Kesi ya Mbowe: Ushauri wa Bure kwa Mawakili Wasomi - Utetezi

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,823
35,829
Awali ya yote pokeeni pongezi za dhati kwa kazi takatifu mnayoifanya ya kuisaka haki katika mazingira magumu.

Kazi yenu ni ngumu zaidi hasa ikizingatiwa kuwa mafanikio yoyote yanayopatikana yanahatarisha matumbo ya watu yenye uchu uliopitiliza.

Jambo moja la hakika lenye kutia moyo ni kuwa tupo watanzania mamilioni nyuma yenu. Hawa wako katika kada zote, weledi mbalimbali na karama za aina zote. Tafsiri halisi ya maneno haya:

IMG_20211110_090602_953.jpg


Ni dhahiri kuwa ipo nia na mikakati ya dhati ya kuipora haki mchana kweupe. Mifano iko mingi na iko wazi.

Albert Einstein anasema:

“Insanity is doing the same thing over and over and expecting different results.”

Tunayo sababu ipi ya kutegemea majibu tofauti sasa?

Muhimu kujipanga kivingine. Muhimu kuendelea kukusanya ushahidi ukiwamo bora zaidi kila inapowezekana dhidi yao.

Wajumbe wa kujitolea kwenye haya tupo wengi. Tusipuuzie wala kudharau jambo. Twende kwenye uhalisia zaidi yakiwamo matumizi ya sayansi, kuwaumbua majambazi hawa wa haki:

IMG_20211111_094418_637.jpg


Tulete mashahidi zikiwemo video kutokea RAU madukani. Kama vipi mahakama iombwe kwenda sehemu zinazotajwa ikiwamo RAU madukani.

Mahita na kundi lake walipita kushoto na wenzao kulia. Eneo kulikuwa wazi na walipaki nyuma ya hilo banda. Waonyeshe Lijenje angeweza kutoweka vipi bila kuonekana.

Mahakama iombwe kutumia mamlaka yake kuwalazimisha kumleta Lijenje, wako naye.

Mahakama iombwe kushurutisha taarifa zozote kupatikana popote kwa mustakabala wa haki.

Mizunguko ya Kingai na kundi lake Moshi - Arusha - Moshi - Dar - Mbweni ithibitishwe siyo kwa maneno matupu.

Maneno matupu hayavunji mfupa na mkono mtupu haulambwi

Aluta Continua!

---------

Detention Register: Jaji Tiganga yuko Majaribuni - Kiza Kinene

(S.M.P2503 - credit kwako mkuu)
 
Hi kesi, waTanzania watakacho ambulia ni kuona kwamba hi serikali haina aibu hata mahakama elisha tekwa na mhimili mgine, Jaji hata jambo ambalo liko wazi anahilisha kesi ili kupata consultation kwa wa ajiri wake, swali la kwanza angekua jaji huru ange hoji hi rejesita imefikaje hapa? na nani kaitoa? sio kuahilisha kesi tena
 
Detention register iliyotakiwa kuwa store ilikuwa tayari tayari ndani mahakamani.

Hiiiiii bagosha!
Ili swali nilijiuliza sana jana. Ilikuwaje ike nyalaka ikawa mahakamani asi if mahakama tayari ilijua kuwa jamaa wangeihitaji.

Kibatala nilipenda sana alivyokuwa anaiattack mahakama indirectly kupitia mawakili wa mashtaka kuwa "Tukiondoa fact kwamba hii nyaraka imetolewa hapa ndani kutoka kwenye makablasha ya mahakama, ila ila haiondoi fact kuwa ilitakiwa iwe store, so hapa tuna assume ni kama vile masijala"
 
Neno Jaji nilikuwa naliogopa hata kulitamka kumbe lilishajifia na akina Mwalusanya. Imebaki kama a mere ceremonial title.

Jiwe katuharibia sana hii nchi leo hii Zimbabwe, Burundi, Msumbiji, Uganda, Rwanda na sisi tuko daraja moja.

Hata ndondo cup hatustahili.
 
Ili swali nilijiuliza sana jana. Ilikuwaje ike nyalaka ikawa mahakamani asi if mahakama tayari ilijua kuwa jamaa wangeihitaji.

Kibatala nilipenda sana alivyokuwa anaiattack mahakama indirectly kupitia mawakili wa mashtaka kuwa "Tukiondoa fact kwamba hii nyaraka imetolewa hapa ndani kutoka kwenye makablasha ya mahakama, ila ila haiondoi fact kuwa ilitakiwa iwe store, so hapa tuna assume ni kama vile masijala"

Yapo mengi. A more robust approach is wanting.
 
Neno Jaji nilikuwa naliogopa hata kulitamka kumbe lilishajifia na akina Mwalusanya. Imebaki kama a mere ceremonial title.

Leo yasikie - Luvanda, Siyani, Tingatinga ni ukakasi mtupu.
 
Shida ni hawa ndugu zangu CCM,, hawataki kuachia madaraka kamwe,,. Kwao madaraka imekuwa kama chakula chao ,hawawezi kuishi bila madaraka,, kwa mm nahisi katika chama chenye madudu mengi ni hawa ndugu CCM,, wanaogopa siku wakitoka ndiyo itakuwa mwisho wa wao.
Kama wakoloni tu
 
Wamenajisi mahakama kwa kweli sasa chombo huru sijui kipi? Jeshi? Daaaa katiba mpys....
 
kama watu wanateuliwa ili watekeleze matakwa yako na siyo sheria unategemea nini? Mahakama ni muhimili uliopata aibu sana kipindi hiki, wenzetu Kenya wanatucheka sana
 
Back
Top Bottom