Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika atema cheche kuhusu kauli ya Mwenyekiti wa CCM ya uchaguzi kuwa huru na haki

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,650
218,130
Hapa ndio utaelewa kwanini Mh Mbowe ameamua John Mnyika awe Katibu Mkuu wa CHADEMA , yaani anatema madini matupu ! Mnyika amesema:

"Sasa nifikishe ujumbe tu kwa Rais Magufuli, ambaye amesema yeye, akiwaambia mabalozi kwamba, uchaguzi wa mwaka 2020 utakuwa uchaguzi huru na haki ujumbe wangu kwa Rais Magufuli uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki kama tayari yeye alishawaita watendaji ikulu akakaa nao wakaharibu uchaguzi wa serelikali za mitaa.

Kama anataka kuwaonyesha mabalozi kwamba anaamini kwenye uchaguzi huru na haki aanze kwa kuusuta uchaguzi wa serikali za mitaa ulioharibiwa na watendaji wake hilo la kwanza.

La pili kama Magufuli, Rais, mheshimiwa kama amejirudi ameanza kuamini kuhusu uchaguzi huru na haki tukwenda kuanza Bunge siku ya Jumanne siku chache zijazo siku ya Jumannne mkutano wa Bunge unakwenda kuanza.

Kama Magufuli anaamini kwenye uchaguzi huru na haki apeleke Bungeni muswada wa sheria kwa hati ya dharula wa marekebisho kwenye katiba yetu kwenye eneo linalohusu uchaguzi, ili moja kuwe tume na huru ya uchaguzi pili aruhusu matokeo ya urais yaweze kupingwa mahakamani lakini tatu mshindi wa uraisi ili atangazwe awe na asilimia zisizopungua hamsini za kura.

Apeleke haya marekebisho Bungeni kama Magufuli anaamini kwenye uwepo wa uchaguzi huru na haki na muswada huu uambatane na marekebisho ya sheria zote ili tume isitumie tena wakurugenzi isitumie watendaji kwenye kata iwe na watumishi huru wa tume wa uchaguzi.Watakaosimamia uchaguzi huru kwenye udiwani ubunge na urais kazi zote za kiuchaguzi na kama Magufulia anaamini kwenye uchaguzi huru na haki afanye haya.

Na ndugu zangu jambo hili halipaswi kuwa sauti ya CHADEMA peke yake, sisi CHADEMA tunachokihitaji sio kupendelewa tunahitaji uchaguzi huru na haki ili wananchi waamue kwa ridhaa yao diwani wanaomtaka raisi wanaemtaka mbunge wanaemtaka rais wanaemtaka sisi tunazo sera tunao uongozi tutakwenda kujinadi kwa wananchi kwenye hatua mwafaka tunachokihitaji ni uwanja sawa wa kisiasa.

Sasa kwa sababu jambo hili halipaswi kuwa la CHADEMA peke yake ni rai yangu kwenu nyinyi dai la kudai tume huru ya uchaguzi tume huru ya uchaguzi lisiwe kauli ya viongozi tu wana CHADEMA wote kwenye mitandao wa kijamii kila mahali na kwenye semina hii mjadiliane muweke mikakati mtadai vipi tume huru ya uchaguzi kila mtu kwa nafasi yake.

Ni rai yangu vilevile kwa taasisi za dini makanisani misikitini ili kuepusha Tanzania isipitie kwenye mlango ambao Zanzibar ilipita Januari 26 ambayo ni siku ya kesho na Januari 27 ambayo ni siku ya kesho kutwa Taifa letu nakumbuka mauaji yaliyofanyika Zanzibar yaliyofanywa na vyombo vya Dola kwa sababu ya kupambana na wananchi waliokuwa barabarani wakitetea haki yao ya kuwa na uchaguzi huru na haki.

Ili Taifa letu lisipite kwenye njia ambayo Zanzibar ilipitia mwaka 2001 ufumbuzi ni mwaka 2020 iwe ni jamii za kimataifa iwe asasi za kiraia iwe ni vyombo vya habari iwe ni taasisi za kidini kila mmoja aimbe tume huru, ya uchaguzi tume, huru ya uchaguzi tume huru ya uchaguzi ili tukafanye uchaguzi kwa amani na haki tulete mabadiliko tunayoyataka.

Sasa ndugu zangu katika kipindi hiki kifupi cha madai ya tume huru ya uchaguzi tuna muda mfupi sana, Bunge limebakisha mikutano niwili tu, mkutano unaoanza Jumanne na unaisha tarehe saba na mkutano wa Bunge unaoanza mwezi Aprili na unaisha mwezi Juni, mkutano wa Juni ni mkutano wa bajeti ni ngumu sana haya marekebisho ninayoyasema kufanyika kwenye mkutano wa Aprili mpaka Juni.

Kwa hiyo Taifa letu limebakiza mkutano mmoja tu wa bunge wa kufanya muujiza wa mabdiliko ya kuwezesha nchi yetu kuwa na uchaguzi huru na haki na ni mkutano unaoanza siku ya jumanne na kuisha tarehe saba.

Katika mazingira kama haya natambua kuna ajenda nyingi katika nchi yetu, kila siku serikali hii inatengeneza ajenda Rais Magufuli na wenzake wanatengeza agenda, anatengeneza ajenda ya kusema kusema kangi lugola aondolewe au ajiuzulu awekwe waziri mpya nchi ijadili kuhusu kangi Lugola kudaiwa kusaini mkataba bila ridhaa ya Bunge.

Halafu nchi impongeze Magufuli bila kumuuliza hivi mikataba ya ujenzi wa kiwanja Chato au mikataba ya ununuzi wa ndege au mikataba mingine ni mingapi ilipelekwa Bungeni ikapata ridhaa ya Bunge.

Nchi ijadili haya isahau kuhusu tume huru ya uchaguzi, nchi ijadili Rais akisaini eti makubaliano na kampuni ya Barrick au Acacia kuzalishwa kwa kampuni ya Twiga nchi ianze kumpongeza Rais kwa kutetea rasilimali za Taifa bila watu kujiuliza hivi zile noa tulizoahidiwa kwa kila mtanzania kutokana na makinikia ziko wapi?"
 
Attachments

  • John mnyika katibu mkuu wa Chadema atema cheche.... Share zaidi ziwafikie ( Source ).mp4
    8.8 MB
Tanzania aisee kuna vipaji sana kuna siku niliwai waza kwamba kwanini vyama vya siasa visibadilishe katiba zao yaani chama kimoja kikichukua dora bahada ya uchaguzi teuzi mbalimbali kama za mawaziri zisiangalie mtu anatoka chama gani bali uwezo binafsi nafikili nchi inaweza piga hatua sana
 
Unajua viongozi wa ccm ni weupe sana kichwani , haya mambo ya uchaguzi huru si mchezo !
 
Hapa ndio utaelewa kwanini Mh Mbowe ameamua John Mnyika awe Katibu Mkuu wa Chadema , yaani anatema madini matupu !

angalia mwenyewe video hii hapa
Hivi unategemea kweli yule yule aliyeharibu uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana, Leo hii "aokoke na kutubu" na kuahidi kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakuwa huru na haki?

I doubt so much on that assurance
 
Tanzania aisee kuna vipaji sana kuna siku niliwai waza kwamba kwanini vyama vya siasa visibadilishe katiba zao yaani chama kimoja kikichukua dora bahada ya uchaguzi teuzi mbalimbali kama za mawaziri zisiangalie mtu anatoka chama gani bali uwezo binafsi nafikili nchi inaweza piga hatua sana
Mnyika ni kichwa sana mkuu, sema tu hii katiba yetu ina ubaguzi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania aisee kuna vipaji sana kuna siku niliwai waza kwamba kwanini vyama vya siasa visibadilishe katiba zao yaani chama kimoja kikichukua dora bahada ya uchaguzi teuzi mbalimbali kama za mawaziri zisiangalie mtu anatoka chama gani bali uwezo binafsi nafikili nchi inaweza piga hatua sana
Ng'ombe na punda hawawezi kuvuta tela moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania aisee kuna vipaji sana kuna siku niliwai waza kwamba kwanini vyama vya siasa visibadilishe katiba zao yaani chama kimoja kikichukua dora bahada ya uchaguzi teuzi mbalimbali kama za mawaziri zisiangalie mtu anatoka chama gani bali uwezo binafsi nafikili nchi inaweza piga hatua sana
Bahada ndo kitu gan?

ARUSHA KWETU
 
Back
Top Bottom