Kesi ya Mbowe bado inadaiwa haijafikishwa katika mahakama yenye uwezo wa kusikiliza kesi ya ugaidi

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
262
500
Mim si Mwanasheria na sijui sharia na siamini kama sheria inaweza kutenda haki hasa hizi sheria za kigeni tulizorithi kutoka kwa wakoloni. Nilishanga malumbano ya jana mahakamani mimi sikuyaelewa ila nilielewa jambo moja tu kuwa kesi ya mwenyekiti wa taifa Mbowe bado haijapelekwa katika mahakama yenye uwezo wa kusikiliza kesi ya ugaidi na zoezi hilo halijulikani litafanyika lini ila ni lazima atafikishwa siku moja katika mahakama hiyo yenye nguvu ya kusikiliza kesi hiyo.

Mpaka sasa najua kesi ipo Kisutu na sijui mahakama ipi ya mwanzo, ya kata, ya wilaya, ya mkoa au ipi, na kupita mahakama zote hizo itachukua miezi mingapi au miaka mingapi kusililizwa na kutolewa hukumu.

Hii inaonyesha kuwa Mbowe atasota sana ndani kwa utaratibu uliopo ndiyo maana kwa ushauri wangu sisi watu wa kanisa kama unaweza kuwa mchunguzi utagundua tunatii mamalaka kama Biblia ilivyo agiza ikija mamlaka inasema tusali tunasali na ikija mamlaka nyingine inasema sasa chanjo au vipi tunahamia huko hii yote kuepuka matatizo kama yanayompata Mbowe.

Na hata wakati wa kampeni najua mmesahau siwakumbushi. Na kutii mamlaka mbona ni rahisi tu. Leo uwezi kukuta mchungaji au sheikh katika mikusanyiko ya kijamii kama misiba, ndoa au kusanyiko lolote lile ambalo si la kidini kusikia akisalimia asalaam alaykum au bwana Yesu asifiwe au tumsifu Yesu Kristo wote ni mwendo wa nawasalimia kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, basi.

Hii nchi Mungu ametupa ni ya amani na utulivu, hivyo kesi hii kwa uzoefu wangu inaweza kuwa kama ile ya watu wa Uhamsho ambayo wao walisota takribani miaka 10 na wametoka selo juzi wameturiaa kinyaa hii ndiyo serikali jamani si kilamtu aote sharubu.

Najua mitusi itaporomoswa lakini ukweli ndiyo huo hapa ndiyo tulipo.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
53,615
2,000
Una changamoto ya R&L mkuu, pia sijaelewa ujumbe wako ni upi haswa?
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
37,262
2,000
Ni dhambi kubwa sana kutii mamlaka iliyoingia madarakani kwa kuiba kura.

Mamlaka unayoambiwa kuwa unapaswa kuitii ni ile yenye kibali cha wananchi,na mamlaka hii ndiyo itokanayo na Mungu.

Vibaka walioiba kura kaa nao mbali.

7654311.png
 
Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,133
2,000
Nikiacha mambo mengine uliyosema, 'kutii mamlaka' unakosema ni fasili ya wanasiasa, lakini siyo fasili ya Biblia. Kwa mfano, Mungu alipomtuma Nabii Musa kwenda kwa farao kwa lengo la kuwakomboa waana wa Israeli utumwani Misri na Musa akafanya hivyo, alitii mamlaka gani?

Yesu mwenyewe hadi ateswe, asulubiwe na kufa msalabani, alitii mamlaka gani? Manabii kwa nyakati mbalimbali mambo waliyokuwa wakiwafundisha watu kumrudia Mwenyezi Mungu na kumwabudu yeye na kuachana na kuabudu miungu wengine, walikuwa wakitii mamlaka gani?

Stefano (kwenye Kitabu cha Matendo ya Mitume) alipotiwa nguvuni na kuuawa na wenye mamlaka alikuwa akitii mamlaka gani? Saulo, ambaye baadaye aliitwa Mtume Paulo, alipokuwa akiwatesa na kuwaua Wakristo alikuwa akitii mamlaka gani? Alipoongoka na kuanza kumhubiri Kristo na hata yeye mwenyewe aliyekuwa akiwatesa na kuwaua Wakristo kuanza kufungwa gerezani, pamoja na mitume wengine, alikuwa akitii mamlaka gani?

Gamalieli alipowaambia viongozi wenzake (katika Kitabu cha Matendo ya Mitume) kuhusu kuwazuia mitume wasimhubiri Yesu kuwa 'kama wanachohubiri watu hawa kinatoka kwa Mwenyezi Mungu hatuweza kuzuia wanachokifanya, lakini kama kinatoka kwa wanadamu kitakufa chenyewe. Hivyo, nashauri tuwaache watu hawa maana tunaweza kujikuta sisi wenyewe tukipingana na Mwenyezi Mungu'. Katika kusema haya, Gamalieli alikuwa akitii mamlaka gani? Katika yote haya unaweza kuona 'kutii mamlaka' kuna maana gani ndani ya fasili ya Biblia na kuna maana gani nje ya yasili ya Biblia.
 
mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
262
500
Nikiacha mambo mengine uliyosema, 'kutii mamlaka' unakosema ni fasili ya wanasiasa, lakini siyo fasili ya Biblia. Kwa mfano, Mungu alipomtuma Nabii Musa kwenda kwa farao kwa lengo la kuwakomboa waana wa Israeli utumwani Misri na Musa akafanya hivyo, alitii mamlaka gani?

Yesu mwenye hadi ateswe, asulubiwe na kufa msalabani, alitii mamlaka gani? Manabii kwa nyakati mbalimbali mambo waliyokuwa wakiwafundisha watu kumrudia Mwenyezi Mungu na kumwabudu yeye na kuachana na kuabudu miungu wengine, walikuwa wakitii mamlaka gani?

Stefano (kwenye Kitabu cha Matendo ya Mitume, alipotiwa nguvuni na kuuawa alikuwa akitii mamlaka gani? Saulo, ambaye baadaye aliitwa Mtume Paulo, alipokuwa akiwatesa na kuwaua Wakristo alikuwa akitii mamlaka gani? Alipoongoka na kuanza kumhubiri Kristo na hata yeye mwenyewe aliyekuwa akiwatesa na kuwaua Wakristo kuanza kufungwa gerezani, pamoja na mitume wengine, alikuwa akitii mamlaka gani?

Gamalieli alipowaambia viongozi wenzake (katika Kitabu cha Matendo ya Mitume) kuhusu kuwazuia mitume wasimhubiri Yesu kuwa 'kama wanachohubiri watu hawa kinatoka kwa Mwenyezi Mungu hatuweza kuzuia wanachokifanya, lakini kama kinatoka kwa wanadamu kitakufa chenyewe.

Hivyo, nashauri tuwaache watu hawa maana tunaweza kujikuta sisi wenyewe tunapingana na Mwenyezi Mungu. Katika kusema haya Gamalieli alikuwa akitii mamlaka gani? Katika yote haya unaweza kuona 'kutii mamlaka' kuna maana gani ndani ya fasili ya Biblia na kuna maana gani nje ya yasili ya Biblia.
Mi sijaona swali lolote hapo labda umejadili, nimeupenda ulivyo jadili na unaonekana kujua au kosoma Biblia sasa katika maelezo yako ongeza kaneno kamaoja tu " Biblia inasema mamlaka iliyo kuu ni ya Baba Muumba' basi. hoja yako yote inajaa humo.
 
Francis fares Maro

JF-Expert Member
Jun 20, 2021
1,138
2,000
Mim si Mwanasheria na sijui sharia na siamini kama sheria inaweza kutenda haki hasa hizi sheria za kigeni tulizorithi kutoka kwa wakoloni. Nilishanga malumbano ya jana mahakamani mimi sikuyaelewa ila nilielewa jambo moja tu kuwa kesi ya mwenyekiti wa taifa Mbowe bado haijapelekwa katika mahakama yenye uwezo wa kusikiliza kesi ya ugaidi na zoezi hilo halijulikani litafanyika lini ila ni lazima atafikishwa siku moja katika mahakama hiyo yenye nguvu ya kusikiliza kesi hiyo.

Mpaka sasa najua kesi ipo Kisutu na sijui mahakama ipi ya mwanzo, ya kata, ya wilaya, ya mkoa au ipi, na kupita mahakama zote hizo itachukua miezi mingapi au miaka mingapi kusililizwa na kutolewa hukumu.

Hii inaonyesha kuwa Mbowe atasota sana ndani kwa utaratibu uliopo ndiyo maana kwa ushauri wangu sisi watu wa kanisa kama unaweza kuwa mchunguzi utagundua tunatii mamalaka kama Biblia ilivyo agiza ikija mamlaka inasema tusali tunasali na ikija mamlaka nyingine inasema sasa chanjo au vipi tunahamia huko hii yote kuepuka matatizo kama yanayompata Mbowe.

Na hata wakati wa kampeni najua mmesahau siwakumbushi. Na kutii mamlaka mbona ni rahisi tu. Leo uwezi kukuta mchungaji au sheikh katika mikusanyiko ya kijamii kama misiba, ndoa au kusanyiko lolote lile ambalo si la kidini kusikia akisalimia asalaam alaykum au bwana Yesu asifiwe au tumsifu Yesu Kristo wote ni mwendo wa nawasalimia kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, basi.

Hii nchi Mungu ametupa ni ya amani na utulivu, hivyo kesi hii kwa uzoefu wangu inaweza kuwa kama ile ya watu wa Uhamsho ambayo wao walisota takribani miaka 10 na wametoka selo juzi wameturiaa kinyaa hii ndiyo serikali jamani si kilamtu aote sharubu.

Najua mitusi itaporomoswa lakini ukweli ndiyo huo hapa ndiyo tulipo.
Ndio umeandika nini?
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
37,262
2,000
Ukiona hizi picha jinsi hawa Askari walivyo busy unaweza kufikiri kuwa ni kweli kuna case!😁😁😁Hizi nchi zenye umasikini wa akili bhana.
MKgtm.jpg
 
Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,133
2,000
Mi sijaona swali lolote hapo labda umejadili, nimeupenda ulivyo jadili na unaonekana kujua au kosoma Biblia sasa katika maelezo yako ongeza kaneno kamaoja tu " Biblia inasema mamlaka iliyo kuu ni ya Baba Muumba' basi. hoja yako yote inajaa humo.
Sijajibu swali, nimeelezea kipengele kimojawapo kati ya hivyo ulivyoviongelea.
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
30,361
2,000
maana kwa ushauri wangu sisi watu wa kanisa kama unaweza kuwa mchunguzi utagundua tunatii mamalaka kama Biblia ilivyo agiza ikija mamlaka inasema tusali tunasali na ikija mamlaka nyingine inasema sasa chanjo au vipi tunahamia huko hii yote kuepuka matatizo kama yanayompata Mbowe.
Rubish, basi subiri ikija amri kuwa leta mke wako, peleka si mnatii mamlaka zilizopo... rubbish!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom