Kumekuwa na matamko tata kutokea LATRA kuhusu magari yenye namba D na E kufanywa ndiyo yaliyo magari pekee.
Hali hii si ya kuvumiliwa hata kidogo. Kesho itakuwa gari kuingia Dar na labda hata kuthubutu tu kuwapo Tanzania ni F na G peke yake. Nani ajuaye?
Ni kawaida kwa wanaojidhania kuwa wako salama au kuwa haiwahusu kuonekana wakikenua (meno nje) wasijue ukiukwaki wa haki za wengine ni sawa na kula nyama ya mtu.
"Taratibu haitakuwa magari ya abiria peke yake, kama tukichagua kukaa kimya."
Kwani kwenye gari kinachogomba ni namba za usajili au ubora wake? Vipi kama mtu alinunua gari lake zamani akaamua kuliweka ndani bila kulitumia hata kwa miaka 20? Hilo nalo LATRA hawalitaki?
Kwanini LATRA wangependa watu kununua magari mapya (kama mazuzu tu) hata kama waliyo nayo ni mazima? Au kwanini LATRA wangependa wamiliki wa magari kuyatupa au kuyaondoa magari yao kimkumbo mkumbo tu hata kama ni mazima?
Kwani LATRA wamekuwa na maslahi gani kwenye biashara ya magari? Kwamba wamekuwa madalali, washirika au wauza magari? Kwani hata magari haya yanatengenezwa hapa nchini? Vipi kuwa mawakala wa mabeberu?
"Ikumbukwe kununua gari au chochote na hasa inapokuwa si kutoka kwenye viwanda vya ndani ni kuwaneemesha mabeberu.'
Cuba yenye kutupa sisi misaada, ni moja ya nchi za kizalendo zenye kujua umuhimu wa kutunza kila walivyo navyo; ili kuepuka unyonywaji na hasa huu wa kupitia katika manunuzi yasiyo ya lazima kutoka nje:
Pichani ndiyo yaliyo magari katika ya maana yaliyojazana kwenye barabara bora kabisa za Havana, Cuba. Magari ya miaka 1950s huko. Spares zake zote ni kutokea katika soko lao la ndani.
Huku kufunguliwa kwetu nchi kwa lazima ya kununua nje, ni ili mabeberu yavune yawezavyo, si ndiko alikokupinga sana bwana JPM (RIP)?
"LATRA mnataka magari mapya pasipo na sababu? Vipi, kwani mmeahidiwa nini na nani wenzetu?"
Kwa hakika kuelekea 17 March mnatufanya kumkumbuka sana shujaa wetu yule tuliyembeza wengine bila kujua. Kwa hakika angekuwapo huu upuuzi wa D na E usingekuwapo.
Pumzika kwa amani baba Magufuli uliowaachia nchi leo wanatusukuma kwa mabeberu kama vipi tukakamuliwe kweli kweli.
"Kwa hakika kwa mema tutakumbuka."