Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda aendelea kutoa ushahidi

Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda aendelea kutoa ushahidi

Mkuu naona sasa hivi watu wameshaanza kukupuuza Yani kama hawakuoni unachokiandika au wamekuIGNORE Kiana?
Gentleman,
sina haja ya kubabaika na uamuzi huru useless wa mdau yeyote wa Jf dhidi yangu au dhidi ya mtu mwingine yeyote yule jukwaani.

be free to do things as you wish and without permission of anybody. This is free platform for everyone 🐒
 
⚖️ TUNDU LISSU AENDELEA KUMHOJI SHAHIDI BRENDA RUPIA

SEHEMU YA 4 — TAREHE 8.9.2026

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo “kukinikisha” ni neno la kawaida.

Brenda: Kukinukisha ni slang, siyo neno la kawaida.

Lissu: Sasa nimekuuliza maana ya neno moja moja:

"Wanasema kitu kimoja sahihi hapa, msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli, ni kweli kwamba tunaomba kukinukisha vibaya sana uchaguzi..."

Hata maneno haya yanaonyesha kosa gani?

Brenda: Maneno haya hayana kosa.

Lissu: Sasa, Shahidi, ushahidi umetolewa Mahakamani hapa kwamba haya maneno yalikuwa katika video ya mtandao wa Jambo TV.

Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo wewe binafsi umeiona video hiyo.

Brenda: Waheshimiwa Majaji, mimi nimeiona video hiyo.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hiyo video ya Jambo TV ina urefu wa masaa mangapi?

Brenda: Waheshimiwa Majaji, masaa 2 na nusu hadi 3.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hiyo video uliyoiona, iwapo haya maneno niliyokusomea ndiyo maneno pekee yaliyopo katika hiyo video.

Brenda: Hapana, siyo maneno pekee.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama ulikuwapo wakati mashahidi wa upande wa mashtaka wanatoa ushahidi wao.

Brenda: Nilikuwepo wakati mashahidi wa upande wa mashtaka wanatoa ushahidi wao kwa kiwango kikubwa.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo umeiona hiyo video hapa Mahakamani.

Brenda: Hapana, sijaiona.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo video yenye haya maneno imeonyeshwa hapa Mahakamani.

Brenda: Hapana, sijaiona.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa uwepo wako Mahakamani, zaidi ya maneno hayo, waeleze Waheshimiwa Majaji uwepo wa ushahidi mwingine wowote zaidi ya maneno.

Brenda: Zaidi ya maneno, hakuna ushahidi mwingine wowote ambao nimeushuhudia.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
⚖️ TUNDU LISSU AENDELEA KUMHOJI SHAHIDI BRENDA RUPIA

SEHEMU YA 5 — TAREHE 8.9.2026

Lissu: Hiyo video ya Jambo TV nadaiwa mimi ndiye niliyeipeleka kwenye mitandao.

Brenda: Waheshimiwa Majaji, hiyo ni impossible. Hawezi kupeleka kwenye mtandao wa Jambo TV, na yeye siyo mfanyakazi wa Jambo TV.

Lissu: Nataka tuzungumze yaliyotokea tarehe 03 Aprili mwaka jana.

Baada ya mimi kufunguliwa mashtaka mwaka jana, palikuwa na kamata-kamata ya viongozi wa chama.

Waeleze Waheshimiwa Majaji kuhusu hii kamata-kamata.

Nassoro Katuga: Tunaomba hili swali lisiingie katika rekodi.

Shahidi hatujamsikia akisema palikuwa na kamata-kamata. Kwa hiyo, siyo ushahidi wake na tunaomba lisiingie hili swali. (Anakaa chini.)

Lissu: Waheshimiwa Majaji, swali langu siyo leading question.

Leading questions ni yale ambayo yana-attract “yes” au “no” answer.

Kamatakamata ni suala ambalo limejitokeza sana katika kesi hii.

Kwa hiyo, siyo leading question.

Kama Wakili Mkuu wa Serikali akisema nimeuliza vibaya, naweza kurudia, lakini siyo swali lisilotakiwa.

Nassoro Katuga: Hakuna sheria inayosema kuwa leading question ni swali ambalo lina-suggest “yes” au “no”.

But leading question ni swali ambalo linapendeleza jibu.

Tulitegemea kusikia kitu gani kilitokea kwa viongozi.

Lakini yeye ameshaambiwa kuwa viongozi walikamatwa na ushahidi umeshatolewa hapa Mahakamani.

Kwa hiyo, huyu ni shahidi wa mashahidi wengine.

Tuwe guided na sheria.

Kifungu cha 160 cha Evidence Act kinasema kuhusu leading questions, na Kifungu cha 159 kinaeleza aina za maswali.

Shahidi akiendelea, haitakuwa ushahidi wake yeye; anakuwa kama tape recorder.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Gentleman,
sina haja ya kubabaika na uamuzi huru useless wa mdau yeyote wa Jf dhidi yangu au dhidi ya mtu mwingine yeyote yule jukwaani.

be free to do things as you wish and without permission of anybody. This is free platform for everyone 🐒
Kaa Kwa kutulia, punguza vipengere
 
⚖️ TUNDU LISSU AENDELEA KUMHOJI SHAHIDI BRENDA RUPIA

SEHEMU YA 5 — TAREHE 8.9.2026

Lissu: Hiyo video ya Jambo TV nadaiwa mimi ndiye niliyeipeleka kwenye mitandao.

Brenda: Waheshimiwa Majaji, hiyo ni impossible. Hawezi kupeleka kwenye mtandao wa Jambo TV, na yeye siyo mfanyakazi wa Jambo TV.

Lissu: Nataka tuzungumze yaliyotokea tarehe 03 Aprili mwaka jana.

Baada ya mimi kufunguliwa mashtaka mwaka jana, palikuwa na kamata-kamata ya viongozi wa chama.

Waeleze Waheshimiwa Majaji kuhusu hii kamata-kamata.

Nassoro Katuga: Tunaomba hili swali lisiingie katika rekodi.

Shahidi hatujamsikia akisema palikuwa na kamata-kamata. Kwa hiyo, siyo ushahidi wake na tunaomba lisiingie hili swali. (Anakaa chini.)

Lissu: Waheshimiwa Majaji, swali langu siyo leading question.

Leading questions ni yale ambayo yana-attract “yes” au “no” answer.

Kamatakamata ni suala ambalo limejitokeza sana katika kesi hii.

Kwa hiyo, siyo leading question.

Kama Wakili Mkuu wa Serikali akisema nimeuliza vibaya, naweza kurudia, lakini siyo swali lisilotakiwa.

Nassoro Katuga: Hakuna sheria inayosema kuwa leading question ni swali ambalo lina-suggest “yes” au “no”.

But leading question ni swali ambalo linapendeleza jibu.

Tulitegemea kusikia kitu gani kilitokea kwa viongozi.

Lakini yeye ameshaambiwa kuwa viongozi walikamatwa na ushahidi umeshatolewa hapa Mahakamani.

Kwa hiyo, huyu ni shahidi wa mashahidi wengine.

Tuwe guided na sheria.

Kifungu cha 160 cha Evidence Act kinasema kuhusu leading questions, na Kifungu cha 159 kinaeleza aina za maswali.

Shahidi akiendelea, haitakuwa ushahidi wake yeye; anakuwa kama tape recorder.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Mwaga vitu, Manyanza!
 
⚖️ TUNDU LISSU AENDELEA KUMHOJI SHAHIDI BRENDA RUPIA

SEHEMU YA 3 — TAREHE 8.9.2026

Lissu: Naomba uwaeleze Waheshimiwa Majaji uwepo wa maneno “tunaenda kupiga watu wanaoenda kupiga kura au kuwakata vidole.”

Brenda: Waheshimiwa Majaji, hayo maneno hayapo.

Lissu: Kuna maneno yamesemwa kuwa kuna askari 17 wameuawa siku ya Uchaguzi Mkuu, tarehe 29 Oktoba. Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo kuna maneno kuwa “tutaua askari wa Polisi.”

Brenda: Hayo maneno hayapo.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji uwepo wa maneno “mkachome vituo vya daladala au mabasi yenyewe.”

Brenda: Hayapo kabisa.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji uwepo wa maneno “tutachoma moto vituo vya kupigia kura na tutawapiga wasimamizi wa vituo hivyo.”

Brenda: Hayo maneno hayapo.

Lissu: Kwa ufahamu wako, Shahidi, mtu akisema “msimamo huu unaashiria uasi,” anakuwa ametenda kosa gani?

Brenda: Mtu akisema “msimamo huu unaashiria uasi” siyo kosa, kwa sababu uasi ni pamoja na kupinga au kukataa jambo.

Lissu: Asante.

Na mtu akisema “tutazuia uchaguzi,” kwa ufahamu wako anakuwa ametenda kosa gani?

Brenda: Siyo kosa kusema “tutazuia uchaguzi.”

Lissu: Shahidi, mtu akisema “tutavuruga uchaguzi,” anakuwa ametenda kosa gani?

Brenda: Mimi siyo mtaalamu wa sheria na sijui sana, ila kwa maoni yangu siyo kosa.

Lissu: Siyo kwa maoni yako, kwa ufahamu wako je?

Brenda: Kwa ufahamu wangu, siyo kosa.

Lissu: Mtu akisema “tutahamasisha uasi,” anakuwa ametenda kosa gani?

Brenda: Anakuwa hajatenda kosa.

Lissu: Mtu akisema “tutakinukisha,” kwa ufahamu wako, hilo neno lina maana gani?

Brenda: Tutakifanya kinukie.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kukifanya kinukie ni kosa gani kwa sheria za nchi hii?

Brenda: Siyo kosa kwa sheria za nchi hii.

Lissu: Hata “kukifanya kinuke” ni kosa kwa sheria za nchi hii?

Brenda: Siyo kosa.⚖️ TUNDU LISSU AENDELEA KUMHOJI SHAHIDI BRENDA RUPIA

Brenda: Siyo kosa.
Tutakifanya kinukie 😊😊
 
08 September 2026
High of Tanzania
Kivukoni Front
Dar es Salaam, Tanzania

Treason case no. 19605 / 2025
Republic versus Tundu Lissu

1788854779122.png
 
⚖️ TUNDU LISSU AENDELEA KUMHOJI SHAHIDI BRENDA RUPIA

SEHEMU YA 6 — TAREHE 8.9.2026

Jaji Ndunguru: Unaweza kusema katika hilo?

Lissu: Nimewema, naweza kurudia swali.

Jaji Ndunguru: Shahidi anatakiwa atoe ushahidi wake kutokana na anachokifahamu. Tuwe directed na hiyo misingi.

Hata sisi tunaona ni leading question.

Muongoze shahidi katika mazingira anayoyafahamu.

Lissu: Asante, Waheshimiwa.

Lissu: Shahidi, kitu gani kilitokea baada ya Mwenyekiti kukamatwa?

Brenda: Baada ya Mwenyekiti kukamatwa, chama kilifungiwa tarehe 10 Juni.

Na baada ya hapo ukaanza ukamatwaji wa viongozi wa chama.

Na mimi mwenyewe nilikamatwa tarehe 12 Juni katika Namanga Border Stop, nikiwa naelekea Nairobi kwa ajili ya kumtembelea ndugu na baadaye nianze safari kuelekea Ujerumani.

Lakini sikufanikiwa kuvuka ile border.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji ulikuwa unaenda Ujerumani kufanya nini?

Brenda: Nilikuwa naenda Ujerumani kwa ajili ya training ya Communication Skills.

Lissu: Ielezee hiyo training, sisi hatujui.

Brenda: Kabla chama hakijafungiwa, Katibu Mkuu alimteua Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi kwenda kwenye mafunzo ya uongozi Ujerumani, lakini sikufanikiwa.

Nilikamatwa pale mpakani, nikasafirishwa kwenye Probox na watu waliokuwa pale mpakani.

Lissu: Probox ni kitu gani?

Brenda: Probox ni gari ndogo ambayo nyuma haina viti.

Wakaniingiza katika hiyo Probox kwa speed ya 120 na kuendelea hadi kituo cha Polisi Longido, lakini hawakuniandikisha pale kituoni.

Lissu: Kituo cha afya?

Brenda: Kituo cha Polisi.

Hawakuniambia kwa nini wamenipeleka Longido na hawakuniambia kwa nini tumesimama pale.

Lissu: Kitu gani kilitokea badala ya pale?

Brenda: Hata nilipouliza hawakuniambia.

Badala yake, palikuwa na confusion nyingi pale kituoni.

Palikuwa na kelele baina yangu na wale maafisa ambao wamenipeleka pale.

Wakaniambia wananipeleka Arusha.

Wakaniambia nipo salama, nipo mikononi mwa Polisi.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, ulipofika Arusha kitu gani kilitokea?

Brenda: RPC wa Arusha alikuja kuongea na mimi nje ya kituo kwenye gari.

Alijitambulisha kama RPC, sikumbuki jina.

Hapo kwa RPC ikaingia katika gari aina ya VX, yenye namba ya usajili ya Zanzibar.

Wakasema tunaelekea Dar es Salaam.

Hii gari ilikuwa ikitembea kwa speed kubwa sana.

Na kila waliposimamishwa walisema ni kazi maalum na tunaruhusiwa kupita.

Lissu: Mlikuwa mnasimamishwa na nani?

Brenda: Na wale traffic wa barabarani, walisema ni kazi maalum.

Lissu: Mlifika Dar es Salaam saa ngapi?

Brenda: Saa 10 alfajiri.

Wakawa wanamtafuta mtu ambaye nilitakiwa kufikishwa kwake. Wakaambiwa siyo hapa, nendeni Central.

Walivyofika Central, wakampigia George Byagemu (Deputy ZCO), akawaambia anakuja.

Lissu: Hiyo ni majira ya saa ngapi?

Brenda: Waheshimiwa Majaji, George Byagemu alifika saa 11 na nusu.

Lissu: Baada ya George Byagemu kufika, kitu gani kilitokea?

Brenda: Baada ya George Byagemu kufika, alisema kwamba ataniweka ndani wiki mbili.

Na baada ya hapo wakaniambia wamenikamata kwa sababu ya taarifa kwa umma niliyotoa tarehe 2 Julai 2025.

Hiyo taarifa kwa umma niliyotoa tarehe 02 Julai inahusiana na Mbunge wa Bunge la Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Nje kwenye Bunge la EU, anaitwa David McAllister.

Ilikuwa juu ya ripoti kwamba kuna mipango ya Mwenyekiti kupewa sumu akiwa kizuizini gerezani.

George Byagemu akakabidhiwa passport yangu yenye namba TAE481364, ambayo mpaka leo hii sijawahi kurudishiwa.

Wala simu yangu.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Back
Top Bottom