Mgogoro wa BAKWATA na Sheikh Ponda, Waislamu tumeshajua nani wa kumfuata

AKASINOZO

JF-Expert Member
Aug 22, 2016
1,367
2,217
Toka juzi tarehe 17 Oktoba, 2020 Sheikh Ponda Issa Ponda kutokeza front line na kuwahimiza Waislamu wamchague mgombea Urais kupitia tiketi ya CHADEMA, Ndugu Tundu Lissu, kumetokea mkanganyiko hivi.

Baadhi ya watu wanojiita masheikh wakingozwa na Sheikh wa Mkoa wa Der es Salaam kupitia BAKWATA Sheikh Alhad Mussa Salum wakilaani na kupinga kauli ya Sheikh Ponda na kusema kuwa Sheikh Ponda sio mwenzao na wala hawajaafikiana naye.

Mmoja wao alienda mbali na kumuita Sheikh Ponda ni muongo, na mwingine akasema Sheikh Ponda haijui Siasa.

Sasa sisi vijana wa Kiislamu tunasema hivi, malumbano hayo, na mikanganyiko hiyo wala haijatuvuruga. Sisi tunaangalia nani mkweli na nani mpigania haki zetu.

Na hoja zetu kuu ni hizi zifuatazo:
1. Tunaangalia ni nani aliyesimama imara kupigania haki za Waislamu toka zama za miaka ya 1998.

- Huyo ndio mkweli, toka yalipotokea mauaji ya Mwembechai mwaka 1998, Sheikh Ponda alikuwa front-line kusema na kuutetea umma wa Kiislamu uliodhulumiwa.

-Dola ikamuandama, akakimbilia nje ya nchi, baada ya muda kupita alirudi nchini na apokelewa kwao Kigoma Ujiji, na baadae akaendelea na safari ya harakati za dini ya kiislamu.

- Mwaka 2001 kwenye mauaji ya Pemba ni Sheikh Ponda aloyetoka front-line kipaza sauti na kupiga kelele dhidi ya mauaji hayo ya Waislamu.

- Mwaka 2012 baada ya wanafunzi wa Ndanda wa Kiislamu kufukuzwa shule kisa kudai eneo na stahiki zao za kufanya ibada.

Ni Sheikh Ponda aliyesimama kuwatetea wanafunzi hao wa Kiislamu hadi wakarudishwa mashuleni na haki yao ikapatikana.

Matukio yapo mengi,

Kutetea haki za waislamu kama kiwanja cha Chang'ombe, kutetea masheikh walokamatwa nakuwekwa magerezani.

Ni Sheikh Ponda ndio alama za mapigano ya haqq za Waislamu wa nchi hii.

2. Tunaangalia istiqama hata katika kujihusisha na Mambo ya Shubha.

- Sharif Majini ni mganga wa jadi, na mfanya anasa.

- Alhad Musa Salim ni mtu ambaye amekuwa akihusika kwenye Shubha mbalimbali

- Tumemuona akialikwa kwenye matamasha ya sanaa.

- Tumemuona Alhad Mussa Salum akiwasifia binadamu wa kawaida kuliko hata mtume Muhammad.

- na hivi karibuni, Tumemuona akiwa kiongozi wa dini mseto, kitu ambacho ni kufru kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya Kiislamu.

- Tumemuona Alhad Mussa Salum akikufuru kwa kuomba dua kwa jina la Yesu. Kitu ambacho ni kinyume zaidi na mafundisho ya dini ya Kiislamu.

Kwa Alhad Mussa Salum Hatuwezi kumsikiliza kwa lolote, na hana nafasi kabisa katika umma wetu wa Kiislamu.

Hajawahi kusimama hata siku moja kwa ajili ya maslahi ya Waislamu, siku zote Alhad Mussa Salum yupo kwaajili ya tumbo lake.

Na huyu Sheikh Hilary Kipozeo naye ni wale wale -- masheikh wa dunia; kipenzi cha wana Bongo Flavour; muigizaji wa Bongo Movie.

Maisha yake yoote, amejikita kwenye kuzungumza maumbile ya wanawake na 'mizigo' ya wanawake.

Hajawahi hata siku moja kusimama, kutetea dhuluma dhidi ya umma wa Kiislamu. Ameweka Tumbo lake mbele kuliko maslahi ya umma wa Kiislamu.

Na wengine wote hao hatujawahi kuwaona wakikemea dhulma dhidi ya umma wa Kiislamu.

Na tunawashangaa hawajawahi kumkosoa Alhad Mussa Salum alipomnadi mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM. Au BAKWATA inavyofanya kumsifia na kumumbia mapambio mwenyekiti wa CCM.

Ila limewauma saaana la Sheikh Ponda kuwahimiza Waislamu wamchague mgombea Urais kupitia tiketi ya CHADEMA ndugu Tundu Lissu.

Sasa, hao masheikh watambue ukweli kwamba:

Sisi Waislamu wa Tanzania tunamsikiliza na kumkubali zaidi Sheikh Ponda kuliko hata wanavyodhani.

Sisi Waislamu wa Tanzania tunajua madhila na dhulma za serikali ya CCM dhidi ya masheikh na uislam kwa ujumla.

Na kwa hili tuko pamoja na Sheikh Ponda.

Na kwakua amesha tuhimiza tumpigie kura Tundu Lissu, kadi zetu za kupigia kura tumekwsha ziandaa.

Tarehe 28 October kura zetu zoooote tunamwaga kwa Tundu Lissu.

Tunapinga dhulma dhidi ya umma wa Kiislamu.

Tunataka masheikh na ndugu zetu walioko magerezani kwa kesi za kubambikiwa woote waachwe huru.

Tunataka maboresho ya BAKWATA.

Bakwata ilivyo kwa sasa ni chombo cha hujuma dhidi ya waislamu. Wala sio chombo kwa maslahi ya Waislamu.

Na Alhad Mussa Salum na genge lako mtambue wazi kuwa ninyi hamna influence yeyote kwa umma wa Waislamu wa nchi hii.

Mmepewa vyeo tu, na majina makubwa Ila hamna legitimacy yeyote ya kusikilizwa na Waislamu wa nchi hii.

Tuko pamoja na Sheikh Ponda Issa Ponda.

Na tarehe 28 Oktoba tutafanya yale tuloagizwa na Sheikh Ponda Issa Ponda.

Rais mpya
Tanzania mpya
 
Baraka LLAH fiik ndugu,

Bakwata haihitaji maboresho yoyote bali inatakiwa kufutwa kabisa ili ianzishwe taasisi kwa ajili ya Waislamu. Mimi, familia yangu, wanaonitegemea wote na marafiki zangu wa kweli tunamuunga mkono Sheikh Ponda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom