Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda aendelea kutoa ushahidi

Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda aendelea kutoa ushahidi

Brenda hadi muda huu anatawanya mawakili uchwara was gvt km ananawa vile. Halafu hawa mawakili uchwara kwanini wanauliza kdg, afu wana acha, hapo wanataka kumuachia nafasi kubwa Katuga bichwa cabbage, na ile mimacho kumchuzi yake, ananiboa yule mbwaa mie.
 
Brenda hadi muda huu anatawanya mawakili uchwara was gvt km ananawa vile. Halafu hawa mawakili uchwara kwanini wanauliza kdg, afu wana acha, hapo wanataka kumuachia nafasi kubwa Katuga bichwa cabbage, na ile mimacho kumchuzi yake, ananiboa yule mbwaa mie.
Brenda eats, breathes and bathes law. Hapo tu sio lawyer, je angekuwa lawyer mbona maCCM wangejinyea!😅🤣😅🤣
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI BRENDA RUPIA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 12.

MAJAJI WAMEREJEA MAHAKAMANI

1. Mawakili wa Serikali wapo tayari.
2. Lissu yupo tayari.
3. Shahidi yupo tayari kizimbani.

Jaji Ndunguru: Tuendelee upande wa mashtaka.

Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji, kolamu ipo vilevile.

Upande wa mashtaka upo tayari kuendelea na maswali ya dodoso.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa.

Lissu: Nipo tayari, Mheshimiwa.

Tawabu: Uliulizwa kuhusu Mwenyekiti kurusha matangazo ya Jambo TV, ukasema hiyo ni uongo kwa sababu Mwenyekiti siyo mfanyakazi wa Jambo TV.

Je, Mshtakiwa alikupitisha katika mashtaka dhidi yake?

Brenda: Alinipitisha wakati ananihoji.

Tawabu: Kwa hiyo, alikupitisha katika mashtaka yake ya kuchapisha kupitia Jambo TV, ndiyo maana ukasema yeye siyo mfanyakazi wa Jambo TV?

Brenda: Ndiyo, alisema hivyo.

Tawabu: Nikuonyeshe sasa hati ya mashtaka. Unionyeshe sasa wapi aliposhitakiwa kuchapisha habari kupitia Jambo TV kwenye hayo mashtaka.

Brenda: Ngoja nisome.

(Anasoma)

Brenda: Tundu...

Haipo.

Tawabu: Kwa hiyo, nitakuwa sahihi nikisema utetezi ulioutoa hapa Mahakamani hauhusiani na hii kesi?

Brenda: Unahusiana kwa asilimia 100.

Tawabu: Kuna watu uliwataja kwenye Sekretarieti, akina John Heche.

Brenda: Sijamtaja John Heche katika Sekretarieti.

Tawabu: John Kitoka?

Brenda: Ni sehemu ya Sekretarieti.

Tawabu: John Pambalu?

Brenda: Ni sehemu ya Sekretarieti.

Tawabu: John Mnyika?

Brenda: Ni sehemu ya Sekretarieti.

Tawabu: Ili uwe Sekretarieti ni lazima uitwe John?

Brenda: Siyo kweli. Mbona mimi naitwa Brenda?

Tawabu: Nilisikia unasema mmiliki wa content ni mwenye chombo cha habari.

Brenda: Ni sahihi.

Tawabu: Unamfahamu mtu anaitwa Diamond Platnumz?

Brenda: Namsikia.

Tawabu: Mboso Khan?

Brenda: Namsikia.

Tawabu: Marioo?

Brenda: Namsikia.

Tawabu: Wanajishughulisha na nini?

Brenda: Muziki.

Tawabu: Kile wanachokiimba kikichezwa kwenye TV siyo chao?

Brenda: Ni chao.

Tawabu: Ila Jambo TV wakicheza ya Lissu ni ya Jambo?

Brenda: Sijui, mimi nimezungumza kwa Lissu na Jambo TV.

Tawabu: Nilikusikia ukisema haya maneno kwenye hati ya mashtaka unaona siyo kosa.

Brenda: Ndiyo, siyo kosa.

Tawabu: Haya maneno ulitaka ayaseme kwa muda gani?

Brenda: Hata angesema asubuhi, mchana au usiku, kwa sekunde mbili, bado siyo kosa.

Tawabu: Kuna mahali alikuwa anakuuliza kama haya maneno alimtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mkurugenzi wa Mashtaka, Mkuu wa Mkoa, na wote ukasema hakuwataja. Na akakuuliza kama haya maneno yanatishia Serikali, ukasema hapana.

Brenda: Ndiyo.

Tawabu: Wewe ni nani kati ya hawa? Wewe ni Rais?

Brenda: Mimi siyo Rais.

Tawabu: Wewe ni Waziri Mkuu?

Brenda: Mimi siyo Waziri Mkuu.

Tawabu: Wewe ni Msemaji wa Serikali wa Tanzania?

Brenda: Mimi siyo Msemaji wa Serikali.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Back
Top Bottom