Uchaguzi 2020 Kauli ya Sheikh Ponda yakanushwa na wahadhiri wa Dini ya Kiislam

Ili uweze kuaminika ktk jamii yakupasa kutenda na kusimamia haki na kuilinda.

Shekhe wa mkoa wa DSM amejitwisha zigo la kuipigia kampeni CCM na amejipa nafasi ya mufti kuwasemea waislam wote nchini Tanzania. Lkn kwa kuwa Shekhe huyu anakipigia debe chama dola hatukuwaona hawa wanaojiita wahadhiri wa dini ya kiislam wakikemea tabia ya sekhe wa mkoa wa DSM.

Lkn kwa Shekhe Ponda ambaye ameanza kampeni juzi tu, tayari wametoka walikotoka mashekhe hawa ambao hata kujulikana hawajulikani na kuanza kutoa matamko ya kulaani kauli ya Shekhe Ponda. Wanadai Shekhe Ponda siyo msemaji wa waislam nchini.

Walikuwa wapi kumkemea Shekhe wa mkoa wa DSM?
 
Sijawahi kuona hao wahadhiri wakiita press conference kuzungumzia hali za Masheikh wanaoozea magerezani.

Kama hilo la kutetea maslahi ya waislamu limewashinda basi hawana moral authority ya kumsema Ponda

Lissu ndo mgombea aliyeonyesha kukerwa na uonevu dhidi ya masheikh, huyo ndiye anayefaa kuungwa mkono na waislamu wote nchini.

Kitendo cha hawa Masheikh kumshirikisha Alhadi kwenye hiyo press conference, mtu anayempigia kampeni Magufuli waziwazi tena kuomba dua zinazokiuka misingi ya uislamu inaonyesha wao wenyewe hawako serious na wanachokisema maana wana double standard!
Kuwepo kwa Alhad kwenye ile press conference kumeondoa imani kidogo iliyokuwepo kwa wale Wahadhir waliojitokeza kupinga kauli ya Ponda. Alhad ni mtu anayependa sifa sana. Yeye alishalikoroga basi angalau angekaa pembeni asiwepo kwenye ule mkutano. Lakini ili aonekane na hao wanaomtuma kua yeye ndio kawakusanya kina Mazinge, Kipozeo na wengine basi akaona aendelee kuuza sura.!
 
Masheikh ubwabwa wote hao hakuna anayethubutu kutamka neno HAKI! Wote wameng'ang'ania neno AMANI kwa vile ndio propoganda kuu ya CCM. Na Allah analitambua kuwa HAKUNA AMANI BILA HAKI! Amani bila haki ni sera/propoganda ya CCM. WaTz ni wavumilivu tu ndio maana wanafikiri amani inaweza kuwepo bila haki!
 
Tunashukuru kwa kutuunga mkono. Tusijali itikadi zetu lengo ni kumuondoa huyu nyoka CCM
Wananchi wote watamiminika kumwondoa wakala wa beberu.
IMG_20201009_233633_761.jpg
 


Mpeleekeni Lissu mpayukaji aone asijifanye ni msahaulifu kilichotokea mwaka 2015. Na mwaka 2020 kitajirudia mara tatu zaidi. Jambo la muhimu ni kuhakikisha kibaraka huyu wa mabeberu na mashogsa hatoroki nchi baada ya 28/10.

Asije akapata nafasi ya kwenda kutumiwa na yule rais wa mashoga dunia kuzunguka ulaya na marekani akiichafua nchi kwa mambo ya kutunga ya uongo na uzushi. Fursa hii ya huyu adui wa Taifa hili kujilete mwenyewe itumiwe vizuri.
 
Sijamsikia pale Dodoma akisema "waislamu wote" alisema sisi waislamu. Na kudhibitisha hilo alipowauliza walisema ndio! Hivyo wale waliokuwa pale wamekubali
Acha kupindisha. Ukisema Waislamu au Wakristu, hiyo ni jumuisho. Huhitaji kusema wote au wachache.
 
Sijawahi kuona hao wahadhiri wakiita press conference kuzungumzia hali za Masheikh wanaoozea magerezani.

Kama hilo la kutetea maslahi ya waislamu limewashinda basi hawana moral authority ya kumsema Ponda

Lissu ndo mgombea aliyeonyesha kukerwa na uonevu dhidi ya masheikh, huyo ndiye anayefaa kuungwa mkono na waislamu wote nchini.

Kitendo cha hawa Masheikh kumshirikisha Alhadi kwenye hiyo press conference, mtu anayempigia kampeni Magufuli waziwazi tena kuomba dua zinazokiuka misingi ya uislamu inaonyesha wao wenyewe hawako serious na wanachokisema maana wana double standard!
Kaka usemacho ni sahihi kabisa. Hao siyo masheikh. Hao ni masheikh ubwabwa. Hawana moral authority ya kumsema sheikh Ponda Issa Ponda. Masheikh ubwabwa hao kwa sbb kwa nini ktk kutetea haki za Waislamu huwa hawaonekani?
 
Ponda sio mufti, hana mamlaka ya kuwazungumzia waislam wa Tanzania, mwambieni awe anajizungumzia mwenyewe.
Sisi waislamu tunamkubali ponda kuliko muft
Tumefuatilis kwa kina kampeni za CCM kuanzia Magufuli. Majaliwa na Bi Samia,,, hakuna hata mmoja anazungumzia hatma ya mashekh zetu waliopo jela kwa mamia bila kufikishwa mahakamani
Tundu Lisssu pekee Ndio ametugusa nyoyo zetu... Kwa hilo tunasema
Takbirr
Allah Akbar
Kura za waislamu wote ni lissu
Pita misikiti yote ambayo si Bakwata waislamu tunajiandaa kummpa kura lissu ✔️
 
Sidhani Kama Itakua Sahihi Yeye Kuwaongelea Waislam Ikiwa Sio Kiongozi Rasmi...
Issa Ponda Ni Mwanazuoni Mzuri Lakini Mihemko ya Kisiasa Imekua Ikimchukua Mara Kwa Mara Na Kuifanya Elimu Aliyonayo Kuwa Useless Kwa Hapa Hapana Ajipange Na Waislam Sio Wakupelekwa Hivo!!
Sisi waislamu wa kweli ambao tunaguswa na udhalim wanaofanyiwa mashekh zetu jela bila kupelekwa mahakamani tunamuunga mkono sh Ponda
Waislamu wa kweli kura kwa Lissu
Waislamu wanafiki kura kwa jiwe
Hata katika historia kulikua na wanafiki katika waislamu na bado wapo wanaishi kwa kujikomba
 
Cdm sjui ni kwa nini huwa mnajinasa kwenye mitego isiyo na sababu.

Kumtumia shehe ponda ni kosa kubwa Sana la kiufundi hasa sahv tunapoelekea mwishoni mwa kampeni.

Lipo kundi kubwa Sana la Wakristo na waislamu wasiomwamini shehe ponda hata kidogo, na wanasababu zao za msingi. Leo ninyi mmeambatana na huyo jamaa sjui mmelenga nini.
 
Back
Top Bottom