mtoto wa mchungaji
JF-Expert Member
- Oct 24, 2020
- 279
- 480
Mim si Mwanasheria na sijui sharia na siamini kama sheria inaweza kutenda haki hasa hizi sheria za kigeni tulizorithi kutoka kwa wakoloni. Nilishanga malumbano ya jana mahakamani mimi sikuyaelewa ila nilielewa jambo moja tu kuwa kesi ya mwenyekiti wa taifa Mbowe bado haijapelekwa katika mahakama yenye uwezo wa kusikiliza kesi ya ugaidi na zoezi hilo halijulikani litafanyika lini ila ni lazima atafikishwa siku moja katika mahakama hiyo yenye nguvu ya kusikiliza kesi hiyo.
Mpaka sasa najua kesi ipo Kisutu na sijui mahakama ipi ya mwanzo, ya kata, ya wilaya, ya mkoa au ipi, na kupita mahakama zote hizo itachukua miezi mingapi au miaka mingapi kusililizwa na kutolewa hukumu.
Hii inaonyesha kuwa Mbowe atasota sana ndani kwa utaratibu uliopo ndiyo maana kwa ushauri wangu sisi watu wa kanisa kama unaweza kuwa mchunguzi utagundua tunatii mamalaka kama Biblia ilivyo agiza ikija mamlaka inasema tusali tunasali na ikija mamlaka nyingine inasema sasa chanjo au vipi tunahamia huko hii yote kuepuka matatizo kama yanayompata Mbowe.
Na hata wakati wa kampeni najua mmesahau siwakumbushi. Na kutii mamlaka mbona ni rahisi tu. Leo uwezi kukuta mchungaji au sheikh katika mikusanyiko ya kijamii kama misiba, ndoa au kusanyiko lolote lile ambalo si la kidini kusikia akisalimia asalaam alaykum au bwana Yesu asifiwe au tumsifu Yesu Kristo wote ni mwendo wa nawasalimia kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, basi.
Hii nchi Mungu ametupa ni ya amani na utulivu, hivyo kesi hii kwa uzoefu wangu inaweza kuwa kama ile ya watu wa Uhamsho ambayo wao walisota takribani miaka 10 na wametoka selo juzi wameturiaa kinyaa hii ndiyo serikali jamani si kilamtu aote sharubu.
Najua mitusi itaporomoswa lakini ukweli ndiyo huo hapa ndiyo tulipo.