Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Status
Not open for further replies.
Someni gazeti la Mwananchi leo wazee wa Chadema wanataka kumpoza Zitto na ukatibu mkuu ili kumuokoa Mbowe.
Kibanda njoo ndugu yetu.
kama ni kweli wazee wamemwita ZItto i wapi demokrasia CHADEMA basi kweli ni chama cha wachaga.Bora wamwache ili democrasia ichukue mkondowe
 
Nimefatilia kwa karibu sana malumbano haya kwa kipindi kirefu,napenda kukiri kuwa Zitto ni mtu ambaye tunafahamina kwa karibu sana,aidha Kibanda najuana nae kwa karibu sana pia.Omary ni classmate wangu na Kitila ni kaka yangu....................kati ya hawa hakuna hata mmoja ni mjinga na wote ni wajuvi wa kutetea hoja zao.Mimi mawazo yangu ni kuwa Zitto Kabwe anafaa na hafai kuwa mwenyekiti wa Chadema:
1.Mimi kama mwana uvccm-anafaa kwa kuwa vijana wenye uwezo ndio wakati wao kujitokeza.
2.Mwanademokrasia-hatupaswi kuogopa haki za watu kugombea basi hakuna maaana ya kuwa na vyama vingi kama tunafinya demokrasia ya ndani ya chama
3.Mwana ccm-Zitto hafai kwa kuwa ana uwezo mkubwa a kupata influence za kimataifa ni itapelekea chadema kupata misaada mingi ya kimataifa na kutusumbua kwenye chaguzi zetu.
4.mzalendo-hasigombee kwa kuwa itakidhoofisha chadema kutokana na kushindwa kutibu majeraha baada ya uchaguzi,as mpaka leo ccm haijapona majeraha ya uchaguzi uliopita
5.Mtanzania-itafuta taswira kuwa chadema ni chama cha watu wa kaskazini

Nchimbi karibu sana maana hatimaye umeamua kuingia .Siku za nyuma ulisema hapa kuna uvumi sana na hakuna ukweli mie nikasema is where we all dare openly karibu.Maneno yako ume yaandika vyema mno na yanavutia .Nadhani mwisho wa siku Zitto atasimama na Mbowe atasimama na kuamuliwa na wana Chadema na si zaidi ya hapo .Wazee kumpa Zitto nafasi itakuwa ni mambo ya huko CCM .Zitto hata akiwa mwenyekiti bado Chama kutakuwa cha wana Chadema wote sioni wasi wasi unatoka wapi juu ya hili .Wazee wanaenda kuwapika mtu na kaka yake ili wawe kampeni ambazi si chafu lakini naamini watawataka wasimame na sisi tushudie demokrasia.
 
http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=282
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kabwe Zitto, amesema hana mpango wa kuondoa fomu yake ya kugombea uenyekiti wa chama hicho, kwa kuwa ni haki yake na ana sifa za kuwa Mwenyekiti.
Pia Zitto amekanusha taarifa kuwa fomu zake zilirejeshwa na watu wanaoshinikiza awanie nafasi hiyo kwa lengo la kukibomoa chama hicho na kusema kama ni shinikizo basi ameshinikizwa na wana Chadema na si mtu wa pembeni. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Zitto alikiri kuchukua fomu na kufuata taratibu zinazotakiwa na kama kuna tofauti ni mbinu za kisiasa.

"Hii ni staili tu, nisingeweza kuchukua mdundiko, kwanza nilikuwa jimboni kisha nilikuwa na safari ya Ujerumani hata fomu zenyewe nilijazia Uwanjani (wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere)," alisema.

Aliongeza kuwa yamesemwa maneno mengi kumhusu pamoja na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, ambayo aliyaita ya siasa za kampeni na kuwa anatarajia yatakwisha baada ya uchaguzi, kwa kuwa wote lengo lao ni kuimarisha chama hicho.

"Chama hiki si changu, wala si cha Mbowe, sisi tutaondoka chama kitabaki hapahapa na uamuzi wangu kugombea, ni jambo la kawaida wala sihitaji mpasuko au mgawanyiko, mwaka 1998 Bob Makani na Philemon Ndesamburo waligombea nafasi hii wakatofautiana, lakini baada ya uchaguzi, waliungana na kuendeleza chama," alisema Zitto.

Alisema alichukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa na uwezo wa kukipeleka mbali chama hicho na hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi, ambapo inatarajiwa kuwapo vijana wapya wapiga kura wapatao milioni 6.3 hivyo ni vyema chama kijipambanue kwa kuongozwa na kijana.

Alitamba kuwa anajiamini kuwa na uwezo katika kukiongoza chama hicho hasa ikizingatiwa kuwa katika nafasi yake ya ubunge wa Kigoma Kaskazini, ameongoza kamati muhimu ya Bunge, ya Hesabu za Mashirika ya Umma, iliyo na mashirika yenye thamani ya zaidi ya Sh trilioni tano.

"Nikiwa kijana kama wanavyodai, kwa nini niweze kuongoza kamati hiyo ila nishindwe chama chenye mapato ya Sh bilioni 72 kwa mwezi? Hata hivyo binafsi sikupenda kugombea uenyekiti, lakini nimeombwa sana na wanachama na kujikuta najaza fomu hizi," alisema.

Alisema amekuwa kwenye chama hicho tangu akiwa na umri wa miaka 16 na kupitia ngazi mbalimbali za uongozi ndani na nje ya chama hicho, hivyo anaamini sifa za kushika wadhifa huo anazo kwa kuwa anakifahamu vyema.

"Na itakuwa ni ajabu kutumiwa kukiharibu chama hiki, haya ni maneno ya siasa na yatakwisha kampeni zikimalizika," aliongeza.

Aliwataka waliozusha na kutunga uongo dhidi yake, watambue kuwa yeye si mtu wa visasi, lakini pia uchaguzi unapita na maisha baada ya hapo yataendelea, lakini pia akasema haamini kama chama hicho kimetawaliwa na ukabila kama inavyodaiwa.

Hata hivyo, alionyesha masikitiko yake kwa gazeti linalotoka kila siku lililoandika habari dhidi yake ikionesha wazi kuwa linatumiwa, na hivyo kuleta dhana kwamba ukabila ndani ya chama hicho upo, kwa kuwa gazeti hilo mmiliki na mhariri wake ni Wachaga.

"Hata hivyo, nikichaguliwa kuwa Mwenyekiti dhana hiyo ya ukabila itaacha kuwa na nguvu," alisema. Alisema leo wazee wa chama hicho wanatarajia kukutana na wagombea hao wawili kujadili na kuangalia tofauti zilizojitokeza. Wanaotarajiwa kukutana ni Profesa Mwesiga Baregu, Bob Makani, Anthony Ngaiza na Edwin Mtei.
Wewe fairplayer!

Acha kumpigia debe huyo kijana wa Kimanyema!

Majigambo ya kuongoza kamati ya kichovu ya CCM ya mashirika yao wanayoyaita(ikiwemo Tanesco) ya umma ni upuuzi mtupu. Zito Zuberi Kabwe alichukua pesa kutoka kwa Rostam Aziz na mawakala wake akaja na hoja ya kitoto ya kushawishi waTZ wakubali kununuliwa mitambo haramu ya DOWANS huku akijua kabisa na kuvunja sheria na maazimio ya Bunge la Six eti kwa maslahi ya umma hivi mmesahau kweli ?mmelogwa au you have a very short memory.

Hiyo hoja ilifuatiwa na hoja ya mwizi mwingine kibaraka wa Rostam Aziz na swahiba wa JMK anayejiita Dr. Idris Rashid hata ubin wake anaficha akatishia kuleta giza nchi nzima ifikapo Agosti 09 mwezi ndio huo unayeya na giza hakuna.

Mashine bado ziko pale ubungo sijui kama wameziondoa hawa wapuuzi akiwemo huyo ZZK wanaombea mvua zisinyeshe ili mitambo iwashwe ni pamoja na JMK na Teddy Lowasa.

Huo uwenyekiti wa CHadema japo chama chenyewe cha wachovu anautaka ili afanye nini? Wote tunafahamu katiba hakuna hata akiwa Chairman itabadili nini?

Kama ni kwa manufaa ya CCM ni sawa tu kwani hamkumbuki yule Dr. Aman Walid Kaburu alivyojeuka hawa watoto wa Mama TAMASHA kwa kweli hawaaminiki kisa njaa kali na shida za Kigoma!

Alikoroma na Dowans eti inunuliwe wakati Kigoma alikotoka ikiwa giza totoro lakini bado bila aibu akachukua Usd( Dola za Kimarekani )kutoka kwa Dr.Idris apige debe lakini watu wakamshtukia kiko wapi!!! Akibisha mitataja kiasi cha dola alizochukua!!

Kama mwenyekiti wa CCM (WEZI) wanatawala na bado anaendelea kutabasamu hivi vyama si vijiwe tu kama vya kahawa na madereva wa Taxi pale Kariakoo!
 
Mkereme una hasira za Zitto sawa lakini kutukana halaiki nzima ni kosa kubwa .Una shida na Zitto na kama una ushahidi wa yeye kuchukua pesa we dare here sema na weka ushahidi wana Chadema wataamua.Lakini unakosa heshima kutukana kila mmoja kwamba ni vyama vya kijiweni .Please hii si haki na itaondoa maana ya wewe kumpinga Zitto kwa madai ya rishwa .Iweke clear watu waelewe na uheshimu watu wengine .Matatizo ya JK kucheka watu wanatuibia si tatizo la kila Chama .Chadema ni wachovu ? Thibitisha uchovu wao tafadhali .
 
Lunyungu!

Kama kwaida unakurupuka maswali niliyaelekeza kwa Fairplayer with purpose sasa kwanza hujaelewa somo hao watu wa Chadema unaowatetea kwani wao hawasomi hapa. Jibu maswali acha hasira na uelewa haba. The contents are serious kuhusu giza; Dowans; na Walid Kabouru pamoja na Dr. Idris ambaye ni mstaafu lakini this double standard CCM gvt imempatia mkataba wa miaka mitatu huku wakijua hafai kwani kote alikopitia hata Vodacom kwenye kampuni binafsi alichemsha!!

Jibu hizi hoja uzuri wa hawa watu ikiwa ni pamoja na ZZK aliyepigania Dowans mpaka kamati za Bunge zitakataka kuwashana ngumi na ukamalizwa kiaina bado you think he is fit kuwa hata katibu kata!!

Tuna mifano hai wasaliti kama hao as Dr. Lamwai huishia ukutani. Narudia kila aliyechukua pesa haramu za RA lazima atafulia keep this in mind !!!
 
Wachaga hawawezi kukubali CHADEMA iondoke mikononi mwao. Labda Zitto aoe Mchaga mwenzao ndio watamwachia hicho chama.

Zitto ana uwezo wa kuongoza CHADEMA kuliko Mbowe; labda tatizo lenu hapa ni Uchaga tu.

Ni uwezo gani huo mnaoongelea kwamba Zitto hana?

Tumegundua janja yenu!

Una uthibitisho wa hayo uliyoandika?

Ama kweli akili ni nywele kila mtu ana zake.
 
Lunyungu!

Kama kwaida unakurupuka maswali niliyaelekeza kwa Fairplayer with purpose sasa kwanza hujaelewa somo hao watu wa Chadema unaowatetea kwani wao hawasomi hapa. Jibu maswali acha hasira na uelewa haba. The contents are serious kuhusu giza; Dowans; na Walid Kabouru pamoja na Dr. Idris ambaye ni mstaafu lakini this double standard CCM gvt imempatia mkataba wa miaka mitatu huku wakijua hafai kwani kote alikopitia hata Vodacom kwenye kampuni binafsi alichemsha!!

Jibu hizi hoja uzuri wa hawa watu ikiwa ni pamoja na ZZK aliyepigania Dowans mpaka kamati za Bunge zitakataka kuwashana ngumi na ukamalizwa kiaina bado you think he is fit kuwa hata katibu kata!!

Tuna mifano hai wasaliti kama hao as Dr. Lamwai huishia ukutani. Narudia kila aliyechukua pesa haramu za RA lazima atafulia keep this in mind !!!

Sitachoka kusema nawe hata ukisema nakurupuka .Kaka kumbuka nimesema machache sana juu ya matamshi yako .Sijamtetea Idrisa wala Dowans nadhani waujua msimamo wangu kila mara hapa forum .Na nimesema na narudia kusema huu ni wakati muafaka badala ya kusema tu weka ushahidi wa Zitto ambaye sasa ni issue hapa .Haya yote yasingalikuja kama Zitto asingalichukua form .Now simtetei kama ana madhambi huko na mnayajua .Nimeomba uaniek hapa mjadala uchukue mkondo mpya .Toa ushahidi why you are so bitter against him.

Hilo tu kaka .
 
Wanajamvi wote

Tukubaliane kupingana bila kupigana. Tumuache Zitto agombee uenyekiti wa Taifa wa Chadema kwa sababu ni haki yake ya kikatiba na kwa wengine wengi ana uwezo na huu ni wakati wake.

Waswahili husema wakati ukuta na tumuombee ashinde na baada ya hapo kila mmoja atakuwa na la kusema baada ya kumpima. Speculative journalism ni kitu cha kawaida duniani na wala si unprofessional or unethical kama alivyoona mwanazuoni mmoja humu.

Makala yangu (Naliona Anguko la Zitto Kabwe) pamoja na mapungufu mengi ambayo hata mimi ninayaona kutokana na michango ya wanajamvi, haikulenga kumkatisha tamaa Zitto na wale waliomlazimisha kujaza fomu uwanja wa ndege la hasha. Ilikuwa ni ya tahadhari tu.

Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba pengine nilishindwa kuufikisha ujumbe niliokusudia. Nimewasiliana na Zitto mwenyewe leo, jana na juzi na tumebadilishana mawazo na kuonyeshana mapungufu ya hapa na pale.

Nimezungumza na Mbowe pia kuhusu maoni ya wanajamvi juu ya kile nilichokiandika na mlichoandika wenzangu. Naamini watatumia fursa hii kuhakikisha wanawanyima mahasimu wao fursa ya kuendelea kuwatuhumu kwa ukabila, ubadhirifu, ubinafsi, utoto na mambo mengi mengine wanayokabiliana nayo. Ni jambo jema kwamba japo kwa maneno wote wanasisitiza kwamba, watahakikisha Chadema inabakia moja hata baada ya Uchaguzi Mkuu.

Zitto amenihakikishia kwamba ameichukua makala ile na nyingine nyingi zilizompinga kama changamoto na kimsingi hawezi kujiangusha yeye mwenyewe, chama chake wala vijana ambao wameonyesha matumaini makubwa kwake. Sina sababu hata moja ya kumtilia shaka kwa msimamo wake huo.

Ni jambo la faraja sana kwamba, hata katika mahojiano yake na vyombo mbalimbali vya habari amekuwa makini kujibu baadhi ya hoja zilizoandika katika makala ile ya anguko kama zile za uchanga wake katika siasa.

Amejenga hoja kuhalalisha uzoefu wake kiuongozi ndani ya chama na ndani ya Bunge. Pamoja na ukweli kwamba, bado naendelea kutofautiana na staili yake ya uchukuaji fomu, ikiwa ni pamoja na kushangazwa na hatua yake ya kukubali kuungwa mkono na baadhi ya watu ambao ama wana visasi, chuki binafsi binafsi dhidi ya Mbowe, Slaa, Komu, Mnyika, John Mrema na watendaji wengine wa makao makuu

Amenukuliwa akisema analo jukumu la kuponya majeraha ya makundi ndani ya Chadema yaliyoibuka kutokana na migogoro iliyowapokonya madaraka watu kama marehemu Chacha Wangwe na kuwakimbiza ndani ya chama hicho watu kama Dk. Walid Kabourou na wengine.

Katika hili naamini atakuwa amejipanga kuhakikisha matokeo ya uchaguzi utakaompa ama yeye au Mbowe ushindi, hayataibua makundi mapya ambayo yatampasa mwenyekiti ajaye kuanza kuyatibu.

Hoja ya Nchimbi ndani ya thread hii kwamba wao CCM hadi sasa wameshindwa kutibu majeraha ya Uchaguzi wa mwaka 2005 ni somo zuri kwa Zitto, Mbowe na viongozi na wanachama wote wa Chadema.

Wito wangu kwa wanajamvi ni kuweka mbele maslahi ya taifa wakati tunapojadili hoja za namna hii, ili kuepuka lugha za kudhalilishana na kupakana matope. Wale wanaoanza kupiga chini ya mikanda na wao wakajibiwa kwa utaratibu wao huo huo wanapaswa kuwa wavumilivu na kukubali kwamba wao ndiyo waanzilishi.

You all deserve my apology. I'm defeated, you have all won. The battle is on but the war have ended.

Goo Zitto...Goo Mbowe...Goo Chadema.. I always wish a strong multi party democracy.
 
Kibanda
Nakupa pongezi sana.Hapa tuko wachache sana katika jamvi hili ambalo watu huwa hata wakiona wamekosa hawawezi kusema samahani.

Kibanda umefanya jambo la kiume sana .Umesema mawazo yako yamepingwa yamekosolewa na mengine umeona mwenyewe uliko jikwaa katika kuwakilisha ujumbe na sasa unasema unakubali kuto kubaliana na hili ndilo jambo hasa .You are not being defeated hapana .Watu wamekataa kusemewa na kukuona wewe mtu ambaye wanakupa heshima kubwa kama kwamba ulikuwa na uapnde .Usiache kuendeleza yale mazuri ambayo umekuwa ukiyafanya wewe na waandishi wenzako kwenye Tanzania Daima .Kama umesema nia yako na upinzani wa nguvu basi mchango uzidishe na sisi tutakusema vyema kama JKN, Teddy Kennedy, Johaness Paulus wa II, ..........................................
 
Wewe fairplayer!

Naam mkuu NIPO!

Acha kumpigia debe huyo kijana wa Kimanyema!

Kwanini Sheikh!!? nimpigie KABILA GANI kampeni? MCHAGA??!

Majigambo ya kuongoza kamati ya kichovu ya CCM ya mashirika yao wanayoyaita(ikiwemo Tanesco) ya umma ni upuuzi mtupu.

Huu ni wivu..kwani hajaongoza kweli?? Vipi Yakhe! Mbona unakuwa kama Absalom Kibanda asiyeelewa maana YA CONFLICT OF INTEREST?

Zito Zuberi Kabwe alichukua pesa kutoka kwa Rostam Aziz na mawakala wake akaja na hoja ya kitoto ya kushawishi waTZ wakubali kununuliwa mitambo haramu ya DOWANS huku akijua kabisa na kuvunja sheria na maazimio ya Bunge la Six eti kwa maslahi ya umma hivi mmesahau kweli ?mmelogwa au you have a very short memory.

Nithibitishie hata kwa kunitumia Private Message. Kama nikipima na nikiona ni kweli...I SWEAR nitaanza kumpigia debe Prof Baregu ambaye ni second choice.

Hiyo hoja ilifuatiwa na hoja ya mwizi mwingine kibaraka wa Rostam Aziz na swahiba wa JMK anayejiita Dr. Idris Rashid hata ubin wake anaficha akatishia kuleta giza nchi nzima ifikapo Agosti 09 mwezi ndio huo unayeya na giza hakuna.

Mashine bado ziko pale ubungo sijui kama wameziondoa hawa wapuuzi akiwemo huyo ZZK wanaombea mvua zisinyeshe ili mitambo iwashwe ni pamoja na JMK na Teddy Lowasa.

Unajua Mkereme, tusipoangalia itafikia hata siku mkeo (wake zetu) akisema/wakisema amechoka/wamechoka anataka kupumzika leo tutakuwa TUNAMWAMBIA WEWE LEO Rostam Azizi amekunaniihhiiii wewe!!.

Mtoro asipoenda shule: Wewe umetumwa na RA husiende shule ili baadaye waje waarabu wa IRAN watawale!!

Huo uwenyekiti wa CHadema japo chama chenyewe cha wachovu anautaka ili afanye nini? Wote tunafahamu katiba hakuna hata akiwa Chairman itabadili nini?

Anataka uenyekiti ili aweke KATIBA ambayo HAIPO kama ulivyosema
- Hii inamfanya Mbowe kuwa na mamlaka makubwa zaidi na kufukuza kila anayepingana nae
- Kuteua wabunge ambao ni kaskazini related (imeongelewa sana)
- Kuondoa chama kutegemea sana wazee na kuamini kuwa wazee pekee ndo wana BUSARA and everything. Ingawa hawa wazee wana support sana kwasababu ya MTOTO/MKWE wao.
- Kurudisha chama kwa wanachama

Kama ni kwa manufaa ya CCM ni sawa tu kwani hamkumbuki yule Dr. Aman Walid Kaburu alivyojeuka hawa watoto wa Mama TAMASHA kwa kweli hawaaminiki kisa njaa kali na shida za Kigoma!

This is a sweeping statement! Hakuna hoja hapa, sio kweli kuwa Kighoma wote njaa kali!!

Alikoroma na Dowans eti inunuliwe wakati Kigoma alikotoka ikiwa giza totoro lakini bado bila aibu akachukua Usd( Dola za Kimarekani )kutoka kwa Dr.Idris apige debe lakini watu wakamshtukia kiko wapi!!! Akibisha mitataja kiasi cha dola alizochukua!!

Kama mwenyekiti wa CCM (WEZI) wanatawala na bado anaendelea kutabasamu hivi vyama si vijiwe tu kama vya kahawa na madereva wa Taxi pale Kariakoo!

Nithibitishie hata kwa kunitumia Private Message. Kama nikipima na nikiona ni kweli...I SWEAR nitaanza kumpigia debe Prof Baregu ambaye ni second choice....

Unajua Mkereme mie niionavyo Chadema, inatakiwa iwe institutionalised, kwa sasa ipo sana mikononi mwa watu fulani fulani wenye hela. Hii sio sahihi. Wazee wakianza kufa chama kitakufa. Inatakiwa mtu/ watu wa kuinusuru chama.

Hayo ni mawazo yangu, sijatumwa na Zitto wala simfahamu na mimi ni mwana CCM.
 
Wanajamvi wote

Tukubaliane kupingana bila kupigana. Tumuache Zitto agombee uenyekiti wa Taifa wa Chadema kwa sababu ni haki yake ya kikatiba na kwa wengine wengi ana uwezo na huu ni wakati wake.

Waswahili husema wakati ukuta na tumuombee ashinde na baada ya hapo kila mmoja atakuwa na la kusema baada ya kumpima. Speculative journalism ni kitu cha kawaida duniani na wala si unprofessional or unethical kama alivyoona mwanazuoni mmoja humu.

Makala yangu (Naliona Anguko la Zitto Kabwe) pamoja na mapungufu mengi ambayo hata mimi ninayaona kutokana na michango ya wanajamvi, haikulenga kumkatisha tamaa Zitto na wale waliomlazimisha kujaza fomu uwanja wa ndege la hasha. Ilikuwa ni ya tahadhari tu.

Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba pengine nilishindwa kuufikisha ujumbe niliokusudia. Nimewasiliana na Zitto mwenyewe leo, jana na juzi na tumebadilishana mawazo na kuonyeshana mapungufu ya hapa na pale.

Nimezungumza na Mbowe pia kuhusu maoni ya wanajamvi juu ya kile nilichokiandika na mlichoandika wenzangu. Naamini watatumia fursa hii kuhakikisha wanawanyima mahasimu wao fursa ya kuendelea kuwatuhumu kwa ukabila, ubadhirifu, ubinafsi, utoto na mambo mengi mengine wanayokabiliana nayo. Ni jambo jema kwamba japo kwa maneno wote wanasisitiza kwamba, watahakikisha Chadema inabakia moja hata baada ya Uchaguzi Mkuu.

Zitto amenihakikishia kwamba ameichukua makala ile na nyingine nyingi zilizompinga kama changamoto na kimsingi hawezi kujiangusha yeye mwenyewe, chama chake wala vijana ambao wameonyesha matumaini makubwa kwake. Sina sababu hata moja ya kumtilia shaka kwa msimamo wake huo.

Ni jambo la faraja sana kwamba, hata katika mahojiano yake na vyombo mbalimbali vya habari amekuwa makini kujibu baadhi ya hoja zilizoandika katika makala ile ya anguko kama zile za uchanga wake katika siasa.

Amejenga hoja kuhalalisha uzoefu wake kiuongozi ndani ya chama na ndani ya Bunge. Pamoja na ukweli kwamba, bado naendelea kutofautiana na staili yake ya uchukuaji fomu, ikiwa ni pamoja na kushangazwa na hatua yake ya kukubali kuungwa mkono na baadhi ya watu ambao ama wana visasi, chuki binafsi binafsi dhidi ya Mbowe, Slaa, Komu, Mnyika, John Mrema na watendaji wengine wa makao makuu

Amenukuliwa akisema analo jukumu la kuponya majeraha ya makundi ndani ya Chadema yaliyoibuka kutokana na migogoro iliyowapokonya madaraka watu kama marehemu Chacha Wangwe na kuwakimbiza ndani ya chama hicho watu kama Dk. Walid Kabourou na wengine.

Katika hili naamini atakuwa amejipanga kuhakikisha matokeo ya uchaguzi utakaompa ama yeye au Mbowe ushindi, hayataibua makundi mapya ambayo yatampasa mwenyekiti ajaye kuanza kuyatibu.

Hoja ya Nchimbi ndani ya thread hii kwamba wao CCM hadi sasa wameshindwa kutibu majeraha ya Uchaguzi wa mwaka 2005 ni somo zuri kwa Zitto, Mbowe na viongozi na wanachama wote wa Chadema.

Wito wangu kwa wanajamvi ni kuweka mbele maslahi ya taifa wakati tunapojadili hoja za namna hii, ili kuepuka lugha za kudhalilishana na kupakana matope. Wale wanaoanza kupiga chini ya mikanda na wao wakajibiwa kwa utaratibu wao huo huo wanapaswa kuwa wavumilivu na kukubali kwamba wao ndiyo waanzilishi.

You all deserve my apology. I'm defeated, you have all won. The battle is on but the war have ended.

Goo Zitto...Goo Mbowe...Goo Chadema.. I always wish a strong multi party democracy.

Safi sana BRO. Nilitaka kuuliza mambo ambayo yangekuudhi..nina uhakika yangekuudhi....

Ila kwa kuwa umejielewa ukitaka nitakuuliza pembeni na nitakwambia kwanini nimekuuliza.

Article yako kama alivyosema Mkandara HAINA MAKOSA you are entitled to your maoni ila kaka CONFLICT OF INTEREST iliyopo inafanya wengine tunaotazama pande zote za shillingi tuwe na DOUBT na wewe kama sio kutumwa au Kutetea ajira etc.

Ila mkuu una akili safi sana na unahitajika humu kamanda Karibu sana!!

Fairplayer
 
Wana JF,

Hivi Zitto anagombea uenyekiti wa Chadema, je kama akishinda atagombea Uraisi mwakani au? Si kuna mahitaji ya umri?
 
Utatu;

Sio lazima mwenyekiti ndio agombee. Kumbuka ya NCCR Mageuzi uchaguzi uliopita

FP
 
Bantu,

Mimi na wewe tunafahamu kwamba Tanzania Daima ni mali binafsi ya Mtuhuru lakini jopo la Watanzania wanachofahamu ni kwamba hilo ni gazeti la Chadema na si mali binafsi ya Mwenyekiti wa Chadema. Ni gazeti la Upinzani. Utata unaanzia hapo.

Haya mdogo wangu ngoja basi kwa pamoja tuwaeleze wadanganyika kuwa TANGANYIKA DAIMA = MTU HURU!
Lakini kumbuka ni wale 5 asilimia tu ndo wataamini! teh, teh, teh!
 
Kibanda
Nakupa pongezi sana.Hapa tuko wachache sana katika jamvi hili ambalo watu huwa hata wakiona wamekosa hawawezi kusema samahani.

Kibanda umefanya jambo la kiume sana .Umesema mawazo yako yamepingwa yamekosolewa na mengine umeona mwenyewe uliko jikwaa katika kuwakilisha ujumbe na sasa unasema unakubali kuto kubaliana na hili ndilo jambo hasa .You are not being defeated hapana .Watu wamekataa kusemewa na kukuona wewe mtu ambaye wanakupa heshima kubwa kama kwamba ulikuwa na uapnde .Usiache kuendeleza yale mazuri ambayo umekuwa ukiyafanya wewe na waandishi wenzako kwenye Tanzania Daima .Kama umesema nia yako na upinzani wa nguvu basi mchango uzidishe na sisi tutakusema vyema kama JKN, Teddy Kennedy, Johaness Paulus wa II, ..........................................

Hisia zangu Kibanda kaandika haya kwa shinikizo la BOSI WAKE-MBOWE.kwani alikuwa kama MBOGO na hasikii la mtu.alisema yuko tayari kubaki peke yake hata apingwe na watu wote.watu watakuwa wamepeleka malalamiko kwa Mbowe kuwa anamtuma.jee vipi kina MSAFIRI ambao wameondolewa kwenye nafasi zao kwa ajili ya Zitto?

Kibanda sisi tulisema hukutusikia,amesema bosi umemsikiliza kweli mkono mtupu haulambwi.
sasa andika makala nyingine kurekebisha sumu hii uliyoisambaza. waombe msamaha wajinga wa Chadema uliyowataja humu kwa majina.
Zitto kakujibu Mwananchi na habari Leo.
 
Wana JF,

Hivi Zitto anagombea uenyekiti wa Chadema, je kama akishinda atagombea Uraisi mwakani au? Si kuna mahitaji ya umri?

Tatu issue ni Uenyekiti na majibumengie umesha pewa hapo juu .Chadema ije na style yao kwamba Mwenyekiti aende Bungeni na mtu mwingine hata Mkandara tutamweka agombee Urais atoke KAFU hahahahahahahha
 
Hisia zangu Kibanda kaandika haya kwa shinikizo la BOSI WAKE-MBOWE.kwani alikuwa kama MBOGO na hasikii la mtu.alisema yuko tayari kubaki peke yake hata apingwe na watu wote.watu watakuwa wamepeleka malalamiko kwa Mbowe kuwa anamtuma.jee vipi kina MSAFIRI ambao wameondolewa kwenye nafasi zao kwa ajili ya Zitto?

Kibanda sisi tulisema hukutusikia,amesema bosi umemsikiliza kweli mkono mtupu haulambwi.
sasa andika makala nyingine kurekebisha sumu hii uliyoisambaza. waombe msamaha wajinga wa Chadema uliyowataja humu kwa majina.
Zitto kakujibu Mwananchi na habari Leo.

Kanda2;

Hebu lete hiyo makala aliyojibu Zitto, tusaidie kaka
 
Home
Zitto aandaliwa cheo kumnusuru Mbowe
broken-heart.jpg

*YADAIWA NI KULINDA MASLAHI YA CHAMA

Waandishi Wetu

KATIKA kile kinachoelezwa kuwa ni kunusuru mustakabali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wazee wa chama hicho leo wanakutana, huku taarifa zikieleza kuwa Zitto Kabwe, ambaye ametangaza kumvaa Freeman Mbowe katika kinyang'anyiro cha Uenyekiti Taifa, anaandaliwa nafasi ya ukatibu mkuu kunusuru mpasuko ndani ya chama hicho.

Mkutano huo unaowahusisha waasisi wa Chadema, akiwamo wenyekiti waliopita, Edwin Mtei na Bob Makani pamoja na wazee wengine kadhaa, unafanyika katika kipindi ambacho tayari wadadisi wa masuala ya siasa wameonyesha wasiwasi wa chama hicho kupasuka iwapo hakutakuwa na busara ya kufanya maamuzi sahihi katika mchakato huo wa uchaguzi.

Iwapo ajenda hiyo ya kumpa Zitto nafasi ya katibu mkuu, itajadiliwa na kupitishwa leo, moja kwa moja itakuwa ni kwa ajili ya kumnusuru Mbowe na chama katika hatari ya kugawanyika. Juzi wazee hao, kwa nyakati tofauti, waliliambia gazeti hili kwamba, uamuzi wa Zitto kugombea ni ukuaji wa demokrasia ndani ya chama hicho.

Mzee Mtei alisema "ndiyo maana kinaitwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo", huku mzee Makani akisema "hakuna mpasuko kwani ni lazima kutakuwa na watu wanaomuunga mkono Zitto na Mbowe, hivyo huo si mpasuko".

Lakini Mwananchi ilipata habari jana jioni zikisema katika kupiga hatua moja mbele kunusuru chama hicho, wazee hao wamepata wazo jipya ambalo ni kufikiria namna bora ya kumtuliza Zitto kwa kumpatia nafasi hiyo ya mtendaji mkuu wa chama ambayo sasa inashikiliwa na Dk Willibrod Slaa, mmoja wa viongozi shupavu ambao wanaheshimika sana katika chama hicho kiutendaji.

Hata hivyo, bado swali linabaki kwamba iwapo Zitto atapewa nafasi hiyo, Dk Slaa atakuwa na nafasi gani kwenye chama hicho.

Tangu kuanza kwa maandalizi ya uchaguzi, Dk Slaa alishawishiwa na wanachama agombee nafasi ya makamu mwenyekiti, lakini alikataa kwa madai anataka kupumzika kazi za chama.

Hata hivyo, wachunguzi wa masuala ya uongozi ndani ya chama hicho wanasema kuwa kuna kundi la wanachama ambao wanataka Dk Slaa agombee urais 2010, lakini mara kadhaa yeye amekuwa akidai hataki nafasi hiyo na kwamba ataendelea kuwatumikia watu wa Karatu kwa nafasi ya ubunge.

Kwa upande wa Mbowe, hali inaonyesha kwamba safari hii hatagombea urais na badala yake ataenda Hai kwa ajili ya kugombea ubunge.

Ingawa watu wengi wanadhani Zitto amekurupuka kugombea nafasi hiyo, lakini watu ambao walio karibu na mwanasiasa huyo wanadai kuwa amejenga mtandao mkubwa kwa muda mrefu ambao utamsaidia sana kupambana na Mbowe.

"Zitto ameshiriki sana kuweka vijana hasa mikoani na Mbowe anakubalika na watu wa mjini na hasa Dar es Salaam na Kilimanjaro, lakini Zitto amejijenga," alisema mmoja wa watu walio karibu na Zitto, 33.

Mapema jana kabla ya taarifa hizo mpya, Zitto, akiwa jijini Dar es Salaam, alisema atakuwa tayari kupokea ushauri wowote utakaotolewa na wazee wa chama hicho.

Alifafanua kuwa huu ni wakati wa uchaguzi, lakini baada ya hapo Chadema itapaswa kuwa chama kimoja kisichokuwa na kambi yoyote.

Zitto alisema kwa mantiki hiyo iwapo atashinda, bado atapaswa kushirikiana na Mbowe na akishindwa, Mbowe atapaswa kushirikiana naye (Zitto), hivyo wanaoeneza propaganda chafu, hawajui nini chama hicho kinapaswa kutendewa.

Zitto, ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, pia alionyesha kuchukizwa na kile kinachoelezwa kwamba anatumiwa na mafisadi na kuhoji: "Ni akina nani hao wanaonitumia... wananitumia ili iweje?"

"Mimi Chadema ni basi langu ambalo nasafiria au sawa na mtumbwi wangu baharini, sasa nitawezaje kuivuruga, halafu nitapata faida gani au nitakwenda wapi,"alihoji.

Alisema kamwe hawezi kutumiwa na mtu yeyote kuvuruga chama hicho kwani ndilo tegemeo la Watanzania kama chama mbadala cha kushika dola.

Zitto hakusita kuweka bayana kwamba Chadema pia ina safari ndefu ya kuunganisha vyama vya upinzani na kujenga umoja imara ambao utakuwa na lengo moja tu la kuleta mageuzi.

"Ukweli ni kwamba NCCR, CUF, TLP na vyama vingine vya upinzani vinatuhitaji na sisi lazima tunavihitaji kushirikiana navyo kwenye maeneo mengi, sasa nitawezaje kuua Chadema badala ya kuimarisha na kuunganisha na wengine," alihoji.

Zitto, mwenye umri wa miaka 33 na mmoja wa wabunge ambao wamekuwa wapambanaji wakubwa ndani ya Bunge, alisema yeye bado mwanasiasa kijana kuliko wote kwenye nafasi ya juu ya uongozi wa Chadema, hivyo haiingii akilini kwamba ataweza kuvuruga chama wakati bado ana malengo ya baadaye kisiasa.

Aliongeza kusema: "Kwa sasa wakati tunajipanga kuelekea katika uchaguzi, mimi nadhani inatupasa tuangalie zaidi maslahi ya chama. Bado kuna maisha baada ya uchaguzi, isije kuwa baada ya uchaguzi tukashindwa kuangaliana.

Kama nikishinda nitakuwa katika nafasi nzuri ya kumpigia kampeni Mbowe huko Hai nikiwa kama mwenyekiti wake katika uchaguzi mkuu ujao," alisema Zitto.

Zitto alifafanua kwamba alilazimika kujaza fomu za kugombea kiti hicho akiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere baada ya kushauriwa sana na wenyeviti mbalimbali wa mikoa wa chama hicho.

"Kuna watu wanasema nilijaza fomu kwa mtindo wa kakakuona, lakini inatakiwa wajue kuwa siasa ni staili.

Mimi binafsi sikutaka kugombea uenyekiti, lakini shinikizo la wanachama ndilo lililo lilinifanya nigombee, nilijaza fomu nikiwa uwanja wa ndege wakati nikielekea Ujerumani baada ya kuona siwezi kuendelea kuyakataa maombi ya wanachama," alisema Zitto.

"Mimi sina ugomvi wowote na Mbowe labda yeye lakini, kesho wazee wa chama chetu tutakutana nao ili kuangalia kama kuna tofauti zozote tuzimalize," alisema Zitto.

Zitto alisema ana uwezo wa kukiendesha chama kutokana na kuwa na uzoefu mkubwa katika siasa za kitaifa na kimataifa.

"Mimi nimekuwa mshauri wa rais wa Ujerumani kuhusu mambo ya kiuchumi wa bara la Afrika kuanzia mwaka 2006, ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali yenye mashirika zaidi ya 193 na thamani ya zaidi ya Sh 3 trilioni, nitashidwa kuiongoza Chadema," alihoji Zitto.

Hata hivyo, alisema kama atashinda na kukishika kiti hicho mwenyekiti wa sasa, wa chama hicho Mbowe atakuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho kama katiba yao inavyosema.

Naye Mbowe alisema propaganda dhidi ya chama hicho haziwezi kukiyumbisha.

Mbowe, ambaye atagombea nafasi kwa mara ya pili, alisema chama hicho kimetoka mbali na kimejengeka katika misingi ya kidemokrasia, hivyo kila jambo linafanywa kwa uwazi na kwa kufuata kanuni na taratibu za chama hicho.

Mbowe aliliambia gazeti hili jana kuwa mamluki hawakosekani katika taasisi yoyote ile na kusisitiza kuwa maamuzi yote yanafanywa na vikao ndani ya chama na hakuna hata kikao ambacho kimeshakaa hadi hivi sasa.

"Propaganda kutoka kwa watu wa nje na hata baadhi ya vyombo vya habari haziwezi kuvuruga chama chetu, ni wazi kuwa mamluki hawakosekani katika taasisi yoyote ile, lakini chama chetu kina utaratibu wa kuamua mambo yake kupitia vikao mbalimbali. Hakuna maamuzi yanayotolewa bila kuafikiwa na vikao," alisema Mbowe.

Mbowe alisisitiza kuwa uamuzi wa Zitto ni matokeo ya demokrasia ndani ya chama na kuongeza kuwa ana imani kuwa chama kitapita katika kipindi ambacho ni kigumu katika siasa za demokrasia.

"Nina imani tutavuka salama; ni vema Watanzania wakaangalia chama si kwa utashi wa mtu anayeongoza bali kwa kile wananchi wanachofanyiwa na chama. Hiki ni chama cha Watanzania na tuna imani tutavuka salama," aliongeza Mbowe.

Aliongeza hata baada ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao, hatarajii kuwa kutakuwa na chuki na kutoelewana kwa viongozi wa chama hicho kwani wote wanafanya kazi kwa kujitolea na hakuna mshahara wanaolipwa.

"Viongozi wote wa ngazi za juu wanafanya kazi kwa kujitolea, tunachotafuta ni kazi ya kujitolea kuwatumikia wananchi na hakuna 'ulaji'…hakuna anayelipwa mshahara," alifafanua Mbowe.

Mwananchi ilipotaka kujua kama atagombea urais kwa tiketi ya Chadema iwapo atabaki kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Mbowe alisema: "Nafasi ya kugombea urais si wajibu wa kudumu wa mwenyekiti. Ni chama ndicho kitakachopendekeza nani na kwa sifa zipi ndio anafaa kugombea nafasi hiyo, alisema.

Mkutano mkuu wa Chadema umepangwa kufanyika Septembe 3 na 4 ambapo utatanguliwa na mkutano wa kamati kuu Septemba 30, na mkutano mkuu wa kwanza wa baraza la wazee utafanyika Septemba 31 mwaka huu.
Mwisho.

Hata hivyo, hadi sasa chama hicho kipo kwenye kipindi cha kigumu cha mpito kuelekea kwenye uchaguzi huo ambao ni mtihaani wa pili baada ya ule wa kifo cha Makamu Mwenyekiti Chacha Wangwe. Habari hii imeandaliwa na Ramadhan Semtawa, Claud Mshana na Fred Azzah
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom