA yuko wapi? Ameshindwa kututumia? Wewe margreth ndiye unayechafua watu.

Waganga njaa wengi huwaona wenzao nao ni waganga njaa. Yaani huyo mtu RA is super human anaweza kumtumia yeyote atakaye. Kwa nini sisi tushindwe kumtumia? Vita tunayopaswa kuipigana ni dhidi ya 'ufisadi dola' au 'ufisadi wa kitaasisi' (state corruption au institutional corruption) unaolitafuna taifa letu kwa namna ambayo haipo katika nchi nyingi duniani, ikijengwa katika mfumo wa CCM kuwa chama dola kilichohodhi mamlaka kwa staili ya vyama vya kikomunisti duniani.

Tatizo letu Watanzania wengi ni mabingwa wa kufikiri kwa ndimi zao
 
Jana nililitaja kundi la 'Vijana Wajinga' kwa majina na wengine wamenijibu kwa sms na simu wakinitaka yaishe kwani wanadai eti tunaelekea kufichua siri nyingi zaidi.

Samahani kaka, Mimi ni kijana na rafiki wa Zitto na pia jana nilikupigia simu nikijaribu kutumia busara kuhusu na mwenendo wako hapa.

Naomba unijibu swali moja hapa mbele ya wanajamiiforum. Je na mimi ni mmojawao hao "vijana wajinga"

Nasubiri jibu lako kaka mwerevu..

omarilyas
 

Mosi: Wewe ni kijana sawa, wewe ni rafiki wa Zitto ndiyo, lakini je wewe ni mwanachama wa Chadema?

Pili: Ujinga ni nini? Mbona kila mtu ni mjinga katika jambo fulani? Marafiki wa Zitto na vijana wa Chadema wasioliona anguko la Zitto lililo dhahiri ni wajinga wa kutoliona hilo. Au nimekosea? Kunradhi.
 
kibanda ni mtumishi wa mbowe hivyo tusimlaumu sana manake anachokifanya yeye ni kufuata matakwa ya bosi wake.
 
Bila kutokea Migogoro Hamuwezi kujuana vilivyo...zinapoteka kashkash kama hizi ndivyo sura halisi ya tunaowaita "wapambanaji" zinavyojulikana....!!!

Kibanda hivi ilishindikana nini kumuita Zitto pembeni(kisiri) mkadiscuss nae hio mikakati mliyonayo wazee wa "chama" kabla hujaenda Public...? Ulichokifanya japo kwa uoni wako its OK, lkn unapokwenda Public hapo ndipo upolikoroga...!!!

Pia Tatizo la Zitto unapolihamisha kwa vijana wote wa Chadema....huo ndio Mtaji wenu...then unawaitwa Wajinga...is it?..Mtu kama Dr.Kitila unajaribu kuhoji PHD yake...Sijui kama wewe hata "degree" unayo...!!!...kama unaona PHD kazi nyepesi hebu itafute kwanza uone Jasho lake...!!!

Huku ukimponda Kitila Kuhama CCM kuja Chadema kuwa Mamluki...the same mmechukua Selasini na Rwekatare....How then?..!!!..hapa una send message nzito kwa wale ambao walishaanza kujenga Iman ya kuhamia Chadema...wafikirie mara2 kabla ya kuja "kundini"

Kuhusu Uchanga wa Zitto..si uChanga wa Zitto, bali ni Uchanga wa Chadema...!!! Ulitakiwa Ujifunze CUF namna wanavyowaondoa wale wanaowaona ni "Virusi" na huo ndio ukomavu wa Kisiasa....!!!

Wale wanaosema Zitto miezi 3 hajafika Makao Makuu na hataki kukutana naViongozi wakuu....Hili dai kubwa sana...Nakumbuka wakati Prof.Lipumba anaingia buguruni aliwakuta wazee wengi wamejaza ofisini buguruni hawana kazi za kufanya kazi kupiga soga, akawaambia watoke waende kwa wananchi...nyie leo Zitto anakwenda kwa wananchi...mnataka akae ofisini apokee simu...is it?au ndio policy za kusubiri Chopa kuwafikia wananchi...?

By the way nionavyo Ka-Mgogoro ndani ya Chadema either baina ya "Wazee" na "Vijana" au Baina ya "Wasomi wa Hali ya Juu" na Wale walioishia "Vidato/certificate"
 

Du hii balaa!Obama nae katoka ubunge hadi uraisi bila kupitia uwaziri leo inakua ajabu Zitto kugombea uenyekiti kisa ni naibu katibu
 

Naomba kama inawezekana utuletee kanuni za kuchukua na kurudisha fomu za uongozi ndani ya CHADEMA hapa ili nasi tuone jinsi Zitto alivyokwenda kinyume na taratibu.

Endapo haiwezekani basi tupe maelezo ya ndani yaliyopelekea wewe kufikia hiyo tamati.
 

Ulitakiwa kulijua hili mapema kabla hujamwaga pumba zako kwenye TD. Makala yako haikuwa/haina/ na haita kuwa tija yeyote katika ujenzi wa demokrasia katika vyama vya upinzani nchini. If anything imeleta mtafaruku usio na lazima.

Tatizo unamtumikia mtu ulie mzidi kwa shule lakini unakubali kufuata ushauri wake m-bovu muradi upate ugali wako aibu kubwa fani imevamiwa!
 
Pamoja na mapungufu ya Kibanda,
Waanzilishi na wachangiaji wengi wa thread hii ni wale wa chama cha kijani ..............😀
Chadema mpo??????????????????
Mwenye macho na masikio na asikie!
 

- Aaahggggrrr!, I love JF maana kila ukihesabu vichwa ni vigumu kuvimaliza idadi!

Respect.


FMEs!
 
Philosopher mzuri siku zote huyaishi anayoyahubiri,nionavyo ni kwamba Chadema inatekeleza dhana yake ya Demokrasia na Maendeleo kwa vitendo,Zito Kabwe anataka kuwaonyesha Walimwengu kwamba demokrasia inayozungumzwa chadema haipo kinadharia bali kwa matendo dhairi yanayopaswa kuigwa na vyama vingine na vijana wengine wa kitanzania.Binafsi nampongeza Zito kwa kuitendea haki demokrasia.Kiukweli Kwa mtu makini hawezi kuibeza kazi aliyofanya Mbowe katika Chadema,lakini kanuni ya demokrasia inataka uongozi wa kupokezana.Watanzania tutakuwa tunafanya makosa makubwa sana tukianza kumuhukumu Zito kwa umri wake badala ya uwezo wake wa kuongoza.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…