Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

sijui bayana nini kitatokea ila Yehova amenionyesha watu wenye maandishi yaliyoandikwa kwa damu Walazendo wa nchi
wakishangilia na kutoa shukrani kwa Mungu na nilipotazama ilikuwa majira ya joto.

Cjaelewa
 
Rais kikwete tuna imani na wewe, tunakuomba ukomeshe vitendo hivi vya kinyama.

Wabongo bwana tu watu wa ajabu. Mwangosi aliuwawa mchana kweupe na askari polisi ambao mhe huyo ndio Amiri Jeshi mkuu wa jeshi hilo na Ulimboko alifanyiwa unyama huo huo kama aliofanyiwa Kibanda. Hawa wote ni watanzania ambao Rais ana wajibu wa kulinda usalama wao. hakufanya kitu wala kukemea. bado una imani naye - unless kama kuna Watanzania kamili na Watanzania nusu hapo nitaamini kuwa una imani naye kwa wale ambao kwake ni watanzania kamili! JK anafanya mambo ya kitoto kama kijana wake, riz1.
 
Bado ninatafakari hii elimu ya kutesa watu kwa KUNG'OA KUCHA, KUNG'OA MENO KWA PRISE KUPASUA VICHWA KWA NONDO, mimi ninafikiri lazima kipo chuo cha kufanya mambo haya kama kweli kuna nia thabiti ya uchunguzi waanzie hapo.

hICHO CHUO MBONA KILIKWISHA TAJWA NA GAZETI LA MTANZANIA NDUGU...
 
Aliitwa akajaa kwenye timing zao, sasa hakuna wa kumlaumu. mtu mzalendo hawezi kufanya kazi na shetani Rostam Aziz.
 
Taarifa kutoka South Africa, kupitia Jukwaa la Wahariri Tanzania

1.
Kibanda leo ameingizwa theater ili kuanza kufanyiwa upasuaji na kujengwa sura baada ya kupungua kwa majeraha na uvimbe vilivyokuwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake, hususan kichwani na usoni.

2. Upasuaji huo unazingatia matokeo ya uchunguzi ulifanywa kwa zaidi ya saa 48 na jopo la madaktari na kubaini kwamba mbali na madhara ya awali, Kibanda pia aliumizwa taya lake la kushoto.

3. Kuhusu jicho lake la kushoto ambalo pia lilijeruhiwa, madaktari walisema wangetoa uamuzi kuhusu aina ya upasuaji ambao wangeufanya baada ya kubaini hali halisi wakati watakapokuwa wakijenga sura yake ambayo iliharibiwa kwa majeraha.

4. Wakati akipelekwa theater ambako alikuwa akifanyia upasuaji ambao uliotarajiwa kuchukua saa zaidi ya nne, alikuwa akilalamikia maumivu kutokana na kidonda kilichopo kwenye mguu wake wa kushoto. Kidonda hicho pia ni matokeo ya unyama aliyofayiwa.

5. Jana Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa mahakamani.

Tutaendelea kufahamishana kila hatua ya tiba ya Mwenyekiti wetu, na tunaomba tuendelee kumwombea ili apone haraka.

--

Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
+255 - 753 - 555556

============Mungu atakuponya.
 
Absalom Kibanda amefanyiwa operesheni ya kuondolewa jicho ambalo yasemekana lilipigwa risasi.Source Tanzania Daima
 
Mchunguzeni anaelia sana Msibani -Roma Mkatolik kwenye nyimbo yake ya mr President, source Tanzania Daima!
 
Aliitwa akajaa kwenye timing zao, sasa hakuna wa kumlaumu. mtu mzalendo hawezi kufanya kazi na shetani Rostam Aziz.

'shetan' ndo anagharamia matibabu yote we upo kwenye key board unajifanya mzalendo umeshindwa hata kupeleka tshs 200 kwa familia yake ziwasaidie!
 
'shetan' ndo anagharamia matibabu yote we upo kwenye key board unajifanya mzalendo umeshindwa hata kupeleka tshs 200 kwa familia yake ziwasaidie!
Wewe ni zoba kabisa, Familia ya Kibanda halafu mimi ndio nipeleke tsh 200? are you serious? na Familia yangu apeleke nani pesa?

Wewe unajuwa Kibanda anamiliki nini na security ya familia yake ikoje? huyo shetani ndio mwajiri wa Kibanda na niwajibu wake kumtibia.
 
Taarifa kutoka South Africa, kupitia Jukwaa la Wahariri Tanzania 1. Kibanda leo ameingizwa theater ili kuanza kufanyiwa upasuaji na kujengwa sura baada ya kupungua kwa majeraha na uvimbe vilivyokuwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake, hususan kichwani na usoni. 2. Upasuaji huo unazingatia matokeo ya uchunguzi ulifanywa kwa zaidi ya saa 48 na jopo la madaktari na kubaini kwamba mbali na madhara ya awali, Kibanda pia aliumizwa taya lake la kushoto. 3. Kuhusu jicho lake la kushoto ambalo pia lilijeruhiwa, madaktari walisema wangetoa uamuzi kuhusu aina ya upasuaji ambao wangeufanya baada ya kubaini hali halisi wakati watakapokuwa wakijenga sura yake ambayo iliharibiwa kwa majeraha. 4. Wakati akipelekwa theater ambako alikuwa akifanyia upasuaji ambao uliotarajiwa kuchukua saa zaidi ya nne, alikuwa akilalamikia maumivu kutokana na kidonda kilichopo kwenye mguu wake wa kushoto. Kidonda hicho pia ni matokeo ya unyama aliyofayiwa. 5. Jana Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa mahakamani. Tutaendelea kufahamishana kila hatua ya tiba ya Mwenyekiti wetu, na tunaomba tuendelee kumwombea ili apone haraka. -- Neville C. Meena, Secretary General, Tanzania Editors Forum - TEF, Dar es Salaam - Tanzania. Cell: +255 - 787 - 675555 +255 - 753 - 555556 ============ UP DATE ============
I love Manyerere Jackton, he is a reall son-of-a-gun. Manyerere Jackton is a Dedicted Journalist who wants right on every side, his and mine too. Lakini Manyerere Jacton is a New-Generation young man who does not know and cannot truely comprehend why (for example) Mwalimu Nyerere was known to have 'kionambali". Ukimwambia Mtemi Fundikira kuhusu kionambali atakwambia anataka wenye nacho ndiyo wamwongoze. Manyerere anataka kiongozi mwenye bashasha, mcheshi, mbunifu n.k. Lakini Manyerere, hii ni Dunia ya Mungu na inaongozwa na Mungu Mwenyewe. Matakwa ya Mungu katika wabadamu hujulikana kwa wenye hivyo unavyoita vionambali. Hao huambiwa kesho kutakuwa na dhoruba, na keshokutwa ukame. Usidanywe na Idd Amini mwenye ndoto za mwendawazimu, waulize wazee wako kama kuna mwenye kionambali katika nchi. Mkimficha wote mnajitafutia majanga, wewe na wazee wako na hili wazee wengi sana huwa hawalitaki kwa sabau ni majanga ya kujitakia. Msimamo wa Manyerere Jackton kama kijana na mwana habari ni kutuingiza vichochoro vya kutoelewa nini maana ya kionambali kwa sababu tu vijana wamepata kusema bila kusahihishwa na wazee.Uhuru wa kuongea hata Masai aliukataa kwa Morani, siyo ujinga, ndiyo ujanja wenyewe wa kujua makubwa ya Mungu. Manyerere, tumwombee ndungu yetu Kibanda apone na arudi salama lakini meno matatu na jicho moja hana. Usidhani nafurahia hali hii ya Kibanda, nasikitikia sana pia na hali ya Dr. Ulimboka ambao sasa hivi nina hakika wataishia kuwa "Siri ya Taifa" kama mnavyowaita. Kinachonikera ni kuwepo akina Manyerere Jackton na kalamu zao wakitamba kila mahali bila kuona hatari wanazoziparamia. Sasa hivi Watz tumegeuka waganga majeraha baada ya kuangukia mikenge badala ya kuikwepa tukaenda salama. Mara mitihani, mara Padri kauwawa, mara Ulimboka katekwa. Tume za kuchunguza haya ni kipofu kusaka sindano gizani ambapo hata Kikwete mwenye macho haioni. Manyerere amka kutoka ujingani, tutakwisha huku tukionana wakati tunahudhuria misiba ya waliotutangulia.
 
Wewe ni zoba kabisa, Familia ya Kibanda halafu mimi ndio nipeleke tsh 200? are you serious? na Familia yangu apeleke nani pesa?

Wewe unajuwa Kibanda anamiliki nini na security ya familia yake ikoje? huyo shetani ndio mwajiri wa Kibanda na niwajibu wake kumtibia.

Lakini jamani nini tena?
 
Dr Robert OUKO,Waziri wa Mashauri ya Kigeni,Kenya Mwaka 1990 ALIDHANIWA KUJIUA NA KUJICHOMA MOTO(INASHANGAZA?)na MTUKUFU(Kama alivyokuwa) RAIS DANIEL ARAP MOI akihudhuria mazishi yake alisema NO STONE WILL BE LEFT UNTURNED na kwa kweli ni miaka zaidi ya 20 sasa mwuaji hakujulikana!
Hii ya Musee kusema Serikali ya Tz ITAWAKAMATA NA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATESAJI WA KAKA KIBANDA,UKIIITA HOAX HUTENDI DHAMBI YOYOTE!
GET WELL SOON BROTHER ABSALOM KIBANDA,MAY GOD, AND GOD ALONE, REVENGE FOR YOU!

Scotland Yard left no stone uturned but the Government had no muscles to rlease the report.
 
Kibanda amefanyiwa upasuaji chini ya madaktari bibwa watatu, kati ya maktari hao wawili wakiwa ni wataalam wa kichwa na mmoja ni mtaalamu wa macho,

katika upasuaji huo madaktari hao wamegundua kuharibika vibaya kwa jicho la mwanahabari kibanda kiasi cha kulazimika kuliondoa nahivyo wanaangalia namna ya kumwekea la plastiki.

eatv
 
Kibanda amefanyiwa
upasuaji chini ya madaktari bibwa watatu, kati ya maktari hao wawili
wakiwa ni wataalam wa kichwa na mmoja ni mtaalamu wa macho,

katika upasuaji huo madaktari hao wamegundua kuharibika vibaya kwa jicho
la mwanahabari kibanda kiasi cha kulazimika kuliondoa nahivyo
wanaangalia namna ya kumwekea la plastiki.

eatv

Looh, OMG!

Jicho la plastic? The enemy is wining ... we must do smthing ...!!
 
Back
Top Bottom