Kenya inaangamia kipuuzi kabisa

Kenya inaangamia kipuuzi kabisa

Mwaka 2010 Nchi ya Kenya kwasababu ya "Pressure" kutoka Vyama vya Upinzani,WAKENYA "walikurupuka" na kuja na KATIBA MPYA ambayo kimsingi ilikuwa na madhara makubwa kwa Nchi hiyo mpaka Jana!Kelele za REFORMS sio mpya sana katika ukanda wa Afrika Mashariki huu!

Pressure hiyo kubwa iliyotokana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007 iliwafanya WAKENYA kudhani kuhitaji(I) REFORMS kubwa kwa(II) wakati Mmoja katika(III) Taasisi Nyeti za Taifa(Political and Legal Reformation s),Makosa makubwa!

Maandamano ambayo unashuhudia leo Nchini Kenya huku Nchi ikiwa katika "panic" kubwa mpaka Rais Ruto kukosa utulivu wa kuendesha Nchi ni matokeo ya kukimbilia kujibu matakwa ya Wapinzani kwa kukurupuka(No Reforms No Election).

Dhana hii ya No Reforms No Election sio dhana mpya watu wakadhani ni dhana ya Chadema bali mambo haya yalishafanyika Nchini Kenya na kwa sasa baada ya KATIBA MPYA ya mwaka 2010 haya sasa ndio matokeo yake!

KATIBA ya Kenya inaruhusu Maandamano bila ukomo!KATIBA ya Kenya inakataza Polisi na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama kutotumia risasi za moto hata kama wandamanaji wanasonga Ikulu 🤣🤣🤣!Ndani ya Bunge la Kenya ni kawaida sana Viongozi kupigana NGUMI!KATIBA MPYA ya Kenya 2010 inatamka Rais kuweza kushitakiwa baada ya kutoka madarakani!Huu👆👆ndio/ndizo REFORMS ambazo WAKENYA walizichagua na sasa zinavuruga AMANI na Usalama wa Nchi!

Tegemea soon kuona WAKENYA wengi wakikimbilia Nchini Tanzania kama maandamano haya👆👆👆👆 yatashika kasi!(I)Maduka yanaporwa na Vijana wahuni wa Upinzani(II)Magari ya Raia wa Kenya yanachomwa moto barabaranii,(III)Polisi wanapigwa na Raia,(IV)Raia wanaiba/pora gari za Polisi(V)Raia wanaua Polisi na kuchukua uniform za Polisi na kuzivaa🤣🤣🤣!Haya ndio "Mazao " ya KATIBA MPYA yaani No Reforms No Election kwa Kenya!

WAKENYA wakafanya mabadiliko makubwa kwenye KATIBA yao wakidhani ndio kuwapa watu wao Demokrasia🤣🤣kumbe wanaenda kuua Nchi yao wenyewe!

Tunasema reforms is a gradual process which with time has to be tested kujua uzuri na ubaya!Niliwahi kuandika hapo nyuma kwamba ni "kichaa" tu ambaye anaweza Kukubali "Full Reformation" kwenye mifumo yake ya Nchi ya (I) Uchaguzi (II) MAHAKAMA (III) KATIBA at per!KATIBA MPYA ya Kenya ulikuwa ni ukichaa uliopitiliza kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama hasa Idara ya Usalama wa Taifa ya Kenya(NIS)kushindwa kuona "shadow" hii ya KATIBA MPYA ya mwaka 2010!

Narudia tena,kwa watu makini,kwa Taifa makini "Reformation chache has to be tested before going to full reforms".

Msije Tanzania kufanya KOSA la Kenya eti kisa Mzee Warioba na Timu yake wanataka fully Reforms!
🙏🙏🙏🙏👍👍👍👍👏👏
Never Test!
👏👏👏👏👏👏👏👏
 
A Sanctimonious Person is composing Poes.
Unajua hata maana ya wachache?..yaani,wachache ukiwaona utawajua ama unajiandikia tu wachache?.
uchumi wa Tanzania umeshikiliwa na watu wa Asia..unajua idadi yao ndani ya Tanzania wapo wangapi?.
ukiondoa hao warangi rangi (walioshikiria uchumi wa Tanzania) ambao hata idadi yao hawafiki hata laki 6 ndani ya ngozi
Ukitaka kupata picha ya hali ya watanzania ebu karibu kufuatilia hata the largest truck and bus companies in Tanzania kuna wabulushi wangapi ?
Then Fanya comparison na Kenya.
Njoo kwenu kilimo wakulima wakubwa Tanzania ni watu wa aina gani the jilinganishe na Kenya.

nyeusi milioni 70 watanzania mnabaki na nini?.
Nadhani hujatembea Tanzania ,
Ukiachana na dar es salaam kuna watu huko mikoan wanatengeneza hela chafu ambazo , most Kenyans ni ndogo , karibu njombe, songea ,ifakara na kadhalika uone watu wanavyotemgeneza hela.
Tembea iringa kuanzia ipogoro upate picha vituo vya mafuta na idadi yake Tena vya wakulima wa miti .
Nenda kule kigoma uone watu wanavyovusha siment kwa mabot kwenda Kongo .
Kenya iwe na maisha magumu wakati omba omba wa Tanzania wanakimbilia kenya.
Issue ya ombaomba ni suala lenu , sababu inakuwaje mnaruhusu foreigners waje kufanya hiyo kazi kwenu? Hiyo inaonesha jinsi vyombo vyenu vya usalama vilivyo weak Wala sio issue ya Tanzania.
Kwanini waombe kwenu kwa wingi ila wasionekane tz kwa wingi🤣🤣🤣
bure kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Akili iko mbali na wewe.
Uchumi wa Tanzania unamilikiwa na wahindi na midlle easterners ambao hata hawafiki laki 3 katikati ya watanzania milioni 70 ila bado unaujasili wa kusema uchumi wa kenya unamilikiwa na wageni.
uko manipulated sana ndiyo mnaujasiri wa kushangilia in your defeat.
Bure kabisa
Prove that kwamba uchumi inamilikiwa wa westerners kwa kuangalia the largest tax payers ni watu wa aina gani the compare na kenya
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Nimeitoa huko kwa mdadisi na aliyekuwa mshiriki wa ujenzi wa katiba ya kenya,
::::::::::::::::::::::::::::::

KENYA INATEKETEA KISA KATIBA MPYA: NI FURSA NA SOMO KWA TANZANIA

Ni dhahiri polisi wa kawaida wamezidiwa. Sasa jeshi limelazimika kuingia kupambana na wanaojiita GenZ.

Bahati niliteuliwa kama mshauri Kwa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Cha Kenya (COTU -K) anachoongoza Brother Francis Atwoli. Ni wakati wa mchakato wa kutunga kilichoitwa katiba mpya. Wafanyakazi walishirikishwa vya kutosha. Hivyo ITUC na ILO wakanipa kibarua Cha kushauri. Vikao vingi tulifanya pale Mombasa.

Nilipopitia rasimu nilistaajabu kuona mambo ya hovyo ndani ya rasimu. Nitapitia machache:

1. Pendekezo kwamba kima cha chini cha mshahara (minimum living wage) kitamkwe kwenye katiba. Wenyewe wakidhani ni jambo zuri mno mshahara wa kima cha chini kulindwa kikatiba. Niliwaeleza huu ni ujinga. Mshahara ni suala la "econometrics". Sio a political issue.

2. Majaji wasailiwe na wananchi kabla ya kuajiriwa kupitia runinga. Wao wakiamini kuwa itazuia majaji kula rushwa au kuendelea serikali. Niliwaeleza upumbavu uliopo. Kwanza jaji hapimwi Kwa kigezo kimoja tu. Pili itawezekana vipi raia ambaye hata kuhesabu mpaka 5 hawezi amsaili jaji? Je baada ya kumsaili nani ataamua huyu aajiriwe yule ailsiajiriwe? n.k.

3. Uhuru wa kuandamana na kukusanyika usio na masharti. Niliwaeleza Nini kitatokea uhuru aina hii ukitolewa na katiba. Ndicho kinatokea Sasa.

4. Kuwe na wabunge wanaowakilisha wafanyakazi. Hili niliwarejesha Kwa Uganda, Tanzania, Cameroon na Cote D'Ivoire. Wafanyakazi huko walikuwa wanadai ubunge huo ufutwe hauwasaidii. Tanzania tulifanikiaa kujiondoa kwenye jumuia za chama na ndio JUWATA ikafa ikaja TFTU, baadae OTTU na Sasa TUCTA. Wafanyakazi walikuja kugundua wawakilishi wao walijali matumbo Yao. Pia ukitoka uamuzi unaowaumiza wanashindwa kupinga Kwa kuwa wawakilishi wao walishiriki kutoa uamuzi.

5. Kuruhusu maofisa na watendaji kushitakiwa binafsi hata wanapofanya kosa wakati wanatekeleza majukumu waliyopewa na katiba. Niliwaambia hii itafanya watumishi wa serikali haswa wa vyombo vya Dola kuzembea. Ndio maana Sasa unaona kisichana kinatikisa makalio mbele ya askari mwenye rungu na bunduki. Watumishi aina hii wanatakiwa waadhibiwe na mahakama ya kijeshi tu.

Nimetaja mifano michache lakini kusema kweli katiba ya Kenya ni mbovu mno na ndio chanzo cha haya machafuko . Wanatuambia ni katiba nzuri tuiige hawajui wasemalo. Nao Wana mawazo na matendo ya kina Shakira, Boniface Mwangi, Martha Karua, Kalonzo na Odinga.

Kuvurugika nchi ndio wanapata maslahi Yao

Tukatae. Tusiichezee katiba. Tusifanye reforms kwa mashinikizo.

Mwisho: nyumba ya jirani ikungua wee Jenga nyingi. Wapangaji wapo. Hakuna mtalii ataenda Kenya sasa. Wawekezaji wanaanza kuhama. Huu ndio muda wetu kuchangamka.

Halafu tuimarishe ulinzi mpakani. Wakimbizi wako njiani wanakuja.

Mwishoooo: tuendelee kudhibiti wakorofi wetu kwa nguvu na ari mpya. Bora walie sasa kuliko kuacha waanze kuchoma majengo na mali za watu
Nakazia tuwachape viboko tu,wanaojibidisha kutupeleka katika majanga ya aina hii,si kila jambo nilakuiga.
Nilisema, na narudia maneno ya wazee: "huwezi kuzuia kuhara kwa kidole kimoja". Hii ndio Kenya, wanaiteketeza huku wakihisi wapo sahihi na ni wasomi wa grade 1. Fikiria hii ni Magunas Supermarket (ipo Makutano, Meru). Vijana wanabomoa, wanachukua/kuiba na kuchoma mali za wafanyabiashara au serikali moto. Wasipodhibitiwa, mzigo wa shida unasambaa Afrika ya Mashariki, hasa hasa sisi majirani wa pande nyingi. Leo Kenya isipotawalika, hata sisi tunaumia kwa kiasi kikubwa sana.
#wanachimba highways yao iliyojengwa Kwa mabilioni ya DollarView attachment 3397922
View attachment 3397877

Kwa hiyo Police wamezidiwa sababu ya Katiba? Na jeshi limekuja na Katiba mpya, au katika inaongezeka nguvu jeshi?
 
Wanajaribu ku-demarket siasa za Kenya ili watanzania wanaendele kubaki Passive.
Issue sio kuwa passive katiba ilitakiwa iwe na limit,
Kwa wizi unaendelea hivi unategemea investor watapachukuliaje.
Mnaweza kuwa na katiba mpya ila isiwe msaada sana.
Laiti polisi wangeachiwa wafanye kazi yao vyema hayo maandamano yanayofanyika yasingefikia hatua ya kuibiana na kuchoma vitu vya watu.
Katiba imewapa uhuru wa kurudi nyuma kimaendeleo badala ya kusonga mbele.
Eti mtu kuchimba barabara uonekane sifa kisa uhuru.
Leo hii kuna watu wanaenda kifirisika completely na wengi tu wataenda kuwa na chuki kwa sababu yakuchomewa vitu
 
Acheni ujinga tunataka katiba mpya

No reform no election
Nyoe ni vijana wa 2000 msiojua hata hii nchi imetoka wapi,ni kukurupuka tu bila kujua wanao waaminisha wanaendeshwa na tamaa za kupata madaraka na pesa
 
Hili suala nilipiga kelele huko reddit watu wakaja juu na kusema eti Rostam, GSM na Dewji ni watanzania mna nina wivu aisee. Wazungu wanashangaa Tanzania inazunguka kutafuta wawekezaji wa nje na Rostam. Eti ni mfanyabishara mzawa . Watu wana ndugu uarabuni na Uhindini halafu unategemea wakipata faida wawekeze hapa Tanzania ?Hili nchi tuko nyuma sana. Ukienda Kenya makampuni makubwa yote yanamilikiwa na wakenya asilia. Mpaka unaenjoy doing business. Kuanzia mashamba ya chai na kahawa mpaka meat processing plants.
Kuna watu ni deliberately ignorant kama mleta mada.
lengo la uzi wake ni kudemarket siasa za Kenya na sio kitu kingine.
Nairobi peke yake ni karibu ya uchumi wa Uganda nzima.
magari yaliyopo Tanzania na Uganda ukiyachanganya pamoja bado hayafikiii idadi ya magari yaliyopo kenya tena ikiwa mbele ya Ethiopia.

wakenya wana strong Healthcare kuliko nchi yoyote Africa mashariki (ni ya tatu kwa Africa) hadi maraisi na watu wakubwa tz wakipatwa na magonjwa mazito brek ya kwanza ni kwenya.
upande wa Elimu ndiyo basi kabisa.. M'bibi uko kenya ndani ndani anachanganua mambo makubwa ya kitaifa kuliko profesa wa Tanzania.
alafu Kuna mtu anasimama anasema kenya si lolote kwa Tanzania kwasababu tuliwai kuwape Sembe!.

kenya wana upungufu wa ardhi si kwasababu ardhi imehodiwa na wachache bali nchi yao ni ndogo kulinganisha na idadi yao.tunawazidi kidogo kitu katika idadi ya watu na Nchi yetu ni kubwa karibu Mara mbili yao nchi yao.
we are rejoicing in our defeat.
 
Matatizo wanayopitia Kenya sasa ni tofauti kabisa na Tz.
Hata tabia za wananchi na mihemko yao iko tofauti kabisa.

Kwani katiba ya Tz ikirekebishwa ni lazima ifanane na ya Kenya??
Hii hoja wanatumia wapumbavu peke, ati ona Kenya wanavyopigana, katiba mpya haisaidii. Sasa kwani utachukua ya Kenya na kuipaste Tz ilhali hatufananii kwa mambo mengi sana.
 
Issue sio kuwa passive katiba ikitakiwa iwe na limit,
Kwa wizi unaendelea hivi unategemea investor watapachukuliaje.
Mnaweza kuwa na katiba mpya ila isiwe msaada sana.
Laiti polisi wangeachiwa wafanye kazi yao vyema hayo maandamano yanayofanyika yasingefikia hatua ya kuibiana na kuchoma vitu vya watu.
Katiba imewapa uhuru wa kurudi nyuma kimaendeleo badala ya kusonga mbele.
Eti mtu kuchimba barabara uonekane sifa kisa uhuru.
Leo hii kuna watu wanaenda kifirisika completely na wengi tu wataenda kuwa na chuki kwa sababu yakuchomewa vitu
Ndugu kuna mda mambo mengine niyakusikitikia maana vijana ambao tunatakiwa kuwa very compressive kwa maendeleo yetu na kupunguza vichochezi maana sisi ndo bado tunasafari ndefu ya kulipeleka taifa letu mbele ndo haoo tunasaport ujinga ,jamani hawa wazee wanaotaka katiba mpya akina WARYOBA umri wao umeisha anasubilia adhabu ya kaburi tu ko sisi vijana tuache ujinga wa kusaport upumbavu utakao tuumiza siye badae,
 
Umeongea sana lakini umeongea utumbo

Kwa hayo Matatizo uliyo yaoanisha katika vipengele vya katiba ya Kenya Ulipaswa kusema kwamba

Tanzania Tunahitaji katiba mpya lakini iwe katiba Bora yenye maono Bora kuliko Ile ya Kenya

Katiba ya Tanzania hata Nyerere mwenyewe Aliipinga Kwa kusema kwamba Endapo kama haito badilishwa basi nchi Ikipata Raisi ambaye ni dikteta Atapata lope hole ya kuitumia vibaya

So it means wewe unajua zaidi kuliko Nyerere mwenye ccm yake !??
 
Issue sio kuwa passive katiba ikitakiwa iwe na limit,
Kwa wizi unaendelea hivi unategemea investor watapachukuliaje.
Mnaweza kuwa na katiba mpya ila isiwe msaada sana.
Laiti polisi wangeachiwa wafanye kazi yao vyema hayo maandamano yanayofanyika yasingefikia hatua ya kuibiana na kuchoma vitu vya watu.
Katiba imewapa uhuru wa kurudi nyuma kimaendeleo badala ya kusonga mbele.
Eti mtu kuchimba barabara uonekane sifa kisa uhuru.
Leo hii kuna watu wanaenda kifirisika completely na wengi tu wataenda kuwa na chuki kwa sababu yakuchomewa vitu
maandamano ya watu kuchimba barabara na siasa za kila Mtu ale kwa urefu kamba yake ni kipi kinarudisha maendeleo nyuma?..
unaumia mwananchi mwenye hasira kuchoma kibanda ama kuchimba barabara uku ukitaka watanzania wawe passive na watu wanaochota mabilion kwa kigezo cha urefu wa kamba zao?.
mwananchi mwenye njaa anaweza haribu kilometer ngapi za barabara kwa sururu uku akiwa frustrated?.
 
Nimeitoa huko kwa mdadisi na aliyekuwa mshiriki wa ujenzi wa katiba ya kenya,
::::::::::::::::::::::::::::::

KENYA INATEKETEA KISA KATIBA MPYA: NI FURSA NA SOMO KWA TANZANIA

Ni dhahiri polisi wa kawaida wamezidiwa. Sasa jeshi limelazimika kuingia kupambana na wanaojiita GenZ.

Bahati niliteuliwa kama mshauri Kwa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Cha Kenya (COTU -K) anachoongoza Brother Francis Atwoli. Ni wakati wa mchakato wa kutunga kilichoitwa katiba mpya. Wafanyakazi walishirikishwa vya kutosha. Hivyo ITUC na ILO wakanipa kibarua Cha kushauri. Vikao vingi tulifanya pale Mombasa.

Nilipopitia rasimu nilistaajabu kuona mambo ya hovyo ndani ya rasimu. Nitapitia machache:

1. Pendekezo kwamba kima cha chini cha mshahara (minimum living wage) kitamkwe kwenye katiba. Wenyewe wakidhani ni jambo zuri mno mshahara wa kima cha chini kulindwa kikatiba. Niliwaeleza huu ni ujinga. Mshahara ni suala la "econometrics". Sio a political issue.

2. Majaji wasailiwe na wananchi kabla ya kuajiriwa kupitia runinga. Wao wakiamini kuwa itazuia majaji kula rushwa au kuendelea serikali. Niliwaeleza upumbavu uliopo. Kwanza jaji hapimwi Kwa kigezo kimoja tu. Pili itawezekana vipi raia ambaye hata kuhesabu mpaka 5 hawezi amsaili jaji? Je baada ya kumsaili nani ataamua huyu aajiriwe yule ailsiajiriwe? n.k.

3. Uhuru wa kuandamana na kukusanyika usio na masharti. Niliwaeleza Nini kitatokea uhuru aina hii ukitolewa na katiba. Ndicho kinatokea Sasa.

4. Kuwe na wabunge wanaowakilisha wafanyakazi. Hili niliwarejesha Kwa Uganda, Tanzania, Cameroon na Cote D'Ivoire. Wafanyakazi huko walikuwa wanadai ubunge huo ufutwe hauwasaidii. Tanzania tulifanikiaa kujiondoa kwenye jumuia za chama na ndio JUWATA ikafa ikaja TFTU, baadae OTTU na Sasa TUCTA. Wafanyakazi walikuja kugundua wawakilishi wao walijali matumbo Yao. Pia ukitoka uamuzi unaowaumiza wanashindwa kupinga Kwa kuwa wawakilishi wao walishiriki kutoa uamuzi.

5. Kuruhusu maofisa na watendaji kushitakiwa binafsi hata wanapofanya kosa wakati wanatekeleza majukumu waliyopewa na katiba. Niliwaambia hii itafanya watumishi wa serikali haswa wa vyombo vya Dola kuzembea. Ndio maana Sasa unaona kisichana kinatikisa makalio mbele ya askari mwenye rungu na bunduki. Watumishi aina hii wanatakiwa waadhibiwe na mahakama ya kijeshi tu.

Nimetaja mifano michache lakini kusema kweli katiba ya Kenya ni mbovu mno na ndio chanzo cha haya machafuko . Wanatuambia ni katiba nzuri tuiige hawajui wasemalo. Nao Wana mawazo na matendo ya kina Shakira, Boniface Mwangi, Martha Karua, Kalonzo na Odinga.

Kuvurugika nchi ndio wanapata maslahi Yao

Tukatae. Tusiichezee katiba. Tusifanye reforms kwa mashinikizo.

Mwisho: nyumba ya jirani ikungua wee Jenga nyingi. Wapangaji wapo. Hakuna mtalii ataenda Kenya sasa. Wawekezaji wanaanza kuhama. Huu ndio muda wetu kuchangamka.

Halafu tuimarishe ulinzi mpakani. Wakimbizi wako njiani wanakuja.

Mwishoooo: tuendelee kudhibiti wakorofi wetu kwa nguvu na ari mpya. Bora walie sasa kuliko kuacha waanze kuchoma majengo na mali za watu
Nakazia tuwachape viboko tu,wanaojibidisha kutupeleka katika majanga ya aina hii,si kila jambo nilakuiga.
Nilisema, na narudia maneno ya wazee: "huwezi kuzuia kuhara kwa kidole kimoja". Hii ndio Kenya, wanaiteketeza huku wakihisi wapo sahihi na ni wasomi wa grade 1. Fikiria hii ni Magunas Supermarket (ipo Makutano, Meru). Vijana wanabomoa, wanachukua/kuiba na kuchoma mali za wafanyabiashara au serikali moto. Wasipodhibitiwa, mzigo wa shida unasambaa Afrika ya Mashariki, hasa hasa sisi majirani wa pande nyingi. Leo Kenya isipotawalika, hata sisi tunaumia kwa kiasi kikubwa sana.
#wanachimba highways yao iliyojengwa Kwa mabilioni ya DollarView attachment 3397922
View attachment 3397877
Yaani umeongea upumbavu
 
Hizi chambuzi za kijinga hizi hazituhusu! Yaani mnataka tuendelee ka katiba inayosema DED asimamie kura?
🤣🤣

Katiba ambayo mkuu wa Taasisi inayo simamia uchaguzi ana chaguliwa na Raisi halafu Wananchi tutegemee kwamba mtu huyo ampinge Raisi Aliye mpatia hicho cheo My foot
 
Back
Top Bottom