Kesi namba 456 ya 2016 JamiiForums vs Jamhuri, Kisutu: Maxence Melo ahukumiwa Mwaka jela au faini ya Tsh. Mil 3. Mwenzake aachiwa huru

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Kesi namba 456 ya mwaka 2016 inawakabili Mkurugenzi wa Jamii Media Ndg. Maxence Melo na mwana hisa mwenzake Mike William itasomwa leo Aprili 08, 2020 mbele ya Hakimu Thomas Simba kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Hukumu hii awali ilipangwa kutolewa Novemba 26, 2019 lakini iliahirishwa mara nne (4) kwa kigezo kwamba Hakimu alikuwa hajamaliza kuandika hukumu hiyo. Tarehe nyingine ilizoahirishwa ni Desemba 06, 2019, Januari 22, 2020, Februari 19, 2020, Machi 19, 2020 na Aprili 02, 2020

Historia ya kesi hii

Kampuni ya Oilcom iliandikwa katika mtandao wa Jamii Forums ikidaiwa kukwepa kulipa kodi na kuchakachua mafuta kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Baada ya taarifa hizo kuandikwa kwenye mtandao wa Jamii Forums, Polisi waliandika barua kwenda kwa “Mkurugenzi wa Jamii Forum” kuomba taarifa za mtu aliyeandika ujumbe kuhusu Oilcom. Polisi wanadai hawakufanikiwa kupata taarifa hizo ndipo walipoamua kumkamata na kumuhoji Ndg. Maxence Melo na kumfungulia shitaka la kuzuia upelelezi kwa kutokutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi alipotakiwa kutoa taarifa za aliyeandika kuhusu Oilcom kwenye mtandao wa Jamii Forums kinyume na kifungu namba 22(1) cha Sheria ya Makosa ya Mitandaoni ya Mwaka 2015.

Ndg. Maxence Melo alikamatwa mnamo Desemba 13, 2016 na alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Desemba 16, 2016 na kufunguliwa kesi tatu (3) tofauti zenye shitaka moja la kuzuia upelelezi kwa kutokutoa ushirikiano kwa Polisi juu ya taarifa za walioandika kwenye mtandao wa Jamii Forums. Hata hivyo, alijikuta analazimika kupelekwa gereza la Keko kwa siku 3 baada ya kuchelewa kupewa dhamana.

Mapema mwaka 2017 upande wa Jamhuri ulimuongeza Micke William (Mushi) kwenye kesi hizo kama mmoja wa wanahisa wa kampuni ya Jamii Media.

Kuhusu kesi zilizofunguliwa mahakamani

Kesi 3 zilizofunguliwa ni zifuatazo:

Mosi, Kesi namba 456 ya mwaka 2016 ambapo Ndg. Maxence Melo alishtakiwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Jamii Media kwa kosa la kuzuia upelelezi kwa kutokutoa ushirikiano kwa polisi juu ya taarifa za aliyeandika kuhusu Oilcom kwenye mtandao wa Jamii Forums. Katika nyakati tofauti za usikilizwaji wa kesi hii namba 456 upande wa Jamhuri umewahi kukiri kwamba Micke William aliingizwa kimakosa kwenye kesi hiyo. Aidha, upande huo wa mashtaka mashahidi wote walikiri watuhumiwa walijibu barua zote za polisi wakisema wapo tayari kutoa ushirikiano endapo jinai ya mwanachama wao itabainishwa na jeshi la Polisi.

Pili, Kesi namba 457 ya mwaka 2016 ambapo washitakiwa walituhumiwa kwa kosa la kuzuia upelelezi wa Polisi kwa kutokutoa ushirikiano juu ya taarifa za aliyeandika kuhusu kampuni za CUSNA Investment na Ocean Link kudaiwa kukwepa kulipa kodi kwenye Bandari ya Dar es Salaam na kunyanyasa wafanyakazi wa kitanzania.

Uamuzi wa shauri hilo (shauri namba 457) ulitolewa Juni 01, 2018 ambapo Hakimu Godfrey Mwambapa aliamua kwamba Washitakiwa hawakuwa na kesi ya kujibu na hivyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwaachia huru.

Katika kesi hiyo pia, Polisi walitaka JamiiForums iwapatie taarifa za mwanzisha mada KWAYU na mchangiaji mmoja AMRISHIPURI ili waweze kuwakamata na kuwahoji kutokana na ukiukwaji wa taratibu. JamiiForums haikutoa taarifa binafsi za wanachama wake kwa kuamini kuwa chanzo hiki cha taarifa kilikuwa na nia njema hivyo kutaka kwanza iwepo Hati ya Mahakama inayoridhia kukamatwa kwa mhusika na kuelezwa kosa lake.

Tatu, Kesi namba 458 ya mwaka 2016 ambapo washtakiwa wanatuhumiwa kwa kosa la kuzuia upelelezi kwa kutokutoa ushirikiano kwa Polisi kuhusu Benki ya CRDB ambapo Polisi ilimtaka Mkurugenzi wa “Jamii Forum” kutoa taarifa kuhusu Wanachama wawili wa Mtandao wa JamiiForums walioandika kuhusu Benki ya CRDB.

Taarifa zilizotakiwa ni za Wanachama walioanzisha mijadala iliyosomeka "Charles Kimei (CRDB) jiuzulu, kashfa ya kontena, tiketi TFF, wanafunzi na ujambazi CRDB" mjadala unaodaiwa kuanzishwa tarehe 18 Januari 2016 pamoja na "Wizi wa Benki ya CRDB - Part II" unaodaiwa kuanzishwa Machi 11, 2015.

Taarifa za Wanachama ambazo zilitakiwa kutolewa ni IP-Address, barua pepe, Majina Halisi ya Wanachama hao. Kesi hii bado inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Huruma Shaidi na haijawa na shahidi tangu Novemba 2018.

=======

UPDATES:

========


















KESI NAMBA 456 (JAMHURI v JAMIIFORUMS): MELO AKUTWA NA HATIA HUKU MIKE AKIACHIWA

Maxence Melo amekutwa na hatia na kuhukumiwa faini ya milioni 3 au kifungo cha mwaka 1 jela. Aidha Mike Mushi amekutwa hana hatia na kuwa aliungwa kwenye kesi kimakosa
IMG_20200408_181411_145.jpg

Mahakaka ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa JamiiForums, Maxence Melo(40) kulipa faini ya Sh3 milioni au kwenda jela mwaka mmoja, baada ya kutiwa hatiani katika shitaka moja la kuzuia jeshi la polisi kufanya uchunguzi.

Pia mahakama hiyo imemuachia huru Mike Mushi ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo ya jinai namba 456/2016.

Mushi ameachiwa huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka dhidi yake.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Aprili 8, 2020 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakamani hiyo, Thomas Simba.

UPDATE:
Tayari faini imeshalipwa na Maxence Melo ameachiwa huru.

Hukumu dhidi yangu: Shukrani kwa watanzania – Maxence Melo - JamiiForums

Kujua kesi Zilizoisha na zile zinazoendelea JamiiForums dhidi ya Jamhuri, soma;

Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums - JamiiForums
 
Sidhani wataendeleza zile fitina za maagizo. Kukubaliwa mashariti WB watoto waliopata ujauzito kurejea masomo ni habari njema kwa wapenda democrasia na uhuru wa habari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana kwa kuandika kwa weledi mkubwa. Hata anayesoma for the first time anaelewa vizuri sana issue nzima kwa namna ulivoisummarize.

Naamini kabisa kwa maelezo haya Tunaenda kushinda, kwa sababu kimsingi tuhuma zote zililenga kuisaidia serikali hii ya JPM ipambane vizuri na UFISADI.

JF ni jamvi ambalo limekuwa msaada mkubwa sana kwa serikali katika kuibua maovu mengi sana.

Mungu Aibariki JF, Mungu awabariki na kuwalinda waanzilishi wa hili jukwaa dhidi ya hila zozote za wanaotaka JF ife.
 
Back
Top Bottom