Kero gani umewahi kukutana nazo kwenye nyumba za kupanga?

King Jody

JF-Expert Member
Oct 8, 2022
914
1,704
Binafsi kero za mwenye nyumba zilisababisha kujenga nyumba yangu na kuhamia faster ilikuwa 2015.

Unalipa kodi mara umeme umekatwa wakati kwake upo, mara kuchota maji mwisho saa 4 asubuhi, hutakiwi kutumia pasi ya umeme wala water heater yani ilimradi uishi kwa mateso.

Ukiongea unaambiwa kajenge nyumba yako kama unadhani ni rahisi, lakini kwa upande mwingine bila hizo changamoto labda nisingeweza kujenga, leo nipo kwangu na pia namalizia room za wapangaji ila sitawanyanyasa kamwe.

Mwenyezi Mungu anisaidie.
 
Nawakumbusha tu usipange nyumba ambapo mwenye nyumba anategemea kodi za wapangaji. Panga nyumba ambapo mwenye nyumba ana miradi yake ya kumuingizia pesa. Mimi nilipanga sehemu moja tu labda kero ni umeme kukatika na parking kuwa ndogo sometimes mgeni kulazimika kupark nje ya geti.

Kuna dada mmoja anapanga sehemu mwenye nyumba ni kivuruge mm siwezi ishi pale yaani tuseme kodi inaishi kesho, siku moja kabla, saa moja kamili asubuhi ashafika huyo dada anakuwa bado kalala kama ni weekend.
Mama mwenye nyumba anamgongea.

1. " wewe fulani, unalala unalala nini? Amka unipe pesa yangu kujenga sio mchezo, kila tofari unalo liona hapo ilikuwa ni gegedo moja🤣"

2. Kuna sehemu tulienda kumuona mzazi kajifungua tulivyofika tu getini tumejivalia suruali zetu tukaletewa vitenge🤣tujifunge ndo tuingie ndani mwenye nyumba ni msabato. Hii imetokea sehemi mbili yofauti.

3: unakula kuku wakati kodi hujalipa? Mdada wa kazini nae alitusimulia kero za mwenye nyumba wake. Huu mtaa naujua sio uswahilini basi tu mwenye nyumba mswahili.

Ukiona mtu kahamia nyumba haijaisha usiulize maswali mengi.
 
Nawakumbusha tu usipange nyumba ambapo mwenye nyumba anategemea kodi za wapangaji. Panga nyumba ambapo mwenye nyumba ana miradi yake ya kumuingizia pesa. Mimi nilipanga sehemu moja tu labda kero ni umeme kukatika na parking kuwa ndogo sometimes mgeni kulazimika kupark nje ya geti.
ngi.
Nilipanga Makongo mwenye nyumba mwalimu mstaafu. Alikuwa anabandika matangazo mlangoni "nimesema ukilala zima taa umeme utalipa Mara mbili jamani mbona mnanifanyia hivi?" 😆
 
Binafsi kero za mwenye nyumba zilisababisha kujenga nyumba yangu na kuhamia faster ilikuwa 2015,
Unalipa kodi mara umeme umekatwa wakati kwake upo, mara kuchota maji mwisho saa 4 asubuhi, hutakiwi kutumia pasi ya umeme wala water heater yani ilimradi uishi kwa mateso.

Ukiongea unaambiwa kajenge nyumba yako kama unadhani ni rahisi, Lakini kwa upande mwingine bila hizo changamoto labda nisingeweza kujenga, leo nipo kwangu na pia namalizia room za wapangaji ila sitawanyanyasa kamwe, Mwenyezi Mungu anisaidie.
Kudekishwa choo katika siku ambazo siyo zamu yangu
 
Nawakumbusha tu usipange nyumba ambapo mwenye nyumba anategemea kodi za wapangaji. Panga nyumba ambapo mwenye nyumba ana miradi yake ya kumuingizia pesa. Mimi nilipanga sehemu moja tu labda kero ni umeme kukatika na parking kuwa ndogo sometimes mgeni kulazimika kupark nje ya geti.

Kuna dada mmoja anapanga sehemu mwenye nyumba ni kivuruge mm siwezi ishi pale yaani tuseme kodi inaishi kesho, siku moja kabla, saa moja kamili asubuhi ashafika huyo dada anakuwa bado kalala kama ni weekend.
Mama mwenye nyumba anamgongea.

1. " wewe fulani, unalala unalala nini? Amka unipe pesa yangu kujenga sio mchezo, kila tofari unalo liona hpo ilikuwa ni gegedo moja🤣"
2. Kuna sehemu tulienda kumuona mzazi kajifungua tulivyofika tu getini tumejivalia suruali zetu tukaletewa vitenge🤣tujifunge ndo tuingie ndani mwenye nyumba ni msabato.
3: unakula kuku wakati kodi hujalipa? Mdada wa kazini nae alitusimulia kero za mwenye nyumba wake. Huu mtaa naujua sio uswahilini basi tu mwenye nyumba mswahili.

Ukiona mtu kahamia nyumba haijaisha usiulize maswali mengi.
Nilipanga Makongo mwenye nyumba mwalimu mstaafu. Alikuwa anabandika matangazo mlangoni "nimesema ukilala zima taa umeme utalipa Mara mbili jamani mbona mnanifanyia hivi?" 😆
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ile kauli usicheke na kima ndio inabidi uifanyie kazi kwenye nyumba za kupanga hata umeme ukiisha wanaanzia kwanza kwa mjumbe kutoa taarifa!,ili uishi kwa raha nyumba za kupanga ni kujitoa ufahamu!
Kero nyingi hasa zinawakuta waliopanga chumba ama chumba na sebule,ni nadra ukapa hizo kero ukipanga nyumba kuanzia laki3 na kuendelea
 
Binafsi kero za mwenye nyumba zilisababisha kujenga nyumba yangu na kuhamia faster ilikuwa 2015.

Unalipa kodi mara umeme umekatwa wakati kwake upo, mara kuchota maji mwisho saa 4 asubuhi, hutakiwi kutumia pasi ya umeme wala water heater yani ilimradi uishi kwa mateso.

Ukiongea unaambiwa kajenge nyumba yako kama unadhani ni rahisi, lakini kwa upande mwingine bila hizo changamoto labda nisingeweza kujenga, leo nipo kwangu na pia namalizia room za wapangaji ila sitawanyanyasa kamwe.

Mwenyezi Mungu anisaidie.
Nilihama baada ya mwenyenyumba kula unyumba mchana wa jua la utosi huku mkewe alikuwa hawezi kuzuia hisia mpaka ikafikia watoto kuwa wanaigiza
 
"wee kijana hao wageni wako uwe unanitambulisha Kwanza kwangu kabla hajapita getini, sitaki watu wa hovyo humu ndani,usije kuniletea mikosi".

Nilishtuka Aiseeh!! Kodi nilipe na kila mgeni wangu nimtambulishe Kwa mwenye nyumba, Hio ni Tisa, Kumi geti linafungwa saa mbili usiku.

Aiseeh Yale maisha ni zaidi ya mateso kibaya nilishalipa Kodi ya miezi 6.

Siku ya tukio ambalo ilibidi nihame kilazima nimerudi job, Kuna vyombo vichafu niliacha kwenye Karo la kuoshea vyombo vina siku mbili nilisahau Kabisa,Naambiwa ww kijana hivi vyombo umemuachia Nani hapa vinanuka au nikatupe?
Mimi "Mama samahani nilijisahau,"
Nikajua kaelewa, Weeh ananiambia hakuna kubadili nguo had uoshe au laah nikavitupe!! Hapo Shati langu la Dark Blue, Tai Safi na Suruali nimechomekea na Begi la PC mgongoni.

Si nikajifanya sijasikia nikageuka kufungua mlango na funguo, mara Mwaaaah maji ya ukoko WA ugali WA juzi na mchuzi Aiseeh!!

Nilmpiga vibaya Yule mama Hadi jicho nikamvimbisha. Ni majirani ndo walikuja kuamua. Kesi Hadi polisi Ila yaliisha.

Nilichojifunza.
1. Usipange nyumba ambayo mwenye nyumba anaishi Hapo Hapo. Yaani lazima ukose ule Uhuru wako binafsi, Ni Sawa Tu na mtu aliyeomba hifadhi ya kuishi na familia asiyoijua Kwa malipo.

2. Usipange nyumba ambayo ni ya urithi.
3. Usipange nyumba Kama mwenye nyumba Hana kitega uchumi chochote zaidi ya hiyo nyumba.
4. Usipange nyumba yenye wapangaji wengi. Wakizidi Sana wawe watatu Tu.
5. Hakikisha unapopanga nyumba muwe wapangaji pekee mwenye nyumba asikae Hapo.
6. Epuka mwenye nyumba kujua shughuli unayoifanya. Ilibidi mdanganye Tu. Mimi nilimwambia ninauza mitumba sokoni. Ikapita miezi 8 akaja ofisi kwetu na mm ndo nilipaswa nimuhudumie Aiseeh!! Mzee alishangaa Sana.
 
Back
Top Bottom