Kelele za upinzani hazinisumbui-JK

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,715
86
Kelele za upinzani hazinisumbui -JK

2007-10-21 10:16:10
Na Juma Thomas, Roma


Rais Jakaya Kikwete, amesema kelele zinazopigwa na viongozi wa vyama vya siasa kuhusu utendaji wa serikali yake hazimsumbui.

Amesema viongozi hao wana uhuru wa kusema ili mradi tu hawachochei vurugu nchini.

``Hali ya siasa ni shwari nchini Tanzania, kelele nyingi zinazopigwa na viongozi wa vyama vya siasa ndio kufanikiwa kwenyewe kisiasa. Hii hainisumbui,`` alisema.

Rais Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiongea na Watanzania wanaoishi nchini Italia.

Kuhusu uraia wa nchi mbili na raia wa nje kupiga kura, Rais Kikwete alisema mambo hayo bado yanashughulikiwa.

Alisema Viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakituhumu baadhi ya watendaji serikalini kuwa ni wabadhirifu wa mali za umma.

Hivi karibuni viongozi hao walitoa orodha ndefu ya maofisa wa serikali ambao walidai kuwa ni mafisadi.

Hata hivyo, Rais Kikwete alisema kuwa katika siasa za vyama vingi shutuma kama hizo, pamoja na kwamba hazina ukweli wowote, haziwezi kuepukika.

``Hiki ndicho tunachokitegemea kwenye siasa za vyama vingi,`` alisema Rais Kikwete.

Kuhusu usalama wa raia na mali zao, Rais Kikwete alisema kuwa wimbi la ujambazi ambalo lilitikisa serikali mwanzoni mwa utawala wake sasa limedhibitiwa.

``Hatuwezi kusema tutaufuta kabisa ujambazi lakini nachoweza kusema ni kwamba hivi sasa tatizo limepungua kwa kiasi kikubwa baada ya kushirikisha majeshi yetu yote katika mapambano dhidi ya ujambazi,`` alisema.

Kuhusu chakula , alisema kuwa nchi imepata mavuno ya kutosha mwaka huu, na kwamba tatizo sasa ni soko kwa ajili ya mazao ya wakulima.

Nchi ilikumbwa na uhaba wa chakula mwaka jana baada ya kukumbwa na kiangazi cha muda mrefu hali iliyoilazimu kuomba chakula cha msaada kutoka nchi wahisani.

Kuhusu elimu rais aliwaeleza Watanzania hao, ambao wengi wao ni mapadri wa Kanisa Katoliki, kuwa serikali imejitahidi kuhakikisha kuwa kila mtoto wa umri wa kwenda shule anapata nafasi hiyo. Alisema kuwa hivi sasa asilimia 97 ya watoto wenye umri wa kuanza shule ya wameingia shule ya msingi.

Kuhusu shule za sekondari, Rais Kikwete alisema kuwa hivi sasa kila kata ina shule ya sekondari ili kuwezesha watoto wanaomaliza elimu ya msingi waweze kujiunga.

Hata hivyo, alisema kuwa changamoto kubwa ni walimu pamoja na maabara. ``Tunataka wanasayansi kwa hiyo suala la kuwa na maabara katika shule hizi ni la muhimu sana,`` alisema.

Alisema ili kuhakikisha kuwa shule hizo zinakuwa na walimu wa kutosha serikali iliamua kubadilisha chuo cha ualimu Changombe pamoja na Mkwawa kuwa vyuo vikuu ili kupata walimu wa sekondari wengi.

Rais alisema kuwa sambamba na hilo serikali pia imevitaka vyuo vikuu binafsi kuanzisha vitivyo vya elimu ili kupata walimu wengi.

Kuhusu gonjwa la ukimwi, rais alisema kuwa serikali imeendelea kuwaelimisha wananchi namna na kupambana na tatizo hilo. Alisema ili kupambana vizuri na tatizo la ukimwi ni bora kila mwananchi akajua afya yake.

Mwezi Julai mwaka huu Rais Kikwete alifungua kampeni maalumu ya kupima kwa hiari virusi vya ukimwi, na tayari watu 700,000 wamekwisha jitokeza kupima.

Kuhusu madini rais alisema kuwa sheria zinafanyiwa marekebisho ili raslimamli ya madini iweze kuwanufaisha Watanzania zaidi.

Alisema hivi sasa serikali inajenga uwezo wa kusimamia vyema madini ili kuhakikisha kuwa wawekezaji pamoja na wananchi wote wananufaika na rasmali hiyo.

Aliwataka Watanzania hao kukumbuka nyumbani pamoja na kuwekeza walikotoka. Aliwataka pia kutafuta misaada ya maendeleo ili kuendeleza nchi yao.

Akisoma risala, Mwenyekiti wa Watanzania wanaoishi Italia, Padri Gaudensi Mushi, alisema kuwa wanaridhishwa na juhudi za rais Kikwete za kuendeleza uchumi pamoja na huduma nyingine za jamii, ikiwemo elimu.

Aliiomba serikali iangalie uwezekano wa kurekebisha sheria ili kuruhusu uraia wa nchi mbili, ikiwa ni pamoja na kuwaruhusu Watanzania walioko nje ya nchi kupiga kura.

Akijibu hoja hizo, Rais Kikwete alisema suala la uraia wa nchi zaidi ya moja linashughulikiwa na Tume ya Kurekebisha Sheria, na kwamba Tume ikimaliza kazi yake itaishauri serikali.

Hata hivyo, Rais alisema kuwa suala hilo halitaki haraka na kuwaomba Watanzania hao kuwa wavumilivu.

Leo Rais Kikwete atahutubia mkutano wa amani ulioandaliwa na Jumuia ya Mtakatifu Egidio utakaofanyika katika jiji la Napels.

SOURCE: Nipashe
 
Kweli JK anakosa dira sasa ... inasikitisha unapoona na kusikia kauli kama hizi zikitolewa na Rais wa nchi. No wonder jamii sasa hivi inamuona na yeye ni mmoja wa mafisadi. Hivi JK anataka ukweli gani zaidi ya report ya CAG ya mahesabu ya BoT? Ina maana CAG haaminiki au na yeye ni mmoja wa wapika majungu wanaotumiwa na wapinzani? Kwani wapinzani walipata wapi hiyo dossier ya List of Shame? Asilimia kubwa ya tuhuma hizo ziko kwenye official document ambayo ni report ya CAG. Sasa uongo wa wapinzani uko wapi? Anasema kwamba anawaacha waseme tu, kama tuhuma hizo zisingekuwa na ukweli Slaa na wenzake wangekuwa Keko wanapumzishwa, kwani hatujui ubabe wa serikali ya CCM?

Halafu anasema eti sasa wanafanya marekebisho ya sheria ya madini, ninauhakika 100% hata hayo marekebisho watakayoyafanya bado wataacha mianya ambayo inampa waziri wa nishati na madini leeway ya kufanya madudu, ndiyo maana akina Karamagi wana uwezo wa kufuta mkataba kwa wino ambao umeishaandaliwa na kubarikiwa na kamati ya ushauri ya madini na mwanasheria. ukiuliza Karamagi ana utaalam gani wa madini kiasi kwamba awe na powers za kufuta sehemu ya vipengele siku ya kutia saini mkataba? Hizo ni kazi za wataalam wa wizara yake na siyo yeye ambaye professionally anaweza kuwa hajui hayo mambo kwa undani. Leo hii huyo mtu anapewa power za kufanya maamuzi mazito ambayo yanakuja kuligharimu taifa!

Wanaandaa uwezo wa serikali wa kusimamia madini ... uwezo gani iwapo sheria na sera ziko loose kiasi kwamba mafisadi wachache wanatumia hiyo mianya kuuza natural resources za nchi? Hapo naona rais wwetu anabwabwaja tu na sijui kama anaelewa anachokisema. He is the very same person aliyesema mikataba inadurusiwa na kwamba haitasainiwa mingine tena mpaka zoezi liishe. No one knew kama zoezi lilikamilika, tukashangaa kuambiwa Bungeni kwamba zoezi lilikamilika na mkataba mpya ambao ni bomu ulisainiwa! Yet anataka tuendelee kumwamini na hizo kauli zake za kisanii!
 
Ukisoma alivyoongea, unajua wazi hizo kelele zinamsumbua. Hataki kukubali ukweli lakini inaonyesha wazi kwamba anaanza ku panic maana mambo hayaendi sawa.
 
Kelele za upinzani hazinisumbui -JK

2007-10-21 10:16:10
Na Juma Thomas, RomaKuhusu madini rais alisema kuwa sheria zinafanyiwa marekebisho ili raslimamli ya madini iweze kuwanufaisha Watanzania zaidi.

Alisema hivi sasa serikali inajenga uwezo wa kusimamia vyema madini ili kuhakikisha kuwa wawekezaji pamoja na wananchi wote wananufaika na rasmali hiyo.


SOURCE: Nipashe

Mimi reaction yangu labda ni hapo, kwa kuanzia, ni nani mwongo kati ya JK anayesema sheria za madini zinapitiwa au karamagi aliyedai bungeni kuwa mchakato wa kupitia sheria za madini ulishamalizika?

Au mwandishi alimnukuu JK vibaya?
 
Dawa ni kumuona uso kwa uso, kama nilivyomuona majuzi ndio utajua ukweli wa mambo kama yanamsumbua au hayamsumbui, ukweli ni kwamba yanamsumbua tena sana,

....ama sivyo asingegombana na Lowassa as he did hivi karibuni...!
 
Waungwana kwa hili Kikwete anajimaliza na for sure atakuwa ndiye Gorbechev wa CCM Tanzania . JK hawezi kukata kama si mla rushwa maana analala na kushinda na wala rushwa. JK hawezi kufanya mabadiliko maana hana uchungu na Tanzania ila ana uchungu na CCM na kuwakumbatia wala rushwa wenzie. JK si msafi hata mara moja na ndiyo maana anawaza na kuthubutu kusema haya akiwa nje ya Nchi . Hivi kwa nini asihutubie Taifa na kusema haya badala yua kusemea Ulaya kila mara ? Ama kweli Watanzania wameliwa na wangoje miaka 5 ijayo . Mkabeni koo huyu Muhuni wa Bagamoyo .
 
Mboana muungwana anatuangusha sasa, yeye majibu yake anayatolea nje ya nchi tu akirudi nyumbani kila kitu shwari? Alafu majibu yake ya Rome na Washington D.C mbona yana pingana.
 
Hapo JK anaonyesha kabisa kuwa amezidiwa haya mambo na kelele za wazee zinampa sana shida.
Nchi inakwenda pabaya kama huyu ndio rais wetu wanawa nchi.
 
Dawa ni kumuona uso kwa uso, kama nilivyomuona majuzi ndio utajua ukweli wa mambo kama yanamsumbua au hayamsumbui, ukweli ni kwamba yanamsumbua tena sana,

....ama sivyo asingegombana na Lowassa as he did hivi karibuni...!

Tumegee kidogo kuhusu huo ugomvi tafadhali. Nukuu chache tu kukidhi kiu yetu.
 
Kikwete welcomes critics.

PRESIDENT Jakaya Kikwete yesterday spoke positively of public criticism of his government by the opposition, saying it reflected success of democracy in the country. “I am not perturbed by the noises. I don’t lose sleep over it. It is healthy for the opposition to speak, even shout at and criticize (us), as long as they don’t incite public unrest,” he told Tanzanians living in Italy here. Opposition politicians have been parading sweeping allegations of corruption against cabinet ministers and senior government officials, some of whom are now processing defamation suits.

Mr Kikwete reassured countrymen and women in the Diaspora that there was no political crisis at home. “The noises are normal in multi-party politics,” he said. He reiterated that future mining contracts would not carry the clause strictly tying the payment of corporate tax to profitability, which allows investors to defer the obligation indefinitely. Elimination of the provision contained in previous contracts would allow investors to keep two thirds of the returns and the government one third, which was a fair deal, said the president. He explained that local capacity would be employed to audit mineral production in place of expensive foreign assayers. Mining companies would be compelled to source supplies and such services as earth excavation and movement locally.

Meanwhile, President Kikwete said the proposal to allow Tanzanians living abroad dual citizenship, reiterated here yesterday, had won hostile reception at home. He urged patience while consensus was summoned on the merits of the proposal. “This has been the wish of every Tanzanian abroad I have met, but the reaction at home is rather hostile and, I am afraid, the proposal will be rejected outright if we push it too hard now,” he explained, adding that the Law Reform Commission was handling the process. He said the government was examining the logistics for another request raised here to enable Tanzanians to vote outside the country.

The president urged Tanzanians in the Diaspora to be good ambassadors and remit resources home to improve the welfare of their families and relatives. Mr Kikwete left here for Naples last evening. He is scheduled to address an international inter-faith conference on peace today before flying to Paris for a three-day visit in France.

Well kama alikuwa hakosi usingizi hakuwa na sababu ya kututangazia kwani huo sio wimbo. Maneno yake ni sahihi wale wanaokosa usingizi ni wenye uchungu na Tanzania.

Tumezoea sasa kila anapokwenda nje anatoa taarifa ambazo zinapingana, hiyo dual citizenship sijui alisemaje alipokuwa London na NY au Tokyo.
 
hazimsumbui kwa sababu hatupendi watanzania..hajui ni nini alichokimbilia ikulu,yeye amekimbilia safari za nje tu na kutudidimiza watanzania..pale ikulu kumemmfanya aoe kwa amani,
nasikia aliyekuwa CAG DK. FRANK MHILU Amepelekwa kuwa mwalimu wa diploma -TIA Mtwara.baada ya kutoa report iliyoibomoa serikali..Muungwana hakupenda hili,ila akatumia usanii kutetea wamefanya kazi nzuri ila kuziba machafu ya EL pale ARUSHA ambayo CAG Alitaka kuyatoa,
 
hazimsumbui kwa sababu hatupendi watanzania..hajui ni nini alichokimbilia ikulu,yeye amekimbilia safari za nje tu na kutudidimiza watanzania..pale ikulu kumemmfanya aoe kwa amani,
nasikia aliyekuwa CAG DK. FRANK MHILU Amepelekwa kuwa mwalimu wa diploma -TIA Mtwara.baada ya kutoa report iliyoibomoa serikali..Muungwana hakupenda hili,ila akatumia usanii kutetea wamefanya kazi nzuri ila kuziba machafu ya EL pale ARUSHA ambayo CAG Alitaka kuyatoa,

Hivi inawezekana? Huyo ni CAG ama CAG general? Maana ninayemfahamu sio huyo labda awe amebadilishwa karibuni!
 
Mwalimu wangu wa Somo la Historia somo ambalo wakati huo sikulitilia maanani sana,aliwahi kuniambia sentensi yenye maneno MATATU kuhusu serikali na watawala wajidanganyao kote Dunia kwamba kuna wakati watawala wanafikia hali ya kuwa FAT AND HAPPY kwa sabau mapenzi yao yote yanatimizwa no matter what.

Kundi moja, aina moja ya watu,Chama kimoja au Mfumo mmoja wa utawala ukikaa madarakani muda mrefu huku ukihodhi nguvu zote za kidola na kuvishikilia vyombo vya Usalama, Sheria,Fedha na Habari kwa mkono wa chuma; mara zote hufikia hatua ya kudhani utawala wao ni wa kimungu na wa milele.

Viongozi hawa fisadi hufikia hatua ya kudhani kwamba hakuna nguvu yeyote kutoka miongoni mwa wananchi wake ndani na nje ya nchi iliyo na thubutu, Nia,Hamu na Uwezo kushindana nao kama viongozi wakuu na watekelezaji wakuu katika ngazi ya Juu kabisa ya Utawaka ndani ya nchi.

Kwa dhana hiyo ya UKITOFI( kunenepa mashavu) viongozi huona hakuna haja ya kuchukua hatua yeyote dhidi ya mfumo wao muflisi wa utawala kukabiliana na hali halisi ya mabadiriko na mwamko katika jamii waiongozayo zaidi ya kusherehekea utimilifu wa njozi hisia na matakwa yao katika kila siku iendayo kana kwamba maumivu na malalamiko ya wananchi ni manukato mazuri na sauti nzuri ya muziki wa kuriwadha Roho na akili zao.

Utawala wowote ufikapo katika hatua hiyo, ndipo suala la FAT AND HAPPY linaingia.

FAT AND HAPPY ni hatua ya juu na ya mwisho ya utawala haramu wowote Duniani kujidanganya na kujikanyaga na kuamini kwamba yote yanayowezekana na yaliyo ndani yauwezo wao wameyafanya kuiendeleza jamii na taifa, na hivyo kujidanganya zaidikwamba maendeleo yaliyopo katika kila tabaka ni juu kabisa ambayo mfumo wowote wa siasa duniani ungeweza kuwafikisha kwa hiyo hawana budi kujipongeza.

Kwa kuamini maono na ndoto zao za kishenzi watawala wanao rithi na kuendeleza Utawala wa wachache wenye Shingo ngumu kama JM Kikwete hujenga mazingira, kwa kutumia vyombo vya habari, yanayo sisitiza na kulazimisha aidiologi isemayo kila tabaka katika jamii litakiwa kuridhika na hali liliyonayo na maendeleo liliyo fikia kwa sababu hakuna mfumo wowte wa kisiasa, uongozi wa chama au mawazo ya watu binafsi au Sayansi na Tekinolojia iwezayo kuwapeleka mbele zaidi ya hapo walipo na kila tabaka halina budi kuendeleza hali liliyonayo na kuirithisha kwa vizazi vyake vyote kwa faida ya nchi na Taifa kwa ujumla.

Pia kwa hekima yao ya kiibilisi husambaza matumaini ya kishetani miongoni mwa tabaka lao la watawala yaimarishayo utamaduni wa kujikweza ujengao imani ya kujitukuza wao na familia zao kwamba, kama kundi lenye hadhi ya juu zaidi na lililofanikiwa zaidi katika taifa wana haki ya Kuendelea kunenepa mashavu kwa kugawana pato la taifa vyovyote vile watakavyo na kufurahia mafanikio yao ya kisiasa na juhudi zao za kuwatoa Wakoloni weupe na wao kujisimika katika viti vile vile, katika sheria zile zile na kutawala katika misingi ileile.

Zaidi ya yote alinacha zao huhimiza akili zao kujenga Kuta kama lile la China kujihakikishia kwamba namna yeyote ya kujaribu kubadili hali iliyopo kwa nia ya kubadiri mwamko,mwelekeo,utamaduni na kubwa zaidi kuwaondoa wao katika Viti vyao vya enzi ni KOSA LA JINAI


Maneno ya MH Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyo yasema nchini Italy kwamba Tuhuma, Malalamiko na Mwito wa kubadiri mwelekeo wa utawala wa SISIEMU nchini Tanzania ni maneno yasiyo mnyima usingizi hata sekunde moja kwa sababu ni kelele zisizo na meno, ni maneno kutoka katika Kinywa cha kiongozi aliwakirishaye kundi la mafisadi walio fichama nyuma chama kilichowatekwa kutoka kwa wananchi SISIEMU.

Maneno ya Rais Kikwete yanahitimisha njozi zake binafsi na za wachache ndani ya SISIEMU kwa lengo la kuendeleza kwa nguvu zote Mwendelezo wa kujlimbikizia madaraka ya kiserikali, Matumizi mabaya ya nguvu za Dola, Ugandamizaji wa Uhuru wa Vyombo vya habari, Utawala wa moja kwa moja wa Vyombo vya fedha kama BOT na umiliki wa Chombo kikuu cha kusimamia Uchaguzi nchini Tanzania kwa lengo la kuzuia maendeleo ya jamii ya watanzania na Taifa kwa ujumla.

Pia maneno yake yana nia ya kuwaambia Watanzania yeye ni Jabari la Ufisadi lisilo Tikisika na lisilo weza kung'olewa.

MH Kikwete na genge lake la Mafisadi wanaamini kwa dhati kwamba uwezo walionao juu ya Dola ya Tanzania wa kufanya watakacho ni mkuu mno kiasi cha malamiko yetu kutowatia hofu na kuwashawishi kushuka kutoka katika Enzi yao kuu hadi tabaka la chini ili kuhangaika na tuhuma ziachazo maswali mengi kutoka kwa Vyama vya upinzani na wananchi wapingao mfumo wa utawala wa SISIEMU.

Maneno ya MH Kikwete yana nia ya kuueleza Umma wa Watanzania kwamba kwa kuunganisha nguvu zao pamoja kama wananchi kama wanajamii na kama jamii ya watu waliodharauliwa waliopuuzwa na kunyanyaswa kwa muda mrefu na utawala wa SISIEMU, na hata pengine kwa kusaidiwa na jamii zote za kimataifa zipendazo mabadiriko ya kweli katika nchi zinazoendelea hawezi shindana na nguvu zao akina Kikwete walizo jilimbikizia kichama na Kiserikali kwa muda wa zaidi ya miaka 46 zilizo wawezesha kuwaweka wananchi walio wengi wa Tanzania katika kapu la ujinga na ufukara mkuu na hofu.

MH Kikwete ana nia ya kutueleza wote tupiganiao maendeleo ya kweli nchini Tanzania na kusisitiza mageuzi makubwa ya mfumo wa utawala bora kwamba hatuna nafasi katika utawala wa Tanzania huru ila wao wachache ndani ya SISIEMu kwani;

" SISIEMU IS FOREVER"

MH Kikwete na mafisazi wenzako wote bila kujali mnamiliki nini na mna fedha kiasi gani mnajidanganya mchana kweupe. Hamjifunzi wala hamtapata nafasi ya kujifunza kuhusu Historia ya mapmbano Afrika na Duniani kote

Tulicho nacho katika mawazo na matendo yetu ndani ya miaka 2 ijayo kitaondoa Enzi yenu yote na kuiweka katika jumba la makubusho, huku ninyi wenyewe mkihaha katika kila pembe ya dunia kutafuta hifadhi za Ughaibuni ili muhifadhi ngozi, nyama, mifupa na roho zenu dhidi ya hasira za wananchi mlio wanyanyasa kwa muda wote watakao taka kwa shauku kuu kuhakikisha Sheria na Haki zinawabana juu ya Uovu wenu kwao.

Amen
 
Kelele za wananchi katika kila kona ya Tanzania hazina tofauti hata kidogo na kelele za Wapinzani. Kwa maana nyingine Kikwete hasumbuliwi na kelele za wananchi, hajui anachozungunza huyu! naona anapayuka tu! Sasa asishangae wananchi wakitia pamba masikioni ili wasibughudhiwe na kelele zake za kuomba kura 2010 na kuamua kuitosa CCM milele.
 
Slaa na wenzake, walipoitisha mkutano pale Mwembeyanga na kutoa list ya mafisadi na ndani ya list ile wakamtaja JK walitegemea nini?

Leo wanasema mbona rais amenyamaza? Walitegemea nini? Hata mimi nikiwa najijua ni msafi halafu ukaniweka kwenye list ya wachafu na kutaka nichukue hatua, siwezi.
Sababu inayomfanya awapuuzie ni kwamba anajijua yeye ni msafi, sasa anaona inawezekana hata wale waliotajwa kwenye ile list wakawa wamepakaziwa kama yeye.

Approach ya Slaa na wenzake inaweza kuleta machafuko na kuturudisha miaka kadhaa nyuma. Wanaweza kuwa na akili sana lakini hawana BUSARA. Sasa rais hajasema kitu, nini kinawazuia kwenda mahakamani? Au huko Hague?
 
Slaa na wenzake, walipoitisha mkutano pale Mwembeyanga na kutoa list ya mafisadi na ndani ya list ile wakamtaja JK walitegemea nini?

Leo wanasema mbona rais amenyamaza? Walitegemea nini? Hata mimi nikiwa najijua ni msafi halafu ukaniweka kwenye list ya wachafu na kutaka nichukue hatua, siwezi.
Sababu inayomfanya awapuuzie ni kwamba anajijua yeye ni msafi, sasa anaona inawezekana hata wale waliotajwa kwenye ile list wakawa wamepakaziwa kama yeye.

Approach ya Slaa na wenzake inaweza kuleta machafuko na kuturudisha miaka kadhaa nyuma. Wanaweza kuwa na akili sana lakini hawana BUSARA. Sasa rais hajasema kitu, nini kinawazuia kwenda mahakamani? Au huko Hague?

Funny enough Rais alimuhakikishia Condi Rice kuwa tuhuma zote za ubadhirifu zitafuatiliwa, sasa kama wamesingiziwa na tuhuma ni za uongo wanafuatilia nini?
 
Slaa na wenzake, walipoitisha mkutano pale Mwembeyanga na kutoa list ya mafisadi na ndani ya list ile wakamtaja JK walitegemea nini?

Leo wanasema mbona rais amenyamaza? Walitegemea nini? Hata mimi nikiwa najijua ni msafi halafu ukaniweka kwenye list ya wachafu na kutaka nichukue hatua, siwezi.
Sababu inayomfanya awapuuzie ni kwamba anajijua yeye ni msafi, sasa anaona inawezekana hata wale waliotajwa kwenye ile list wakawa wamepakaziwa kama yeye.

Approach ya Slaa na wenzake inaweza kuleta machafuko na kuturudisha miaka kadhaa nyuma. Wanaweza kuwa na akili sana lakini hawana BUSARA. Sasa rais hajasema kitu, nini kinawazuia kwenda mahakamani? Au huko Hague?


machafuko hayawezi kuletwa na approach, yataletwa na wale wanaodhania kuwa nchi hii ni ya kwao peke yao na ambao kwa vile hawafurahishwi na "approach" basi wanajifanya miungu watu. "Mbona hamkupiga magoti mlipoomba".. hatapigiwa mtu magoti tena katika TAnzania, na sadaka ya sifa za uongo haitatolewa tena! CCM bora ing'amue hilo mapema.

Kile wananchi wanakitaka watakisema bila kuambiwa ni "jinsi gani waseme". CCM haiwezi na haina uwezo wa kuamulia ujumbe wa wananchi utolewe vipi! Kama ameamua kukaa kimya hilo ni uamuzi wake, lakini kwa kukaa kwake kimya haina maana ametuamulia ni jinsi gani tumfikishie ujumbe!

Tanzania haina wafalme, na hatuwezi kuruhusu viongozi watende kama wafalme! Hilo tumewakatilia na tutaendelea kuwakatalia, ndio maana nilishatoa pendekezo huko nyuma kuwa kama hawafurahishwi na ujumbe na jinsi ujumbe unatolewa, na kama wanaona wanapigiwa kelele za msingi waamue kututangazia tu kuwa Tanzania imekuwa nchi ya kiimla ili na sisi tujue! Lakini kama nchi yetu ni huru na watu wake ni huru na wenye hadhi sawa, watawala wetu watambue kuwa hata ufalme wa Alexander ulivunjika na majeshi ya farao yalitumbukia bahari ya shamu! Wasijidanganya hata kidogo kuwa wataondoka madarakani on their own terms.. hapana, wataondoka kwani wananchi hawatafuata masharti ya "approach" gani itumike!!
 
Icadon, ulichosema ni kweli ! Lakini sidhani kama mheshimiwa rais alitoa deadline ya ukamilishaji wa uchunguzi ! kama alisema zitafuatiliwa, basi tusubiri na definitely hawezi kufuatilia yeye mwenyewe rais kikwete, so kama alipromise yeye ni matumaini yangu kwamba katoa amri na watu wanashughulikia, lakini yeye binafsi hatochunguza chochote, bali atatoa ripoti tu baada ya uchunguzi kumalizika ! so tumuache kwa sasa.
 
Icadon, ulichosema ni kweli ! Lakini sidhani kama mheshimiwa rais alitoa deadline ya ukamilishaji wa uchunguzi ! kama alisema zitafuatiliwa, basi tusubiri na definitely hawezi kufuatilia yeye mwenyewe rais kikwete, so kama alipromise yeye ni matumaini yangu kwamba katoa amri na watu wanashughulikia, lakini yeye binafsi hatochunguza chochote, bali atatoa ripoti tu baada ya uchunguzi kumalizika ! so tumuache kwa sasa.

Ahadi kuwa ni deni, na kama Rais ameahidi kufanya jambo ni bora afuatilie na kuona linafanyika. Ndiyo sehemu mojawapo ya Urais wake, sasa kusema tumuache bila kuulizia ni kumpa kibali cha kutawala kwa amri! Kama anataka kufanya mambo kimya kimya anaweza lakini akitoa ahadi hadharani basi wananchi wanayo haki na sababu ya kuuliza ahadi hiyo imefikiwa wapi. So, Icadon endelea kuuliza!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom