Katoliki ni zaidi ya uijuavyo!

Katoliki ni zaidi ya uijuavyo!

Hivi unafahamu kama mimi ni mkatoliki na ninijuwa vizuri historia ya Catholic?
Tukufahamu ili iweje..?? Ukiwa nyuma ya keyboard unaweza sema mimi ni Magufuli...(who cares)

Naomba nikuambie kuijua historia ya Kanisa Katoliki ni kuuijua historia ya dunia...!!! Sasa wewe nyanya yako wa Dongobesh hujui historia yake, utawezea kujua historia ya Kanisa lilibeba Ustaarabu wa Dunia...

Hujui ukitaka kusoma Historia ya Western Civilization au European Civilization shurti usome Historia ya Kanisa...

Sasa wewe kapuku uijulie wapi..?? Unachokijua ni Negative side ya Kanisa...
 
Malcom Lumumba Mkuu uko vizuri sana. Hakuna jambo usilolijua. Unaonekana ni mtu unayependa sama kusoma vitabu na mwenye IQ kubwa. Au ni Zitto Kabwe wewe? Naomba nikutembelee kijana wako nina mengi ya kujifunza kutoka kwako.
 
Ni dhehebu pekee linaloongoza kunyoonyo wafuasi masikini barani Africa
 
Tukufahamu ili iweje..?? Ukiwa nyuma ya keyboard unaweza sema mimi ni Magufuli...(who cares)

Naomba nikuambie kuijua historia ya Kanisa Katoliki ni kuuijua historia ya dunia...!!! Sasa wewe nyanya yako wa Dongobesh hujui historia yake, utawezea kujua historia ya Kanisa lilibeba Ustaarabu wa Dunia...

Hujui ukitaka kusoma Historia ya Western Civilization au European Civilization shurti usome Historia ya Kanisa...

Sasa wewe kapuku uijulie wapi..?? Unachokijua ni Negative side ya Kanisa...
Aliyeleta ustaarabu duniani ni Mtume Muhammad s.a.w
Acha kuongopea watu!
 
Sawa mkuu. Na kuwepo kwa Roman Empire kulichagizwa na uwingi wao. Ndo maana wakajiona ni kama watu wa nchi moja waliokiwa scattered katik mataifa mbalimbali, ila wanaunganishwa na kiongozi mmoja POPE, ambaye ukicheki ana hadhi au wadhifa sawa au karibu sawa na president. Yote hii ni katika kurahisisha jamii hii kubwa iliyotawanyika ktk nchi mbalimbali.

Pope ni president wa Vatican
Hivyo usiseme ni kama au Ni ....
Akitembelea nchi yeyote duniani
Ni red carpet treatment ,mizinga 21 na kukagua gwaride,

Sio km viongozi wa makanisa ya chini ya miti.

Pope Ni Habari nyingine kabisa.
 
Upo kwenye promosheni? Maana sijaelewa mlengo wa kupost hii shudu
 
Kanisa Katolike ni Kasa la Majeshi, kama Mungu aitwavyo Mungu wa Majeshi. Katika Historia ya kanisa katoliki, vita vilishawahi kuanzishwa na viongozi wake. Pia amani ilishalindwa na viongozi wa kanisa katoliki. Hata kwa nyakati tulizonazo ni ukweli usiopingika kuwa Kanisa katoliki limehifadhi amani ya dunia. Bila uongozi dhabiti wa kanisa katoliki amani ya dunia ingekuwa imetikiswa vibaya kuliko ilivyotikiswa na vita vikuu vya dunia. Kiongozi wa kaniza Papa Mtakatifu ana nguvu nyingi na ambazo wengi hawazifahamu, zingine zikiwa ni siri kuu.

Mbali na yaho kanisa katoliki ndilo pioneer mkubwa wa elimu na afya duniani. Kanisa katoliki kwa enzi na enzi limekuwa likitoa elimu kwa jamii, tena elimu bora kabisa. Limejenga mashule na vyuo. shule zingine zilikabidhiwa kwa serikali za nchi husika. Pia Kanisa katoliki limesaidia katiaka huduma za kijamii hasa afya kila lilipopita. zahanati na hospitali nyingi zilijengwa na kanisa, na hadi leo kuna hostpitali na zahanati zinazotoa huduma nzuri na za kutegemewa, zote zimejengwa na kanisa katoliki. Mengine ni maji, na barabara kwa baadhi ya maeneo.

Historia inalibeba kanisa hili. Ni kanisa la kwanza kabisa kuasisiwa na jamii ya kikristo ilyoanzishwa miaka takribani 50 baada ya Yesu kuzaliwa. Mtume Petro ndiye kiongozi wake mkuu wa kwanza. Alikuwa Papa wa kanisa katoliki baada ya kufika Roma na kuliasisi kanisa kama Yesu alivyomuahidi. Makanisa yote ya kikristo yameanzia katika kanisa katoliki baada ya kuasi na mengine kujitenga.

Kanisa Katoliki ndio kanisa kongwe zaidi duniani. Kila mtu analionea husuda zaidi ya anavyoonea husuda dini yake.
Hivyo unaamini katika kanisa katoliki kama mimi?
 
Kumbe walishiriki mauaji ya kimbali.
Sio Kimbali tu ata vita vinavyoendelea sasa ivi world wide nyuma ya ivyo vita wapo wao
Na wanajikweza kwa njia ya kutoa misaada kwa wahanga lakin ukifatilia in deep utaona wao ndio source
 
Eti, ndilo kanisa Nabii Isa alimwambia Petro atakua Mwamba na juu yake litajengwa Kanisa? Ukumbuke Nabii Isa hakua mwanasiasa
 
Tukufahamu ili iweje..?? Ukiwa nyuma ya keyboard unaweza sema mimi ni Magufuli...(who cares)

Naomba nikuambie kuijua historia ya Kanisa Katoliki ni kuuijua historia ya dunia...!!! Sasa wewe nyanya yako wa Dongobesh hujui historia yake, utawezea kujua historia ya Kanisa lilibeba Ustaarabu wa Dunia...

Hujui ukitaka kusoma Historia ya Western Civilization au European Civilization shurti usome Historia ya Kanisa...

Sasa wewe kapuku uijulie wapi..?? Unachokijua ni Negative side ya Kanisa...

Mkuu wangu nadhani hatuna haja ya kukashifiana hapa.Wote tuko hapa kujifunza na kuelimishana kwa kutoa ushahidi wa kihistoria na kinadharia halafu mwishoni tunapata muda wa kupima ukweli wa mambo sisi wenyewe
Haya hebu tuwekane sawa kidogo katika hasa kwenye madai yako ya Kihistoria.

Mosi, wajenzi wa huu ustaarabu wa Ustaarabu wa nchi za Magharibi katika mtizamo wa kiasilia ni Wayunani na Warumi (Wale wapagani kabla ya kuanza kwa dini ya kikristo ndani ya Rumi) wataalamu wanasema Greco-Romano Influence. Japo kanisa la Katoliki lina mchango mkubwa sana katika kujenga utamaduni wa Ulaya lakini ushawishi wake siyo mkubwa kama ule wa Dola la Mrumi kabla ya Kaisari Constantine au kabla ya Wagiriki wa Athene.

Pili, kusoma historia ya katoliki siyo kuijua dunia yote ndugu yangu. Huwezi kuielewa dunia kwa kuelekeza macho sehemu moja na kupuuza sehemu nyingine. Binafsi naweza kupinga hoja yako kwa kusema bila kusoma historia ya kuzaliwa na kuenea kwa dini ya Kiislamu basi utakuwa hujasoma historia ya dunia na kama ni mtihani basi wote tukampelekea mwalimu haya majibu na tukapata alama sawa. Yote hii ni kwasababu historia ya dunia haijengwi na mtu moja wala taifa moja bali mataifa mengi sana.

Tatu,mtazamo wako wa kihistoria umekaa Kimagharibi sana na inabidi ubadilike. Kanisa la Katoliki katika uhalisia wa mambo kama taasisi limeanza baada ya Kaisari Constantine kutwaa madaraka ya nchi. Hiyo ni kama Karne ya Nne hivi, lakini ukweli ni kwamba kabla ya Wakatoliki kuwepo kulikuwa na Wamisri, Waajemi, Waarabu na Wayunani kama wajenzi wa ustaarabu wa binadamu.

NB: Kila jamii duniani ina mchango wake katika ujenzi wa ustaarabu na tamaduni za dunia yetu. Kuna historia ya dini kama Uyahudi, Upagani na Buddhism ambazo zimechangia sana ustaarabu kuwepo leo.
 
Back
Top Bottom