Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Status
Not open for further replies.
kibanda,,,, kibanda,,, badilika uwe nyumba, utakuwa kibanda mpaka lini?

Zitto asubiri kuona kama Mbowe atagombea au la?? Kwanini basi Mbowe asiseme kama atagombea au hapana?

Watanzania tubadilike, leo mnasema CCM ni wezi, wana makundi, hawana demokrasia. Demokrasia ipo wapi? Hata CHADEMA tulikotegemea nako tunasikia haya!

Waandishi wa habari nao njaa mbele - huyu kibanda ni kibanda kweli na hana mpango wa kuwa nyumba
 
Kwa maana nyingine ina maana watu hao walimfanyia favour, maana hakustahili. Swali, kwanini wamfanyie upendeleo yeye wakati wabunge wengine wa upinzania hata wale wapinga ufisadi ndani ya CCM majimbo yao yametelekezwa hakuna kupeleka fedha wala miradi yoyote ya maendeleo (rejea mjadala wa Mwakyembe Vs Mwakalinga).

Nawasilisha

Mkuu,
Hili swali lako Zitto aliliwekea MAJIBU na sisi tukaelezea wazi kabisa. Naona hukuelewa neno LOBBYING lina maana gani. Tumeandika faida ya kuchagua WABUNGE wazuri ili waweze kuwafanyia watu wao lobbying. Kama hukuelewa au hukusoma basi rudi huko ukasome maelezo yangu, Bluray na Masanja na umalizie ya Zitto (kumbuka Zitto yuko kamati ya fedha na alitumia hiyo GIA ku-lobby kama hukuelewa basi elewa sana).

Zaidi ya hapo tuendelee na mjadala ambao hadi sasa unakwenda safi sana.

Nyani anakomwa huku ameangaliwa usoni.
 
Haya ni majibu yangu kwa Dk. Kitilya Mkumbo.

Wakati mwingine unaweza ukajiuliza hivi hizi PhD huwa zinatolewa kwa watu wenye uwezo kiasi gani, hasa unapokutana na wasomi wa ajabu ajabu. Siwezi kuamini kwamba miaka mingi baada ya kumaliza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi leo hii Daktari wa Falsafa ndugu yangu Kitilya ambaye amehamahama vyama kadhaa vya siasa akizungumzia suala la itikadi au falsafa. Huu ni mzaha wa hatari kwa msomi.

Kitilya amepata kuwa kada wa CCM na amepata kuwa Chadema pia ambako yuko sasa. Inavyoonekana huyu jamaa ni mtu anayefanya mambo yake pasipo kuongozwa na falsafa yoyote, ingawa yeye mwenyewe anapata jeuri ya kuwaonyesha wenzake njia kuhusu masuala yanayohusu falsafa.

Kumbe wewe si msomaji mzuri wa makala za Jenerali Ulimwengu ambaye umemtaja hapo juu. Siku zote Jenerali amekuwa akiwalalamikia ninyi wanasiasa kwamba mmepoteza mwelekeo kwa sababu mnaongozwa na matakwa ya kimadaraka na fursa za kimaslahi mnapoenda katika vyama vya siasa badala ya itikadi.

Ni jambo la kusikitisha kwamba kumbe wewe na Zitto Kabwe mliamua kujiunga na Chadema (mwenzako alijiunga akiwa na miaka 16 akiwa hajafikia umri wa kupiga kura au wa kuwa na maamuzi ya busara) mkiwa na lengo la kuitikisa hata itikadi ya chama hicho? Kwa hiyo mlijiunga na Chadema kwa sababu mlikuwa na fursa ya kufanya hivyo au kwa sababu mlivutiwa na haiba binafsi ya wazee wa chama hicho kama akina Mtei na wengine hata kabla hamjasoma katiba na itikadi za chama mnachotaka kujiunga nacho. Zinakwenda wapi siasa za nchi yetu ambazo kumbe hazina dira?

Katika hili la Itikadi na Falsafa naweza nikasema wazi kabisa kwamba kumbe Kitilya na Zitto ni 'mamluki ndani ya Chadema' na kwa hakika wanapaswa kuanza kuchunguzwa mienendo yao ili isije ikawa ni mapandikizi hatari katika chama. Future will Tell.

Nayatambua mabadiliko si ya kiitikadi bali ya kimtazamo na kisera ya vyama vya Democratic, Labour (New Labour), Republicans na vingine vingi kikiwapo Chama Cha Kikomunisti cha China. Nimesoma kwa ufasaha Thatcherism na Reaganism. Ni mwanafunzi mzuri wa falsafa za Hegel, Lenin, Karl Marx na wanazuoni wengi. Nimesoma ujamaa wa Nyerere na The Fabian Socialism aliko copy ujamaa wake na namna alivyoukarabati kutoka katika ukomunisti na Ufabian akirejea misingi ya ujima na kuiboresha. Mimi ni mwanafunzi mzuri wa Historia kwa level yangu.

Nakushauri Dakta Kitilya kwamba ni makosa kuangalia jina la chama na kuvutiwa nalo kabla haujasoma itikadi ya msingi ya chama husika. Kosa hili ndilo lililokufanya katika utu uzima uhame mara CCM mara Chadema na ukaondoka baada ya kukosa madaraka (Lilikupata ukiwa UVCCM). Hii ni fedheha ya kisiasa ambayo tunaivumilia kwa sababu tu ya uchanga wa demokrasia wetu.

Viongozi wa chama kimoja cha siasa wanaweza kutofautiana katika mitazamo, sera, mbinu na mipango na si katika itikadi. Haiwezekani mjamaa na bepari, mmoja akawa mwenyekiti na mwingine Naibu Katibu Mkuu ndani ya chama kimoja. Huu ni upofu ambao ndiyo msingi mkuu uliosababisha Zitto Kabwe kwa ushauri wako wewe na vijana wengine kadhaa niliowaita wajinga ndani ya Chadema aamue kugombea kwa staili hii ya kakakuona.

Napenda tu kukueleza dakta kwamba falsafa ya kimantiki inayoniongoza katika uandishi wangu siku zote ni 'ukweli kwanza'. Journalism haina ya leo imepita zama za cold war, kwa hiyo katika masuala kadhaa hakuna leftist writers au rightist writers kama unavyotaka iwe.

Ni kweli kwamba siku zote nimekuwa nikimuona Zitto kuwa ni hero wangu. Ukweli huo hautabadilika bado itabakia pale pale kwamba japo nimempinga kwa hili kama nilivyopata kumpinga kwa mengi tu, ninamheshimu.

Muulize Zitto atakueleza, hii ni makala ya pili au ya tatu kumkosoa (si kumshambulia), nimepata kufanya hivi huko nyuma kupitia safu yangu ya kawaida ya Tuendako kila Jumatano. Nimepata kumkosoa mara nyingi katika mazungumzo ya ana kwa ana au ujumbe wa simu ya mkononi ama yeye mwenyewe au kupitia kwa watu wake wa karibu na mara kadhaa kupitia kwa mama yake mzazi.

Kwa sababu hiyo basi, mimi si kasuku ambaye Zitto akiimba wimbo hata kama wimbo huo ni wa matusi nicheze eti kwa sababu Zitto ni hero wangu. Nitakuwa mpumbavu sana. Na hakika wenye mawazo ya namna hiyo ni watu wa kuwasikitikia.

Nimepata kumpinga Mbowe pia katika makala zangu nyingi na Zitto Kabwe na wengine ambao wamekuwa wakisoma makala zangu wanalitambua hilo.

Kimsingi nilikuwa nikisubiri nikuone ukichangia na nilipoona uko kimya zaidi ya kutuma ujumbe mmoja tu wa kunikejeli ukinitaka nichukue fomu ya kugombea, niliamua kuingia na kuwapa darasa baadhi ya vijana wajinga ndani ya Chadema kama wewe, ambao kwa sababu ya upofu wenu mmeamua kumfanya Zitto ngazi ya mafanikio yenu ili akipata nafasi ya uenyekiti ambao kwenu mmeufanya ni ulaji, aweze kuwateua kushika nafasi za juu. Huku ni kumuangusha Zitto sana.

Napenda niliweke hili wazi kwamba, siupingi hata kidogo uamuzi wa Zitto kugombea uenyekiti wa Chadema. Ninachokipinga ni timing yake na kimsingi utaratibu alioutumia kugombea kiti hicho ambao gazeti ninaloliongoza limeuita 'kakakuona'.

Nimeshangazwa na kushtushwa na uamuzi wa Zitto kuingia mitini na akachukua fomu 'mafichoni' na akairejesha kupitia kwa Msafiri Mtemelwa. Huu si ujasiri wa kiuongozi ambao Zitto alipaswa kuwa nao.

Staili hii ya Zitto ambaye anapokuwa Dar es Salaam anafanya vikao vya usiku na mchana na wanahabari (nikiwamo mimi) na wanasiasa wengine wa CCM na CUF huku akikataa kukutana na viongozi wenzake wa Chadema wakiwamo wakuu wake kama Mbowe na Dk. Slaa ni wa kusikitisha kama si wa kukemewa.

Mimi ni mwana habari, ninazijua hisia za viongozi wengine wa Chadema ambao ni watu makini kabisa kama Dk. Slaa, John Mnyika na John Mrema juu ya mwenendo huo wa Zitto. Hawa jamaa wote pamoja na kutambua uwezo mkubwa wa kuona mambo alionao kijana mwenzao huyo wanaujua udhaifu wake kama kiongozi (si kama Zitto)> Naamini wameamua kukaa kimya wakiogopa kukijeruhi chama chao. Mimi sina sababu ya kukaa kimya ni wajibu wangu kuandika hata kama nitapingwa na maelfu. Msome Ibsen 'The strongest man is the one who stands alone'

Ni kweli kwamba mimi ni judgemental. Inaonekana unaliogopa neno anguko ambalo ni linafafana na la Kiingereza la 'fall' ambalo ni la kawaida katika vyombo vya habari duniani kote.

Si kweli kwamba nimekuwa cynical au sadist. Hata hivyo ni kweli nimekuwa judgemental. Huo ni wajibu wangu kama Mhariri Mtendaji. Ninao wajibu wa kusimamia sera ya gazeti na kuonyesha njia. Unatumia maneno poor and unprofessional katika hoja ambazo wewe mwenyewe unaonekana dhahiri kuubeba udhaifu huo.

Mtu anaweza akaanguka na akasimama. Anguko si kifo, ni pigo la kipindi fulani na si la milele. Nashangaa wewe na Zitto mnafanya spinning kupitia JF ili kutimiza malengo yenu ya kisiasa ambayo kwa mtazamo wangu ni ya hatari (Nasisitiza huu ni mtazamo wangu).

Sipendi kujisifu, ninayo rekodi ya kuyaona matukio mengi na makubwa ya kisiasa kwa miaka mingi kabla hayajatokea. Waulizeni wanasiasa waliowatangulia ambao baadhi yao walipuuza maandishi yangu kwa matusi na kejeli kabla ya kufikwa na mianguko ya namna hii hii ambayo naiona inataka kumpata rafiki yangu na mwanasiasa ninayemuunga mkono siku zote; Zitto Kabwe.

Hata hivyo, yako mambo mengi tu ambayo nimepata kuyaandika kwa makosa na hayakutokea kama nilivyotafakari. Makosa kama haya wamepata kufanya wanazuoni na wachambuzi mbalimbali duniani. Inapotokea hali ya namna hiyo nimekuwa mwepesi siku zote kuomba radhi na kusonga mbele.

Nimemlinganisha Zitto na Mbatia kwa minajili ya kubeba ajenda ya vijana na kwa taarirfa yako, ulinganifu huu aliuanzisha huyo mgombea wako Zitto ambaye kwa maneno yake mwenyewe alipata kuniambia kuwa anasita kugombea ili asije akakiporomosha chama na kukizika kama alivyofanya Mbatia.

Kwa hiyo scenario niliyoanza nayo ni uchaguzi uliomng'oa Marando (aliyeonekana kapitwa na wakati kama Mbowe kwa mtazamo wenu) na kumpa wadhifa Mbatia (kijana kama Zitto zama hizo) na siyo historia ya misukosuko ya wakati wa Mrema. Nadhani Kitiliya somo la 'Comparative Analysis' linakupa shida sana si kidogo.

Unataka nieleze tatizo la Zitto kugombea ni nini? Nimekujibu kidogo hapo nyuma, lakini nianze kusema, tatizo kubwa la kwanza ni kupokea ushauri mbaya kutoka kwa watu wenye nia mbaya kama wewe na wengine walio ndani na nje ya Chadema. Pili 'timing' yake si sahihi kwake yeye na kwa chama chake, tatu msingi wa kugombea kwake ambao wapambe wake wamekuwa wakisema ni kumuonyesha jeuri Mbowe ambaye eti alikuwa na mpango wa kumng'oa.

Ni wazi kwamba iwapo Mbowe alikuwa akifirikia kumng'oa Zitto ndani ya Chadema basi uamuzi huo ungekuwa ni wa hatari kama ulivyo huu ushindani wao ambao umejengwa katika misingi ya chuki, fitina na uchonganishi.

Pili si kweli kwamba kwa kuandika kwa maana ya ku foresee baadhi ya mambo ya mbele (Dhima ya Safu ya Tuendako) hakumaanishi kuwa na wasiwasi bali kumtakia mema Zitto, Mbowe Chadema na kimsingi demokrasia ya vyama vingi iliyoanza kufufuka baada ya kupwaya kwa muda mrefu.

Nimeandika bayana kuhusu anguko la Zitto na si anguko la Chadema nikijua kwa uhakika kwamba Chadema itabakia imara ingawa Zitto na Mbowe wanaweza kuanguka kutokana na uchaguzi. Soma historia ya chaguzi ndani ya vyama duniani kote na uone iwapo haziandamani na mianguko ya watu.

Zitto anasema anataka kukiandaa chama kuchukua dola, dhana ambayo Mbowe amekuwa akiifanya kwa vitendo tangu akiwa mbunge alipoanzisha ziara za kukijenga chama kwa wabunge, kufanya ziara za kitaifa na baadaye akawaleta vijana wasomi ndani ya chama kabla ya kuja na sera mchanganyiko zilizoifikisha Chadema hapa kilipo leo.

Pili, Chadema inapaswa kuepuka aina yoyote ile ya mtikisiko ambao utawalazimisha viongozi wa juu wa chama hicho kuanza kujipanga upya kuendeleza operesheni mbalimbali za chama hicho. Uamuzi wa Zitto kuingia sasa na kwa staili ya 'kakakuona' inatia shaka sana na kwa hakika kama haitadhibitiwa inaweza ikawa 'break' kwa Chadema.

Hivi Kitilya ukiwa msomi ulitaka waandishi wote tuimbe wimbo wa Goo Zitto, Goo Zitto kama ambavyo wana mtandao walitufanyia kwa Kikwete mwaka 2005? Hivi unadhani umaarufu wa Zitto ni kielelezo tosha cha kuwa na uwezo wa kuongoza? Mbona akina Augustine Mrema na Kikwete wamepata kuwa maarufu wakubwa na leo tunaona matunda yake! Hamlioni hilo? Nilidhani makala yangu ingechukuliwa kama changamoto na si dharau.

Angalia Zitto unaanguka, unaangushwa na akina Kitilya, Kafulila, Umar, Msafiri na wengine wengi. Angalia Zitto, saa yako ya ushindi inakuja ndani ya Chadema na hakuna atakayeweza kukuzuia wakati wako ukifika. Leo hii baadhi yetu tumetuhubutu kwa kuwa tunathamini uwezo wako. There's always tomorrow.
 
Last edited:
Mmh! nimesoma yote waliyoandika wenzangu, naona kila mjumbe amepata picha TOFAUTI na kuoanisha na yale anayofahamu kuhusu Zitto au CHADEMA.

Kwa mimi roho inaniuma sana..... kwani naanza kuamini kwamba CCM sasa wameweza kujipenyeza CHADEMA, na kuna mambo mawili nahisi yanaweza kutokea. La kwanza CCM watafanikiwa kuisambaratisha CHADEMA kupitia Zitto. La pili kama la kwanza litashindikana basi Zitto kujitoa CHADEMA kwa kutumia sababu zisizo na msingi kabisa kwasababu tu ameshashawishiwa na kupewa ahadi nzito.

CHADEMA naamini mpo makini.....be very careful with this man called Zitto; if possible uenyekiti msimpe (anatafuta pa kuanzia) and let him go...go for good.

Nawasilisha.
 
Haya ni majibu yangu kwa Dk. Kitilya Mkumbo.

1. Wakati mwingine unaweza ukajiuliza hivi hizi PhD huwa zinatolewa kwa watu wenye uwezo kiasi gani, hasa unapokutana na wasomi wa ajabu ajabu.

2. Siwezi kuamini kwamba miaka mingi baada ya kumaliza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi leo hii Daktari wa Falsafa ndugu yangu Kitilya ambaye amehamahama vyama kadhaa vya siasa akizungumzia suala la itikadi au falsafa. Huu ni mzaha wa hatari kwa msomi.

3. Kitilya amepata kuwa kada wa CCM na amepata kuwa Chadema pia ambako yuko sasa.

4. Inavyoonekana huyu jamaa ni mtu anayefanya mambo yake pasipo kuongozwa na falsafa yoyote,
.

- Mkuu Kibanda, with all due respect, stop it right there unasema Dr. Kitila ni msomi wa ajabu ajabu ambaye hana falsafa kwa sababu alianzia CCM na sasa yupo CHADEMA?

- Does this apply the same to Mzee Mtei, aliyeanzia CCM na kuanzisha Chadema? Dr. Slaa si alianzia CCM na kuhamia Chadema? Sasa unasema hawa wote hawana falsafa? au?

- Halafu kuna nini unachojaribu kukipitisha mbona unashambulia sana personal badala ya ku-stick na hoja yako mwenyewe kuhusu uchanga wa kisiasa wa Zitto na utabiri wako wa kuanguka kwake?

Respect.

Field Marshall Es!

Field Marshal please!

Uko bias. Kitilya anapo-attack personality yeye yuko sahihi? Mko tayari kusifia personality mnazotaka. Be tolerant, stop there too.

Nimezungumzia kuhama kwa Kitilya kwa kuoanisha na hoja yake ya Itikadi. Sikuhoji sababu za kuhama, read between the lines.

Pitia hoja zako za nyuma wewe na za dakta Kitilya uone iwapo ninyi hamgusi 'personality' stop this senseless habits
 
- Mkuu Kibanda, with all due respect, stop it right there unasema Kitla ni msomi wa ajabu ajabu ambaye hana falsafa kwa sababu alianzia CCM na sasa yupo CHADEMA?

- Does this apply the same to Mzee Mtei, aliyeanzia CCM na kuanzisha Chadema? Dr. Slaa si alianzia CCM na kuhamia Chadema? Sasa unasema hawa wote hawana falsafa? au?

- Halafu kuna nini unachojaribu kukipitisha mbona unashambulia sana personal badala ya ku-stick na hoja yako mwenyewe kuhusu uchanga wa kisiasa wa Zitto na utabiri wako wa kuanguka kwake?

Respect.

Field Marshall Es!

FMES,

Waambie when they come they better come correct, wasiamshe mizimu ya Bluray kuja ku bulldoze na ku murder machete hoja zisizo afya. Maana tunaweza kwenda kwenye nitty gritty hapa na kuamua kuhamisha lile subatomic particle smasher la CERN kulileta hapa wazee wazima wakajiona kama hawajavaa nguo.

Hatukatai Zitto anaweza kuwa criticized, unapom criticize njoo na nondo husika, ama sivyo kwa mtu mwenye promise kama Zitto kumletea hoja za mizinguo unatia watu kichefuchefu.Hususan katika nchi iliyojaa wanasiasa wasioelewa lolote au kuweza kutoa message kwenye level ya Zitto.

Not to say Zitto is infallible -in my book even Benedict XVI, that pontif bishop of Rome and his godhead are not- but when criticizing any person, especially one that is assuming a statesmanlike gravita, you better produce the requisite researched data, not mere politrickin.
 
Field Marshal please!

Uko bias. Kitilya anapo-attack personality yeye yuko sahihi? Mko tayari kusifia personality mnazotaka. Be tolerant, stop there too.

Nimezungumzia kuhama kwa Kitilya kwa kuoanisha na hoja yake ya Itikadi. Sikuhoji sababu za kuhama, read between the lines.

Pitia hoja zako za nyuma wewe na za dakta Kitilya uone iwapo ninyi hamgusi 'personality' stop this senseless habits

- Mkuu Kibanda, my bad! with all due respect I am out of this thread!, endelea na wengine maana hapa JF ni full loaded kwenye Kumkoma Nyani,

- Lakini karibu sana na usipotee mkuu, JF tunahitaji watu kama wewe kutupa muongozo!

Respect & Later!

FMEs!
 
Hii inaitwa Busara.
 
Kibanda: well una haki kabisa ya ku-doubt udaktari wangu wa falsafa hiyo ni hiari yako, wala mimi sipo hapa kuonyesha usomi wangu au kutetea PhD. Nilishaitetea panapostahili na hapa sio mahala pake kufanya hivyo. Lakini kwa hakika huwezi kupima usomi au ujinga wa mtu kwa kuangalia amehama chama A na kwenda chama B; nafikiri FMES amekujibu vizuri sana na akakupa mifano kemkem ya wapinaji wengine waliohama CCM na kuja CHADEMA.

Kuhusu falsafa na itikadi, naheshimu mawazo yako japokuwa naweza kusahihisha kitu kimoja tu kuwa "ukweli" sio miongoni mwa itikadi au falsafa za kisiasa tunazozijua, lakini endelea inawezekana tukaibuka na ingine.

Katika hili la ugombeaji wa Zitto na Mbowe, the fact is wewe ukiwa mwajiriwa wa kampuni ya Mbowe anayegombea uenyekiti kwa kushindana na Zitto, ni rahisi kuelewa utakuwa upande gani. Ni vigumu kujua hapa unachofanya ni kutetea msimamo wako au upo kutetea ajira yako. Kwa kifupi ningekuwa mimi ndiye wewe nisingethubutu kusema neno katika mjadala unaomhusu Mbowe na Zitto. Hata mtoto mdogo kabisa anayeanza kusoma elimu ya uraia darasa la nne anaelewa kwamba katika mazingira kama haya kuna clear conflict of interest. Lakini ajabu ni kwamba Mhariri Mkuu wa Gazeti maarufu linalopendwa la Tanzania Daima haelewi mgongano wa maslahi uliopo.

Lakini kwa kuwa mimi sio wewe na wewe sio mimi, endelea kumtetea boss wako na kumponda mpinzani wake. Kila la heri, lakini ujue kuwa kwa kujaribu ku-taint image ya Zitto haisaidii CHADEMA wala huyo unayemtetetea.
 
Bongo watu kama hawa kina Kibanda hawaelewi -au wana ignore- hata maana ya "full disclosure", let alone "conflict of interest".

Aibu kwa kweli, taaluma imevamiwa.
 
Haya ni majibu yangu kwa Dk. Kitilya Mkumbo.

Wakati mwingine unaweza ukajiuliza hivi hizi PhD huwa zinatolewa kwa watu wenye uwezo kiasi gani, hasa unapokutana na wasomi wa ajabu ajabu. Siwezi kuamini kwamba miaka mingi baada ya kumaliza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi leo hii Daktari wa Falsafa ndugu yangu Kitilya ambaye amehamahama vyama kadhaa vya siasa akizungumzia suala la itikadi au falsafa. Huu ni mzaha wa hatari kwa msomi.

Kitilya amepata kuwa kada wa CCM na amepata kuwa Chadema pia ambako yuko sasa. Inavyoonekana huyu jamaa ni mtu anayefanya mambo yake pasipo kuongozwa na falsafa yoyote, ingawa yeye mwenyewe anapata jeuri ya kuwaonyesha wenzake njia kuhusu masuala yanayohusu falsafa.

Kumbe wewe si msomaji mzuri wa makala za Jenerali Ulimwengu ambaye umemtaja hapo juu. Siku zote Jenerali amekuwa akiwalalamikia ninyi wanasiasa kwamba mmepoteza mwelekeo kwa sababu mnaongozwa na matakwa ya kimadaraka na fursa za kimaslahi mnapoenda katika vyama vya siasa badala ya itikadi.

Ni jambo la kusikitisha kwamba kumbe wewe na Zitto Kabwe mliamua kujiunga na Chadema (mwenzako alijiunga akiwa na miaka 16 akiwa hajafikia umri wa kupiga kura au wa kuwa na maamuzi ya busara) mkiwa na lengo la kuitikisa hata itikadi ya chama hicho? Kwa hiyo mlijiunga na Chadema kwa sababu mlikuwa na fursa ya kufanya hivyo au kwa sababu mlivutiwa na haiba binafsi ya wazee wa chama hicho kama akina Mtei na wengine hata kabla hamjasoma katiba na itikadi za chama mnachotaka kujiunga nacho. Zinakwenda wapi siasa za nchi yetu ambazo kumbe hazina dira?

Katika hili la Itikadi na Falsafa naweza nikasema wazi kabisa kwamba kumbe Kitilya na Zitto ni 'mamluki ndani ya Chadema' na kwa hakika wanapaswa kuanza kuchunguzwa mienendo yao ili isije ikawa ni mapandikizi hatari katika chama. Future will Tell.

Nayatambua mabadiliko si ya kiitikadi bali ya kimtazamo na kisera ya vyama vya Democratic, Labour (New Labour), Republicans na vingine vingi kikiwapo Chama Cha Kikomunisti cha China. Nimesoma kwa ufasaha Thatcherism na Reaganism. Ni mwanafunzi mzuri wa falsafa za Hegel, Lenin, Karl Marx na wanazuoni wengi. Nimesoma ujamaa wa Nyerere na The Fabian Socialism aliko copy ujamaa wake na namna alivyoukarabati kutoka katika ukomunisti na Ufabian akirejea misingi ya ujima na kuiboresha. Mimi ni mwanafunzi mzuri wa Historia kwa level yangu.

Nakushauri Dakta Kitilya kwamba ni makosa kuangalia jina la chama na kuvutiwa nalo kabla haujasoma itikadi ya msingi ya chama husika. Kosa hili ndilo lililokufanya katika utu uzima uhame mara CCM mara Chadema na ukaondoka baada ya kukosa madaraka (Lilikupata ukiwa UVCCM). Hii ni fedheha ya kisiasa ambayo tunaivumilia kwa sababu tu ya uchanga wa demokrasia wetu.

Viongozi wa chama kimoja cha siasa wanaweza kutofautiana katika mitazamo, sera, mbinu na mipango na si katika itikadi. Haiwezekani mjamaa na bepari, mmoja akawa mwenyekiti na mwingine Naibu Katibu Mkuu ndani ya chama kimoja. Huu ni upofu ambao ndiyo msingi mkuu uliosababisha Zitto Kabwe kwa ushauri wako wewe na vijana wengine kadhaa niliowaita wajinga ndani ya Chadema aamue kugombea kwa staili hii ya kakakuona.

Napenda tu kukueleza dakta kwamba falsafa ya kimantiki inayoniongoza katika uandishi wangu siku zote ni 'ukweli kwanza'. Journalism haina ya leo imepita zama za cold war, kwa hiyo katika masuala kadhaa hakuna leftist writers au rightist writers kama unavyotaka iwe.

Ni kweli kwamba siku zote nimekuwa nikimuona Zitto kuwa ni hero wangu. Ukweli huo hautabadilika bado itabakia pale pale kwamba japo nimempinga kwa hili kama nilivyopata kumpinga kwa mengi tu, ninamheshimu.

Muulize Zitto atakueleza, hii ni makala ya pili au ya tatu kumkosoa (si kumshambulia), nimepata kufanya hivi huko nyuma kupitia safu yangu ya kawaida ya Tuendako kila Jumatano. Nimepata kumkosoa mara nyingi katika mazungumzo ya ana kwa ana au ujumbe wa simu ya mkononi ama yeye mwenyewe au kupitia kwa watu wake wa karibu na mara kadhaa kupitia kwa mama yake mzazi.

Kwa sababu hiyo basi, mimi si kasuku ambaye Zitto akiimba wimbo hata kama wimbo huo ni wa matusi nicheze eti kwa sababu Zitto ni hero wangu. Nitakuwa mpumbavu sana. Na hakika wenye mawazo ya namna hiyo ni watu wa kuwasikitikia.

Nimepata kumpinga Mbowe pia katika makala zangu nyingi na Zitto Kabwe na wengine ambao wamekuwa wakisoma makala zangu wanalitambua hilo.

Kimsingi nilikuwa nikisubiri nikuone ukichangia na nilipoona uko kimya zaidi ya kutuma ujumbe mmoja tu wa kunikejeli ukinitaka nichukue fomu ya kugombea, niliamua kuingia na kuwapa darasa baadhi ya vijana wajinga ndani ya Chadema kama wewe, ambao kwa sababu ya upofu wenu mmeamua kumfanya Zitto ngazi ya mafanikio yenu ili akipata nafasi ya uenyekiti ambao kwenu mmeufanya ni ulaji, aweze kuwateua kushika nafasi za juu. Huku ni kumuangusha Zitto sana.

Napenda niliweke hili wazi kwamba, siupingi hata kidogo uamuzi wa Zitto kugombea uenyekiti wa Chadema. Ninachokipinga ni timing yake na kimsingi utaratibu alioutumia kugombea kiti hicho ambao gazeti ninaloliongoza limeuita 'kakakuona'.

Nimeshangazwa na kushtushwa na uamuzi wa Zitto kuingia mitini na akachukua fomu 'mafichoni' na akairejesha kupitia kwa Msafiri Mtemelwa. Huu si ujasiri wa kiuongozi ambao Zitto alipaswa kuwa nao.

Staili hii ya Zitto ambaye anapokuwa Dar es Salaam anafanya vikao vya usiku na mchana na wanahabari (nikiwamo mimi) na wanasiasa wengine wa CCM na CUF huku akikataa kukutana na viongozi wenzake wa Chadema wakiwamo wakuu wake kama Mbowe na Dk. Slaa ni wa kusikitisha kama si wa kukemewa.

Mimi ni mwana habari, ninazijua hisia za viongozi wengine wa Chadema ambao ni watu makini kabisa kama Dk. Slaa, John Mnyika na John Mrema juu ya mwenendo huo wa Zitto. Hawa jamaa wote pamoja na kutambua uwezo mkubwa wa kuona mambo alionao kijana mwenzao huyo wanaujua udhaifu wake kama kiongozi (si kama Zitto)> Naamini wameamua kukaa kimya wakiogopa kukijeruhi chama chao. Mimi sina sababu ya kukaa kimya ni wajibu wangu kuandika hata kama nitapingwa na maelfu. Msome Ibsen 'The strongest man is the one who stands alone'

Ni kweli kwamba mimi ni judgemental. Inaonekana unaliogopa neno anguko ambalo ni linafafana na la Kiingereza la 'fall' ambalo ni la kawaida katika vyombo vya habari duniani kote.

Si kweli kwamba nimekuwa cynical au sadist. Hata hivyo ni kweli nimekuwa judgemental. Huo ni wajibu wangu kama Mhariri Mtendaji. Ninao wajibu wa kusimamia sera ya gazeti na kuonyesha njia. Unatumia maneno poor and unprofessional katika hoja ambazo wewe mwenyewe unaonekana dhahiri kuubeba udhaifu huo.

Mtu anaweza akaanguka na akasimama. Anguko si kifo, ni pigo la kipindi fulani na si la milele. Nashangaa wewe na Zitto mnafanya spinning kupitia JF ili kutimiza malengo yenu ya kisiasa ambayo kwa mtazamo wangu ni ya hatari (Nasisitiza huu ni mtazamo wangu).

Sipendi kujisifu, ninayo rekodi ya kuyaona matukio mengi na makubwa ya kisiasa kwa miaka mingi kabla hayajatokea. Waulizeni wanasiasa waliowatangulia ambao baadhi yao walipuuza maandishi yangu kwa matusi na kejeli kabla ya kufikwa na mianguko ya namna hii hii ambayo naiona inataka kumpata rafiki yangu na mwanasiasa ninayemuunga mkono siku zote; Zitto Kabwe.

Hata hivyo, yako mambo mengi tu ambayo nimepata kuyaandika kwa makosa na hayakutokea kama nilivyotafakari. Makosa kama haya wamepata kufanya wanazuoni na wachambuzi mbalimbali duniani. Inapotokea hali ya namna hiyo nimekuwa mwepesi siku zote kuomba radhi na kusonga mbele.

Nimemlinganisha Zitto na Mbatia kwa minajili ya kubeba ajenda ya vijana na kwa taarirfa yako, ulinganifu huu aliuanzisha huyo mgombea wako Zitto ambaye kwa maneno yake mwenyewe alipata kuniambia kuwa anasita kugombea ili asije akakiporomosha chama na kukizika kama alivyofanya Mbatia.

Kwa hiyo scenario niliyoanza nayo ni uchaguzi uliomng'oa Marando (aliyeonekana kapitwa na wakati kama Mbowe kwa mtazamo wenu) na kumpa wadhifa Mbatia (kijana kama Zitto zama hizo) na siyo historia ya misukosuko ya wakati wa Mrema. Nadhani Kitiliya somo la 'Comparative Analysis' linakupa shida sana si kidogo.

Unataka nieleze tatizo la Zitto kugombea ni nini? Nimekujibu kidogo hapo nyuma, lakini nianze kusema, tatizo kubwa la kwanza ni kupokea ushauri mbaya kutoka kwa watu wenye nia mbaya kama wewe na wengine walio ndani na nje ya Chadema. Pili 'timing' yake si sahihi kwake yeye na kwa chama chake, tatu msingi wa kugombea kwake ambao wapambe wake wamekuwa wakisema ni kumuonyesha jeuri Mbowe ambaye eti alikuwa na mpango wa kumng'oa.

Ni wazi kwamba iwapo Mbowe alikuwa akifirikia kumng'oa Zitto ndani ya Chadema basi uamuzi huo ungekuwa ni wa hatari kama ulivyo huu ushindani wao ambao umejengwa katika misingi ya chuki, fitina na uchonganishi.

Pili si kweli kwamba kwa kuandika kwa maana ya ku foresee baadhi ya mambo ya mbele (Dhima ya Safu ya Tuendako) hakumaanishi kuwa na wasiwasi bali kumtakia mema Zitto, Mbowe Chadema na kimsingi demokrasia ya vyama vingi iliyoanza kufufuka baada ya kupwaya kwa muda mrefu.

Nimeandika bayana kuhusu anguko la Zitto na si anguko la Chadema nikijua kwa uhakika kwamba Chadema itabakia imara ingawa Zitto na Mbowe wanaweza kuanguka kutokana na uchaguzi. Soma historia ya chaguzi ndani ya vyama duniani kote na uone iwapo haziandamani na mianguko ya watu.

Zitto anasema anataka kukiandaa chama kuchukua dola, dhana ambayo Mbowe amekuwa akiifanya kwa vitendo tangu akiwa mbunge alipoanzisha ziara za kukijenga chama kwa wabunge, kufanya ziara za kitaifa na baadaye akawaleta vijana wasomi ndani ya chama kabla ya kuja na sera mchanganyiko zilizoifikisha Chadema hapa kilipo leo.

Pili, Chadema inapaswa kuepuka aina yoyote ile ya mtikisiko ambao utawalazimisha viongozi wa juu wa chama hicho kuanza kujipanga upya kuendeleza operesheni mbalimbali za chama hicho. Uamuzi wa Zitto kuingia sasa na kwa staili ya 'kakakuona' inatia shaka sana na kwa hakika kama haitadhibitiwa inaweza ikawa 'break' kwa Chadema.

Hivi Kitilya ukiwa msomi ulitaka waandishi wote tuimbe wimbo wa Goo Zitto, Goo Zitto kama ambavyo wana mtandao walitufanyia kwa Kikwete mwaka 2005? Hivi unadhani umaarufu wa Zitto ni kielelezo tosha cha kuwa na uwezo wa kuongoza? Mbona akina Augustine Mrema na Kikwete wamepata kuwa maarufu wakubwa na leo tunaona matunda yake! Hamlioni hilo? Nilidhani makala yangu ingechukuliwa kama changamoto na si dharau.

Angalia Zitto unaanguka, unaangushwa na akina Kitilya, Kafulila, Umar, Msafiri na wengine wengi. Angalia Zitto, saa yako ya ushindi inakuja ndani ya Chadema na hakuna atakayeweza kukuzuia wakati wako ukifika. Leo hii baadhi yetu tumetuhubutu kwa kuwa tunathamini uwezo wako. There's always tomorrow.
KIBANDA
mbona Lwakatare amepewa kadi bila kusoma itikadi ya chama?
inaonekana Mbowe unataka awe Mwenyekiti kwani umekuwa mkali sana mkuu.
 
Kibanda ,umesha sema vya kutosha .Yeyote aliyetaka kusikia umesema ama umetetea kama hili lipo basi atakuwa ameona. Mbowe ni mwanachama hapa .Naamini anasoma na anajua watu wanavyo ipenda Chadema. Nakushauri sasa pumzika acha wengine waseme maana wewe watu wanakuona na hidden agenda. Kaa pembeni sasa acha wengi wangojee kampeni.

Jihadhari na comments zaidi kwenye gazeti dhidi ya Chadema na wagombea 2. Mshauri Mbowe pia aelewe kwamba anaheshimiwa sana na mchango wake kwa Chadema ni mkubwa so akubli uhalisia kama kuna lolote gumu.

Ushauri kwa Zitto na Mbowe wote ni nyie ni wana chadema na wapenda mageuzi , basi kampeni ziwe ka hoja na demokrasia zaidi. Mbowe is bad kwamba akina Makani waliachia nawe labda ungalipenda kuachia kwa njia ile ile lakini pia nakutambua kwa uelewa hutajali kama utashindwa ama utashinda .

Wote wewe na Zitto yeyote atayekuwa mwenyekiti ninawataka mwende majimboni mkaombe kuwa wabunge na atokee mwingine agombee Urais ila nyie wote 2 mkawashe moto kule Bungeni , naombeni sana badilisheni mambo kisiasa Tanzani kuweni kioo na kichocheo cha maendeleo na siasa za haki.

Asante
 
Bongo watu kama hawa kina Kibanda hawaelewi -au wana ignore- hata maana ya "full disclosure", let alone "conflict of interest".

Aibu kwa kweli, taaluma imevamiwa.
Wagombea wa nafasi hii wangekuwa zaidi ya wawili tungekuwa tunaongea lugha nyingine nadhani.

Mjadala huu umenifungua macho sana... Lakini kuna kitu tunaandaa, kitafungua ukurasa mpya kwenye siasa za Tanzania!
 
Kibanda: well una haki kabisa ya ku-doubt udaktari wangu wa falsafa hiyo ni hiari yako, wala mimi sipo hapa kuonyesha usomi wangu au kutetea PhD. Nilishaitetea panapostahili na hapa sio mahala pake kufanya hivyo. Lakini kwa hakika huwezi kupima usomi au ujinga wa mtu kwa kuangalia amehama chama A na kwenda chama B; nafikiri FMES amekujibu vizuri sana na akakupa mifano kemkem ya wapinaji wengine waliohama CCM na kuja CHADEMA.

Kuhusu falsafa na itikadi, naheshimu mawazo yako japokuwa naweza kusahihisha kitu kimoja tu kuwa "ukweli" sio miongoni mwa itikadi au falsafa za kisiasa tunazozijua, lakini endelea inawezekana tukaibuka na ingine.

Katika hili la ugombeaji wa Zitto na Mbowe, the fact is wewe ukiwa mwajiriwa wa kampuni ya Mbowe anayegombea uenyekiti kwa kushindana na Zitto, ni rahisi kuelewa utakuwa upande gani. Ni vigumu kujua hapa unachofanya ni kutetea msimamo wako au upo kutetea ajira yako. Kwa kifupi ningekuwa mimi ndiye wewe nisingethubutu kusema neno katika mjadala unaomhusu Mbowe na Zitto. Hata mtoto mdogo kabisa anayeanza kusoma elimu ya uraia darasa la nne anaelewa kwamba katika mazingira kama haya kuna clear conflict of interest. Lakini ajabu ni kwamba Mhariri Mkuu wa Gazeti maarufu linalopendwa la Tanzania Daima haelewi mgongano wa maslahi uliopo.

Lakini kwa kuwa mimi sio wewe na wewe sio mimi, endelea kumtetea boss wako na kumponda mpinzani wake. Kila la heri, lakini ujue kuwa kwa kujaribu ku-taint image ya Zitto haisaidii CHADEMA wala huyo unayemtetetea.
Labda ili gazeti liendelee nafasi ya uenyekiti ni muhimu iwe kwa muajiri wake.
 
Mengi yamesemwa, mengi yameandikwa lakini ukweli unabaki pale pale kwamba, katika hili Tanzania Daima linaiangalia kambi ya upinzani zaidi kuliko Mbowe au Zitto. Hatuko tayari kuona upinzani ukidhoofishwa na nguvu yoyote ile iwe ni ya kutoka ndani au nje ya Chadema. Yeyote anayetishia kuiua Chadema au CUF kwa njia zozote zile wakati tukiwa na vyama hivyo viwili pekee vyenye kuonyesha mwelekeo kwa sasa, wapenda mageuzi hatuna budi kukemea tena kwa sauti kali na wakati mwingine kwa lugha isiyo ya kawaida.

Uandishi wa habari hauna itikadi bali unaongozwa na dhana ya ukweli 'TRUTH' ambayo hata wanafalsafa wangali wakitafuta kujua maana yake halisi kwani UKWELI nao ni relative na si objective.
 
Ni kweli kwamba gazeti ni la Mbowe? Mbona huja address hili?
 
Mkuu Kibanda
..kwa lugha rahisi ulitaka Mbowe apambane na nani katika uchaguzi huo? na nini kinakushawishi kumtaka Zitto asigombee? Mbowe kuwa kwake CHADEMA kuna mkataba na uenyekiti?
Usiturudishe kwenye siasa za Ndiyo au Hapana. Mbowe anahitaji mpinzani mwenye nguvu kabisa kwenye nafasi hiyo ya uenyekiti, labda tumwombe tu asikufukuze kazi ikitokea akaukosa uenyekiti.
Kama uliyoyawakilisha hapa yanashabihiana na mawazo ya Mbowe hata kwa asilimia 10, naanza kupata mashaka kuhusu yeye pia.
 
Mengi yamesemwa, mengi yameandikwa lakini ukweli unabaki pale pale kwamba, katika hili Tanzania Daima linaiangalia kambi ya upinzani zaidi kuliko Mbowe au Zitto. Hatuko tayari kuona upinzani ukidhoofishwa na nguvu yoyote ile iwe ni ya kutoka ndani au nje ya Chadema. Yeyote anayetishia kuiua Chadema au CUF kwa njia zozote zile wakati tukiwa na vyama hivyo viwili pekee vyenye kuonyesha mwelekeo kwa sasa, wapenda mageuzi hatuna budi kukemea tena kwa sauti kali na wakati mwingine kwa lugha isiyo ya kawaida.

Uandishi wa habari hauna itikadi bali unaongozwa na dhana ya ukweli 'TRUTH' ambayo hata wanafalsafa wangali wakitafuta kujua maana yake halisi kwani UKWELI nao ni relative na si objective.
hivi kumbe kibanda mwenyewe ni mwanajamvi?mzee kama ndiyo ww fikra zako hazijakomaa kwa yale uliyoyaandika,vinginevyo nashawishika kusema tena kwa uchungu kwamba we pia fisadi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom