Yeye hakutumwa hayo unajua kilichomkuta ? Alitorokea porini na kuacha unabii kabisa baadavya Jezebeeli kutangaza kuwa atamuuua na akagoma kuendelea kuwa nabii akamwambia Mungu hataki tena
Mungu akasema sawa kakabidhi kazi kwa Elisha wewe ondoka duniani tena haraka akapaa mbio
Yohana Mbatizaji pia alitumwa kuhubiri ubatizo uletao toba akaacha hilo lake alilopewa na Mungu akaenda kwenye kukemea wanasiasa akeanda kumkemea mwanasiasa Herode
Na Herode akamuua kwa kumkata kichwa
Kuna red line kati ya Kanisa na siasa ambayo kila upande unahitaji kubaki kwenye line yake
Manabii wana ruka ruka na kuvuka mstari ni at their own risk .Ulinzi wa Mungu huwa hauko guaranteed huko wanakorukia nje ya mipaka ya wito
Zamani mapdre walikuwa watu wa kushinda sehemu za upweke na kwenye monastery wakisali sana na kufanya kazi huko huko maeneo ya kanisani walipo ukiwaona mtaani wana kanzu zao wanaenda kuzika au kumpa mtu mpako wa wagonjwa basi tena hawi peke yake.Kaongozana na watumishi wa kanisa.Walikuwa na utisho wa kuheshimika hasa.Ukimuona padre mtaani ni kama umeona mungu.Akisema kitu watu wanatii tena kwa unyenyekevu mkubwa
Sasa hivi mapadre wamezagaa mitaani kwenye mabaa,ma guest house na kwenye vijiwe vya umbeya wa siasa nk wakisikiliza ya vijiweni mitaani wapate vya kuhubiri kanisani huku wakiwa wamevaa kiraia tu sio kanzu wala na misalaba tena..
Mapadre hawafugiki misheni aunjwenye parokia wamekuwa kama kuku wa kienyeji wanazurura hovyo mitaani na vijiweni .Nao hao ndio wanakuwa maaskofu inatisha
Heshima haipo tena wanabezwa ns wsumini hadi kwenye vigango na jumuiya
Padre anaonekana ni msela tu ambaye kachagua tu njia ya kupata riziki ni kupitia upadre lakini si anaonekana wa heshima kivile kama wa zamani
Kanisa lijitathmini.Hixi sauti za watu kutaka kanisa likae mbali na siasa zina hoja