Katoliki ni zaidi ya uijuavyo!

Katoliki ni zaidi ya uijuavyo!

Ulieanzisha thread hii hujaianzisha kwa bahati mbaya hata kidogo.
........hapa Mungu kunakitu anataka tujifunze ntatoa michango yangu mbeleni ila kw kifupi.......
....... kanisa katoliki ndio kanisa lenye utajiri mkubwa kuliko kanisa lolote,
........linaongoza kuwa ni kanisa ambalo viongozi wake ni wasomi mashuhuri kwa kweli, na waaumini wake wengi wao ni wanyenyekevu sana,
.......ni kanisa ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa sana kuisaidia jamii kwa kuanzisha hospitali, mashule, vyou vikuu, vituo vya watoto yatima, na mambo mengine ambayo yanaisaidia jamii kwa hilo sidhani kama mtu mwenye akili timamu anaweza akayapinga,
..........na niseme hivi wapo wakaroliki wengi tu ambao wataurithi ufalme wa mbinguni
.......lakini jee unaliajua vizur kanisa katoliki hapa nazungumzia mfumo wa kanisa si zungumzii mtu binafsi kwa bahati mbaya na ukweli mchungu halimtuku Mungu wa mbinguni
.....mhhh eti nini halimtukuzi Mungu wa mbinguni? Ndio halimtukuzi tutazidi kujifunza
 
Tatizo nini?


upload_2017-10-9_9-34-45.png
 
Ni kanisa pekee wanakunywa pombe bila kujificha
 
Ufunuo wa Yohana 13:11-12,16,18
[11]Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.
[12]Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.
[16]Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;
[18]Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
 
Ni kanisa, madhehebu ni nyie mliojichetua mkajitenga kwa kujioa mamlaka.

Ni kanisa pekee linalopigwa Mawe kutoka kila kona.
 
Niliisoma historia yao, dah hawa jamaa ni hatari wana secret agencies ambazo nyingine zinaongozwa kwa nguvu za giza

Unasoma kutoka anti-catholic sources unategemea nini? Church history ukiisoma sawasawa utagundua kanisa la kweli ni hill pekee.
 
Unasoma kutoka anti-catholic sources unategemea nini? Church history ukiisoma sawasawa utagundua kanisa la kweli ni hill pekee.
Sasa mkuu unavyonifkiria wewe wataeleza secret issues zao hadharani ila kuna watu walikuwemo kwenye iyo secret agencies wakajitoa kuanzisha secret agencies nyingne.. Sasa hao walojitoa ndio wamepambanua yaliyomo kwenye jesuits secretarial
 
Unasoma kutoka anti-catholic sources unategemea nini? Church history ukiisoma sawasawa utagundua kanisa la kweli ni hill pekee.
Ingia Google search One Evil jesuits secret agencies.. Utajua na utakaokutana nayo huko utuletee mrejesho tafadhali
 
mbona umeruka swali ili uwahi mbwembwe. Nakuuliza katika hao wawili Pengo na Mwinzie nani hataolala usingizi?Pengo karuka utaratibu wa ndani kumwanika mwingine ktk mahakama ya umma, kisha kahalailisha kwa kwa utetezi huo huo aliouvunja. Nini huajaelewa wakati unaanza mbwembwe.
Angesema Rais wa Maaskofu Tz
 
Ndilo dhehebu pekee ambalo ni dola kamili km lilivyo dola la Tz na mengineyo hapa duniani!

Ndilo dhehebu pekee lenye mfumo imara wa ukusanyaji taarifa zihusuzo dhehebu lao na madhehebu mengine!

Ndilo dhehebu pekee hapa duniani lenye ushawishi usiomithiliwa na jengine!

Ndilo dhehebu pekee lenye mfumo imara wa kiinterijensia na uigwao na mataifa mengi hapa duniani!

Ndilo dhehebu pekee viongozi wao wakuu wakihitaji kuongea na mkuu wa dola wa nchi husika kwa mda wautakao wao-huweza!

Ndilo dhehebu pekee lenye idadi kubwa ya wafuasi kuliko dhehebu lolote hapa duniani!

Kifupi,Katoliki ni zaidi ya dini!

Na pia usisahau kuwa Kanisa Katoliki pia ndiyo dhehebu pekee lenye Waumini wenye akili kubwa, nyingi na zilizotukuka kabisa duniani kuliko madhehebu mengine yote yale. Great Thinkers, Think Tank, World Intellectuals na Philosophers wengi huwa ni Roman Catholics ( Wakatoliki )
 
Ulieanzisha thread hii hujaianzisha kwa bahati mbaya hata kidogo.
........hapa Mungu kunakitu anataka tujifunze ntatoa michango yangu mbeleni ila kw kifupi.......
....... kanisa katoliki ndio kanisa lenye utajiri mkubwa kuliko kanisa lolote,
........linaongoza kuwa ni kanisa ambalo viongozi wake ni wasomi mashuhuri kwa kweli, na waaumini wake wengi wao ni wanyenyekevu sana,
.......ni kanisa ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa sana kuisaidia jamii kwa kuanzisha hospitali, mashule, vyou vikuu, vituo vya watoto yatima, na mambo mengine ambayo yanaisaidia jamii kwa hilo sidhani kama mtu mwenye akili timamu anaweza akayapinga,
..........na niseme hivi wapo wakaroliki wengi tu ambao wataurithi ufalme wa mbinguni
.......lakini jee unaliajua vizur kanisa katoliki hapa nazungumzia mfumo wa kanisa si zungumzii mtu binafsi kwa bahati mbaya na ukweli mchungu halimtuku Mungu wa mbinguni
.....mhhh eti nini halimtukuzi Mungu wa mbinguni? Ndio halimtukuzi tutazidi kujifunza
Mkuu hujakosea sana,
Wakatoliki ni wabia wakubwa wa maendeleo ya Kiuchumi na kielimu hapa duniani. Wamesaidia sana watu wengi masikini kielimu na kiafya nchini Tanzania hasa baada ya kupata Uhuru na kwa hili niseme ukweli tunawashukuru sana bila Unafiki wowote ule.

Lakini ukweli mchungu ni kwamba shughuli zao nyingi zina maslahi mapana sana kwao binafsi zaidi ya ambavyo wewe unaweza kufikiri au kudhani. Hivi unadhani kuwa mashirika mengi yanayosaidia elimu na afya hapa duniani yanafanya kazi hizo bure ???

Shirika kama The Rockefeller Foundation limesaidia sana watanzania wengi kama Dr. Augustine Mahiga na Professor Justinian Rweyemamu kuwa wasomi wenye ushawishi mkubwa duniani na Tanzania lakini unadhani hao Rockefellers walianzisha hizo kazi bure tu au kukusaidi mtu masikini peke yake???

Kuna Shirika kubwa linaitwa The Cecil Rhodes Foundation. Hili limekuwa likitoa misaada mikubwa ya Kielimu kwa Wamarekani na Waingereza, limesomesha watu wengi sana kwenye nchi hizo. Lakini ukisoma kwa umakini utajua Cecil Rhodes alipendekeza kwamba Marekani na Uingereza watakuwa karibu sana kama Wasomi wao watakuwa wana mtazamo moja wa kifikra. Hivyo kwenye Diary yake aliandika kwamba Uingereza isitumie tena nguvu kutaka kutawala Marekani kwasababu haitawezekana kirahisi kama alivyofikiri hapo mwanzo lakini mifumo ya Elimu ya Oxford na Harvard ikilingana basi wasomi ni lazima watakuwa na mtazamo moja wa dunia.

Leo hii Wamarekani na Waingereza ni kama nchi moja zilizotengwa na bahari tu. Wanaendana sanaaa na mtazamo wao wa dunia hii THE ANGLO-AMERICAN WORLD VIEW umejengwa juu ya huo ujanja wa akina Cecil Rhodes.

Wakatoliki baada ya kugundua ukweli mchungu walijifunza kitu kikubwa kwamba hata uwe na nguvu vipi huwezi kumtawala mwanadamu kama Mnyama. Hili hata Mungu muumba halifanyi kwasababu anaheshimu utashi wa viumbe wake (Free Will)

Basi wakaja na mifumo ya kielimu hapa duniani. Wakajenga Mavyuo na Mashule makubwa ili hata kama mwanadamu atafikiria basi atafiria ndani ya duara fulani la mawazo na hawezi kutoka nje sana ya hapo. Mfano Mzuri leo hii umchukue mwanafunzi wa Seminari ya Katoliki ya Maua, Don Bosco na Mafinga utakuja fahamu kwamba wote wana tabia moja na hata namna yao ya kufikiri inaendana sanaa. (Similar Thought Pattern)

Tafuta tena mwanafunzi wa vyuo kama LOYOLA, GEORGE TOWN UNIVERSITY, PONTIFICIA UNIVERSIDAD CATOLICA DE CHILE na SAUTI MWANZA (hapa kwa SAUT nazungumzia wale vipanga wa kweli kweli) ukawakalisha pamoja utakuta wote wana namna moja ya kufikiri. Unaweza kushangaa lakini ndivyo mifumo ya kitaaluma ya vyuo hivyo inawatengeneza wanafunzi wake.

Kibaya zaidi hata awe mtoto wa Kiislamu,kiprotestant, Kilokole, Kibahai,Kihindu au Kipagani. Yaani akiishasoma hayo mashule na mavyuo ya Kikatoliki basi kuna namna moja ya kufikiri itaendana sana na Wakatoliki hata kama kuna mengi atapishana nao. Tayari ashatengenezwa kiakili. (Jiulize kwanini watoto kutoka hizo shule hata wawe na uwezo wa kawaida mwishoni huwa wanakuwa na ufaulu mkubwa sana??) Tayari ashatengenezwa akili hapo.

Teh teh teh teh,
Hakuna msaada wa bure kwenye dunia yetu mkuu. Mfano mwingine kipindi kile cha Ujamaa unahisi kwanini Mzee Nyerere alisomesha sana watanzania Urusi, Uchina,Cuba na India ambako ni nchi za Kijamaa ??? Jibu ni rahisi tu, wajamaa wa Urusi ya Kisovyeti na Uchina walisomesha sana Waafrika, Waarabu na Walatini kwasababu walikuwa wanajenga kambi ya Ujamaa. Leo hii mchukue mtu kama Issa G Shivji halafu umpeleke chuo kama Peking cha Uchina akafundishe pale ni atakubalika na kueleweka balaaa lakini mpeleke chuo kama University of New York kwa mabepari ni lazima atapuyanga sana na watampuuza balaa.

NB: There is no free lunch or free ride home. Once you eat devil's food you got to pay devil's bill. Tujifunze kuangalia nini kipo nyuma ya misaada hata kama wewe unahisi hakuna hela ya moja kwa moja wanapata. Faida wanayopata ndugu zetu Wakatoliki kwa kutoa hii misaad ni kubwa mnooo kwa kanisa.
 
Back
Top Bottom