KadaMpinzani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 3,715
- 86
- Thread starter
- #21
machafuko hayawezi kuletwa na approach, yataletwa na wale wanaodhania kuwa nchi hii ni ya kwao peke yao na ambao kwa vile hawafurahishwi na "approach" basi wanajifanya miungu watu. "Mbona hamkupiga magoti mlipoomba".. hatapigiwa mtu magoti tena katika TAnzania, na sadaka ya sifa za uongo haitatolewa tena! CCM bora ing'amue hilo mapema.
Kile wananchi wanakitaka watakisema bila kuambiwa ni "jinsi gani waseme". CCM haiwezi na haina uwezo wa kuamulia ujumbe wa wananchi utolewe vipi! Kama ameamua kukaa kimya hilo ni uamuzi wake, lakini kwa kukaa kwake kimya haina maana ametuamulia ni jinsi gani tumfikishie ujumbe!
Tanzania haina wafalme, na hatuwezi kuruhusu viongozi watende kama wafalme! Hilo tumewakatilia na tutaendelea kuwakatalia, ndio maana nilishatoa pendekezo huko nyuma kuwa kama hawafurahishwi na ujumbe na jinsi ujumbe unatolewa, na kama wanaona wanapigiwa kelele za msingi waamue kututangazia tu kuwa Tanzania imekuwa nchi ya kiimla ili na sisi tujue! Lakini kama nchi yetu ni huru na watu wake ni huru na wenye hadhi sawa, watawala wetu watambue kuwa hata ufalme wa Alexander ulivunjika na majeshi ya farao yalitumbukia bahari ya shamu! Wasijidanganya hata kidogo kuwa wataondoka madarakani on their own terms.. hapana, wataondoka kwani wananchi hawatafuata masharti ya "approach" gani itumike!!
this is what i was talking about ! CCM/WAPINZANI, CCM, CCM, CCM, CCM, CCM , CCM , CCM CCM, CCM, CCM, CCM, CCM, !! Mwanakijiji unaweza ukawa na point nzuri lakini wewe kuihusisha CCM na kila jambo baya basi huondoa maana kabisa ya ujumbe uliokuwa unataka kufikisha. Mentality yako i guess will take another 10 years to clear up, maana inaelekea una imani fulani hivi kwamba something ni wrong hata kama ni right, unaona mabaya tu na sio mazuri !
Ushauri wa bure: Utazeeka mapema, so i suggest you as your fellow mate to sometimes give up space to your mind, rather than kufikiria hivyo (mentality) which will benefit you for a short term period !