Kenani Kihongosi afungua kampeni ya uhamasishaji wananchi hususani vijana kwa ajili ya kujiandaa na ushiriki wa Sensa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
KATIBU MKUU UVCCM NDUGU KENANI KIHONGOSI AMEFUNGUA RASMI KAMPENI YA UHAMASISHAJI SENSA YA WATU NA MAKAZI

VIJANA WATAKIWA KUWA 'MACHAMPION' WA SENSA

KATIBU MKUU wa Jumuiya ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndugu Kenani Kihongosi amefungua rasmi kampeni ya uhamasishaji wananchi hususani vijana kwa ajili ya kujiandaa na ushiriki wa sensa ya watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu tarehe 23 Agosti, 2022.

Tukio hilo limefanyika Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam katika viwanja vya Mwembeyanga huku likipambwa na elimu mbalimbali kutoka kwa maafisa na waratibu wa Sensa sambamba na burudani za wasanii mbalimbali waliotumia sanaa zao kuwahamasisha vijana kujitokeza kuhesabiwa na kuwapa elimu kuhusu umuhimu wa zoezi hilo.

Kulingana na Kenani Kihongosi, Katibu Mkuu wa UVCCM, kampeni hiyo ya hamasa na elimu kuhusu Sensa 2022 inatarajiwa kufanyika nchi nzima chini ya uratibu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi nchini Tanzania.

Akizungumza na mamia ya vijana katika viwanja vya Mwembeyanga, Katibu Mkuu Kenani amesema Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini, kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalum. Kwa maana nyingine, sensa ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi, kwa umri na jinsia, mahali wanapoishi na hali yao ya elimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo na hali ya makazi.

Amesema Takwimu hizi za msingi ndiyo zinazoweza kuainisha mahitaji halisi ya wananchi yakiwemo makundi maalum yenye uhitaji maalum kwa mfanano, watu wenye ulemavu, wanawake, watoto, vijana na wazee hivyo kurahisisha uandaaji wa sera na mipango ya maendeleo kulingana na uhitaji na mazingira yaliyopo.

Katibu Mkuu wa UVCCM ndugu Kenani Kihongosi amesema umuhimu wa zoezi hilo ni kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa.

Aidha, Kihongosi amesema taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya na Serikali Kuu katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali za taifa.

Kulingana na makamishna wa sensa, miongoni mwa maswali yatakayoulizwa yatahusu:-
  • Taarifa za kidemografia (umri, jinsi, uhusiano, hali ya ndoa, uraia, n.k.);
  • Maswali yanayohusu ulemavu; Taarifa za Elimu;
  • Maswali ya uhamaji,
  • Taarifa za Watanzania wanaoishi nje ya nchi
  • Taarifa za Uzazi na Vifo vilivyotokea ndani ya kaya.
#TujitokezeKuhesabiwa
#KuwabaloziKwaMwigine
#SensaNiYetuVijana

IMG-20220623-WA0028.jpg
 
Arudishe pesa za halmashauri ya arusha alizowekewa kienyeji na mkurugenzi wa jiji.
Arudishe pesa kwamba alichukua yeye au mkee wake? Achana na Gambo ana majambo yake yule. Kama mke wa Kenani ndiyo aliwekewa pesa kwenye account kwanini atajwe Kenani? Si aende amchukulie hatua mke wake! Achana na watu wasiojua uongozi kama Gambo. Gambo alidhamiria kumchafua Kenani
 
Arudishe pesa kwamba alichukua yeye au mkee wake? Achana na Gambo ana majambo yake yule. Kama mke wa Kenani ndiyo aliwekewa pesa kwenye account kwanini atajwe Kenani? Si aende amchukulie hatua mke wake! Achana na watu wasiojua uongozi kama Gambo. Gambo alidhamiria kumchafua Kenani
Muambie huyo kenani atazitapika hizo pesa.
 
Arudishe pesa kwamba alichukua yeye au mkee wake? Achana na Gambo ana majambo yake yule. Kama mke wa Kenani ndiyo aliwekewa pesa kwenye account kwanini atajwe Kenani? Si aende amchukulie hatua mke wake! Achana na watu wasiojua uongozi kama Gambo. Gambo alidhamiria kumchafua Kenani
Mke wa Kenani alichukua pesa?

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Hapana, hajachukua maana halina aliye na ushahidi, ni wehu wa wanasiasa wa mchongo wakitaka kujisafisha kwenye jamii wanatafuta wa kumtupia zigo
Nilitaka nishamgae amechukua vipi,na wakati yeye si kiongozi.

Halafu yule dada kwao siyo kukavu sana..uwezo wanao.
 
Back
Top Bottom