Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda aendelea kutoa ushahidi

Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda aendelea kutoa ushahidi

Hii mihimili haiheshimiani, Leo Tuko Msibani wao wanaendelea na kazi?
⚖️ TUNDU LISSU AENDELEA KUMHOJI SHAHIDI BRENDA RUPIA

SEHEMU YA 4 — TAREHE 8.9.2026

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo “kukinikisha” ni neno la kawaida.

Brenda: Kukinukisha ni slang, siyo neno la kawaida.

Lissu: Sasa nimekuuliza maana ya neno moja moja:

"Wanasema kitu kimoja sahihi hapa, msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli, ni kweli kwamba tunaomba kukinukisha vibaya sana uchaguzi..."

Hata maneno haya yanaonyesha kosa gani?

Brenda: Maneno haya hayana kosa.

Lissu: Sasa, Shahidi, ushahidi umetolewa Mahakamani hapa kwamba haya maneno yalikuwa katika video ya mtandao wa Jambo TV.

Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo wewe binafsi umeiona video hiyo.

Brenda: Waheshimiwa Majaji, mimi nimeiona video hiyo.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hiyo video ya Jambo TV ina urefu wa masaa mangapi?

Brenda: Waheshimiwa Majaji, masaa 2 na nusu hadi 3.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hiyo video uliyoiona, iwapo haya maneno niliyokusomea ndiyo maneno pekee yaliyopo katika hiyo video.

Brenda: Hapana, siyo maneno pekee.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama ulikuwapo wakati mashahidi wa upande wa mashtaka wanatoa ushahidi wao.

Brenda: Nilikuwepo wakati mashahidi wa upande wa mashtaka wanatoa ushahidi wao kwa kiwango kikubwa.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo umeiona hiyo video hapa Mahakamani.

Brenda: Hapana, sijaiona.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo video yenye haya maneno imeonyeshwa hapa Mahakamani.

Brenda: Hapana, sijaiona.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa uwepo wako Mahakamani, zaidi ya maneno hayo, waeleze Waheshimiwa Majaji uwepo wa ushahidi mwingine wowote zaidi ya maneno.

Brenda: Zaidi ya maneno, hakuna ushahidi mwingine wowote ambao nimeushuhudia.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
a
 
⚖️ TUNDU LISSU AENDELEA KUMHOJI SHAHIDI BRENDA RUPIA

SEHEMU YA 8 — TAREHE 8.9.2026

Lissu: Baada ya hapo, kilitokea kitu gani?

Brenda: Wakasema wanaenda kunipekua nyumbani Bashihaya, nikiwa kwenye karandinga la Polisi.

Lissu: Karandinga la Polisi ni yale malori?

Magari ya Polisi yale makubwa ambayo hayana milango?

Lissu: Mlipofika nyumbani, ikawaje?

Brenda: Wakapekua kila chumba na nguo zote.

Hawakuaniambia wanatafuta nini.

Lakini hawakukuta walichokuwa wanakitafuta.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo walikuwa na search warrant.

Brenda: Sikumbuki, nilikuwa under a lot of stress.

Lissu: Baada ya hapo?

Brenda: Tukarudi Central, wakaniweka mahabusu.

Lissu: Baada ya hapo, nini kilitokea?

Brenda: Nilikaa Central kwa siku 4 na nusu, mpaka mawakili wa chama walipokuwa wananifuatilia.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, ulikuwa chini ya uangalizi wa Polisi kwa siku ngapi?

Brenda: Siku 4 na nusu.

Lissu: Tarehe ngapi?

Brenda: Tarehe 15.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, tangu siku hiyo, kitu gani kinaendelea?

Brenda: Tangu siku hiyo sijawahi kupelekwa Mahakamani kushitakiwa mpaka leo.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa wewe kutoa taarifa kwa umma kwamba Mbunge wa Bunge la Ulaya na Mwenyekiti wa Mambo ya Nje wa Bunge la Ulaya alitoa taarifa juu ya kuwekewa sumu akiwa gerezani, wewe ulitenda kosa gani?

Brenda: Sikutenda kosa lolote lile.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kitu gani kilitokea baada ya hapo?

Brenda: Hakuna kilichotokea.

Lissu: ...

---

⚖️ Jaji Ndunguru: Mshtakiwa, tulikuwa tunajadiliana kuhusu shahidi kuongelea kukamatwa kwa wenzake, kama litakuwa ni fact na maana gani.

Lissu: Ishu ya direct knowledge, kinachotokea kwa mfanyakazi mwenzake.

Na ndiyo utetezi wangu kuhusu wafanyakazi wenzake na chama chake.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Brenda: Wakati mimi nakamatwa usiku wa tarehe 12, Mtaalamu wa Rasilimali wa chama, Leonard Magere, alikamatwa Airport ya Julius Kambarage Nyerere.

Lissu: Mtaalamu huyu naye alikamatwa kwa muda gani na kushikiliwa na Polisi?

Brenda: Sikumbuki kwa muda gani, ila nakumbuka kukutana naye mahabusu ya Central.

Nakumbuka pia Amani Sam Golugwa alikamatwa Airport akielekea Belgium.

Pia pakawa na muendelezo wa ukamataji wa viongozi wa chama. Makamu pia alikuja akakamatwa na kukaa mahabusu kwa muda mrefu.

Lissu: Ulisema ulikutana na Magere mahabusu Central...

Nassoro Katuga: (Anasimama.)

Lissu: Basi hilo naliacha.

Waeleze Waheshimiwa Majaji kwamba wewe umekamatwa, Magere amekamatwa, Amani amekamatwa na Makamu amekamatwa.

Je, ni nani amefunguliwa kesi kati ya hawa?

Brenda: Hakuna aliyefunguliwa mashtaka.

Lissu: Kwa kifupi, ulieleza Waheshimiwa Majaji hotuba yangu ilichukua masaa 2 hadi 2 na nusu.

Hiyo hotuba ya masaa 2 hadi 2 na nusu ilihusu mambo gani makuu?

Brenda: Waheshimiwa Majaji, Mwenyekiti katika hotuba ya masaa 2 hadi 2 na nusu ilikuwa inahusu:

  • Matatizo ya mfumo wa uchaguzi.
  • Matatizo ya chaguzi zilizopita.
  • Kwa nini nchi inahitaji electoral reforms.
  • Kwa nini tunatakiwa kuwaeleza wananchi kuhusu msimamo wetu wa No Reform, No Election.
  • Kwamba hajawahi kupatikana uchaguzi wa kidemokrasia.
  • Na mwisho, hayo maneno ya “tutahamasisha uasi” yalitokana na G55.

Lissu: G55 ni kitu gani?

Brenda: Ilikuwa ni kundi ndani ya chama lililotaka kushiriki uchaguzi.

Kwamba msimamo wa No Reform, No Election unaashiria uasi.

Mwenyekiti alikuwa anaelezea kwa nini kama chama tupinge uchaguzi usio huru na wa haki.

Lissu: Asante.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
⚖️ TUNDU LISSU AENDELEA KUMHOJI SHAHIDI BRENDA RUPIA

SEHEMU YA 8— TAREHE 8.9.2026

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama kwenye maelezo yangu kuna nia ya kutishia Serikali.

Brenda: Katika maelezo yako hakuna sehemu umetishia Serikali.

Lissu: Umenifahamu kwa muda gani?

Brenda: Kwa miaka 13, kama kiongozi anayepigania haki na mgombea urais.

Kama Mwenyekiti wa chama.

Mpiganaji aliyeumizwa na Serikali ya Tanzania kwa kutokupewa mafao yake ya Kibunge.

Kwa kuwa harassed, kukamatwa mara kadhaa na kuwekwa mahabusu na kutolewa kwa sababu ya misimamo yake ya kupambania haki itendeke na ionekane ikitendeka.

Pia, kama Mwenyekiti wa chama kikuu cha siasa cha Demokrasia na Maendeleo.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kwamba mtu akikwambia huyo mtu uliyemwelezea hivyo ni muhaini, wewe utasemaje?

Brenda: Inaonyesha ni mzalendo, very patriotic, na mtu mwenye mapenzi mema na nchi yake. Ni vigumu kuwa muhaini.

Lissu: Nimemaliza, Waheshimiwa Majaji.

Asante. (Anakaa.)

⚖️ Jaji Ndunguru: Upande wa Mashtaka, tuendelee na cross-examination.

Ajuaye Zegeli: Mheshimiwa Jaji, ataanza Wakili wa Serikali Mwanuka, halafu wengine watafuatia.

Lissu: Naomba break ya dakika tano.

Jaji Ndunguru: Sawa.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
⚖️ MAHAKAMA YAENDELEA NA MASWALI YA DODOSO

SEHEMU YA 9— TAREHE 8.9.2026

Jaji Ndunguru: Tuendelee na maswali ya dodoso.

Kasara: Pole kwa ushahidi mrefu.

Brenda: Asante.

Kasara: Katika ushahidi wako mrefu, ni sahihi nikisema hujaeleza kwamba una elimu yoyote ya uandishi wa habari?

Brenda: Sijaeleza.

Kasara: Ni sahihi nikisema kwamba unafanya kazi kwa mazoea na siyo professionalism? Unafanya kazi kimazoea, huna taaluma yoyote ya uandishi wa habari?

Brenda: Hapana.

Kasara: Ni sahihi, katika maelezo yako hujaiambia Mahakama una uzoefu wa muda gani?

Brenda: Waheshimiwa Majaji, niliiambia Mahakama kwamba nilichaguliwa tarehe 1 Machi 2025 hadi mwaka huu, tarehe 12 Machi, ni mwaka mmoja.

Kwa sasa nina mwaka mmoja na miezi mitano kazini.

Kasara: Ni sahihi, Shahidi, katika ushahidi wako hujaeleza ni majukumu gani unayofanya katika nafasi yako ya Mkurugenzi wa Mawasiliano?

Brenda: Ni sahihi.

Kasara: Nilikusikia katika ushahidi wako unasema wewe uliandaa matangazo na kuandika katika pages mbalimbali.

Brenda: Ni sahihi.

Kasara: Ni sahihi nikisema hapa Mahakamani hukutaja hizo pages?

Brenda: Ni sahihi.

Kasara: Shahidi, unaweza kuiambia nini Mahakama mtu akikwambia “live streaming”?

Brenda: It is to show live broadcasting, that's what I can say.

Kasara: Ni sahihi nikisema kwamba mnafanya kazi na Jambo TV bega kwa bega?

Brenda: Tunafanya kazi na waandishi wa habari wote. Sijui bega kwa bega ndiyo nini.

Kasara: Mwenyekiti katika ushahidi wake alisema kwamba mnafanya kazi na Jambo TV kwa ukaribu zaidi.

Kati yako na Mwenyekiti, nani yupo sahihi?

Brenda: Wote tupo sahihi. Tunafanya kazi na wote.

Kasara: Katika Mkutano wa tarehe 03 Aprili 2025, kuna wakati wowote mliwaondoa waandishi wa habari mkabaki viongozi?

Brenda: Ni sahihi.

Kasara: Wakati unaongozwa na Mshtakiwa/Mwenyekiti wako wa chama, ni sahihi kwamba ulikuwepo katika mkutano huo?

Brenda: Ni sahihi, nilikuwapo.

Kasara: Ni sahihi ulisikia maneno kama “kukinikisha” na “kuzuia uchaguzi”?

Brenda: Ni sahihi.

Kasara: Yapo katika hati ya mashtaka?

Brenda: Ni sahihi.

Kasara: Ni sahihi kwamba chama chenu mlisusia uchaguzi mwaka jana?

Brenda: Hatukususia.

Kasara: Mlichukua fomu zozote katika uchaguzi huo?

Brenda: Hatukuchukua.

Kasara: Ni sahihi kwamba mlしたutana na watia nia wa kugombea nafasi mbalimbali?

Brenda: Ni sahihi.

Kasara: Unaelewa nini kuhusu No Reform, No Election?

Brenda: Hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi.

Tulitaka Rais asiwe na mamlaka ya kuchagua wajumbe wa Tume.

Rais asiwe anateua Mwenyekiti wa Tume.

Tulitaka matokeo ya Urais yahojiwe Mahakamani.

Tulitaka wasimamizi katika kata wasiwe Watendaji wa Kata.

Kasara: Kwa haya yote unayosema, ndiyo mkaona ni sahihi kususia uchaguzi?

Brenda: Hatukususia. Tulitaka hata watawala waendelee kwa miaka 3 ili tupate uchaguzi huru na wa haki.

Kasara: Nilikusikia hapa Mahakamani kwamba Mwenyekiti wako alisema kuzuia uchaguzi siyo kosa, ukasema siyo kosa.

Je, ni sahihi kwamba chaguzi zote zipo kwa mujibu wa sheria za nchi?

Brenda: Ni sahihi, zipo kisheria.

Kasara: Ni kweli sasa mtu akizuia uchaguzi anakuwa amevunja sheria?

Brenda: Siyo kweli.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Brenda bhana -> Uchaguzi upo kwa mujibu wa sheria, ameulizwa ukivunja sheria utakuwa umetenda kosa anasema hapana.

Tukiwaambia CHADEMA ni kundi la wapumbavu mnakataa
 
⚖️ MAHAKAMA YAENDELEA NA MASWALI YA DODOSO

SEHEMU YA 10 — TAREHE 8.9.2026

Kasara: Umeeleza hapa kukamatwa kwako, ukaja Mahakamani Namanga, na kwamba ulikuwa unaenda Ujerumani katika training ya Communication Skills.

Brenda: Ni sahihi.

Kasara: Je, umeleta uthibitisho hapa Mahakamani kwamba ulikuwa unaenda Ujerumani kwa training ya Communication Skills?

Brenda: Ni sahihi, sijaleta.

Kasara: Ni sahihi, katika ushahidi wako hapa Mahakamani hujaieleza Mahakama ni namna gani uliweza kuchaguliwa kupata cheo cha namna hiyo?

Brenda: Nilieleza Mahakamani.

Kasara: Kuhusu utaratibu wa namna gani mtu anachaguliwa katika nafasi hiyo?

Brenda: Sijaulizwa.

Kasara: Unaelewa nini maana ya uasi?

Brenda: Kwa maana yangu ni kupinga, kukataa na kukataa kwa nguvu kubwa.

Kasara: Kwa hiyo Mwenyekiti aliposema “kuhamasisha uasi” alikuwa anamaanisha kupinga kwa nguvu kubwa?

Brenda: Sijasema hivyo.

Kasara: Una uelewa gani katika muktadha wa kile kikao, Mwenyekiti wako aliposema “kukinikisha”?

Brenda: Kukinukisha ni kutoa harufu.

Kwa hiyo, kwa mujibu wa kile kikao, kukinikisha ilikuwa ni kufanya kila mtu ajue tunapinga.

Kasara: Waheshimiwa Majaji, mimi naishi hapa.

Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji, anaendelea Cuthbert.

Cuthbert: Shahidi, habari yako?

Brenda: Salama.

Cuthbert: Kwa sasa utakubaliana na mimi kuwa hakuna ubishi kwamba Mwenyekiti alisema yale maneno?

Brenda: Nakubali.

Cuthbert: Kuhamasisha uasi?

Brenda: Alisema.

Cuthbert: Kuzuia uchaguzi?

Brenda: Alisema.

Cuthbert: Kukinukisha?

Brenda: Alisema.

Cuthbert: Unajua Mshtakiwa anashitakiwa na nini?

Brenda: Najua, ila naweza kujikumbusha.

Cuthbert: Kwa hiyo wewe umekuja kutetea kitu usichokijua?

Brenda: Najua.

Cuthbert: Ulisema ulikamatwa Namanga?

Brenda: Ndiyo, nilisema.

Cuthbert: Ukasema hawakukwambia kosa?

Brenda: Waliniambia kuwa ni kwa taarifa ya tarehe 02 Julai 2025.

Cuthbert Mbilinyi: Unajua kwamba kuna msemo kuwa “jinai haiozi”?

Brenda: Najua.

Cuthbert: Kwa hiyo unajua kwamba hata siku zikapita, wanaweza kukukamata na kukupeleka Mahakamani?

Brenda: Watakavyoona inafaa.

Cuthbert: Nilisikia unasema kwamba Leonard naye alikamatwa. Ni yeye tu au kuna wengine?

Brenda: Ni yeye tu ndiye nimemtaja.

Cuthbert: Kuna uthibitisho wowote umeleta kuonyesha Leonard alikamatwa?

Brenda: Kuna taarifa ya Jeshi la Polisi ilitoka.

Cuthbert: Hiyo taarifa uliileta hapa Mahakamani?

Brenda: Sijaileta hapa Mahakamani.

Cuthbert: Hebu tueleze namna ya kumpata Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi.

Brenda: Kuna kuwa na mashauriano kati ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu.

Baada ya hapo, Katibu Mkuu anapeleka mapendekezo katika Kamati Kuu.

Na Kamati Kuu inateua.

Cuthbert: Ni sahihi kwamba huwezi kuchaguliwa kama siyo mwanachama?

Brenda: Ni sahihi.

Cuthbert: Unafahamu au hufahamu nani aliyekupendekeza?

Brenda: Sifahamu.

Cuthbert: Utakubaliana na mimi ni mmoja kati ya viongozi ndani ya chama ndiye aliyependekeza?

Brenda: Nitakubaliana.

Cuthbert: Na utakubaliana na mimi utendaji wako wa kila siku unaripoti kwa viongozi wakuu wa chama?

Brenda: Direct Boss ni Katibu Mkuu, lakini natoa taarifa kwa Sekretarieti ya chama.

Cuthbert: Ni sahihi kwamba unapofanya makosa, ngazi yako ya kinidhamu ni ipi ndani ya chama?

Brenda: Kamati Kuu.

kuzuia kitu (hata kama kitu hicho Kiko kwa mujibu wa Sheria) lazima pia pawepo na Sheria inayotamka kuwa ni kosa. Sasa ni Sheria ipi inayosema kuzuia uchaguzi ni kosa.

got me?
 
Asante sana mkuu Manyanza
 
Brenda bhana -> Uchaguzi upo kwa mujibu wa sheria, ameulizwa ukivunja sheria utakuwa umetenda kosa anasema hapana.

Tukiwaambia CHADEMA ni kundi la wapumbavu mnakataa
20250826_193745.jpg

Haya ndio yanayokataliwa.
 
Back
Top Bottom