Uchaguzi 2020 A night with Tundu Lissu and Sheikh Ponda at Karatu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,795
It might be a memorable moment to remember!

Mgombea urais mwenye ushawishi mkubwa kwa tiketi ya CDM ametua mjini Karatu muda wa jioni akiwa kachelewa. Na kwa kuheshimu sheria za uchaguzi ameamua kuahirisha mkutano mpaka kesho saa tatu asubuhi.

Kuna mambo kadhaa ya kuvutia na kufutahisha yametokea

1. Lissu amesema anaweka kambi hapo uwanjani. HATOKI atalala hapo. Just imagine wananchi atakaokesha nao na kumbukumbuku watakayotengeneza, ni siku muhimu sana hii.

2. Ujio wa Sheikh mtata kwenye kampeni za Lissu. Sheikh Ponda Issa Ponda, kuna common interest kati ya wawili hawa, wanajiamini sana.

Hawaogopi. Wamefunguliwa makesi mengi kwa nyakati tofauti. Wamekamatwa mara nyingi na kuwekwa mahabusu mara nyingi pia
Wana ushawishi wa ajabu. Imagine usiku huu watakapokuwa pamoja na story watakazopiga. A HISTORY MADE!

3. Kauli ya Sheikh Ponda kuwa 'wamekubaliana' kura zote za Waislam kwa Lissu na CHADEMA! Hili limezua taharuki kubwa upande wa pili maana hawakulitegemea hili hasa kwa kipindi ambacho wameelemewa mno.

Wakati Lissu na Ponda wakiwa Karatu wanapiga story za furaha na wananchi. Huko mjini dalisalama kilinge cha masheikh kimekusanywa kutoa tamko la kulaani na kuikana kauli ya Ponda.

Kuna wakati kuna mambo yanachekesha sana wakati wanakusanywa manabii mia nne tulikaa kimya, baadae wakaitwa viongozi kundi zima wa dini mbalimbali kusifia mazuri ya hii awamu, hatukusema kitu pia. Leo hii kauli moja tu ya Ponda imewatoa nyoka wote pangoni.

Ponda keshasema na wakusikia wamesikia. Ufuasi wa Ponda na ushawishi wake kwa watu mbalimbali unafahamika wazi. Ushawishi wa Tundu Lissu pia uko wazi. Usiku mmoja wa wawili hawa ni unabii mwingine unaopeleka hofu kubwa na bayana huko kwingine!

Usiku mmoja na Lissu na Ponda hapo uwanjani Karatu na wananchi wao na chopa lao. Ni nani angependa kuikosa siku hii muhimu na ya kihistotria?

Nitajiunga nao usiku huu KIROHO niwe sehemu ya historia.

A NITE WITH LISSU AND PONDA; POLITICIAN and SPIRITUAL LEADER. History made!
 
Katika mashehe wasio wanafiki na wasioogopa kukosoa watawala mafisadi,katili,waongo,walaghai ni Huyu Sheikh Ponda ,tangu utawala wa Kikwete amekua akipambana kutetea haki ya Watanzania,acheni wale mashehe ubwabwa Alhaji na yule mufti wanafiki tu na bakwata yao
 
Wambulu wanasifika sana kwa nyota. 1995 Mrema alivyotoka Mbulu hali ilibadilika sana. Tutegemee mananau kuwa mengi hapo uwanjani nyakati za usiku na kama Lissu alikubali kuvishwa ule mgorori mweusi ndio shughuli imeshaisha hiyo.
 
Back
Top Bottom