Katoliki ni zaidi ya uijuavyo!

Katoliki ni zaidi ya uijuavyo!

Kuhudhuira ibada sio kuwa unaifahamu vizuri historia ya Katoliki. Ok, kama unawafahamu wakatoliki nijibie maswali haya saba tu.
  1. Papa wa Tatu wa kanisa katoliki aliitwa nani na alikuwa na sifa gani za kipekee/
  2. Hadi sasa kanisa katoliki lishatangaza Idadi) watakatifu wangapi katika historia yake?
  3. Ni mapapa wangapi wa kanisa katoliki ambao hawajawahi kuitwa watakatifu?
  4. kanisa katoliki lina mashirika mangapi ya kitume?
  5. Ni makadinali wangapi walishiriki kwenye mchakato wakumpata Papa wa sasa (papa Francis)
  6. Ni nchi zipi duniani ambapo papa hajawahi kuwa na balozi wake? (hakuna balozi anaemuwakilisha)
  7. mabadiliko ya hivi karibuni ya kanuni za ibada yalisababishwa au kuletwa kwa sabahu zipi?

halafu basi kwa vile umeng'ang'ania ushiriki wa kanisa kule rwanda basi tuletee hoja yako hapa. uweke na ushahidi zisiwe hisia zako potofu tu.
Tumsifu yesu kristu mkuu..
 
Ndio dhehebu pekee hata ulikuwa jambazi ukifa unaagwa kwa kuombewa uende mbinguni
Ndio dhehebu pekee ambalo hakuna sheria inayokufunga unafanya yote mabaya hata hadharani
Ndio dhehebu pekee watu kama Pengo wanapatikana
Ndio dhehebu pekee linalopingana na kitabu linalokitumia biblia kuzui wakuu wake kuoa.
 
ni kanisa la amani bwana, usilifanye lionekane ni kanisa la hila!!
Maana vitisho vyako ni as if siyo Janisa la Yesu aliyefundisha Rehema!
Ukitaka kujua ukweli wa mbivu na mbichi jiweke kama mtu usiye na maslahi ya kidini kisha fanya utafiti wa kina utagundua ukweli mchungu ama mtamu
 
Labda wana influence hiyo ktk bara giza, lakini ukienda maeneo kama ya Asia, hawana influence ya kiasi hicho, actually huko wao ni minority kama wasabato masalia.

Philippines ipo ulaya?
 
Walivyogoma kumzika yule bilionea wa Arusha, na utapotaka kuoa ndo utajua jamaa wanamsimamo na misingi.
 
Wewe umeona pombe ndio ishu. Wewe usieruhusu kunywa pombe una vituo vingapi vya yatima, mna shule ngapi, hospitali ngapi za kuhudumia jamii?, au mnaneemesha wachungaji?
Wapuuzi, wameona Pombe ndiyo kosa, ilhali wanafukia madhambi makubwa makubwa makanisani mwao, ila hawa wanaokunywa ndiyo wadhambi,
 
Mathayo 15:7-9
[7]Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema,
[8]Watu hawa huniheshimu kwa midomo;
Ila mioyo yao iko mbali nami.
[9]Nao waniabudu bure,
Wakifundisha mafundisho
Yaliyo maagizo ya wanadamu.
 
Ufunuo wa Yohana 3:14-18
[14]Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika;
Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
[15]Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
[16]Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
[17]Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
[18]Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
 
Ndilo dhehebu pekee ambalo ni dola kamili km lilivyo dola la Tz na mengineyo hapa duniani!

Ndilo dhehebu pekee lenye mfumo imara wa ukusanyaji taarifa zihusuzo dhehebu lao na madhehebu mengine!

Ndilo dhehebu pekee hapa duniani lenye ushawishi usiomithiliwa na jengine!

Ndilo dhehebu pekee lenye mfumo imara wa kiinterijensia na uigwao na mataifa mengi hapa duniani!

Ndilo dhehebu pekee viongozi wao wakuu wakihitaji kuongea na mkuu wa dola wa nchi husika kwa mda wautakao wao-huweza!

Ndilo dhehebu pekee lenye idadi kubwa ya wafuasi kuliko dhehebu lolote hapa duniani!

Kifupi,Katoliki ni zaidi ya dini!
hayo yanawasaidiaje waumini kwenda mbinguni, mbona waumini wake tuko nao kitaa wamechoka kama sisi?
 
Back
Top Bottom