Mkasa gani umewahi kukutana nao kwenye nyumba za kulala wageni (gesti) mpaka ukajisemea nini hii?

Yaleyale

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
1,790
2,383
Leo naomba tuambiane visa mbalimbali ambazo tumekutana nayo kwenye nyumba za kulala wageni (guest houses) ambazo kimsingi umeshindwa kuelewa kilichotokea kwa macho ya kawaida.

Binafsi nitaelezea visa viwili ambavyo sijawahi kuelewa kilichonitokea.

Kisa cha kwanza kilinikuta Jijini Arusha mwaka 2014. Baada ya kupatiwa chumba na kuanza kulala ghafla nikahisi kama watu wako chumbani kwangu wanatembea na wamefungua mpaka mlango wa choo.

Nilikuwa sijalala usingizi ikabidi niwashe taa ila sikuona kitu. Hilo jambo likajirudia kama mara tatu kila nikizima taa. Nikaamua kusali kwa imani yangu ndipo nilipopata usingizi na sikusikia kitu tena.

Kisa cha pili kilinikuta Dodoma mwaka 2018. Siku hiyo niliamua kuchukua kipoozeo nikapita nako lakini nikakiondoa room maana kulala na vipozeo unaweza jikuta huna hata bukta ikawa noma asubuhi.

Baada ya kumwondoa bi mdada nikaanza kulala. Majira ya saa 8 hivi nikashtuka damu zinanitoka puani hatari mpaka shuka limeanza kuloa damu. Ikabidi nikurupuke kwenda kunawa huku nikizuia damu kwa kitambaa. Jambo hilo lilidumu kwa takriban dakika 3 damu ikakata.

Wewe umwahi kukutana na kisa gani huko gesti house ukabaki unajiuliza, heee nini hii?
 
Nililala guest maeneo ya Chato (nilikwama safarini) usiku wa manane nikasikia naitwa jina langu LA ukoo, sauti kubwa Nene! Nilistuka usingizini lakini sikuitika. Nilisali nikalala.
 
Mnakumbuka enzi zile gesti ni korido then vyumba huku na huku then choo na bafu viko uani kama nyumba ya kiswahili. Basi bwana niliingia gesti pale Buguruni na dem. Baada ya dkk 45 za kwanza nikaenda chooni. Kule chooni ile natoka nakutana na njemba nae amekuja kujisaidia.

Mimi na mipombe yangu si nikasahau chumba changu nikaingia chumba cha ile njemba na nikaenda fasta mpaka kitandani naanza kuingia kwenye neti huku demu wa njemba akiwa katulia. Ebwanae kufumba na kufumbua njemba hii hapa. Inauliza.

Wewe ni nani unamparamia mke wangu? Aisee nilijieleza mpaka nikamwonyesha njemba chumba changu na demu wangu ndio kidoogo akapunguza munkari
 
Lete na kashata
Mnakumbuka enzi zile gesti ni korido then vyumba huku na huku then choo na bafu viko uani kama nyumba ya kiswahili. Basi bwana niliingia gesti pale Buguruni na dem. Baada ya dkk 45 za kwanza nikaenda chooni. Kule chooni ile natoka nakutana na njemba nae amekuja kujisaidia. Mimi na mipombe yangu si nikasahau chumba changu nikaingia chumba cha ile njemba na nikaenda fasta mpaka kitandani naanza kuingia kwenye neti huku demu wa njemba akiwa katulia. Ebwanae kufumba na kufumbua njemba hii hapa. Inauliza. Wewe ni nani unamparamia mke wangu? Aisee nilijieleza mpaka nikamwonyesha njemba chumba changu na demu wangu ndio kidoogo akapunguza munkari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo naomba tuambiane visa mbalimbali ambazo tumekutana nayo kwenye nyumba za kulala wageni (guest houses) ambazo kimsingi umeshindwa kuelewa kilichotokea kwa macho ya kawaida.

Binafsi nitaelezea visa viwili ambavyo sijawahi kuelewa kilichonitokea.

Kisa cha kwanza kilinikuta Jijini Arusha mwaka 2014. Baada ya kupatiwa chumba na kuanza kulala ghafla nikahisi kama watu wako chumbani kwangu wanatembea na wamefungua mpaka mlango wa choo.

Nilikuwa sijalala usingizi ikabidi niwashe taa ila sikuona kitu. Hilo jambo likajirudia kama mara tatu kila nikizima taa. Nikaamua kusali kwa imani yangu ndipo nilipopata usingizi na sikusikia kitu tena.

Kisa cha pili kilinikuta Dodoma mwaka 2018. Siku hiyo niliamua kuchukua kipoozeo nikapita nako lakini nikakiondoa room maana kulala na vipozeo unaweza jikuta huna hata bukta ikawa noma asubuhi.

Baada ya kumwondoa bi mdada nikaanza kulala. Majira ya saa 8 hivi nikashtuka damu zinanitoka puani hatari mpaka shuka limeanza kuloa damu. Ikabidi nikurupuke kwenda kunawa huku nikizuia damu kwa kitambaa. Jambo hilo lilidumu kwa takriban dakika 3 damu ikakata.

Wewe umwahi kukutana na kisa gani huko gesti house ukabaki unajiuliza, heee nini hii?
Ilikuwa morogoro mwaka 2002 guest moja pale,nikachukua chumba nikalala kuamka nikakuta kitanda kimegeuka na kila kitu mpaka corridor ilibidi nimwambie Jamaa alikuwa chumba jirani anisaidie nitoke nje,mauzauza,sikuthubutu kuendelea kulala hapo,
 
Hahahaha. Hii ilikiwahi kumtokea mshikaji wangu maeneo ya Gereji pale karibu na Tabata Reli. Jamaa ni mkazi wa muda tu Dar. Siku moja akachukua kimeo maeneo ya Hostel Mabibo akaenda kujipigia hapo gereji. Jamaa alikuwa anakaa Tabata. Anasema alivyoamka asubuhi ameenda kupanda daladala alishindwa kujua Buguruni ni wapi na Ubungo ni wapi. Ikabidi akae stendi mpaka alivyosikilizia konda wanavyoita abiria.
 
Sasa hivi nimelala guest flani ya kati hapa Iringa.Kuna askari hapa wanakagua watu waliolala vyumbani karibu masaa mawili sasa..yaani ni kelele kama kilabuni tu huwezi pumzika na masaa machache yajayo naingia barabarani.
Bora ningeegesha tu kwenye gari sio kwa huu upuuzi!
 
Nilikuwa sijawahi kulala lodge siku moja nimechelewa kufika mwanza nilikuwa natokea dar nimefika kama saa sita usiku so nikachukua room pale nyegezi....nimelala nasikia mlango unagongwa kama saa nane hivi....kufungua bimdada mhudumu namuuliza vip kuna shida aakniuliza “ kweli unalala mwenyewe kabisa” shenzi nikamwambia unataka nilale na nani sasa ambaye kanisaidia kulipia

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ilikuwa morogoro mwaka 2002 guest moja pale,nikachukua chumba nikalala kuamka nikakuta kitanda kimegeuka na kila kitu mpaka corridor ilibidi nimwambie Jamaa alikuwa chumba jirani anisaidie nitoke nje,mauzauza,sikuthubutu kuendelea kulala hapo,

Kwa hiyo mkuu ukatoka nje huku unatembelea kichwa

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Niliwahi kulala gesti moja mjini Morogoro,ilkuwa na Kunguni balaa,muda nilioingia ilikuwa saa 6 usiku baada ya kutafuta sana na kukuta nyingi zimejaa,kwahiyo sikuwa na choice nyingine,ile kulala tu wakaanza kunishambulia kwa kasi ya ajabu,nilipowasha taa nikawakuta wako rundo kwenye mashuka mpaka kwenye godoro,kilichoniponya ni kuamua kuchukua taulo na kulitandika chini na kulala pale mpaka asubuhi,ila kwakweli sitaisahau ile siku...
 
Niliwahi kulala guest house moja ipo Mbeya karibu na stand ya zamani ya mabasi ya mikoani. Mauzauza niliyokutana nayo nilishindwa hata kumsimulia mtu. Sijaamini mpaka leo kilichotokea usiku ule, na mara zote uwa nashindwa kusimulia. nimeandika hii nikiamini haikuanzia kwangu kuna mwingine atatoa ushuhuda
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom