Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
2,436
4,429
Taarifa kutoka South Africa, kupitia Jukwaa la Wahariri Tanzania

1. Kibanda leo ameingizwa theater ili kuanza kufanyiwa upasuaji na kujengwa sura baada ya kupungua kwa majeraha na uvimbe vilivyokuwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake, hususan kichwani na usoni.

2. Upasuaji huo unazingatia matokeo ya uchunguzi ulifanywa kwa zaidi ya saa 48 na jopo la madaktari na kubaini kwamba mbali na madhara ya awali, Kibanda pia aliumizwa taya lake la kushoto.

3. Kuhusu jicho lake la kushoto ambalo pia lilijeruhiwa, madaktari walisema wangetoa uamuzi kuhusu aina ya upasuaji ambao wangeufanya baada ya kubaini hali halisi wakati watakapokuwa wakijenga sura yake ambayo iliharibiwa kwa majeraha.

4. Wakati akipelekwa theater ambako alikuwa akifanyia upasuaji ambao uliotarajiwa kuchukua saa zaidi ya nne, alikuwa akilalamikia maumivu kutokana na kidonda kilichopo kwenye mguu wake wa kushoto. Kidonda hicho pia ni matokeo ya unyama aliyofayiwa.

5. Jana Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa mahakamani.

Tutaendelea kufahamishana kila hatua ya tiba ya Mwenyekiti wetu, na tunaomba tuendelee kumwombea ili apone haraka.

--

Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
+255 - 753 - 555556

============
UP DATE
============

Wapendwa, habari za uhakika zilizofika sasa hivi kutoka hospitalini Afrika Kusini alikolazwa Kibanda ni kwamba ameshatolewa jicho moja ambalo liliharibiwa kabisa na wavamizi. Tayari ameshatoka Theater.Tutaendelea kujuzana.



 
Pole Mpiganaji, Allah yu pamoja na wenye Subira. Kwa rehma zake nakuombea UPONE haraka urejee nyumbani
 
Suala sio kuwasaka hao watu suala ni kwamba idara zetu za usalama zimekua dhaifu sana...haya masuala ya watu kutekwa kupigwa hayakuepo haya siku hizi kila mtu anajiita usalama wa Taifa hakuna hatua yeyote wanachukuliwa huu ni udhaifu wa Utawala wala hakuna lingine...
 
Dr Robert OUKO,Waziri wa Mashauri ya Kigeni,Kenya Mwaka 1990 ALIDHANIWA KUJIUA NA KUJICHOMA MOTO(INASHANGAZA?)na MTUKUFU(Kama alivyokuwa) RAIS DANIEL ARAP MOI akihudhuria mazishi yake alisema NO STONE WILL BE LEFT UNTURNED na kwa kweli ni miaka zaidi ya 20 sasa mwuaji hakujulikana!
Hii ya Musee kusema Serikali ya Tz ITAWAKAMATA NA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATESAJI WA KAKA KIBANDA,UKIIITA HOAX HUTENDI DHAMBI YOYOTE!
GET WELL SOON BROTHER ABSALOM KIBANDA,MAY GOD, AND GOD ALONE, REVENGE FOR YOU!
 
Suala sio kuwasaka hao watu suala ni kwamba idara zetu za usalama zimekua dhaifu sana...haya masuala ya watu kutekwa kupigwa hayakuepo haya siku hizi kila mtu anajiita usalama wa Taifa hakuna hatua yeyote wanachukuliwa huu ni udhaifu wa Utawala wala hakuna lingine...

nafikiri wewe jamaa hujawahi kusikia kitu kinaitwa ORGANISED CRIME toka uzaliwe si ndio.
Haya mambo yanatokea hata katika nchi zilizoendelea tofauti ya hapa na huko ni kuwa huko yameanza miaka mingi nyuma ,wakati hapa bado ni kitu kipya.
 
5. Jana Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa mahakamani.
Nigekuwa na uwezo wanafiki wote nigewa***, Walio mvamia kubenea mpaka leo hawajakamatwa licha ya kwamba kubenea anawajua na kikwete alitoa kauli kama hii akiwa India kama sikosei lakini mpaka leo hakuna hatua yoyote iliochukuliwa, likaja swala la Ulimboka tukapewa matumaini hakuna kitu mpaka leo, Mwandishe wa channel Ten Kikwte akamuua akasema ni kitu kizito hakuna hata funza ali wajibika na kuna mwandishi wa habari huko bukoba aliuwawa kinyama haja kamatwa hata sisimizi lakini alipo uwawa RPC wa Mwanza haikuchukua siku tatu watu zaidi ya 10 walikuwa wananyea debe....ni bora viongozi wote tanzania wafe ili tuanze upya kumbe wanajari maisha yao na jamaa zao
 
nafikiri wewe jamaa hujawahi kusikia kitu kinaitwa ORGANISED CRIME toka uzaliwe si ndio.
Haya mambo yanatokea hata katika nchi zilizoendelea tofauti ya hapa na huko ni kuwa huko yameanza miaka mingi nyuma ,wakati hapa bado ni kitu kipya.
Watu wanawafahamu kabisa kuwa nilivamiwa na furani na kisa ni hiki lakini kikwete kimya kwa kuwa waliomvamia ni watu waliotumwa na swaiba yake...
 
Sasa Makunga anakaimu ukusanyaji wa bahasha za mishiko toka NSSF, PPF, TCRA, NHC na nk. Hiki ni kizazi cha wahariri wa hovyo na wanaojirahisi sana. Usitarajie TEF ya namna hii ikasimamia maadili.
 
Kikwete nae mara yupo south..
Ya kubenea ilimkutia huko na hii ya kibanda hukohuko. Sijui ni coincidence au ndo kutotulia nyumbani?
 
Nchi ya viongozi wasanii! Hivi waliompiga risasi padri Ambross, waloomuua padri Mushi hivi wameshakamatwa?.. Waliomwagia tindikali shekhe kule znz? Na waliomwagia tindikali Said kubenea je?
HII NI NCHI YA VIONGOZI WASANII
 
JK anapingana na kauri ya mwanae sioni ukweli wa maneno yake hapo ndo imeisha. Angalia waliomtenda uli bado mwangosi bado fr mushi bado waliomtia tindikali kubenea waliomcharanga mapanga yule shekh bado walioua mchungaji geita bado walioua waendesha pikpiki songea bado endelea sijui kibanda lakini waliomtusi Makinda walishakamatwa

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
huyu jamaa hapa namnukuu "Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania." ni mnafiki sana.....kulikuwa na haja gani ya kuripoti upasuaji na kutuambia ya Jekey?.....ni heri wange kuumiza wewe Neville kwa kuwa ni mnafiki kuliko watu wote ninao wajua
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom