Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Status
Not open for further replies.
Swahiba wa karibu wa Kibanda alikuwa na haya ya kusema kuhusu huyu jamaa



Absalom Kibanda – The editor of Tanzania Daima is really an attack pit-bull that Freeman Mbowe unleashes once in a while. (Deodatus Balile is a pitbull for Rostam Aziz). The problem with Kibanda is the "Mbeya problem". He hasn't gotten over the fact that Mwandosya lost to JK fairly and squarely in 2005.
 
Makala ya Kibanda yalikuwa ni mazuri lakini yalionesha kuwa kwa sasa ni Mbowe peke yake anayeweza kuiongoza CHADEMA na wala si mtu mwingine kitu ambacho si sahihi kwani chama kama hiki kina misingi ambayo anyejitokeza yeyote kugombea ni lazima aisimamie.

Binafsi nadhani kitendo cha kuonesha nia ya kumpinga mwenyekiti wa sasa hakimaanishi kuwa kashindwa kuongoza, la bali ni hali ya kukua kwa demokrasia na kuona kuwa kwa mujibu wa katiba, kila mwanachama anayetimiza sifa kugombea nafasi
.


Demokrasia haipimwi kwa kigezo cha umri wala fedha, demokrasia ni kila kitu
 
- Mkuu Kibanda, again naomba kukuelewa hebu niweke sawa kwa haya maneno hapo juu ulikuwa na maana gani hasa? Je ni maneno yako kweli au?

- Unasema Zitto ajifunze tabia za ki-CCM, halafu tena unakuja na maneno mapya na kuwalaumu CCM kumshinikza Zitto kugombea? Mbona unajichanganya sana mkuu?

Respect

Field Marshall Es!

Hapa Mr Kibanda ndo HUTAJUTA KUJIUNGA JF ila UTAJUTA KUCHELEWA KUJIUNGA JF. Mkuu FMES Respect! Na burudani iendelee.
 
Wakuu nimeona wengi mmesema sana na maoni yenu na hata hisia kali zimechochewa na Kibanda .Kitila , Kibanda, Mbowe , Zitto , Mnyika, Halisi , Mrema John , sisi sote tunajuana wka karibu .Narudia sote tunajuana kwa sura na majina na makazi yetu , sote tuko katika harakati graundini na si JF pekee .Nadhani sasa Kibanda atakuwa ame elewa kwa nini watu hatujapenda maandiko yake hapa.Kibanda umepelekea Mbowe kushutumiwa kwamba anakutumia kumtukana Zitto .Badio naamini Freeman MBowe hawezi kuwa low this much kutumia kampeni chafu through wewe .Nasema bado mimi Mvutakamba siamini ila lolote laweza kutokea .Nadhani sasa urudi tena kwanza sirini waite wote ambao wako involved na makala yako muongee kama wanaume na kuombana msamaha then wewe nenda Public like what you did rekebisha hali ya hewa. Zitto na Mbowe wako OK na hakuna wa kukiua chama ila wewe nadhani unaweza kuwa unatumia tokea CCM ama kwa Mwandosya kuimaliza Chadema.Wana chadema msikubali rafiki yangu wa karibu sana Kibanda wachanganye na kuleta harufu ya mtafaruku kwenye Chama .

Kibanda hawa watu inaonekana wamekuwa wakikutumia kuweka issues kama boss wa gazeti lako sasa uache kutumia nafasi CCM wapande bei ili uwamalize hawa na Chadema kama alivyo fanya yule jamaa wa RA anaitwa Balile nadhani .Tafadhali tuachie chama chetu in one peace na acha kampeni zifanyike wanachama wataamua .

maoni yangu haya .
 
Duh kweli kazi ipo, mjadala ni mkali ila cha kutia moyo wengi tunatofautiana kwa nia njema. Naamini iko nuru mpya mbele, hata Zitto na Mbowe wakitofautiana kwa nia njema ni vyema mno kwa ndio mwanzo wa kujenga.

Kibanda makala yako haikustahili kuandikwa nawe, sikujui ila nakusikia but I had a respect on ur name. umenifanya nianze kukufikiria mara 2.

Lazima kuwe na flat platform ili demokrasia ishamiri.

Chadema as chama kisimame makini na wagombea wafuate na kuamini kwenye haki zao za kikatiba then tutakuwa na mambo mazuri.

To Me I say Gooo Zitto, Gooo Mbowe
 
Kwanza niseme hivi muandishi wa hiyo article anaonyesha dhahiri kwamba maono yake ya kisiasa ni ya mwaka 1950s.

Naomba niseme kwamba mimi ni mmoja wa watu walikuwa wakiomba kwa Mungu Zitto agombee uwenyekiti.
Mwaka 2008 nilipoonana na Zitto, nakumbuka wakati naendesha kuelekea sehemu ambayo tungekutana na watanzania wengine, swali langu likuwa mmoja tuu, WHY Freeman Mbowe ni kiongozi wako?? Zitto alijibu kwamba Mbowe ni model wake na amemkuza kiasiasa. Kitu ambacho nilikubaliana nacho 100%. Na nikamwambia kuna potential candidate ambao wanataka kujiunga na CHADEMA lakini Mbowe ni kizuizi kikubwa sababu ya political strategy zake ni za 1940s.

Niseme kwamba kama Mbowe ataangushwa chini na Zitto basi CHADEMA in future nzuri ahead. Ukweli ni kwamba mwenyekiti ndio strategic planner wa chama, ambaye anatakiwa kuimpose vision and direction ya chama, na Mbowe ameshindwa kufanya hilo. Kama alivyoshindwa Seif and Lipumba.

Nafurahi kusikia Zitto amekubali kuingia kwenye ring na mtu mzima, and that is what i call challenge in politics. Na wale mnalia lia, mezeni piritoni mkalale.

Katika karne hii huwezi kuendesha mchakato wa ushindi kwa kutumia ufisadi as your strategic plan, au kutumia chopper au kuinvest kwenye majimbo ambayo unajua utashindwa. So, Mbowe is a good person i believe, but he is not the agent of change that CHADEMA is preaching.

Zitto if you will win, believe me the number of strong and potential candidate will match behind you and join the forces.
 
Last edited:
Kibanda.
Leo uko kimya nasubiri list ya vijana wajinga wa Chadema.
swali la pili jee Gazeti la Tanzania Daima linaendeshwa kwa nguvu za uenyekiti? au ruzuku za chama ni sehemu ya mtaji wa Gazeti?
maneno mazito uliyompa Kitila Mkumbo yameniacha sina mbavu na wenye Chadema yenu.
Kazi yote wanayoifanya kina Kitila Mkumbo ya kuifagilia Chadema hapa JF bado wanaoneka ni Mamluki? kweli tunatakiwa tusiingie kwenye vyama hivi kichwa kichwa bila kufanya tafiti za kutosha.KITILA somo hilo umesoma?jee mtu kama Mkandara ataaminiwa na Chadema kama akijiunga.
 
Kwangu bado haja-hit points HATA MOJA zinazonifanya niamini kuwa Zitto HAWEZI kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA na wala chini ya uenyekiti wa Zitto eti CHADEMA haitakuwa bora!Nasisitiza tena SABABU ZA KIBANDA NI LEGELEGE MNO na HAZINA NGUVU YEYOTE KIKATIBA!

Kibanda tuache demokrasia ichukue mkondo wake hasa ukitilia maanani kuwa ndani ya katiba ya CHADEMA hamna sehemu inayomkataza mtu yeyote mwanachama asigombee wala eti ashauriane na incumbent akitaka kugombea!

Malafyale,
Wala siamini ni wewe unaandika. Wewe na kundi lako ni wiki kadhaa nyuma mlikuwa mkilalama na kushambulia hadi kwa meno (kama Tyson vile) baada ya Mwakyembe kupata mpinzani huko Kyela. Ni vizuri umeandika haya maneno ili kesho tuwe tunakukumbusha.
Ama kweli MKUKI KWA NGURUWE. Sasa hivi kwa kuwa anawekwa sawa Mbowe, aka. Hilo wala halikupi shida. Jamani tuwe wakweli maana hapa wengine wanamkalia kooni KIBANDA ila wakigeuziwa kibao wataanza ahh huyu hafai, mtoto, anadhaminiwa na Mafisadi, alikuwa Monduli, ni mamluki wa CCM na maneno mengine kibao.
Ndugu Kibanda, hapa wako wengi tu kama wewe (si ajabu hata mie) na hapo labda itabidi ufanye hitimisho kama ushauri wa wengi hapa kuwa UKUBALI kulifanyika kosa. Hili wengi tu tungelifanya/tumefanya.

NB: Hivi neno MNAFIKI maana yake nini?
 
KIBANDA
mbona Lwakatare amepewa kadi bila kusoma itikadi ya chama?
inaonekana Mbowe unataka awe Mwenyekiti kwani umekuwa mkali sana mkuu.

nadhani itakuwa alifanya distance learning huyo....
 
Kibanda sijuhi cha nyasi au mabua!Acha ujinga hapa inaonekana wazi tatizo ni ukabila kwavile Zitto hatoki kaskazini,acha hizo.Mpiganaji Zitto endeleza mapambano ndani na nje ya Chadema,kura yangu ipo palepale tarehe 4/9/2009 tunataka utuongoze kuanzia Chadema hadi Taifa.
 
Sio mbowe anayeandamwa na hoja ya udini na ukabila ni Chadema ndio inayoandamwa. Atoke mbowe aje zitto bado Chadema itaandamwa, as long as it is a threat to CCM. Spin doctors wamejaa CCM, vingunge kwa vijana, hawawezi kuishiwa cha ku-spin eti kwa vile mbowe ameondoka.

Nyumbu nimekupata. Umemaliza yote
 
Tatizo haliwezi kuwa Zitto kuchukua fomu kwani ana haki zote za kugombea uenyekiti na amefuata taratibu zote, Dr slaa amethibitisha hili. Mbowe amekakaririwa na magazeti akisema kwamba hana tatizo na hilo. Zitto nae amesema amechukua fomu ili aimarishe chama. Ni vema tukawaamini mpaka hapo watakapokwenda kinyume na maneno yao.

Tatizo nionavyo mimi ni wapambe. Wapambe wa wanasiasa siku hizi kampeni kwao ndio dili. They will go to any length kuhakikisha mtu wao anapita, yote haya kwa sababu ya kulinda maslahi yao ama kutegemea kupewa vyeo mgombea wao akipita. Wanapiga kampeni kama vile uchaguzi ukishapita basi walioshindwa watajitoa kwenye chama na kutokomea kusikojulikana. Hawa wakina RA na EL wako sana hata kwenye vyama vya upinzani. Zitto anatakiwa awe mwangalifu sana kushauriwa na marafiki ambao wanaiona chadema kama kituo cha polisi. Hawajali mustakabali wa chama. Hawa ndio wakina umar na msafiri mtalemwa "vijana wajinga" anayewaongelea huyu mhariri aliyekurupuka wa gazeti la mbowe.

Kibanda amejieleza vizuri sana hapa JF, mimi nimemwelewa. Anamfahamu zitto fika, hilo halina ubishi. Lakini kama kweli alikuwa anataka kukisaidia chadema haya maelezo aliyoyatoa humu angeyaweka kwenye makala yake angeeleweka na hata hiyo heading ya makala angeibadilisha. Alichokifanya ni kumshambulia zitto na kuchochea uhasama uliopo kati ya wapambe wa hawa viongozi wawili. Anaiendeleza hii vita kwa faida ya nani? Mwisho wa siku Kibanda nawe unakuwa kama hao "vijana wajinga", makala yako is very damaging to the party, ungekaa kimya kama bosi wako usubiri chadema waamue wenyewe. Upende usipende gazeti lako ambalo ni la mwenyekiti wa chadema lina influence sana kwa wanachama wa kawaida wa chadema. Kwa kutumia maneno yako mwenyewe "Lina shepu" mwelekeo wa chama....

Nimejifunza kwako. Jamvi lina vichwa vinavyoona mambo kama wewe. Hekima yako nimeikubali 99.5%. Wanajamvi wengine wajifunze kwako. Ndugu yangu Halisi akusome na kukuelewa.

U deserve my apology.
 
Nimejifunza kwako. Jamvi lina vichwa vinavyoona mambo kama wewe. Hekima yako nimeikubali 99.5%. Wanajamvi wengine wajifunze kwako. Ndugu yangu Halisi akusome na kukuelewa.

U deserve my apology.

Mkuu Kibanda, kwani Halisi ameandika nini kinachotofautiana sana na hicho alichoandika Nyumbu?
 
Hebu tuachane na Kibanda hana mantiki,

Turudi katika maswali aliyouliza Mkumbo na nilililouliza mimi. Kwanini Zitto uchaguliwe kuwa Mwenyekiti?

Je Rostam ni fisadi?

Zitto tupatie hayo majibu hata kwa mistari miwili tu

Nimefuatilia huu mjadala tokea mwanzo.

Nd. Kibanda nilishaandika tokea mwanzo kuwa huyu ni muandishi wa Kuogopa kwani ameanzia mbali tokea huko kwa Sitta anakuja kwa Zitto kazi yeye ni kuchafua tu watu . Pia ukijumlisha wajumbe wengi waliochangia humu JF wote wamemponda nadhani hilo ni fundisho arudi shule au abadilishe fani hii anavuruga kama sio kulikoroga.

Ukifuatilia JF Kibanda na Zitto wanatumiwa na RA kwani historia nzima tokea nyuma zinajieleza. (Mungu atatuhukumu kama ni hisia)

Sasa vita hii tulioyo nayo na ambayo tunapaswa kuipigania ni kwa huyu Muhindi RA. Tusiwatukane au kuwakebehi hawa waganga njaa Zitto/Kibanda, CCM - NEC na waandishi uchwara wengi, hapana! vita ya kuipigania na kujikomboa Tanzania ni dhidi ya RA full stop. Tutapoteza muda mwingi lakini jibu tunalijua. Msikilize MJJ anasemaji kuhusu nchi yetu. Kwahiyo jifunge mikanda Watanzania wengi wameshaelewa kwani saa ya UKOMBOZI NI SASA.

Nawasilisha.
 
Mkuu Kibanda, kwani Halisi ameandika nini kinachotofautiana sana na hicho alichoandika Nyumbu?

Mkuu NL,
Naona huyu Kibanda haelewi neno WAPAMBE.

Au ni wale wakisikia WAPAMBE, basi anajiona yeye hayumo wakati na yeye ni MPAMBE wa kutupwa.
Mkuu Kibanda, jamaa kaandika:

Tatizo nionavyo mimi ni wapambe. Wapambe wa wanasiasa siku hizi kampeni kwao ndio dili. They will go to any length kuhakikisha mtu wao anapita, yote haya kwa sababu ya kulinda maslahi yao ama kutegemea kupewa vyeo mgombea wao akipita. Wanapiga kampeni kama vile uchaguzi ukishapita basi walioshindwa watajitoa kwenye chama na kutokomea kusikojulikana. Hawa wakina RA na EL wako sana hata kwenye vyama vya upinzani. Zitto anatakiwa awe mwangalifu sana kushauriwa na marafiki ambao wanaiona chadema kama kituo cha polisi. Hawajali mustakabali wa chama. Hawa ndio wakina umar na msafiri mtalemwa "vijana wajinga" anayewaongelea huyu mhariri aliyekurupuka wa gazeti la mbowe.
 
Mengi yamesemwa, mengi yameandikwa lakini ukweli unabaki pale pale kwamba, katika hili Tanzania Daima linaiangalia kambi ya upinzani zaidi kuliko Mbowe au Zitto. Hatuko tayari kuona upinzani ukidhoofishwa na nguvu yoyote ile iwe ni ya kutoka ndani au nje ya Chadema. Yeyote anayetishia kuiua Chadema au CUF kwa njia zozote zile wakati tukiwa na vyama hivyo viwili pekee vyenye kuonyesha mwelekeo kwa sasa, wapenda mageuzi hatuna budi kukemea tena kwa sauti kali na wakati mwingine kwa lugha isiyo ya kawaida.

Uandishi wa habari hauna itikadi bali unaongozwa na dhana ya ukweli 'TRUTH' ambayo hata wanafalsafa wangali wakitafuta kujua maana yake halisi kwani UKWELI nao ni relative na si objective.

Hivi kumwambia Zitto asubiri zamu yake itafika ndiyo ukweli?

Binafsi nayakumbuka vizuri maneno yako ambayo asili yake ni wakongwe wa CCM, lakini sasa yamepakwa rangi ya Bluu na kutumika ndani ya kambi ya mageuzi.

Ukisema hatuko tayari una maana gani? Wewe na kina nani wengine nyuma yako?
Mmekaa kikao au ni msimamo ulopitishwa siku nyingi??

Hoja yako ni mawazo binafsi yenye kuegemea upande mmoja bila kuangalia maslahi ya chama au ukweli wa mambo.

Mwanachama wa CHADEMA kutangaza kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Taifa anakimega au kukigawa chama kivipi?

Katiba ya CHADEMA inasema nini juu ya haki ya Mwanachama kugombea nafasi yeyote ya uongozi ndani ya CHADEMA??

Naomba ujitetee juu ya dhana yako ya kusema ukweli kuliko kujikomba ili tukome kukupa kibano kama tulivyo koma kunyonya maziwa ya mama zetu.
 
Last edited:
Ukifuatilia JF Kibanda na Zitto wanatumiwa na RA kwani historia nzima tokea nyuma zinajieleza. (Mungu atatuhukumu kama ni hisia)

Wewe ndio unatoa shutuma kwa Wahindi na Zitto na RA, kwa hiyo hukumu ya Mungu jiongelee mwenyewe.

Hujui kama wote tuna sense of guilt kama yako, hujui kama wote tuna Mungu kama wewe. Jiongelee wewe!

Kama uko guilt kwa kumsingizia Zitto kuwa kibaraka wa RA Mungu atakuhukumu wewe. Si sote, wewe Magreth!
 
Suala hili la Zitto mimi nililiona la kawaida na linalenga kudumisha demokrasia. Lakini sasa ninaliangalia kwa hisia mbaya. Hii inatokana na habari nilizozipata leo kwamba Mhe. Zitto alimtumia Ndg. Msafiri (Afisa Uchaguzi - CHADEMA) kumchukulia na kurudisha fomu. Wakati Msafiri akifanya shughuli hiyo ndo alikuwa mezani kutoa na kupokea fomu za wagombea. Hali hiyo ililazimu kuondolewa ktk kazi hiyo na kupewa Katibu Mkuu Dr. Slaa.

Sasa, ninaamini kwamba Bw. Msafiri anajua vizuri taratibu na maadili ya uchaguzi kwamba anayesimamia zoezi la uchaguzi hatakiwa ku-base upande wowote wa wagombea au kuwa shabiki wa mgombea mmoja wapo.

Pili naamini kwamba Mhe. Zitto anajua vizuri maadili na taratibu za uchaguzi kwamba hakupaswa kumtumia Afisa uchaguzi kuchukua na kurejesha fomu yake. So, kwanini Zitto na Msafiri walifanya hili? Je, wanataka kuvuruga uchaguzi? au ni utoto wa kisiasa?

Anyway, CHADEMA mnapaswa kupita salama ktk uchaguzi huu, ili kujiandaa vema kwa uchaguzi mwakani. Hivyo, busara kubwa inapaswa kutumika.
 
Kitila humu JF wengine hatuna upande sisi kwetu ni Maslahi ya Taifa kwanza. Kitila ulivyomjibu Kibanda ukweli ni kuwa na wewe tulivyokusoma umeegemea Upande wa Zitto au sijui ndo Kampeni sielewi.

Nadhani Kibanda amemchambua Vizuri Mh. Zitto na pia na Mbowe ingawa ya Mbowe hatuna haja nayo kwani amekuwa madarakini miaka mitano tunamjua. Jitahidi kuelezea Zitto atatufanyia nini kwenye haya mageuzi zaidi ya Mbowe siyo blaa blaa za goo goo hapana!! hii ni hatari kutoka naibu katibu kuruka mpaka Uenyekiti! Kitila tueleze na wana JF wengi wa goo goo huyu je ataweza kwa lipi na amefanya lipi ndani ya chama???
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom