SoC04 Katika kuboresha mpira wa miguu nchini kwa Vijana, napendekeza UMITASHMITA na UMISETA iwekwe chini ya TFF na kutolewa TAMISEMI

Tanzania Tuitakayo competition threads

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,090
1,882
Hili ni andiko langu kwa wapenda soka nchini.
Bila shaka mtakubaliana nami, kwamba, tangu kuanzishwa kwa UMITASHMITA na UMISETA, kumekuwa na malalamiko mengi kwa walimu na wadau wengine kuwa, UMITASHMITA NA UMISETA hazijatusaidia sana kwenye sekta ya michezo hususani mpira wa miguu, hii nikwasababu, UMITASHMITA na UMISETA imewekwa chini ya wizara ya TAMISEMI.

Ki uhalisia, TAMISEMI hawajawahi kuwa serious katika kuendeleza vipaji vya Vijana walioko mashuleni. Moja ya changamoto ya TAMISEMI kusimamia michezo shuleni, hawatoi pesa ya kutosha kwa ajili ya michezo, na hii nikwasababu TAMISEMI wanamambo mengi ya kusimamia, thus why inapokuja suala la michezo kwa wanafunzi, wanachukulia ni minor case sana. Unakuta watoto wanashiriki UMISETA au UMITASHMITA lakini hawana hata jezi, hawana sanduku la huduma ya kwanza, watoto hawana viatu nk nk.

Na hata wanapofaulu kwenda ngazi za tarafa na wilaya, bado mazingira siyo rafiki kusema mtoto na walezi wake wafurahie kijana wao kishiriki mashindano hayo. Siwezi kubeza juhudi wanazozionesha lakini kwa maendeleo ya michezo tunayoyatamani, TAMISEMI atatuchelewesha sana, hivyo napendekeza TFF isimamie michezo hii, iwe chini ya ligi za under 20, 19,18,17,15,14 nk na iendeshwe Kila harimashauri. TFF wasimamie shule zote za serikali na private, usajili wa watoto uwe kupitia mifumo ya electronic, na Kila shule iliyosajili itagharamia baadhi fomu ya usajili, maana yake, TAMISEMI atawajibika kulipia shule zitakazokidhi vigezo. TFF watatumia mashindano hayo ya UMITASHMITA na UMISETA kama mbadala wa mashindano yaliyopo ya Vijana.

TFF wataelekezwa tu kupanga ligi hizo za Vijana kwa kufuata kalenda ya masomo itolewayo na wizara ya elimu sayansi na Teknolojia. Hii itatusaidia kupata vipaji halisi vya Vijana kwenye mpira wa miguu.

Mwisho
Michezo ni ajira, serikali iongeze bajeti kwenye sekta ya michezo ili tuwe na taifa linalosifika duniani kwa michezo
 
usajili wa watoto uwe kupitia mifumo ya electronic, n
Itasaidia sana hata ufiatiloaji wa umri, maana mfumo utataka cheti cha kuzaliwa hivyo tutajua tu.

Mwisho
Michezo ni ajira, serikali iongeze bajeti kwenye sekta ya michezo ili tuwe na taifa linalosifika duniani kwa michezo
Ni ajira inayotengeneza mamilionea wachaache sana halafu wengine wanabaki tu kujenga afya na burudani kama washangiliaji. Tusisahau hilo.

Ni lama kubeti tu, wachache watapata mamilioni lakini wengi wengine watakula leo ma kesho imeishaa.
 
Back
Top Bottom