Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

''Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa mahakamani''......

Hizi ndizo kauli Watanzania wanapenda kusikia............Baada ya hapa kila mtu anasahau na maisha yanaendelea; Hivi kesi ya aliyemuua Mwangosi inaendeleaje????
 
Pole sana kamanda mpiganaji. Mungu akujalie upone haraka na kurejea nyumbani kujenga taifa letu lililovamiwa na ibilisi.
 
All things are possble for who believe!!naamini siku si nyingi tutaujua huu mtandao wa kimafia na wafadhili wao..
Mungu amponye Kibanda na ampe unafuu wa maumivu yake
 
Taarifa kutoka South Africa, kupitia Jukwaa la Wahariri Tanzania

1. Kibanda leo ameingizwa theater ili kuanza kufanyiwa upasuaji na kujengwa sura baada ya kupungua kwa majeraha na uvimbe vilivyokuwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake, hususan kichwani na usoni.

2. Upasuaji huo unazingatia matokeo ya uchunguzi ulifanywa kwa zaidi ya saa 48 na jopo la madaktari na kubaini kwamba mbali na madhara ya awali, Kibanda pia aliumizwa taya lake la kushoto.

3. Kuhusu jicho lake la kushoto ambalo pia lilijeruhiwa, madaktari walisema wangetoa uamuzi kuhusu aina ya upasuaji ambao wangeufanya baada ya kubaini hali halisi wakati watakapokuwa wakijenga sura yake ambayo iliharibiwa kwa majeraha.

4. Wakati akipelekwa theater ambako alikuwa akifanyia upasuaji ambao uliotarajiwa kuchukua saa zaidi ya nne, alikuwa akilalamikia maumivu kutokana na kidonda kilichopo kwenye mguu wake wa kushoto. Kidonda hicho pia ni matokeo ya unyama aliyofayiwa.

5. Jana Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa mahakamani.

Tutaendelea kufahamishana kila hatua ya tiba ya Mwenyekiti wetu, na tunaomba tuendelee kumwombea ili apone haraka.

--

Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
+255 - 753 - 555556

============
UP DATE
============

Tunaposema kuwa CCM imechoka kutawala na inapaswa kupisha uwa tunaonekana kama wajinga. Unyama huu ati kwasababu mnataka kutawala milele, kweli jamani? Kwanini tusibishane kwa hoja? Hivi kama Kibanda uwa anaandika hoja zanazogusa maslahi yao, na wao si wana magazeti yao na vyombo vyao vya habari? kwanini wasimjibu huko? Kweli unamuweka mwenzako kilema cha maisha kwasababu ya siasa na madaraka? Very sad!!
 
Pole sana ndugu yangu Kibanda! Mimi uvumilivu wangu umefika kikomo!

Haiwezekani tuiache Tanzania mikononi mwa wahuni!

Inatosha!
 
Serikali ya jk at work!so sad!Get well soon kibanda!tutashinda tu vita!
 
Hivi KJ alishawahi hudhuria au tembelea familia ya Mwangosi, Ile ya Morogoro, Songea, Uli. au na watanzania wawezaotembelewa na Rais na wasio watanzania KJ inabidi ashauriwe
 
Pole sana brother Mwenyezi Mungu akujalie rehema zake upone haraka
 
Nchi ya viongozi wasanii! Hivi waliompiga risasi padri Ambross, waloomuua padri Mushi hivi wameshakamatwa?.. Waliomwagia tindikali shekhe kule znz? Na waliomwagia tindikali Said kubenea je?
HII NI NCHI YA VIONGOZI WASANII
Wapo umeambiwa kuwa Rais kasema serikali itajitahidi ................. kumbuka kujitahidi una maana gani. Kama wameshindwa kujifanya kitu kwenye kesi ya Ulimboka ambaye mpaka aliwapa jina la muhusika, sijui hapa tutegemee nini!!!!!!?
 
Hivi KJ alishawahi hudhuria au tembelea familia ya Mwangosi, Ile ya Morogoro, Songea, Uli. au na watanzania wawezaotembelewa na Rais na wasio watanzania KJ inabidi ashauriwe

kwa kujibu swali lako ndugu yangu, ni kwamba at least kwa case ya ulimboka hakwenda na sababu ni kwamba ULIMBOKA yeye mwenyewe alikataa kwa kusema hawezi na hakubali unafiki hata kidogo. Uli alimgomea JK
 
sijawahi kuona rais SHETANI kama rais wangu! LORD HAVE MERCY ON US! ugua pole muandishi! MUNGU WA HAKI ATATOA HUKUMU YA HAKI!
 
Pole sana ndugu yangu Kibanda! Mimi uvumilivu wangu umefika kikomo!

Haiwezekani tuiache Tanzania mikononi mwa wahuni!

Inatosha!
Pole kama mpaka leo ulikuwa hujaishiwa uvumilivu, mimi naendelea na google search yangu namna ya kuhudhuria mafunzo ya Udunguaji, najuwa hii itakuwa ajira inayolipa sana baada ya mwaka 2015.

Kuna harufu ya wizi wa kura sasa kutakuwa na njia mbadala za kuwaondowa viongozi ambao hamkuwachaguwa ila wamepora madaraka
 
sijawahi kuona rais SHETANI kama rais wangu! LORD HAVE MERCY ON US! ugua pole muandishi! MUNGU WA HAKI ATATOA HUKUMU YA HAKI!
Mungu anatuhurumia lakini hata shetani naye ana nguvu zake, Mungu ametuhurumia Fastjet haikuruka kwenda Venezuela kumzika Hugo Chaves kesho yake miguu ikamuwasha naona kaibukia South Africa anacheza Kwaito na Zuma, kwa kifupi tumeliwa.
 
Kweli kabisa!
''Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa mahakamani''......

Hizi ndizo kauli Watanzania wanapenda kusikia............Baada ya hapa kila mtu anasahau na maisha yanaendelea; Hivi kesi ya aliyemuua Mwangosi inaendeleaje????
 
"..............Navumilia tu ipo siku yatakwisha................"
 
Kauli za jk dhidi ya uhai hazina tija!
Na msitarajie wahusika kukamatwa.
Nakubaliana na ww mkuu. Watekaji na watesaji wa dr. ulimboka wanatesa tu mitaani.so it's bizness as usual!!:rockon:
 
Hivi KJ alishawahi hudhuria au tembelea familia ya Mwangosi, Ile ya Morogoro, Songea, Uli. au na watanzania wawezaotembelewa na Rais na wasio watanzania KJ inabidi ashauriwe

hapana ila alimsaidia teja mmoja na kumkaribisha ikulu kupata chakula cha jioni na kupiga picha..
 
Back
Top Bottom