Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Status
Not open for further replies.
..Mbowe awaachie wengine wajaribu.

..nadhani akiondoka Mbowe basi hoja za kuiandama Chadema kwa Udini na Ukabila zitakwisha.

Sio mbowe anayeandamwa na hoja ya udini na ukabila ni Chadema ndio inayoandamwa. Atoke mbowe aje zitto bado Chadema itaandamwa, as long as it is a threat to CCM. Spin doctors wamejaa CCM, vingunge kwa vijana, hawawezi kuishiwa cha ku-spin eti kwa vile mbowe ameondoka.
 
Kibanda anatetea ajira yake ndio maana amekuwa mpiga debe wa bosi. Kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa Bongo mimi simlaumu Kibanda lazima atetee ugali wake ili watoto waende choo.

Njaa mbaya sana!
 
hivi kumbe kibanda mwenyewe ni mwanajamvi?mzee kama ndiyo ww fikra zako hazijakomaa kwa yale uliyoyaandika,vinginevyo nashawishika kusema tena kwa uchungu kwamba we pia fisadi
Amejiunga jana kwa ajili ya mjadala huu wa Zitto vs Mbowe.
 
Kibanda anatetea ajira yake ndio maana amekuwa mpiga debe wa bosi. Kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa Bongo mimi simlaumu Kibanda lazima atetee ugali wake ili watoto waende choo.

Njaa mbaya sana!

Kwa hiyo unatetea uozo huu? Unatetea mtu anayelipwa na Mbowe kuandika hii story iliyo one sided bila hata kutoa disclosure kwamba ni muajiriwa wake? Unatetea hii obvious conflict of interest?

Eti kisingizio "Bongo"?
 
Mengi yamesemwa, mengi yameandikwa lakini ukweli unabaki pale pale kwamba, katika hili Tanzania Daima linaiangalia kambi ya upinzani zaidi kuliko Mbowe au Zitto. Hatuko tayari kuona upinzani ukidhoofishwa na nguvu yoyote ile iwe ni ya kutoka ndani au nje ya Chadema. Yeyote anayetishia kuiua Chadema au CUF kwa njia zozote zile wakati tukiwa na vyama hivyo viwili pekee vyenye kuonyesha mwelekeo kwa sasa, wapenda mageuzi hatuna budi kukemea tena kwa sauti kali na wakati mwingine kwa lugha isiyo ya kawaida.

Uandishi wa habari hauna itikadi bali unaongozwa na dhana ya ukweli 'TRUTH' ambayo hata wanafalsafa wangali wakitafuta kujua maana yake halisi kwani UKWELI nao ni relative na si objective.

Mhariri Mtendaji kwani Zitto kugombea kiti hicho ni kuiua Chadema? kukemea kwa sauti ya ukali ndio haya maneno uliyompa DR.KITILA MKUMBO?

mimi nadhani kwa kazi hii unayomfanyia Mbowe naona utaongezwa mshahara kwani maneno uliyompa Kitila Mkumbo yamenifanya nihisi kuwa Chadema ina wenyewe.
 
Kanda,

I guess Kibanda hakuwa too careful ku mask intentions zake.Kwa hiyo Zitto kushindania uenyekiti kutadhoofisha chama? Isn't this so CCM? Isn't this type of non democratic leadership the type of style that makes CCM so stale?

Watu tunategemea CHADEMA ionyeshe demokrasia ya kweli (look, democracy is even in the party's name) sasa haya mambo ya kuleta UCCM na Usultani/ Ukikwete (mtu anayepalilia kugombea peke yake) yanatoka wapi?
 
Kibanda,
Mkuu hapa ume smell.. kubali yaishe, kuendelea kubishana na mizunguko wala haitasaidia kitu, ndio kujifunza mkuu wangu kesho haitatokea tena.. Ukirudia makosa kama haya hapo tena itatuchosha sote!
 
- Mkuu Kibanda kama kweli unaajiriwa na Mwenyekiti wa Chadema kwenye biashara zake binafsi, kama ninavyoona wengi hapa wakisema then please drop this debate, maana huna moral authority kabisaa mkuu wangu na hii subject!

- Ni ushauri wa bure tu ndugu yangu, na tafadhali sana usipotee in the future maana tunakuhitaji sana hapa JF, nakuonea huruma sana maana you have good intentions za kutetea mlo wako, ila tu huna enough reasonable facts za kutetea unachokitaka, infact wala hakiko clear exactly ni nini hasa? Halafu picking up on Kitila, ni the worst strategy ndani ya hii forum.

- Halafu what you call the truth kwenye uandishi wako, huna facts za kuutetea hapa, just drop it ili uwastahi Zitto na Mbowe, na hasa Chadema.

Respect.

Field Marshall Es
 
Wagombea wa nafasi hii wangekuwa zaidi ya wawili tungekuwa tunaongea lugha nyingine nadhani.

Mjadala huu umenifungua macho sana... Lakini kuna kitu tunaandaa, kitafungua ukurasa mpya kwenye siasa za Tanzania!

- Saafi sana mkuu na tupo pamoja sana hapo, na ubarikiwe! by the way mkuu can you imagine wahariri wote wakubwa bongo wangeletwa hapa kuchambuliwa article zao, si tungelisaidia sana taifa letu jamani, I mean mind you gazeti lenye hiyo habari hapo juu limesomwa sana na wananchi, ambao siku zote wananyimwa the otherside yaani critique kama hii ya JF, ambayo ni the best ever kifungua macho,

- Unajua why JF ni the best kifungua macho? Ni kwa sababu sisi JF we have nothing to lose never, na hatulipwi na yoyote kutoa maoni yetu,

- Mkuu Kibanda, for once jaribu kuwasiliza watazamaji wa mchezo, badala ya wachezaji!

Respect.

FMEs!
 
Pamoja na kuwapa THANKS wachangiaji wengi, hasa Kitila na Kibanda, kwa kweli sijapendezwa kabisa na muelekeo wa mjadala huu ambao uko LIVE kwa maana ya kwamba wanasoma hata watu ambao baadhi ya mambo humu hayawahusu ama yanawasaidia kubomoa mambo ambayo wengi wetu tunayasimamia na hata wachangiaji hao wanayasimamia.

Kibanda ni kweli kwamba ukweli ndio msingi mkuu wa uandishi wa habari, lakini unafahamu fika kwamba si ukweli wote unaoandikwa kwa kuwa katika uandishi na katika maisha, utakumbana na mambo mengi mno, mengine huwezi na wala hutathubutu kuyaweka hadharani kama hapa na pengine hutamnong'oneza mtu yeyote hata mtu wa ndani ya familia yako hadi kifo. Tunayo/unayo mengi ambayo utakufa bila kuyasema ama kuyaandika.

Sasa katika hii mada, nimegundua kuna tatizo kubwa sana ambalo pengine kwa kujua ama kutojua linatupunguzia nguvu muhimu sana katika ujenzi wa demokrasia yenye maslahi kwa taifa. Naungana na mwana JF mmoja anayetaka kuwepo kwa dikteta mwenye visheni ili kupunguza mambo kama haya.

Kibanda katika hili, hujasaidia upinzani, hujaisaidia Chadema, hujamsaidia Mbowe, hujamsaidia Zitto na wala hujatusaidia sisi tulio nyuma yako kiimani. Sababu ya maneno yangu ni wazi kwamba maneno yako yanatoa picha mbaya sana hata kwako binafsi, jambo ambalo mimi nikiwa rafiki ya wahusika wote wakuu katika mada hii NAUMIA SANA.

Sioni maslahi ya kuwakosa wote, Zitto, Mbowe, Kitila na Kibanda, lakini katika hili dalili si nzuri kabisa na maandiko yako Kibanda yalipaswa kuzingatia kuwaunganisha watu hawa watatu na wewe ukiwa wa nne na si kuzidi kujenga ufa. Hapa umeongeza ufa.

Kuna watu uliowataja kama Mnyika na John Mrema ambao wana mengi mazito ndani ya vifua vyao na hata Zitto na Mbowe wana mengi ndani ya vifua vyao, lakini hakuna kati yao aliyevianika humu, bali kwa uchache baadhi wamekuwa wakijadiliana na wasiri wao ukiwamo wewe. Wahusika wote hao hapo juu akiwamo Zitto wamekuwa wakikushirikisha katika mambo mazito na ya siri na hivyo maandiko yako ni lazima yawe na mipaka kaka.

Mwisho naomba tumwamini Zitto kwa dhamira yake. Naamini anachosema kwamba hana nia mbaya na chama chake na Kibanda unajua kwamba hata ikitokea kwamba yeyote (hata Zitto) akiwa na nia mbaya na Chadema au upinzani kwa sasa atapotea njia hata bila kusema ataanguka ama atakwisha, Anguko liko pale pale kwa yeyote anayeshindana na upepo. Tumeshuhudia jinsi CCM inavyopata shida kushindana na upepo na vivyo hivyo hakuna mwanasiasa makini kama Zitto atakayekubali kushindana na upepo.
 
- Duh! Mkuu Halisi, this is it, naenda kulala sasa, maana hii yako ni the end of the story line, mshaurini sana Ndugu Kibanda kwamba hapa JF sio mahali pa mchezo wa kampeni za siasa! Nafikiri coming form you labda ataelewa zaidi.

Respect.

FMEs!
 
Uchaguzi huu lazima uzingatie hali halisi ya nchi kwa sasa. Wananchi wamechoshwa sana na CCM, na wanategemea Chadema iwakomboe toka kwenye makucha ya CCM.

Wakati wa kuchagua viongozi wa Chadema, lazima kwenye background tunawaza ni nani kati yao ni Presidential Material. They are, in my considered opinion, Slaa and Mbowe, in that order.

Si lazima Slaa awe mwenyekiti wa Chadema, lakini ni muhimu Slaa awe ndiye mgombea urais kwa ticket ya Chadema.
 
Haya ni majibu yangu kwa Dk. Kitilya Mkumbo.

Wakati mwingine unaweza ukajiuliza hivi hizi PhD huwa zinatolewa kwa watu wenye uwezo kiasi gani, hasa unapokutana na wasomi wa ajabu ajabu. Siwezi kuamini kwamba miaka mingi baada ya kumaliza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi leo hii Daktari wa Falsafa ndugu yangu Kitilya ambaye amehamahama vyama kadhaa vya siasa akizungumzia suala la itikadi au falsafa. Huu ni mzaha wa hatari kwa msomi.

Kitilya amepata kuwa kada wa CCM na amepata kuwa Chadema pia ambako yuko sasa. Inavyoonekana huyu jamaa ni mtu anayefanya mambo yake pasipo kuongozwa na falsafa yoyote, ingawa yeye mwenyewe anapata jeuri ya kuwaonyesha wenzake njia kuhusu masuala yanayohusu falsafa.

Kumbe wewe si msomaji mzuri wa makala za Jenerali Ulimwengu ambaye umemtaja hapo juu. Siku zote Jenerali amekuwa akiwalalamikia ninyi wanasiasa kwamba mmepoteza mwelekeo kwa sababu mnaongozwa na matakwa ya kimadaraka na fursa za kimaslahi mnapoenda katika vyama vya siasa badala ya itikadi.

Ni jambo la kusikitisha kwamba kumbe wewe na Zitto Kabwe mliamua kujiunga na Chadema (mwenzako alijiunga akiwa na miaka 16 akiwa hajafikia umri wa kupiga kura au wa kuwa na maamuzi ya busara) mkiwa na lengo la kuitikisa hata itikadi ya chama hicho? Kwa hiyo mlijiunga na Chadema kwa sababu mlikuwa na fursa ya kufanya hivyo au kwa sababu mlivutiwa na haiba binafsi ya wazee wa chama hicho kama akina Mtei na wengine hata kabla hamjasoma katiba na itikadi za chama mnachotaka kujiunga nacho. Zinakwenda wapi siasa za nchi yetu ambazo kumbe hazina dira?

Katika hili la Itikadi na Falsafa naweza nikasema wazi kabisa kwamba kumbe Kitilya na Zitto ni 'mamluki ndani ya Chadema' na kwa hakika wanapaswa kuanza kuchunguzwa mienendo yao ili isije ikawa ni mapandikizi hatari katika chama. Future will Tell.

Nayatambua mabadiliko si ya kiitikadi bali ya kimtazamo na kisera ya vyama vya Democratic, Labour (New Labour), Republicans na vingine vingi kikiwapo Chama Cha Kikomunisti cha China. Nimesoma kwa ufasaha Thatcherism na Reaganism. Ni mwanafunzi mzuri wa falsafa za Hegel, Lenin, Karl Marx na wanazuoni wengi. Nimesoma ujamaa wa Nyerere na The Fabian Socialism aliko copy ujamaa wake na namna alivyoukarabati kutoka katika ukomunisti na Ufabian akirejea misingi ya ujima na kuiboresha. Mimi ni mwanafunzi mzuri wa Historia kwa level yangu.

Nakushauri Dakta Kitilya kwamba ni makosa kuangalia jina la chama na kuvutiwa nalo kabla haujasoma itikadi ya msingi ya chama husika. Kosa hili ndilo lililokufanya katika utu uzima uhame mara CCM mara Chadema na ukaondoka baada ya kukosa madaraka (Lilikupata ukiwa UVCCM). Hii ni fedheha ya kisiasa ambayo tunaivumilia kwa sababu tu ya uchanga wa demokrasia wetu.

Viongozi wa chama kimoja cha siasa wanaweza kutofautiana katika mitazamo, sera, mbinu na mipango na si katika itikadi. Haiwezekani mjamaa na bepari, mmoja akawa mwenyekiti na mwingine Naibu Katibu Mkuu ndani ya chama kimoja. Huu ni upofu ambao ndiyo msingi mkuu uliosababisha Zitto Kabwe kwa ushauri wako wewe na vijana wengine kadhaa niliowaita wajinga ndani ya Chadema aamue kugombea kwa staili hii ya kakakuona.

Napenda tu kukueleza dakta kwamba falsafa ya kimantiki inayoniongoza katika uandishi wangu siku zote ni 'ukweli kwanza'. Journalism haina ya leo imepita zama za cold war, kwa hiyo katika masuala kadhaa hakuna leftist writers au rightist writers kama unavyotaka iwe.

Ni kweli kwamba siku zote nimekuwa nikimuona Zitto kuwa ni hero wangu. Ukweli huo hautabadilika bado itabakia pale pale kwamba japo nimempinga kwa hili kama nilivyopata kumpinga kwa mengi tu, ninamheshimu.

Muulize Zitto atakueleza, hii ni makala ya pili au ya tatu kumkosoa (si kumshambulia), nimepata kufanya hivi huko nyuma kupitia safu yangu ya kawaida ya Tuendako kila Jumatano. Nimepata kumkosoa mara nyingi katika mazungumzo ya ana kwa ana au ujumbe wa simu ya mkononi ama yeye mwenyewe au kupitia kwa watu wake wa karibu na mara kadhaa kupitia kwa mama yake mzazi.

Kwa sababu hiyo basi, mimi si kasuku ambaye Zitto akiimba wimbo hata kama wimbo huo ni wa matusi nicheze eti kwa sababu Zitto ni hero wangu. Nitakuwa mpumbavu sana. Na hakika wenye mawazo ya namna hiyo ni watu wa kuwasikitikia.

Nimepata kumpinga Mbowe pia katika makala zangu nyingi na Zitto Kabwe na wengine ambao wamekuwa wakisoma makala zangu wanalitambua hilo.

Kimsingi nilikuwa nikisubiri nikuone ukichangia na nilipoona uko kimya zaidi ya kutuma ujumbe mmoja tu wa kunikejeli ukinitaka nichukue fomu ya kugombea, niliamua kuingia na kuwapa darasa baadhi ya vijana wajinga ndani ya Chadema kama wewe, ambao kwa sababu ya upofu wenu mmeamua kumfanya Zitto ngazi ya mafanikio yenu ili akipata nafasi ya uenyekiti ambao kwenu mmeufanya ni ulaji, aweze kuwateua kushika nafasi za juu. Huku ni kumuangusha Zitto sana.

Napenda niliweke hili wazi kwamba, siupingi hata kidogo uamuzi wa Zitto kugombea uenyekiti wa Chadema. Ninachokipinga ni timing yake na kimsingi utaratibu alioutumia kugombea kiti hicho ambao gazeti ninaloliongoza limeuita 'kakakuona'.

Nimeshangazwa na kushtushwa na uamuzi wa Zitto kuingia mitini na akachukua fomu 'mafichoni' na akairejesha kupitia kwa Msafiri Mtemelwa. Huu si ujasiri wa kiuongozi ambao Zitto alipaswa kuwa nao.

Staili hii ya Zitto ambaye anapokuwa Dar es Salaam anafanya vikao vya usiku na mchana na wanahabari (nikiwamo mimi) na wanasiasa wengine wa CCM na CUF huku akikataa kukutana na viongozi wenzake wa Chadema wakiwamo wakuu wake kama Mbowe na Dk. Slaa ni wa kusikitisha kama si wa kukemewa.

Mimi ni mwana habari, ninazijua hisia za viongozi wengine wa Chadema ambao ni watu makini kabisa kama Dk. Slaa, John Mnyika na John Mrema juu ya mwenendo huo wa Zitto. Hawa jamaa wote pamoja na kutambua uwezo mkubwa wa kuona mambo alionao kijana mwenzao huyo wanaujua udhaifu wake kama kiongozi (si kama Zitto)> Naamini wameamua kukaa kimya wakiogopa kukijeruhi chama chao. Mimi sina sababu ya kukaa kimya ni wajibu wangu kuandika hata kama nitapingwa na maelfu. Msome Ibsen 'The strongest man is the one who stands alone'

Ni kweli kwamba mimi ni judgemental. Inaonekana unaliogopa neno anguko ambalo ni linafafana na la Kiingereza la 'fall' ambalo ni la kawaida katika vyombo vya habari duniani kote.

Si kweli kwamba nimekuwa cynical au sadist. Hata hivyo ni kweli nimekuwa judgemental. Huo ni wajibu wangu kama Mhariri Mtendaji. Ninao wajibu wa kusimamia sera ya gazeti na kuonyesha njia. Unatumia maneno poor and unprofessional katika hoja ambazo wewe mwenyewe unaonekana dhahiri kuubeba udhaifu huo.

Mtu anaweza akaanguka na akasimama. Anguko si kifo, ni pigo la kipindi fulani na si la milele. Nashangaa wewe na Zitto mnafanya spinning kupitia JF ili kutimiza malengo yenu ya kisiasa ambayo kwa mtazamo wangu ni ya hatari (Nasisitiza huu ni mtazamo wangu).

Sipendi kujisifu, ninayo rekodi ya kuyaona matukio mengi na makubwa ya kisiasa kwa miaka mingi kabla hayajatokea. Waulizeni wanasiasa waliowatangulia ambao baadhi yao walipuuza maandishi yangu kwa matusi na kejeli kabla ya kufikwa na mianguko ya namna hii hii ambayo naiona inataka kumpata rafiki yangu na mwanasiasa ninayemuunga mkono siku zote; Zitto Kabwe.

Hata hivyo, yako mambo mengi tu ambayo nimepata kuyaandika kwa makosa na hayakutokea kama nilivyotafakari. Makosa kama haya wamepata kufanya wanazuoni na wachambuzi mbalimbali duniani. Inapotokea hali ya namna hiyo nimekuwa mwepesi siku zote kuomba radhi na kusonga mbele.

Nimemlinganisha Zitto na Mbatia kwa minajili ya kubeba ajenda ya vijana na kwa taarirfa yako, ulinganifu huu aliuanzisha huyo mgombea wako Zitto ambaye kwa maneno yake mwenyewe alipata kuniambia kuwa anasita kugombea ili asije akakiporomosha chama na kukizika kama alivyofanya Mbatia.

Kwa hiyo scenario niliyoanza nayo ni uchaguzi uliomng'oa Marando (aliyeonekana kapitwa na wakati kama Mbowe kwa mtazamo wenu) na kumpa wadhifa Mbatia (kijana kama Zitto zama hizo) na siyo historia ya misukosuko ya wakati wa Mrema. Nadhani Kitiliya somo la 'Comparative Analysis' linakupa shida sana si kidogo.

Unataka nieleze tatizo la Zitto kugombea ni nini? Nimekujibu kidogo hapo nyuma, lakini nianze kusema, tatizo kubwa la kwanza ni kupokea ushauri mbaya kutoka kwa watu wenye nia mbaya kama wewe na wengine walio ndani na nje ya Chadema. Pili 'timing' yake si sahihi kwake yeye na kwa chama chake, tatu msingi wa kugombea kwake ambao wapambe wake wamekuwa wakisema ni kumuonyesha jeuri Mbowe ambaye eti alikuwa na mpango wa kumng'oa.

Ni wazi kwamba iwapo Mbowe alikuwa akifirikia kumng'oa Zitto ndani ya Chadema basi uamuzi huo ungekuwa ni wa hatari kama ulivyo huu ushindani wao ambao umejengwa katika misingi ya chuki, fitina na uchonganishi.

Pili si kweli kwamba kwa kuandika kwa maana ya ku foresee baadhi ya mambo ya mbele (Dhima ya Safu ya Tuendako) hakumaanishi kuwa na wasiwasi bali kumtakia mema Zitto, Mbowe Chadema na kimsingi demokrasia ya vyama vingi iliyoanza kufufuka baada ya kupwaya kwa muda mrefu.

Nimeandika bayana kuhusu anguko la Zitto na si anguko la Chadema nikijua kwa uhakika kwamba Chadema itabakia imara ingawa Zitto na Mbowe wanaweza kuanguka kutokana na uchaguzi. Soma historia ya chaguzi ndani ya vyama duniani kote na uone iwapo haziandamani na mianguko ya watu.

Zitto anasema anataka kukiandaa chama kuchukua dola, dhana ambayo Mbowe amekuwa akiifanya kwa vitendo tangu akiwa mbunge alipoanzisha ziara za kukijenga chama kwa wabunge, kufanya ziara za kitaifa na baadaye akawaleta vijana wasomi ndani ya chama kabla ya kuja na sera mchanganyiko zilizoifikisha Chadema hapa kilipo leo.

Pili, Chadema inapaswa kuepuka aina yoyote ile ya mtikisiko ambao utawalazimisha viongozi wa juu wa chama hicho kuanza kujipanga upya kuendeleza operesheni mbalimbali za chama hicho. Uamuzi wa Zitto kuingia sasa na kwa staili ya 'kakakuona' inatia shaka sana na kwa hakika kama haitadhibitiwa inaweza ikawa 'break' kwa Chadema.

Hivi Kitilya ukiwa msomi ulitaka waandishi wote tuimbe wimbo wa Goo Zitto, Goo Zitto kama ambavyo wana mtandao walitufanyia kwa Kikwete mwaka 2005? Hivi unadhani umaarufu wa Zitto ni kielelezo tosha cha kuwa na uwezo wa kuongoza? Mbona akina Augustine Mrema na Kikwete wamepata kuwa maarufu wakubwa na leo tunaona matunda yake! Hamlioni hilo? Nilidhani makala yangu ingechukuliwa kama changamoto na si dharau.

Angalia Zitto unaanguka, unaangushwa na akina Kitilya, Kafulila, Umar, Msafiri na wengine wengi. Angalia Zitto, saa yako ya ushindi inakuja ndani ya Chadema na hakuna atakayeweza kukuzuia wakati wako ukifika. Leo hii baadhi yetu tumetuhubutu kwa kuwa tunathamini uwezo wako. There's always tomorrow.

Pamoja na barua-pepe nyingi humu za mwandishi Kibanda hasa kutetea waraka wake kwa nini Zitto asishindane na incumbent Mbowe kugombea uenyekiti wa CHADEMA,lkn ukweli unabaki palepale;SABABU ALIZOZITOA mwandishi Kibanda KWA NINI ZITTO ASIGOMBEE UENYEKITI WA CHADEMA ZINABAKI KUWA NI LEGELEGE SANA!

Kwangu bado haja-hit points HATA MOJA zinazonifanya niamini kuwa Zitto HAWEZI kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA na wala chini ya uenyekiti wa Zitto eti CHADEMA haitakuwa bora!Nasisitiza tena SABABU ZA KIBANDA NI LEGELEGE MNO na HAZINA NGUVU YEYOTE KIKATIBA!

Kibanda tuache demokrasia ichukue mkondo wake hasa ukitilia maanani kuwa ndani ya katiba ya CHADEMA hamna sehemu inayomkataza mtu yeyote mwanachama asigombee wala eti ashauriane na incumbent akitaka kugombea!
 
Tatizo haliwezi kuwa Zitto kuchukua fomu kwani ana haki zote za kugombea uenyekiti na amefuata taratibu zote, Dr slaa amethibitisha hili. Mbowe amekakaririwa na magazeti akisema kwamba hana tatizo na hilo. Zitto nae amesema amechukua fomu ili aimarishe chama. Ni vema tukawaamini mpaka hapo watakapokwenda kinyume na maneno yao.

Tatizo nionavyo mimi ni wapambe. Wapambe wa wanasiasa siku hizi kampeni kwao ndio dili. They will go to any length kuhakikisha mtu wao anapita, yote haya kwa sababu ya kulinda maslahi yao ama kutegemea kupewa vyeo mgombea wao akipita. Wanapiga kampeni kama vile uchaguzi ukishapita basi walioshindwa watajitoa kwenye chama na kutokomea kusikojulikana. Hawa wakina RA na EL wako sana hata kwenye vyama vya upinzani. Zitto anatakiwa awe mwangalifu sana kushauriwa na marafiki ambao wanaiona chadema kama kituo cha polisi. Hawajali mustakabali wa chama. Hawa ndio wakina umar na msafiri mtalemwa "vijana wajinga" anayewaongelea huyu mhariri aliyekurupuka wa gazeti la mbowe.

Kibanda amejieleza vizuri sana hapa JF, mimi nimemwelewa. Anamfahamu zitto fika, hilo halina ubishi. Lakini kama kweli alikuwa anataka kukisaidia chadema haya maelezo aliyoyatoa humu angeyaweka kwenye makala yake angeeleweka na hata hiyo heading ya makala angeibadilisha. Alichokifanya ni kumshambulia zitto na kuchochea uhasama uliopo kati ya wapambe wa hawa viongozi wawili. Anaiendeleza hii vita kwa faida ya nani? Mwisho wa siku Kibanda nawe unakuwa kama hao "vijana wajinga", makala yako is very damaging to the party, ungekaa kimya kama bosi wako usubiri chadema waamue wenyewe. Upende usipende gazeti lako ambalo ni la mwenyekiti wa chadema lina influence sana kwa wanachama wa kawaida wa chadema. Kwa kutumia maneno yako mwenyewe "Lina shepu" mwelekeo wa chama....
 
Last edited:
Binafsi niliposikia habari za Zitto kugombea uenyekiti CHADEMA, nilishtuka.

Zitto ni mwanasiasa ambaye ninamkubali sana nchi hii and he can make a very good leader in the future lakini sio siri uamuzi wake wa kugombea uenyekiti CHADEMA si uamuzi sahihi.

Unajua Zitto ana laengo yake kisiasa, ya sasa na baadaye, hivyo uamuzi wake wa kugombea uenyekiti unaweza kumpotezea malengo yango yote kisiasa au kumjenga, lakini kwa kuzingatia umri wake zaidi utampotezea. Kwa umri wake wa 32 yrs now, atalazimika kusubiri takribani 10 yrs later. Hivyo, itamlazimu kwa kipindi hiki cha miaka 10 asiharibu katika uenyekiti wake (kama ataupata), kitu ambachi ni kigumu sana
 
naungana kabisa na Bw Kibanda. Zito ingawa katiba inakuruhusu pasi na shaka lakini wewe bado kabisa kukomaa kisiasa anahitaji takriban miaka mitano zaidi ya kujijenga kisiasa kabla ya kuamua kugombea uongozi wa juu kabisa wa chama.

Zito kama kweli unataka uongozi wa juu kabisa katika siasa unahitaji upate uzoefu zaidi. uwe na subra.
lakini ukiangalia kwa upande mwingine inaweza ikawa ni ujanja wa kisiasa wa chadema kuonyesha kuwa Mbowe nae kapata mpinzani.

Mkuu Barubaru,
umetoa mtazamo wako lakini sijajua kama wewe na wengi wanaohitaji mtu kupata uongozi wa juu wa siasa awe na umri mkubwa na uzoefu mmewahi kujiuliza vema kuwa je awe na sifa zipi na labda uzoefu huwa unapatikana wakati mtu akihudumu katika wadhifa gani, maana kuna watu wanakuwa viongozi makini bila hata historia ya kuwa mabalozi wa nyumba kumi kumi na yawezekana kwa Zitto kuchukua nafasi ya mwenyekiti wa Chadema taifa ndio akawa na huo uzoefu mnaouhitaji.
Nadhani tusisukumwe na fikra finyu na hoja chakavu za watu ambao pengine yanaweza yakawa ni mawazo yao binafsi yasiyo na maana ni kuyumbisha fikra makini za watu ama misukumo mbalimbali kutoka kwa wanaowapa mkate wa kila siku au michezo tu ya kisiasa.
 
hata mimi naona kawahi kiasi chake walau 2014 ndio angegombea yes; 10 yrs ukiwa mwenyekiti lazima mizengwe itakuwa ilikuangushwa kisiasa; alitakiwa awe underground na msimamo wake uonekana; isije ikawa mtu ukipiga kamsimamo fulani watu wakapiga makofi hapo hapo unataka kugombea urais/uenyekiti; no; kama wamepanga is good sasa wanatangazwa lakini kama ana malengo ya muda mrefu; no thanks; amepiga hesabu somewhere kimakosa; anyway ndio demokrasia
 
Kibanda ni kweli kwamba ukweli ndio msingi mkuu wa uandishi wa habari, lakini unafahamu fika kwamba si ukweli wote unaoandikwa kwa kuwa katika uandishi na katika maisha, utakumbana na mambo mengi mno, mengine huwezi na wala hutathubutu kuyaweka hadharani kama hapa na pengine hutamnong'oneza mtu yeyote hata mtu wa ndani ya familia yako hadi kifo. Tunayo/unayo mengi ambayo utakufa bila kuyasema ama kuyaandika.

Sasa katika hii mada, nimegundua kuna tatizo kubwa sana ambalo pengine kwa kujua ama kutojua linatupunguzia nguvu muhimu sana katika ujenzi wa demokrasia yenye maslahi kwa taifa. Naungana na mwana JF mmoja anayetaka kuwepo kwa dikteta mwenye visheni ili kupunguza mambo kama haya.

Kibanda katika hili, hujasaidia upinzani, hujaisaidia Chadema, hujamsaidia Mbowe, hujamsaidia Zitto na wala hujatusaidia sisi tulio nyuma yako kiimani. Sababu ya maneno yangu ni wazi kwamba maneno yako yanatoa picha mbaya sana hata kwako binafsi, jambo ambalo mimi nikiwa rafiki ya wahusika wote wakuu katika mada hii NAUMIA SANA.

Sioni maslahi ya kuwakosa wote, Zitto, Mbowe, Kitila na Kibanda, lakini katika hili dalili si nzuri kabisa na maandiko yako Kibanda yalipaswa kuzingatia kuwaunganisha watu hawa watatu na wewe ukiwa wa nne na si kuzidi kujenga ufa. Hapa umeongeza ufa.

Kuna watu uliowataja kama Mnyika na John Mrema ambao wana mengi mazito ndani ya vifua vyao na hata Zitto na Mbowe wana mengi ndani ya vifua vyao, lakini hakuna kati yao aliyevianika humu, bali kwa uchache baadhi wamekuwa wakijadiliana na wasiri wao ukiwamo wewe. Wahusika wote hao hapo juu akiwamo Zitto wamekuwa wakikushirikisha katika mambo mazito na ya siri na hivyo maandiko yako ni lazima yawe na mipaka kaka.

Mkuu Halisi,

You have nailed the point.........! Respect sana
 
Kwa hiyo unatetea uozo huu? Unatetea mtu anayelipwa na Mbowe kuandika hii story iliyo one sided bila hata kutoa disclosure kwamba ni muajiriwa wake? Unatetea hii obvious conflict of interest?

Eti kisingizio "Bongo"?

Hujaelewa! sitetei uozo kwa namna yeyote ile bali kusema kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa Bongo haina maana kuwa ninan tetea uozo.

If you read between the lines you can see the obvious sarcastical nature of the post!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom