Kama wataka kuishi kwa amani kwenye nyumba ya kupanga

BradFord93

JF-Expert Member
Oct 11, 2017
910
2,164
Naamini wengi wetu tupo kwenye daraja la kujikomboa kutafuta pesa ya kujenga makwetu huku bado tukiwa ndani ya nyumba za wenzetu(tumepanga)

Na pia ni kwa wale ambao wapo njiani kuelekea kupanga

1.Kuwa Bize na mambo yako
Asubuhi salimia wakiitikia au wasipoitikia waachie wao wenyewe

2.Weka Pembeni Mazoea na wake za watu au wanafunzi. Kiukweli kama wataka uishi kwa amani mazoea na hilo kundi tajwa acha, maana kumbuka hao ni watoto na wake wa watu(so kuna mtu anaumiza kichwa kugharamia)

3.Kuwa msafi
Mara moja moja ingia chooni fanya usafi...!! Hapa utajipa CV ya kutendewa wema pia

4.Lipa Bili kwa wakati
Hapa nasemea kodi na bili zingnezo zinazokuhusu. Weka kichwani tarehe utakayohusika na bili yoyote na uitoe kwa wakati husika.

Kama huna omba muda na hakikisha unawapa kwa muda uliomba(hii hujenga uaminifu)

5.Punguza ngono chumbani kwako
Sio kwa kuwa una chumba unacholipia kodi ndo iwe ruhusa kuleta wanawke tofauti tofauti

Kama upo kwenye mahusiano chagua mmoja ambaye ndie atakayekuwa anakuja room. Hao vikojozi wengine chapia nje(hii itakuletea heshima kwa wapangaji wenzio lkn pia hata kwa landlord.

6.Kelele za radio
Sauti iwe ya kuridhisha na isiwe kero kwa wenzio.Sio lazima kila mtu asikie kuwa unamuangalia Shokosugi...!!

7.Marafiki wanaojielewa. Wengi tunapenda kuleta wageni wa jinsia zetu lkn pia yatubidi kuangalia rafiki wa kumleta.Jua kuwa utakayemleta atakuwakilisha wewe humo ndani. (ukileta mwizi then nawe ni mwizi)

8.Kumbuka angalau kutoa zawadi kwa majirani zako(sio lazima lakini).
Kuna muda waweza kurudi hata na machungwa ukawagawia wenzio hata watoto wao kama huna uwezo wa kumpa kila mtu

Hii itakusaidia kujenga uhusiano mzuri na wenzio. Yawezkana wao wakakukumbuka kwa jambo kubwa baadae

Ni mtazamo wangu tu.
 
8.Kumbuka angalau kutoa zawadi kwa majiran zako(sio lazima lakin)
Kuna muda waweza kurudi ht n machngwa ukawagawia wenzio hata watoto wao kama huna uwezo wa kumpa kila mtu
Hii itakusaidia kujenga uhusiano mzuri na wenzio....yawezkana wao wakakukumbuka kwa jambo kubwa baadae

Ni mtazamo wangu tu

Wakila wakaharisha utajibu
 
Naweza kufanya yote bila shida yoyote ila naomba nisipangiwe cha kufanya kwa hiyo namba 5, 6 & 7 napinga kabisa. Yan tuzingatie mipaka yetu kama watashindwa hapo basi watashindwa kuishi na wengine pia.
 
Hahahahaa mimi mwenyew inakuaga ngum lkn ndo hvyo....!!kujiheshim muhim
kodi unalipa mfano.. 30k.. gesti nikalipe 10k.. nikitiana kwa mwezi mara 4 na kimada changu.. jumla 40.. yaan hela nitakayolipa gesti izidi hela niliyopangia????

masela.. hoja namba 5 tuikataeee

#nazngua
 
Hahahahaa mimi mwenyew inakuaga ngum lkn ndo hvyo....!!kujiheshim muhim
hahaha heshima ndio nin bhana kila mtu na maisha yake.. ku pretend sana jau..

kitu ambacho nakiona kwangu kinashusha heshima nikiwa geto ni

KURUHUSU MSHKAJI ALETE DEM GETO AMCHAPE.. hio nakataaga kama hana hela ya lodge huwa namtoa tu akajiponee sio.. kuja kuleta mikos geton
 
Cha msingi kuwajibika kwa kile unachopaswa kuwajibika, salamu inatosha
Na kushiriki jambo muhimu linalowaleta pamoja
 
Hapa pa wake za watu, ukiwa na TV na king’amuzi cha Azam. Unaweza kuletewa wali kuku na mchicha wa nazi, juu si ya ukwaju. Wakati huo imetoka mihangaikoni tumbo halina kitu na ndani una mkate tu.


Unaambiwa umkumbiwa umkumbushe Sultan ikianza.
Sio utani....ndo maana mim mazoea nao staki....maana wapangajill wenzangu wa3 n mapolisi....nsije nkaenda jela bila kupitia mahakaman
 
Hapa pa wake za watu, ukiwa na TV na king’amuzi cha Azam. Unaweza kuletewa wali kuku na mchicha wa nazi, juice ya ukwaju. Wakati huo umetoka mihangaikoni tumbo halina kitu na ndani una mkate tu.


Unaambiwa umkumbushe Sultan ikianza.
Aki wewe ni mtaalamuna na inaonekana ume ishi sana hizi nyumba zetu za huku uswahilini.
 
Back
Top Bottom