Baada ya Tundu Lissu kukiri kutamka maneno ya uasi na kukinukisha Jamuhuri imekosa mashahidi. Mawakili wa Serikali walidhani kuwa Lissu angekanusha matamshi yake kwa hiyo wakaandaa mashahidi, video na clips lukuki ambazo zingeonyesha hotuba alizozitoa kwa watia nia wa Chadema, mikutano ya hadhara aliyofanya katika Kanda zote alizotembelea na mazungumzo yote aliyofanya na vyombo vya habari.
Kwa mshangao wa Mawakili wa Serikali Lissu amekubali yote na sasa wana jukumu la kuchimbua katika vitabu vya sheria kama je matamshi yake ni uhaini? Hapo nawaona Mawakili wa Serikali jasho jembamba likiwatoka na misuli ya vibofu vya mikojo na utumbo mnene inayobana vinyesi ikilegea!
Kazi kwao Mawakili wa Serikali, na kwa hakika Lissu ni Big Brain Defender!
Nakumbu mh lissu kwenye press ile makao makuu ya chama alisema kwa kumnukuu.
(Kwamba wanasema kuzuia uchaguzi ni uhaini ,jibu ni ndio)
Hapa mweshimiwa aliwapeleka chaka nao wakajaa kibra, sasa ni jamuhuri kudhibitisha kwamba tangu lini kuzuia uchaguzi ni uhaini.
Mwanzo niliandika humu kwamba hii kesi inaweza fika mahala ikaibua hata kura za waliokuwa wagombea wa ccm na kushinda 2020 katika uchaguzi.
Pili mh lissu kwa wasilisho lake la juzi anaweza kumtaka yoyote kuwa shahidi upande wake atakavyoona inafaa, wakiwemo mashahidi wa siri, Mbowe, kigaila, mgombea wa chauma, n.k kwenye list yake ya mashahidi tiyari amewataja watatu (top 3), Tulia pia anaweza kuitwa .
Singinda inaenda kutoa Rais wa nchi hii nje ya ccm ,wanasinginda kesheni kwa kuimba nyimbo za kumtukuza Mungu.
Wanadoria kwenye mitandao ya kijamii mnatakiwa kuanza kutubu ila msikimbie nchi ,hakuna kulipa visasi asema Bwana